Mjadala kuhusu Mke asiye wa Ndoa na Mtoto wa nje ya Ndoa kwenye urithi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
mtoto-analia.jpg

Kumekuwepo na utata mkubwa kuhusu urithi wa mali za marehemu hasa inapotokea kuwa marehemu alikuwa na mke zaidi ya mmoja na hapohapo watoto wanaotokana na mama tofauti. Tumeshashuhudia magomvi makubwa misibani lakini pia tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia utitiri wa mashauri kuhusu mkanganyiko wa mali za marehemu ambaye familia yake ni ya watoto wanatokana na mama tofauti.

Kutokana na hayo kuna umuhimu mkubwa wa kueleza sheria inasemaje kuhusu mazingira ya namna hiyo ili anayemua kuchukua hatua au kulalamika alalamikie kitu ambacho ni haki yake kweli na anayeamua kuacha aache akiwa ameridhika kuwa hajaonewa isipokuwa hicho alichopata ndiyo haki yake kisheria.

1. NINI MAANA YA MKE WA NJE YA NDOA?

Mke wa nje ya ndoa ni mke ambaye ameishi na mume kama mke na mume lakini akiwa hajafunga ndoa yoyote ya kiislamu, ya kanisani, ya serikali au ya kimila. Ndoa ya kiislamu hufungwa kwa taratibu za kiislamu ambazo huhusisha masheikh, makadhi n.k. Ndoa ya kikiristo hufungiwa kanisani na yaweza kufungishwa na mchungaji, askofu, padre n.k. Ndoa ya serikali hufungwa katika mamlaka za serikali kama kwa mkuu wa wilaya ubalozini n.k.

Na ndoa za kimila ni ndoa ambazo hufungwa kutokana na mila na desturi za jamii fulani kwa mfano ndoa za kihaya, ndoa za kichaga n.k. Kwa hiyo kama mwanamke hana ndoa yoyote katika hizi basi yeye ni mke wa nje ya ndoa.

2. NINI MAANA YA MTOTO WA NJE YA NDOA?

Mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto aliyetokana na ndoa isiyohalali au mahusiano yasiyo halali. Hapo juu nimetaja aina za ndoa halali. Hii ina maana kuwa iwapo mtoto amepatikana nje ya ndoa hizo basi huyo ndiye anayeitwa mtoto wa nje ya ndoa.

3. MKE ASIYE NA NDOA HARITHI

Kwa mujibu wa sheria zetu hapa Tanzania zikiwemo tafsiri mbalimbali za sheria hizo ambazo hutolewa na Mahakama Kuu pamoja na mahakama ya rufaa mke wa wa nje ya ndoa hutambulika kama kimada. Neno kimada sio tusi isipokuwa ni neno la kitaalam linalomwakilisha mwanamke anayeishi na mwanaume bila ndoa na ndio maana neno hilihili limetumiwa na mahakama katika hukumu zake mbalimbali.

Kutokana na hilo ieleweke wazi kuwa mwanamke asiye wa ndoa hata kama anaishi na mwanaume kwa mtindo ambao ukiungalia utadhani ni mke na mume bado ikitokea mwanaume huyo kufa mwanamke wa namna hiyo hawezi kudai chochote katika mali za yule mwanaume. Mke halali ni mke ambaye mahusiano yake na mwanaume yametokana na ndoa halali. Nje ya ndoa halali hakuna urithi.

Hii isimfanye mtu yeyote ajisikie vibaya isipokuwa kinachotakiwa ni kuhalalisha mahusiano ili ndoa halali ipatikane.

Aidha ieleweke kuwa wakati ambao sio wa kifo kwa mfano wakati wa kuachana baina ya mke na mume ambao wameishi kama wanandoa lakini wakiwa hawana ndoa mwanamke asiye wa ndoa ana haki ya kupata mgao wa mali. Na hii ni ikiwa wameishi wote kwa zaidi ya miaka miwili kama mke na mume na ikiwa kuna mali waliyochuma kwa pamoja .

Kwa maana hiyo kwa mazingira ya kuachana ya kawaida mwanamke asiye na ndoa anaweza kudai mali lakini baada ya kifo hawezi kudai mali.

4. MTOTO WA NJE YA NDOA HARITHI

Hapo juu nimetaja aina za ndoa ambazo hutambuliwa na sheria zetu hapa nchini. Nikasema kwamba watoto waliotoka nje ya ndoa hizo ndio watoto wa nje ya ndoa. Ni watoto haohao ambao hawaruhusiwi kurithi. Katika kutafsiri sheria hii mahakama nyingine zimekwenda mbali kwa kusema kuwa mtoto wa nje ya ndoa haingii katika tafsiri ya neno mtoto lililo katika sheria ya ndoa.

5. KUMHALALISHA MTOTO WA NJE YA NDOA

Sheria inasema kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa anaweza kuhalalishwa kwa kufuata taratibu za mila na desturi za jamii husika na hatimaye kuwa mtoto halali ambaye anaweza hata kurithi. Kwa mfano hapa kwetu kila kabila wanazo taratibu zao katika kulitekeleza hili. Kwa kutumia taratibu hizo mtu anaweza kumhalalisha mtoto wa nje ya ndoa na hatimaye akawa na hadhi ya kurithi.

6. MTOTO WA NJE YA NDOA KURITHI IWAPO KUNA WOSIA

Maelezo niliyotoa hapo juu kuhusu mtoto wa nje ya ndoa kutokurithi yanahusu pale tu marehemu anapokuwa hajaacha wosia. Kawaida marehemu anapokuwa hajaacha wosia familia ya marehemu au ndugu ndio hushughulika na kugawana mali za marehemu na ndipo hapo mtoto wa nje ya ndoa hatakuwa na nafasi ya kurithi. Lakini iwapo kuna wosia na marehemu amemtaja mtoto wa nje ya ndoa kama mrithi basi atapewa hiyo mali aliyoamrishwa aipate katika wosia.

Hii ndio sababu kubwa ya kuhimiza watu kuandika wosia ili kuondoa utata wa vitu kama hivi.

7. USHAURI WA NAMNA YA KUMSAIDIA MTOTO WAKO KAMA NI WA NJE YA NDOA

Kama unataka mtoto wako uliyempata nje ya ndoa asipate taabu baada ya kufa kwako basi andika wosia naye umpe chake. Nje ya wosia mtoto wako hatopata kitu na wewe waweza kuwa sababu ya kumfanya mwanao kuwa mtoto wa mitaani( chokoraa) kwa kukosa msingi wa kipato. Nimesema hapo juu kuwa sheria haina shida kama mtoto wa nje ya ndoa amepewa mgao katika wosia.

Lakini nje ya wosia sheria inamzuia kupata mali.
 
Mkuu dubu nashukuru kwa hii elimu hapa umenifungua macho.

Nina jambo naomba uniweke sawa sababu mimi siyo mtaalam wa sheria. Swali langu ni kwamba ikiwa ninaishi na binti na nimebahatika kupata nae mtoto ila ikatokea mikwaruzano na kutoelewana nami nikiamua kuachana nae hapa sheria inasemaje?

Kwani nimesikia kuna sheria mpya ikiwa umekaa na binti kwa zaidi ya miezi sita na ukamwacha anaweza kukufungulia mashtaka na kudai fidia juu.

Hebu mkuu dubu tuweke sawa na hii sheria kama kweli ipo.
 
Waisilamu tuna raha, masuala kama haya yaliyoletwa hapa yote yamo katika kitabu chetu kitakatifu, Quran.

Kwa hiyo penye suala la kufa mtu na kama pana masuala ya kurithi basi watu huwa hawagombani kwa vile kila kitu huwa tayari kinaeleweka ingawa bado hutokezea wale wenye tamaa za binafsi na kuzusha fujo.

Ila tu kwenye Uisilamu hawara huwa hana urithi pamoja na mtoto wa nje ya ndoa.

Hayo mengine siwezi kuyaingilia kutokana yameletwa kutokana na dini ya Kikristo au sheria za mahakama kwa hiyo sina haja ya kuzozana.
 
mtoto-analia.jpg

Kumekuwepo na utata mkubwa kuhusu urithi wa mali za marehemu hasa inapotokea kuwa marehemu alikuwa na mke zaidi ya mmoja na hapohapo watoto wanaotokana na mama tofauti. Tumeshashuhudia magomvi makubwa misibani lakini pia tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia utitiri wa mashauri kuhusu mkanganyiko wa mali za marehemu ambaye familia yake ni ya watoto wanatokana na mama tofauti.

Kutokana na hayo kuna umuhimu mkubwa wa kueleza sheria inasemaje kuhusu mazingira ya namna hiyo ili anayemua kuchukua hatua au kulalamika alalamikie kitu ambacho ni haki yake kweli na anayeamua kuacha aache akiwa ameridhika kuwa hajaonewa isipokuwa hicho alichopata ndiyo haki yake kisheria.

1.NINI MAANA YA MKE WA NJE YA NDOA.

Mke wa nje ya ndoa ni mke ambaye ameishi na mume kama mke na mume lakini akiwa hajafunga ndoa yoyote ya kiislamu, ya kanisani, ya serikali au ya kimila. Ndoa ya kiislamu hufungwa kwa taratibu za kiislamu ambazo huhusisha masheikh, makadhi n.k. Ndoa ya kikiristo hufungiwa kanisani na yaweza kufungishwa na mchungaji, askofu, padre n.k. Ndoa ya serikali hufungwa katika mamlaka za serikali kama kwa mkuu wa wilaya ubalozini n.k.

Na ndoa za kimila ni ndoa ambazo hufungwa kutokana na mila na desturi za jamii fulani kwa mfano ndoa za kihaya, ndoa za kichaga n.k. Kwa hiyo kama mwanamke hana ndoa yoyote katika hizi basi yeye ni mke wa nje ya ndoa.

2. NINI MAANA YA MTOTO WA NJE YA NDOA.

Mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto aliyetokana na ndoa isiyohalali au mahusiano yasiyo halali. Hapo juu nimetaja aina za ndoa halali. Hii ina maana kuwa iwapo mtoto amepatikana nje ya ndoa hizo basi huyo ndiye anayeitwa mtoto wa nje ya ndoa.

3. MKE ASIYE NA NDOA HARITHI.

Kwa mujibu wa sheria zetu hapa Tanzania zikiwemo tafsiri mbalimbali za sheria hizo ambazo hutolewa na mahakama kuu pamoja na mahakama ya rufaa mke wa wa nje ya ndoa hutambulika kama kimada. Neno kimada sio tusi isipokuwa ni neno la kitaalam linalomwakilisha mwanamke anayeishi na mwanaume bila ndoa na ndio maana neno hilihili limetumiwa na mahakama katika hukumu zake mbalimbali.

Kutokana na hilo ieleweke wazi kuwa mwanamke asiye wa ndoa hata kama anaishi na mwanaume kwa mtindo ambao ukiungalia utadhani ni mke na mume bado ikitokea mwanaume huyo kufa mwanamke wa namna hiyo hawezi kudai chochote katika mali za yule mwanaume. Mke halali ni mke ambaye mahusiano yake na mwanaume yametokana na ndoa halali. Nje ya ndoa halali hakuna urithi.

Hii isimfanye mtu yeyote ajisikie vibaya isipokuwa kinachotakiwa ni kuhalalisha mahusiano ili ndoa halali ipatikane.

Aidha ieleweke kuwa wakati ambao sio wa kifo kwa mfano wakati wa kuachana baina ya mke na mume ambao wameishi kama wanandoa lakini wakiwa hawana ndoa mwanamke asiye wa ndoa ana haki ya kupata mgao wa mali. Na hii ni ikiwa wameishi wote kwa zaidi ya miaka miwili kama mke na mume na ikiwa kuna mali waliyochuma kwa pamoja .

Kwa maana hiyo kwa mazingira ya kuachana ya kawaida mwanamke asiye na ndoa anaweza kudai mali lakini baada ya kifo hawezi kudai mali.

4. MTOTO WA NJE YA NDOA HARITHI.

Hapo juu nimetaja aina za ndoa ambazo hutambuliwa na sheria zetu hapa nchini. Nikasema kwamba watoto waliotoka nje ya ndoa hizo ndio watoto wa nje ya ndoa. Ni watoto haohao ambao hawaruhusiwi kurithi. Katika kutafsiri sheria hii mahakama nyingine zimekwenda mbali kwa kusema kuwa mtoto wa nje ya ndoa haingii katika tafsiri ya neno mtoto lililo katika sheria ya ndoa.

5. KUMHALALISHA MTOTO WA NJE YA NDOA.

Sheria inasema kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa anaweza kuhalalishwa kwa kufuata taratibu za mila na desturi za jamii husika na hatimaye kuwa mtoto halali ambaye anaweza hata kurithi. Kwa mfano hapa kwetu kila kabila wanazo taratibu zao katika kulitekeleza hili. Kwa kutumia taratibu hizo mtu anaweza kumhalalisha mtoto wa nje ya ndoa na hatimaye akawa na hadhi ya kurithi .

6. MTOTO WA NJE YA NDOA KURITHI IWAPO KUNA WOSIA.

Maelezo niliyotoa hapo juu kuhusu mtoto wa nje ya ndoa kutokurithi yanahusu pale tu marehemu anapokuwa hajaacha wosia. Kawaida marehemu anapokuwa hajaacha wosia familia ya marehemu au ndugu ndio hushughulika na kugawana mali za marehemu na ndipo hapo mtoto wa nje ya ndoa hatakuwa na nafasi ya kurithi. Lakini iwapo kuna wosia na marehemu amemtaja mtoto wa nje ya ndoa kama mrithi basi atapewa hiyo mali aliyoamrishwa aipate katika wosia .

Hii ndio sababu kubwa ya kuhimiza watu kuandika wosia ili kuondoa utata wa vitu kama hivi.

7.USHAURI WA NAMNA YA KUMSAIDIA MTOTO WAKO KAMA NI WA NJE YA NDOA .

Kama unataka mtoto wako uliyempata nje ya ndoa asipate taabu baada ya kufa kwako basi andika wosia naye umpe chake. Nje ya wosia mtoto wako hatopata kitu na wewe waweza kuwa sababu ya kumfanya mwanao kuwa mtoto wa mitaani( chokoraa) kwa kukosa msingi wa kipato. Nimesema hapo juu kuwa sheria haina shida kama mtoto wa nje ya ndoa amepewa mgao katika wosia.

Lakini nje ya wosia sheria inamzuia kupata mali.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com
Mbona unaandika masuala ya kisheria kama hekaya za abunuwasi? Sijaona authority yeyote hapo, iwe case law ama statute!
 
Waisilamu tuna raha, masuala kama haya yaliyoletwa hapa yote yamo katika kitabu chetu kitakatifu, Quran.

Kwa hiyo penye suala la kufa mtu na kama pana masuala ya kurithi basi watu huwa hawagombani kwa vile kila kitu huwa tayari kinaeleweka ingawa bado hutokezea wale wenye tamaa za binafsi na kuzusha fujo.

Ila tu kwenye Uisilamu hawara huwa hana urithi pamoja na mtoto wa nje ya ndoa.

Hayo mengine siwezi kuyaingilia kutokana yameletwa kutokana na dini ya Kikristo au sheria za mahakama kwa hiyo sina haja ya kuzozana.

Naona sheria yenu haipishani na sheria ya kibabiloni, safi sana, kwa hilo hakuna haja ya mahakama ya kadhi.
 
mtoto-analia.jpg

Kumekuwepo na utata mkubwa kuhusu urithi wa mali za marehemu hasa inapotokea kuwa marehemu alikuwa na mke zaidi ya mmoja na hapohapo watoto wanaotokana na mama tofauti. Tumeshashuhudia magomvi makubwa misibani lakini pia tumeshuhudia na tunaendelea kushuhudia utitiri wa mashauri kuhusu mkanganyiko wa mali za marehemu ambaye familia yake ni ya watoto wanatokana na mama tofauti.

Kutokana na hayo kuna umuhimu mkubwa wa kueleza sheria inasemaje kuhusu mazingira ya namna hiyo ili anayemua kuchukua hatua au kulalamika alalamikie kitu ambacho ni haki yake kweli na anayeamua kuacha aache akiwa ameridhika kuwa hajaonewa isipokuwa hicho alichopata ndiyo haki yake kisheria.

1.NINI MAANA YA MKE WA NJE YA NDOA.

Mke wa nje ya ndoa ni mke ambaye ameishi na mume kama mke na mume lakini akiwa hajafunga ndoa yoyote ya kiislamu, ya kanisani, ya serikali au ya kimila. Ndoa ya kiislamu hufungwa kwa taratibu za kiislamu ambazo huhusisha masheikh, makadhi n.k. Ndoa ya kikiristo hufungiwa kanisani na yaweza kufungishwa na mchungaji, askofu, padre n.k. Ndoa ya serikali hufungwa katika mamlaka za serikali kama kwa mkuu wa wilaya ubalozini n.k.

Na ndoa za kimila ni ndoa ambazo hufungwa kutokana na mila na desturi za jamii fulani kwa mfano ndoa za kihaya, ndoa za kichaga n.k. Kwa hiyo kama mwanamke hana ndoa yoyote katika hizi basi yeye ni mke wa nje ya ndoa.

2. NINI MAANA YA MTOTO WA NJE YA NDOA.

Mtoto wa nje ya ndoa ni mtoto aliyetokana na ndoa isiyohalali au mahusiano yasiyo halali. Hapo juu nimetaja aina za ndoa halali. Hii ina maana kuwa iwapo mtoto amepatikana nje ya ndoa hizo basi huyo ndiye anayeitwa mtoto wa nje ya ndoa.

3. MKE ASIYE NA NDOA HARITHI.

Kwa mujibu wa sheria zetu hapa Tanzania zikiwemo tafsiri mbalimbali za sheria hizo ambazo hutolewa na mahakama kuu pamoja na mahakama ya rufaa mke wa wa nje ya ndoa hutambulika kama kimada. Neno kimada sio tusi isipokuwa ni neno la kitaalam linalomwakilisha mwanamke anayeishi na mwanaume bila ndoa na ndio maana neno hilihili limetumiwa na mahakama katika hukumu zake mbalimbali.

Kutokana na hilo ieleweke wazi kuwa mwanamke asiye wa ndoa hata kama anaishi na mwanaume kwa mtindo ambao ukiungalia utadhani ni mke na mume bado ikitokea mwanaume huyo kufa mwanamke wa namna hiyo hawezi kudai chochote katika mali za yule mwanaume. Mke halali ni mke ambaye mahusiano yake na mwanaume yametokana na ndoa halali. Nje ya ndoa halali hakuna urithi.

Hii isimfanye mtu yeyote ajisikie vibaya isipokuwa kinachotakiwa ni kuhalalisha mahusiano ili ndoa halali ipatikane.

Aidha ieleweke kuwa wakati ambao sio wa kifo kwa mfano wakati wa kuachana baina ya mke na mume ambao wameishi kama wanandoa lakini wakiwa hawana ndoa mwanamke asiye wa ndoa ana haki ya kupata mgao wa mali. Na hii ni ikiwa wameishi wote kwa zaidi ya miaka miwili kama mke na mume na ikiwa kuna mali waliyochuma kwa pamoja .

Kwa maana hiyo kwa mazingira ya kuachana ya kawaida mwanamke asiye na ndoa anaweza kudai mali lakini baada ya kifo hawezi kudai mali.

4. MTOTO WA NJE YA NDOA HARITHI.

Hapo juu nimetaja aina za ndoa ambazo hutambuliwa na sheria zetu hapa nchini. Nikasema kwamba watoto waliotoka nje ya ndoa hizo ndio watoto wa nje ya ndoa. Ni watoto haohao ambao hawaruhusiwi kurithi. Katika kutafsiri sheria hii mahakama nyingine zimekwenda mbali kwa kusema kuwa mtoto wa nje ya ndoa haingii katika tafsiri ya neno mtoto lililo katika sheria ya ndoa.

5. KUMHALALISHA MTOTO WA NJE YA NDOA.

Sheria inasema kwamba mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa anaweza kuhalalishwa kwa kufuata taratibu za mila na desturi za jamii husika na hatimaye kuwa mtoto halali ambaye anaweza hata kurithi. Kwa mfano hapa kwetu kila kabila wanazo taratibu zao katika kulitekeleza hili. Kwa kutumia taratibu hizo mtu anaweza kumhalalisha mtoto wa nje ya ndoa na hatimaye akawa na hadhi ya kurithi .

6. MTOTO WA NJE YA NDOA KURITHI IWAPO KUNA WOSIA.

Maelezo niliyotoa hapo juu kuhusu mtoto wa nje ya ndoa kutokurithi yanahusu pale tu marehemu anapokuwa hajaacha wosia. Kawaida marehemu anapokuwa hajaacha wosia familia ya marehemu au ndugu ndio hushughulika na kugawana mali za marehemu na ndipo hapo mtoto wa nje ya ndoa hatakuwa na nafasi ya kurithi. Lakini iwapo kuna wosia na marehemu amemtaja mtoto wa nje ya ndoa kama mrithi basi atapewa hiyo mali aliyoamrishwa aipate katika wosia .

Hii ndio sababu kubwa ya kuhimiza watu kuandika wosia ili kuondoa utata wa vitu kama hivi.

7.USHAURI WA NAMNA YA KUMSAIDIA MTOTO WAKO KAMA NI WA NJE YA NDOA .

Kama unataka mtoto wako uliyempata nje ya ndoa asipate taabu baada ya kufa kwako basi andika wosia naye umpe chake. Nje ya wosia mtoto wako hatopata kitu na wewe waweza kuwa sababu ya kumfanya mwanao kuwa mtoto wa mitaani( chokoraa) kwa kukosa msingi wa kipato. Nimesema hapo juu kuwa sheria haina shida kama mtoto wa nje ya ndoa amepewa mgao katika wosia.

Lakini nje ya wosia sheria inamzuia kupata mali.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241
bashiryakub@ymail.com

What about the presumption of marriage under s.160(1)of the Law of Marriage Act??
 
Tunashukuru kwa elimu ako nzuri ila nakushauri ukasome vizuri LAW OF THE CHILD ACT,2009 utajua sheria inasemaje kuhusu hao watoto waliozaliwa nje ya ndoa (outwedlock children).

asante...you just read my mind, sheria ya mtoto imeleta mabadiliko hapo...tena makubwa tu.
 
mke asiye kwenye ndoa iwapo mwaume akifariki mke huyo anaweza kupata sehemu ya jasho lake kama atapata wakili mzuri na akatengeneza vizuri cause of action.
 
Kinachomfanya mwanamke kuitwa mke au mwanaume kuitwa mume si ni ndoa ? Mke nje ya ndoa ndio maana yake nini ?
 
Kuna kitu kinaitwa will hiyo ni document muhimu sana kwa mwenye family kuiandika kabla hajakufa, wenzetu wazungu wao wanafanya sana hivyo kwa kuweka mazingara sawa kabla mtu hajakufa, maandiko ka haya ndio solution ya migogoro mingi ndani ya families nyingi. Mr Murage:usa2:
 
Mtoto wa nje ya ndoa sheria inamtambua kama mrithi wa mali ya baba yake endapo baba atamtambulisha kwa mke mkubwa na atatoa faini ya mtoto huyo na kukabidhiwa mtoto huyo na kuishi nae nyumbani.

Hivyo katika mgawo wa mali lazima atapewa sehemu ya mali ya baba yake kama mtoto halali.
 
Mtoto wa nje ya ndoa sheria inamtambua kama mrithi wa mali ya baba yake endapo baba atamtambulisha kwa mke mkubwa na atatoa faini ya mtoto huyo na kukabidhiwa mtoto huyo na kuishi nae nyumbani.Hivyo katika mgawo wa mali lazima atapewa sehemu ya mali ya baba yake kama mtoto halali.
Tuambie sheria ulioitumia na kifungu gani ? Je ! ni sheria ya mtoto? Je! ni affiliation act? je! ni declaration of local customary law? je ! ni sheria ya ndoa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom