Ijue sheria (ndoa batilifu)

chapangombe

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
362
286
Ndoa batilifu ni zile ndoa ambazo kwa mtazamo ni halali lakini uwezekano wa kuzifanya ziwe batili unakuwepo pale tu mmoja wa wanandoa anapoamua kudai iwe batili

Kwa maneno mengine wanandoa wakiamua kukaa kimya ndoa itabaki hai

SABABU ZA NDOA KUWA BATILIFU
1.kutotumia ndoa( kukosa uwezo wa tendo)
2.kukataa tendo kwa makusudi
3.magonjwa ya zinaa
4.mimba ya mtu mwingine
5.kukosekana idhini ya wazazi

VIZUIZI VYA KUBATILISHA NDOA
1. Muda maalumu sharti ndoa iwe na miaka miwili.
2. Kugundua kasoro Kama umeingia kwenye ndoa na unajua kasoro

MADAI YA TARAKA
Kuna aina mbili za utengano wa wanandoa

1.utengano wa ridhaa wanandoa wanaamua wenyewe hapa wanaweza kurudiana
2.utengano wa mahakama

SABABU ZA TARAKA
1.Uzinzi
2.Kutelekezana
3.ukatili

MAMLAKA NA UWEZO WA MAHAKAMA KATIKA TARAKA
1.Lazima mgogoro uanze kwenye Baraza la usuruhishi la dini au kata ndio baadaye lipelekwe mahakamani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom