Ijue Sheria ya Ardhi: Taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ijue Sheria ya Ardhi: Taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,858
  Trophy Points: 280
  Taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi
  [​IMG]

  Allan Kajembe

  [​IMG] UTATUZI wa migogoro ya ardhi, ni mojawapo ya mambo yalitengenezewa mchakato mahsusi katika kupata suluhu ya matatizo ya ardhi.
  Baada ya kutungwa kwa sheria mpya za ardhi mwaka 1999, yaani Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji, utaratibu wa utatuzi wa migogoro ya ardhi, pia umebadilika.
  Miongoni mwa mambo makubwa yaliyofanywa na sheria hizi, ambazo ni matokeao ya sera ya ardhi ya taifa, ni kutengeneza mfumo wa kipekee wa kutatua matatizo ya ardhi.
  Sehemu ya tano ya sheria ya ardhi ya vijiji, namba 5 ya mwaka 1999, inahusu utatuzi wa migogoro ya ardhi ya kijiji.
  Kwanza kabla hatujajua njia hizi za utatuzi wa migogoro ya ardhi, ni vema tukajua maana ya vitu vifuatavyo, ambavyo vinauhusiano wa moja kwa moja na sheria hii ya ardhi ya vijiji na utatuzi wa migogoro kwa ujumla.
  Kwanza ni hati ya hakimiliki ya kimila kama ambavyo imeelezea na kifungu cha 2 cha sheria hii, ambacho kinafanya rejea katika kifungu cha 25(2) amabcho kinaelezea kwamba hatimiliki ya kimila itatolewa katika fomu maalum iliyoainishwa na sheria.
  Na itakuwa na sahihi ya mwenyekiti wa halmashauri ya kijiji na katibu wake. Pia hati hii itatakiwa kuwekewa sahihi au alama ya dole gumba na mtu atakayepewa hati hii kama mmiliki, pia itatakiwa kutiwa sahihi na kuwekwa na ofisa ardhi wa wilaya ambayo kijiji husika kipo.
  Dhana ya pili ambayo ndugu msomaji utatakiwa uwe nayo akilini wakati wa kutatua migogoro ya ardhi ya kijiji ni ya mwanakijiji aliyepewa sheria hii chini ya kifungu cha 2 kwamba ni mtu ambaye kwa kawaida ni mkazi wa kijiji au ni mtu ambaye anatambuliwa na halmashauri ya kijiji huisika.
  Vilevile, vizuri tukajua tasfiri ya halmashauri ya kijiji kama inavyoelezewa na sheria hii kwamba ni tasfiri iliyotolewa na sheria ya serikali za mitaa (mamlaka za wilaya) ya mwaka 1982.
  Pia baraza la ardhi la kijiji pia limepata tafsiri ndani ya sheria hii kwamba ni baraza la lililoanzishwa maalum kwa ajili ya kusuluhisha na kusaidia kupatikana kwa muafaka kwa pande mbili zinazopingana katika mgogoro wa ardhi ya kijiji.
  Baada ya kuangalia dhana hizo, basi tuanze kuangalia taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi za kjiji.
  Chini ya kifungu cha 16 cha sheria hii, kila kijiji kimeamuriwa kiuende baraza lake la ardhi la kijiji, ambalo, kama tulivoona hapo awali, litakuwa na kazi kubwa mbili, kwanza kusuluhisha migogoro yote inayotokana na ardhi katika kijiji kilichopo, na kazi ya pili ni kusaidia kusuluhisha pande zinazohusika katika mgogoro wa ardhi za kijiji, kufikia muafaka.
  Baraza hili kwa mujibu wa sheria hii, linatakiwa kuwa na wajumbe saba ambao watatu kati yao watakuwa ni wanawake, ambao sheria chini ya kifungu cha 60(2) kifungu kidogo cha (a) na (b) kimeweka taratibu za kuwapata na kwamba watatakiwa kuwa wameteuliwa na halmashauri ya kijiji na pia watatakiwa kuafikiwa na mkutano wa kijiji.
  Mkutano huu, umetafsiriwa na sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982.
  Kwa mantiki hiyo, mtu anapokuwa anataka kupitia sheria hii, basi anatakiwa kutilia maanani pia sheria hiyo ya Serikali za Mitaa (mamlaka za wilaya) ya mwaka 1982.
  Chini ya sheria hii, kuna athari pale mtu ambaye kama mjumbe. anatakiwa kuthibitishwa na akashindwa kuthibitishwa basi mtu mwingine atatakiwa kuteuliwa na kuthibitishwa kuchukua nafasi kama mjumbe wa baraza la ardhi la kijiji.
  Hali hii pia itatokea kama mjumbe husika atajiuzulu nafasi yake, au kama atafariki dunia, au kama atakosa heshima na sifa nzuri za kuwa na ufahamu wa sheria za mila za ardhi na kama mtu mwenye msimamo.
  Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 60(3) cha sheria hii.
  Itendelea.
   
 2. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu!! Ila naona uwepo wako katika jukwaa la sheria umepungua kidogo
   
 3. K

  Kaseko Senior Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Samahani, ninauliza na baraza la ardhi la kata linaundwa na sheria namba ngapi na ya mwaka gani?
   
 4. N

  Nagoya Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je iwapo baraza zima la ardhi la kijiji limekiuka maadili, mfano kula rushwa. Lina adhibiwa na nani na kwasheria ipi? Nauliza hivi kwa sababu mabaraza mengi yamekuwa yakijihusisha na vitendo vya rushwa na kuhukumu kesi vibaya kinyume cha sheria. Ni nani mwenye mamlaka ya kulisimamisha au kulifuta baraza la kijiji?
   
 5. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,024
  Likes Received: 8,508
  Trophy Points: 280
  Sheria za ardhi mijini je,zipo?
   
 6. O

  OleSeuri Member

  #6
  Mar 8, 2013
  Joined: Mar 3, 2013
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
   
 7. NG'HOMELE

  NG'HOMELE JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2016
  Joined: Jan 13, 2014
  Messages: 468
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  watu km nyinyi tunawahitaji sana
   
 8. g

  gelevahekejr Senior Member

  #8
  Mar 14, 2016
  Joined: Feb 24, 2014
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Habari yako kaka pole na kazi naomba kujua kama Nina haki kwenye kesi yangu ya ardhi iliyo hukumu baraza la ardhi la kata. Mm nmenunua kiwanja 2014 na kujenga na nakaa baada ya kujenga yapata miezi 7 anatokea MTU anasema kiwanja hiki nilinunua mm ninamuuliza umenunua kwa nani ananitajia jina (mtoto wa mwenye mashamba kabla hayaja pimwa na serikali.) naomba nikupe historia fupi ya kiwanja hiki mnamo mwaka 2002 serikali ya kijiji ilipima maeneo haya viwanja kwa sababu yalikuwa mashamba walikubaliana kuwa viwanja kilichokuwa kinafanyika wanapima eneo jingine wanakuachia lingine wanamwachia mwenye Shamba sasa yule aliye pewa eneo like alishakufa kabaki mwanae ndie aliye niuzia mm sasa kwa sababu mwanaye huyu anaishi mbali kidogo na eneo hili alipofika aliambiwa eneo hili anamiliki mwenyekiti kitongoji kamuuzia mwanaye ikabidi mtoto huyu aende baraza la kata ndipo Huyu mwenyekiti kuitwa aka andika hati ya baraza la kata kumkabizi kiwanja huyu mtoto mbele ya balaza hili hili .shauri;mm ilibidi nimtafute mwenye kiti aliyegawa haya maeneo na mjumbe lakini sio mwenye kiti huyu alikabizi kwa sababu kipindi mile hakuwa mwenye kti)akatoa ushaidi kama walivyo gawa na kupima maeneo haya na mm niliwapa karatasi ya wao kama balaza alio andika mwenyekiti na makabiziano ya balaza ya kiwanja hiki ;hukumu ya utata;hukumu inampa haki aliye nishitaki kuwa nimevamia eneo lile kwa sababu wamemhoji mwenye kiti kitongoji aliye andika barua ile ya kumkabizi wakati kpindi eneo lile linagawiwa yy hakuwa mwenye kiti lakini alifahamishwa kuwa kiwanja hiki ni cha flani lakini yy alimpa mwanaye tena baada ya kugundua kuwa aliyepewa amekufa baada ya kumpa mwanaye kumbe tena mwenye kiti huyu tena akamtafuta mtoto wa mwenye mashamba yale ili auze tena bila MTU kujua wakamtafuta mteja mwingine wakamuuzia huyu ndie aliye nishitaki mm na kunipola uwanja (huyu mwenye mashamba Alisha kufa muda mrefu tu) na mm hapa ndipo napoishi sina pengine harafu nipo kuwa namhoji huyu mtoto wa mwenye mashamba niliambiwa mwisho maswali matatu,inakuweje MTU ambaye sijahojiana Nate maelezo ya ingie kwenye hukumu hapo ni sahihi kwa mjibu wa sheria? naomba msaada wako wa kisheria
   
 9. jaffari yogo

  jaffari yogo JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2016
  Joined: Apr 3, 2014
  Messages: 681
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Pole na majukumu.
  Naomba kujua haki yangu hapa.
  Mwaka 1986 watu walihamia kwenye mahame na tukaishi huko Miaka zaidi ya 20 halafu baadae wanajitokeza watu kuwa eneo ni la kwao nasi mda wote huo tuko hapo. Sasa wanalazimisha tuondoke tuwaachie eneo hilo na kwa sasa ni miaka 30.
  Je, hapo sheria inasemaje? Naomba kuelewa maana sasa inakuwa kero.
   
 10. Mastamind

  Mastamind JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2016
  Joined: Apr 30, 2013
  Messages: 622
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
   
 11. Michael Ngusa

  Michael Ngusa JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2016
  Joined: Aug 4, 2014
  Messages: 1,647
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu kwa elimu hii. Hakika sitakuja kudhurumiwa ardhi yangu!!
   
 12. king kan

  king kan JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2016
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,264
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
   
 13. king kan

  king kan JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2016
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,264
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Mkuu andika vizuri maelezo yako yaeleweke. Kuna issues za msingi ambazo hujaeleza vizuri. Mfano hujatuambia walipopima viwanja walitoa nyaraka zozote kwako mfano Kama barua ya Toleo (letter of offer) au hati. Pili maelezo yanakuwa magumu kuyaelewa vizuri. Nakusihi utulie halafu ujielezee vizuri.

  Labda swali jingine hilo eneo liko mahala gani? Maake mamlaka za kusimamia maeneo zinatofautiana kutokana na aina ya Ardhi. Mfano kama Ardhi yako ipo kijijini kuna taratibu zake na hata shauri lako lilitakiwa lipelekwe kwenye baraza la ardhi la kijiji kama hatua ya mwanzo.

  Pili kuna issue ya wewe ulinunua vipi hilo eneo (iwapo ni ardhi ya ujumla), kuna kasumba ya watu kununua viwanja bila kufuata taratibu matokeo yake huishiwa kutapeliwa. hilo nalo sidhani kama umesema. Nakushauri utulie na ujieleze vizuri hata usiogope.
   
 14. king kan

  king kan JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2016
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,264
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama kuna jambo gumu katika ardhi ni hili. Kiuhalisia iwapo hao jamaa ni kweli wanamiliki eneo kihalali, nyinyi ni wavamizi na hamstahili kuwepo mahala hapo.

  Japo kwa kuwa mmekaa muda mrefu natumaini mpo wananchi wengi. Kama mpo wengi nadhani ninaweza kuwashauri njia ya kufanya.

  Pili je mmeendeleza hilo eneo? Kama ndio nawashauri kucheki status ya hao wanaodai wanamiliki (inawezekana milki yao kisheria ishaisha kwani miaka 30 ni mingi) iwapo itakuwa imeshaisha fanyeni mpango fasta wa nyie kupewa milki halali.
   
 15. Y2k

  Y2k Member

  #15
  Aug 17, 2016
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari za majukumu wana jamii foroum. Kuna issue moja inanisumbua nataka kufahamu kisheria imekaaje. Kuna eneo tumenunua mimi na wenzangu na pia yumeshaanza kujenga, aliyetuuzia ni mmiliki halali wa eneo ila kuna issue kwamba lile eneo lilipimwa na kuna plani ya shule ya sekondari ya private. Ila wanazengo wanasema yale mapimo sio halali kwani hawakuwashirikisha wanazengo wa lile eneo na Mwenyekiti wa kijiji nae pia hajashirikishwa na wanasema mapimo ya lile eneo sio halali ukienda ardhi wanakuonyesha plani kua ni eneo la shule na kunajamaa anakuja anasema ni lakwake na documents zake zinaonesha ni za kitapeli. So kisheria imekaaje hii ama kwa mnaofahamu sheria mnaweza kutusaidia apa.
   
 16. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2016
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mkuu naomba unisaidie ushauri katika situation hii;
  Wakati wa operesheni vijiji mtu alipewa eneo bila nyaraka zozote (early 1970's) na aliishi hapo, na hadi sasa wazee wote jirani wanaeleza hivyo. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 1980, mtu huyo alihama kwa hiari yake kwenda mbali, ila eneo hilo hakuliacha bila mtu, bali alimwachia mwanamke ambaye kwa mahusiano walikuwa ni mtu na shemeji yake kwa kuwa aliyeachiwa eneo ni dada wa mke wa mtu. Huyu mama aliendelea kulima na kuishi eneo hilo na kuilea familia yake mahali pale hadi pale utofauti kati ya watoto wake ulipojitokeza ambapo mkubwa anadai kuwa ardhi ile ni yake mwenyewe kwa kudai kupewa na serikali ya kijiji mwaka 1986....! Kwa bahati mbaya mtu aliyemwachia yule mama ardhi ile ameshafariki, na hakukuwa na makabidhiano ya kimaandishi, ila mke wake na watoto wake wote wamejitokeza na kudhibitisha kuwa ardhi ile walimwachia yule mama siku wanahama....!

  Sasa naomba niulize;
  1. Iwapo serikali ya kijiji ina mamlaka ya kupeana ardhi yenye mtu, tena bila ridhaa wala taarifa kwa mwenye ardhi husika.
  2. Iwapo ni halalali kwa mtu binafsi anapohama kwenda mbali na ardhi yake ana haki ya kumwachia mtu mwingine.
  3. Utofauti wa watoto wa mama huyu utasuluhishwa vipi?
  4. Je, kuna sheria iliyowahi kutungwa Tanzania inayomzuia mwanamke kumiliki ardhi?
  sijajua kama nimeeleweka, lakini nipo tayari kueleza zaidi nieleweke...
   
 17. joshydama

  joshydama JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2016
  Joined: May 10, 2016
  Messages: 2,612
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  1.Kijiji hakina mamlaka ya kutoa ardhi kwa mtu mwingine bila kufanya utafiti wajue hiyo ardhi ipo chini ya nani. Kwahiyo kama kuna ardhi imeachwa halafu kijiji kinataka kimpatie mtu mwingine lazima kitoe taarifa na hiyo taarifa isiwe chini ya siku thelathini.

  2.Unapokuwa umeenda mbali una haki ya kumuachia mtu mwingine hiyo ardhi kwa ajili ya kuiendeleza/ kuwa muangalizi wako anaweza kuwa ndugu n.k.

  3.Hakuna Sheria inayomnyima mwanamke kuwa na ardhi kuwa na ardhi Mkuu. Kama itakuwepo hivyo itakuwa inaenda kinyume na katiba ya Tanzania. Hivyo yafaa kuitwa ni batili.

  Pia tambua kuwa ardhi ipo chini ya raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo sisi ni kama wapangaji tu.
   
 18. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2016
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Asante sana mkuu...!
   
 19. k

  krdilunga Member

  #19
  Aug 3, 2017
  Joined: Jan 28, 2017
  Messages: 8
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 5
  Je mtu mwenye miliki ya ardhi ya kijiji ilio chini ya hatimiliki ya kimila anaweza kupokonywa kwa kosa la kutoiendeleza .... Kma jibu ni ndio ni ndan ya muda gani mtu yampasa aendeleze na kw baada ya muda gani atapokonywa asipoendeleza.....NAOMBA MSAADA WAKUU
   
 20. Msemaji_

  Msemaji_ JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2017
  Joined: Oct 22, 2016
  Messages: 347
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  mkuu hawawezi kupewa hati kwa kuwa eneo lina mgogoro
   
Loading...