Ijue sababu Kuu ya kwanini Injinia Hersi Said aliambatana na Haji Manara kwenda kumuomba Radhi Rais wa TFF Karia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,468
108,621
Kwa mlundikano wa Makosa ya Mhamasishaji wa Yanga SC na Jeuri zake pamoja na Dharau anazowafanyia Watendaji wa TFF Injinia Hersi Said na hata Watu wa Yanga SC wenye Akili wanajua kuwa kwa Haji Manara kuingia Kwake Mwenyewe katika 18 za TFF na Sekretarieti yake safari hii haponi na anaenda Kufungiwa.

Kwakuwa tayari Injinia Hersi Said ndiyo anaenda kuwa Rais mpya wa Yanga SC (japo Uchaguzi Mkuu wao bado) ila kwa Ukaribu mkubwa wa Haji Manara na Injinia Hersi Said ni kwamba tayari kuna Kitengo Kipya cha Habari na Mawasiliano kimeandaliwa na aliyeandaliwa kuwa hapo kama Mkuu wake ni Haji Manara.

Injinia Hersi Said anajua kuwa endapo Rafiki yake Mkubwa Haji Manara atafungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF itampa wakati mgumu wa Kumtafuta Mtu wa kufanya nae Kazi kwani siyo Siri Msemaji wa Yanga SC Hassan Bumbuli hatakiwi na Injinia Hersi Said japo wakikutana Wawili hawa huonyesha wana Mahusiano mema ila wanaojua wanasema ni Paka na Panya ndani ya Yanga SC.

Na endapo Haji Manara hatofungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF tutaamini Tetesi zilizopo kuwa hata ile Juzi Injinia Hersi Said alipoambatana na Mhamasishaji wa Yanga SC Haji Manara kuna Ahadi ya Fedha (kutoka GSM) iliahidiwa Kwake Rais wa TFF Wallace Karia na Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya TFF kama wasipomuadhibu Haji Manara ambaye Injinia Hersi Said anamhitaji sana katika Sekretarieti yake mpya ya Uongozi ndani ya Yanga SC mara baada ya Kuchaguliwa rasmi kuwa Rais Jumamosi ya Wiki hii.

Hassan Bumbuli anza Kutafuta Ajira ( Kazi ) Kwingineko au rejea pale ulikokuwa kwa muda mrefu kama Mwandamizi MWANANCHI Tabata, ila Injinia Hersi Said akiwa Rais wa Yanga SC rasmi Jumamosi hii ijayo basi jua hutohitajika tena Klabuni.
 
Hili suala la Manara sijui kwa nini linakuzwa sana. Yeye ni mwanafamilia wa mpira kama wanafamilia wengine wa mpira. Kwa hiyo kama ana makosa aadhibiwe kama wengine walivyoadhibiwa huko siku za nyuma. Kama hana makosa aachwe aendelee na shughuli zake kama kawaida.

Kuomba msamaha ni sehemu tu ya ubinadamu baada ya kugundua kuwa umtenda kosa na hili lazima Manara apongezwe kwani ni watu wachache sana huwa wanakubali kujishusha na kuomba msamaha wanapotenda makosa. Lakini kuomba msamaha hakufuti taratibu nyingine zote zinazotakiwa kufuatwa ikiwemo na adhabu anayostahili iwapo atakutwa na hatia.
 
nadhan hata kocha wa mbeya kwanza alifungiwa miaka 5 na aliomba msamaha the some to shaffi dauda endapo manara atafungiwa basi nitaamini TFF nichombo imara cha kusimamia mpira Tz ila akisamehewa nitajua TFF na GSM ni tako na chupi na ndani yake kutakua kumejaa harufu za rushwa
 
Maandiko yanasema mke atamuacha babaye ataambatana na mumewe
Kama hivi?
JamiiForums-1748518016.jpg
 
nadhan hata kocha wa mbeya kwanza alifungiwa miaka 5 na aliomba msamaha the some to shaffi dauda endapo manara atafungiwa basi nitaamini TFF nichombo imara cha kusimamia mpira Tz ila akisamehewa nitajua TFF na GSM ni tako na chupi na ndani yake kutakua kumejaa harufu za rushwa
Huenda akapunguziwa adhabu
 
Kwanini unatumia caps katikati ya sentensi? Nashauri jifunze uandishi
 
Makolo msimu huu walianza na Yanga kama kawaida yao uwa wanaongoza round ya kwanza tu ikifika round ya pili tunarudi kwenye nafasi yetu

2-Oooh!GSM ananunua match

3-Haiwezekani GSM awe mdhamini wa ligi sababu ya fair competition(juzi hapa wakaumbuka kwenye fa maana Yanga na coastal wote wanadhaminiwa na GSM lakini mpira waliocheza kila mtu aliona)

4-mayele wa kawaida sana tu(ingawa usiku na mchana walikua wanapambana hadi kichawi ili asiwe mfungaji bora,hili walifanikiwa

5-wakaja kwa abdul sopu

6- sasa hivi wapo kwa karia huku kwa mbali wakiwa na fukuto ndani ya uongozi wao kuna baadhi hawamtaki dada ceo
 
Hili suala la Manara sijui kwa nini linakuzwa sana. Yeye ni mwanafamilia wa mpira kama wanafamilia wengine wa mpira. Kwa hiyo kama ana makosa aadhibiwe kama wengine walivyoadhibiwa huko siku za nyuma. Kama hana makosa aachwe aendelee na shughuli zake kama kawaida.

Kuomba msamaha ni sehemu tu ya ubinadamu baada ya kugundua kuwa umtenda kosa na hili lazima Manara apongezwe kwani ni watu wachache sana huwa wanakubali kujishusha na kuomba msamaha wanapotenda makosa. Lakini kuomba msamaha hakufuti taratibu nyingine zote zinazotakiwa kufuatwa ikiwemo na adhabu anayostahili iwapo atakutwa na hatia.
Nakubaliana na hoja yako. Ni Tanzania pekee kosa dogo linaweza kuadhibiwa Kwa adhabu ya kifo kama alivyofanyiwa Kocha wa Mbeya Kwanza. Mtu anatetea Usalama wa Wachezaji hata kama oalichokifanya sikishabikii Kwa sababu ya mazingira ya nchi yetu, lakini kumfungia miaka 5 Mtu ambaye kazi aliyosomea ni hiyo ya kufundisha soka ni Sawa na kumnyonga.
Shafii ni mwandishi wa michezo na Ndiko alikokuwa anapatia ridhiki yake na soka inachangamka Kwa maandiko yake, lakini kakosana na Wenye mpira kahukumiwa kunyongwa.
Kuna mwaka mwandishi mmoja toka mkoa wa Rukwa, kama sikosei ni Sammy Kisika aliwahi kuripoti Taarifa isiyo sahihi kwamba Mwewe kabeba Ng'ombe na kiruka naye hewani kisha baada ya kumla huko huko juu kadondosha mifupa. Kama ingekuwa ni TFF Kisika angehamishwa nchi na kuitwa raia wa Burundi na tusingemsikia tena maana hata vyeti vyake wangebeba. Lakini aliadhibiwa Kwa kosa lile Kwa adhabu iliyomfanya ajute kutoa Taarifa zisizotafitiwa na baada ya kuomba radhi na kuikanusha habari hiyo, mpaka Leo Samy ni mwandishi anayetegemewa kuripoti toka Rukwa.
Nchi hii wengi tuna hulka mbovu za kutaka Kila anayekosea apewe adhabu kuuuubwa huku yakitutokea Sisi maumivu yanakuwa mazito. Haishangazi kuona Wabunge wanapitisha sheria Kali baada ya utekelezaji wanashangaa zilipitishwa na Nani!!
Manara kukwaluzana na Karia ni kosa la kawaida Sana, lakini naona Kila anayeinuka toka mahali Fulani anataka Manara afungiwe maisha, afungwe jela maisha, anyongwe bila kujali mchango wake Kwa soka la nchi hii.
Nimekuwa mtetezi wake Tangu akiwa Msemaji wa Simba japokuwa Nilikuwa natofautiana naye kwenye style yake ya uwasilishaji mada, malalamiko, au hoja. Tatizo la Manara ni mihemko na kujiona Yuko sahihi Kila mahali. Anapenda kuchukulia masuala ya kazini kwake kama masuala yake binafsi na ndo maana anashambuliana na watu binafsi Kila mara badala ya Taasisi. Suala lake na Karia ni la kikazi lakini ni too personal ndo maana wameombana radhi wawili wakiwa na shahidi Kati yao (Mathayo 18:15-16).
Ndani ya soka kuna Mambo mengi, kuna matusi, kuna Faraja, kuna hasira, kufoka, kutiana moyo, kukatiahana tamaa NK. Lakini kuna watu wanaofanya soka uwe mchezo Wenye radha ndani na nje ya uwanja. Leo tungewafungia maisha Wachezaji wanaotukana Waamuzi au viongozi wao Jonas Mkude angekuwa Segerea, Juma Nyoso angekuwa Butimba, Barbara angeshafutiwa ruhusa ya kufanya kazi Tanzania.
Tuchukuliane, Soka ina Mambo mengi.
 
manara kaanza kubeba mikoba ya makonda zile tabia.nilipogundua ile siku anapiga simu uwanjani .

kweli maskininhakipata matako ni mbwata.

watu wanabadilika
 
Back
Top Bottom