Ijue Sheria Wiki Hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ijue Sheria Wiki Hii

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mkombozi, Jun 6, 2008.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  JAJI: Nakuhukumu kwa kukutwa na mitambo ya kutengenezea gongo.

  MTUHUMIWA: Lakini ni mitambo tu, siyo gongo mheshimiwa!

  JAJI: Hicho ni kithibiti tosha kabisa.

  MTUHUMIWA: Basi nihukumiwe kwa kosa la kubaka.

  JAJI: Kumbe ulibaka pia?

  MTUHUMIWA: Hapana, ila hapa ninacho pia kifaa kinachotumika wakati wa kubaka

  (Akimaanisha uume].

  JAJI: Basi upo huru.
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Serikali inabidi ikate rufaa kwa sababu Jaji amekosea hukumu.

  Kifaa kinachotumika kubaka kinaweza kutumika kutengeneza vitu halali, kama vile watoto, lakini mtambo unaotumika kutengeneza gongo ni kidhibiti hitimisho kwa sababu, zaidi ya kutengeneza gongo, hautumiki kutengeneza maziwa ya watoto!
   
 3. J

  Jobo JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuhani Mkuu usije ukawa unatumia dini kufikia hii conclusion! Gongo kwa baadhi ya makabila ni dawa ya kipindupindu na hata malaria, so it is justifiable isnt it?
   
 4. K

  Kizito Member

  #4
  Jun 28, 2008
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Jaji ana matatizo hata mashahidi hana? Kwa nini asingetafuta mashahidi kuhakikisha kama jamaa kweli anachokifaa cha kubaka?
   
 5. Mswahilina

  Mswahilina Senior Member

  #5
  Jun 28, 2008
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule Mzee Mangi Lyatonga Mrema alipokuwa anagombea URAHISI mwaka 1995, alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara hapa Shinyanga alisema kuwa akiwa RAHISI ataagiza mitambo ya kuchuja gongo ili inywewe kama Konyagi.
  Kuhani, unasemaje hapo.
   
 6. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Alikuwa anawadanganya baadhi ya Wananchi wasio na uelewa sana. Plan yake ilikuwa ni kulitia maji Tembo halafu akaliuza bila kusema hili sio Tembo tena.

  Gongo ni marufuku kwa sababu ni kemikali hatari ambayo haina vipimo. Ina michangonyiko ya aina za vilevi ethanol na methanol ambavyo vinaweza kukuua.

  Mrema aliposema atachuja Gongo, ana maana kupunguza kiasi cha ethanol na kuchuja byproducts nyingine za alcohol fermantation, hususan methanol - ambayo ukinywa ovyo ovyo unapofuka macho.

  Sasa ukisha punguza ethanol, na kuondoa hayo ma byproducts makali makali mengine, hiyo sio gongo tena.

  Kwa hiyo sio kweli kwamba angewasaidia Wananchi kuhalalisha gongo.
   
 7. paulsifa

  paulsifa Member

  #7
  Jun 29, 2008
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  well,sheria ni sheria tu hatuangalii kama makabila fulani wanaitumia kama dawa ya kipindupindu au la..kama ndo hivyo basi na bangi iwe justifiable to some people wanaoitumia kama dawa au kama "holly sacrament" according to some rastafarins........
   
 8. paulsifa

  paulsifa Member

  #8
  Jun 29, 2008
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  lakini najua kwa nchinyingine kama uturuki wana kinywaji ambacho basically ni kama gongo ambacho kwa sasa kinapromote sdana nchi yao.wanasema hujafika uturuki kama hujaonja "raki".kwa hiyo ni swala la kuwawezesha watengenezaji locals kuweza kutengeneza gongo amabayo itakuwa salama kwa matumizi...
   
 9. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Labda hufahamu components za mtambo wa kutengenezea gongo, ngoja nikupe kidogo kama sijasahau- huwa kunakuwa na at least debe au pipa mbili(inategemea na scale ya uzalishaji), pia kunakuwa na pipes na karai au sufuria kubwa. Ukiangalia hivyo vifaa vyote vina matumizi mengine na havikutengenezwa ili vitumike kwa kuzalisha gongo.
   
 10. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Assuming unachokumbuka ni sahihi, bado kuna tatizo hapa. Madebe, mapipa na mabomba vyote ni halali na vina matumizi chanya. Ila ukiifunga na kuinganisha kutengeneza mtambo, hicho kitu kipya hakina matumizi mengine yoyote, ila kutengeneza gongo. Ndio maana ukikutwa na mtambo basi umekwisha, isipokuwa labda uweze kuwashawishi na kuwaonyesha polisi jinsi unavyotumia mtambo huo huo wa madebe na ma pipe kumwagilia mchicha. Kitu ambacho umeshakubali hakifanywi na huo mtambo.

  By the way, Kana-Ka-Nsungu, huwezi kumwambia mtu "wewe hufahamu X, Y, Z..." halafu hapo hapo , katika kumsahisha, na wewe unakuja na habari za "kama sijasahau." Jana tulikuwa na mjadala kwenye thread ya "Zanzibar hakuna Ufisadi" mtu aka demand source ya idea ya mwenzake kwamba wanaoutaka Muungano ni wachache, akasema sio kweli. Cha kusikitisha, yeye akaja na arguments zake kwamba wasioutaka ndio wachache, lakini akasema " I bet." Huwezi kutumia guesswork kumwambia mtu 'you are wrong.' Acha tumrukie!
   
 11. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  Lakini bado naamini Kuhani, kuna tofauti kati ya kusahau na kutolijua jambo kabisa.
   
Loading...