Ijue sayansi ya upara na uwezekano mkubwa wa kuutibu kwake

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,161
15,839
Habari yako ndugu msomaji.

Ama baada ya salamu na kumshukuru mungu naomba nianze kwa kusema kwamba MIMI NAAMINI MATATIZO YA KURITHI YANATIBIKA(hii ni imani yangu)

Baada ya kusema hivi naomba niingie kwenye mada yangu ya upara ama kupoteza nywele kichwani hasa ule wa kurithi wataalamu wanauita androgenic alopecia.

Utajua kwamba una upara wa kurithi kwa kuangalia wazazi wako baba ama babu ukiona wanao na wewe unao basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuwa na upara wa urithi(androgenic alopecia)

Nitabase sana katika aina hii ya upara kwa sababu ndio unaowakumba watu wengi zaidi hapa duniani.

Nini sababu ya upara huu ?

Kuna kitu kinaitwa TESTOSTERONE HORMONE hii ni hormoni ambayo inapatikana katika mwili kwa wanaume inafanya kazi mbalimbali za kumkuza na kumfanya awe na umbile na sifa za kiume pia.

homoni hii kwa wanaume huwa inazalishwa kwa wingi kuliko wanawake,homoni hii inaweza kubadilishwa na mpuuzi mmoja hivi anayeitwa 5-Alpha reductase enzyme(5-ARD).

Huyu bwana 5-ARD enzyme anauwezo wa kuibadilisha testosteron na kuwa dihydrotestosteron.

Homoni huwa zinasafirishwa kwa njia ya damu kutoka sehemu inapozalishwa mpaka sehemu inayohitajika katika mwili,hivyo damu ndio daladala ya kuzipakia hizo hormone,na njia inayopita damu ndio hiyo mishipa ya damu.

Sasa bwana hii hormone iliyobadilishwa na 5-ARD enzyme yaani dihydrotestosterone(DHT) katika kusafiri kwake ikiwa ndani ya damu hufika mpaka kwenye mzizi wa nywele na hukaa pale.

Baada ya mchakato huo ile homoni ya DHT inaziba ule mzizi wa nywele na kufanya nywele isiweze kwenda juu na kutokea kichwani ikaota vizuri ikaonekana.

Mambo ya kujua ni kwamba,tatizo sio teatosteron bali tatizo ni hii teatosteron ikibadilishwa na kuwa DHT na ikawa nyingi katika mwili inaleta madhara kama tuliyosema hapo juu

Kwa mantiki hiyo mtu akiwa na kiwango cha testosteron nyingi ambayo inabadilishwa na kuwa DHT hapo shida ndipo inapoanzia.

Sasa jee madai ya kwamba upara ni kwa sababu damu haifiki kwenye nywele ni ya ukweli ?

Madai haya naona sio kweli kwa mujibu wa maneno hapo juu kwa sababu tatizo sio ddamu kwamba haifiki kwenye nywele hapana,damu inafika ila tatizo ni kuwa hiyo damu ndiyo inaleta yule jamaa DHT ambaye ndio mbaya kwa nywele zetu.

Hivyo unaweza kumuambia mtu afanye massage ya kupeleka damu kwenye nywele ili aondoe kipara kumbe ndio unamuongezea tatizo

kwa sababu kadri hiyo damu itakavyokuwa inaenda nyingi kwenye nywele na ndivyo damu hiyo inazidi kupeleka maadui wa nywele akina DHT kwa sababu damu ndio msafirishaji.

NINI SULUHISHO ?

Suluhisho kwanza tuweze kupata tiba itakayopunguza kubadilisha testosteron isiwe dihydrotestosteron.

Lakini pia tupate tiba itakayowezesha kuzuia hawa enzymes watoke wasikae katika nywele zetu na nywele zetu zitakuja juu vizuri.

Je kuna anayefahamu tiba hizo hata kama za asili tuanze kuondoa shida ya upara katika jamii ?

Pia mtu mwenye upara inasemekana kwamba anakuwa na kiwango kiukubwa cha teatosterone ambayo hubadilishwa na kuwa DHt.

Na ninahisi hii ni katika sababu ya kusema kwamba wanaume wwnye vipara wanakuwa na akili wengi kwa sababu wanakuwa na hormone za testosteron nyingi na homoni hizi zinaboresha fikra ya mtu na kumfanya awe na uwezo mzuri wa kufikiri.

Kutokana na hayo

Kuna baadhi ya products zinadai kwamba zinablock hawa enzymes na kufanya nywele iote lakini kuna baafhi ya feefback kutoka youtube comment zinasema ni ututapeli haziponeshi wengine wakidai zinaponya.

Nimejaribu kuelezea kwa lugha ambayo itakuwa rahisi kwwngu pengine na kwenu,wataalamu watakuja kukosoa na kurekebisha kwa sababu naamini yapo mapungufu mengi katika uzi wangu huu.

Je ndugu mwana JF una mchango wowote katika mada hii ?
 
Back
Top Bottom