Ijue povu formula na jinsi inavyofanya kazi

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,122
5,223
Tafadhali ongozana nami kwenye tafakuri hii. Kwa nini katika miili ya viumbe hai kuna kuna ute ute ambao huwa katika formula ya kunata, kuvutika au kuteleza iwe ni mate, shahawa, kamasi, jasho, utomvu, poleni n.k

Bila shaka utakapozungumzia shahawa, kamasi au mate hasa yale yanayovutika vutika utagundua havitofautiani sana hata DNA yake uweza mtofautisha huyu na yule.

Unapofua nguo zako kwa kutumia sabuni ya unga bila shaka unaloweka sabuni yako ndani ya maji kwanza kisha unapikicha kupata povu, je ushawahi kujiuliza kuwa kwanini hata harufu yako ya manii inashahawiana na harufu ya povu la sabuni achilia mbali kukauka/kusharabiwa kwake juu ya ngozi.

Bila shaka unaanza kupata picha taratibu kuhusu dhana ya udadisi wangu ulipoanzia, sasa rudi katika ngozi za mamalia ukianza na binadamu, mifugo n.k ukichuna ngozi cha kwanza kukumbana nacho ni hali ya mapovu juu ya ngozi(huwa kwenye ngozi fulani nyepesi nyeupe)

Pasina shaka kazi ya haya mapovu yenye mtetemo fulani nikutuma signal za hisia, kubalance joto, kuprovide protein kwenye ngozi n.k na kama ndivyo then uhisi kuwa maisha yalianzia katika formula ya povu dogo lililotokana na tone la maji (chanzo chake kikiwa hydrogen,

vumbi vumbi na gesi zingine angani) hivyo kutokana na hali hii tone lile likakumbana na gesi zenye asili ya kujivuta au kunata likatengeneza povu fulani ambalo baadae povu lile kama lilivyo povu la sabuni uunda duara ambalo ndani yake uwa empty lakini lidumupo pasipo kupikichwa povu hili upasuka au kukauka.

Hivyo povu hili ambalo pengine lilitokea katikati ya majabali mawili au kwenye plunge pool au sehemu yenye maporomoko yaliyoruhusu mtikisiko wa mara kwa mara wa maji nakutoruhusu matone ya maji yale kutoweka haraka kulianzisha maisha ya kiumbe

kilichotokana na povu na hata povu lile lilipofikia wakati wa kupasuka ile hewa iliingia moja kwa moja ndani ya kile kiumbe nakujaza ile empty space inside ile shape ya duara ndani ya kile kiumbe kitokanacho na povu

hivyo hata mwisho wa uhai wa kile kiumbe pia ni mfanano wa povu linapotokomea na asili ya mwili ule wa povu pia uhitaji mtetemo(mithili ya mpekecho) kila mara maana utakapo poa ndiyo kwaheri. Ndiyo maana hili uwe hai sharti kuwepo na mjongeo wa aina yeyote kimwili muda wote.

Na pia kiumbe huyu maumbile ya mazingira yake na hata baadhi ya viungo vyake kama macho, n.k yametawaliwa na umbile la mduara mfano wa asili ya chanzo chake yaani duara la mapovu.

Hivyo wale wasemao mwanadamu alitokana na udongo (maji na vumbi) nakubaliana nao isipokuwa kupuliziwa pumzi,

pia na wale wa big bang theory pia sipishani nao mbali, maana nilielezea katika hatua hii ya kulisababishia povu lile la maji mtetemo ili liendelee kudouble maduara kutoruhusu kupasuka mapema nakusababisha kiumbe kisiundwe lazima kuna kitu kilichosababisha mnyumbuliko huu ukawezekana,

sasa kama miamba haikuepo au maporomoko basi bila shaka mtetemo huu wa ghafla uliletwa na big bang ndipo pressure ile ya mtikisiko wa ghafla na mpasuko au mgongano mkubwa wa particles mbalimbali uliingiza pumzi kwa ndani kwenye maduara yale ya povu baadaye kiumbe kinachopumua kikaanzia hapo.

Hivyo chanzo cha uhai wa viumbe vyote ni maji ambayo utokana na muunganiko wa gesi fulani na vumbi vumbi ambapo vumbi hili chanzo chake ni sayari, nyota, vimondo na magimba yote yanayoelea katika anga hewa,

na kile kiitwacho hewa pia huwa na vumbi jingi ndani yake, hivyo ni nini chanzo cha vumbi lililounda sayari na magimba yote bila shaka ni mgandamizo mkubwa katika anga hewa uliopelekea joto kali na joto hili likaunda mlipuko wa mioto mbalimbali(nyota na majua) ambapo jivu lake likapelekea vumbi ambayo litakuwa na muunganiko wa gesi za asili ya mioshi/mnatiano na jotoridi fulani ambalo likaruhusu kuundwa kwa maji na hatimaye uhai.

NB: Mwanasayansi huyu mwafrika mashariki, member wa JF na mvumbuzi wa povu formula kama chanzo cha uhai ni muhitimu wa form four kwenye mchepuo wa HKL , hivyo rukhsa kumtemea povu na kumkosoa endapo utakuja na hoja zenye mashiko kutetea arguments zako.
 
Umeelezea theory yako kuwa inapingana na pumzi ya mwanadamu, kivipi??

Kwa sababu kila chenye uhai kina pumzi na pumzi imetoka wapi??

Kama theory inasema kila kitu kimeanza na povu, development yake hiyo ya kutoka kwenye povu hadi kwenye uhai wa mtu/kiumbe ipo wapi??
Maana kama mfanano wa shahawa..development yake ni kuwa lazima iingie kwenye uterus ili kuzalisha embryo. Hata vyura, ni mbegu zao zinatokea kumwagika kwenye maji yaliyotuama ndio ndubwi wanatokea.

Hii ina maanisha kuwa binadamu, alitokana na maji? Udongo? Au particles za nje ya dunia? (Coz either way, kuna sehwmu lazima atakuwa ametokea ili theory yako ya povu iwe applicable)

Na kama jibu ni ndio from any of above, upi uhusiano wa sasa kati ya binadamu na jibu lako, ukilinganisha na ulivyosema kuwa povu lina mnato na kuvutika mfanano na lile la sabuni??

Ukiweza kuclear haya yote vizuri, nakuwa muumini nà mfuasi wako, kwani utakuwa umefanya ugunduzi mzuri na wa kipekee kuliko maelezo.

Wanasayansi sasa wakataa chini kuanza ku-prove au kuendeleza fikra yako.

Sayansi haijali sana kama umesoma sanaa au la. Ukijua tuu, unajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakazia.
 
Sasa kama ni hivo mbona hio povu formula haiendelei ku take place? Nini imefanya iache ku produce viumbe?
 
Yaleyale ya akina fulani eti nyoka alikuwaga na miguu😅😅, viumbe hai vimetokana viumbe visivyo hai( nadhani theory yako ya mapovu iingie hapa kama mfano ila usio na ushahidi kisayansi)

Naheshimu waliosema origin of life ni Mungu. Ameen🙏, pia namweshimu yule mwanafalsafa aliyesema origin of life comes huko kusiko julikana. Nikwel hatujui ni wap tunachokiamini ni nadharia tu.
 
Umeelezea theory yako kuwa inapingana na pumzi ya mwanadamu, kivipi??

Kwa sababu kila chenye uhai kina pumzi na pumzi imetoka wapi??

Kama theory inasema kila kitu kimeanza na povu, development yake hiyo ya kutoka kwenye povu hadi kwenye uhai wa mtu/kiumbe ipo wapi??
Maana kama mfanano wa shahawa..development yake ni kuwa lazima iingie kwenye uterus ili kuzalisha embryo. Hata vyura, ni mbegu zao zinatokea kumwagika kwenye maji yaliyotuama ndio ndubwi wanatokea.

Hii ina maanisha kuwa binadamu, alitokana na maji? Udongo? Au particles za nje ya dunia? (Coz either way, kuna sehwmu lazima atakuwa ametokea ili theory yako ya povu iwe applicable)

Na kama jibu ni ndio from any of above, upi uhusiano wa sasa kati ya binadamu na jibu lako, ukilinganisha na ulivyosema kuwa povu lina mnato na kuvutika mfanano na lile la sabuni??

Ukiweza kuclear haya yote vizuri, nakuwa muumini nà mfuasi wako, kwani utakuwa umefanya ugunduzi mzuri na wa kipekee kuliko maelezo.

Wanasayansi sasa wakataa chini kuanza ku-prove au kuendeleza fikra yako.

Sayansi haijali sana kama umesoma sanaa au la. Ukijua tuu, unajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu kwa maswali mazuri na tafakarishi ngoja niandae majibu
 
Sasa kama ni hivo mbona hio povu formula haiendelei ku take place? Nini imefanya iache ku produce viumbe?
Uwepo wa mabadiliko ya kimazingira ambayo yalipelekea ugumu na kutokuruhusu kuendelea tena kwa process ya mwanzo na hali ya kiumbe kuweza kuyamudu mazingira yake mapya kuliletelezea ile hali ya ukamilifu wa kiumbe husika kuweza kuendeleza kizazi kupitia miili yao pasipo kutegemea tena chimbuko.
 
Umeelezea theory yako kuwa inapingana na pumzi ya mwanadamu, kivipi??

Kwa sababu kila chenye uhai kina pumzi na pumzi imetoka wapi??

Kama theory inasema kila kitu kimeanza na povu, development yake hiyo ya kutoka kwenye povu hadi kwenye uhai wa mtu/kiumbe ipo wapi??
Maana kama mfanano wa shahawa..development yake ni kuwa lazima iingie kwenye uterus ili kuzalisha embryo. Hata vyura, ni mbegu zao zinatokea kumwagika kwenye maji yaliyotuama ndio ndubwi wanatokea.

Hii ina maanisha kuwa binadamu, alitokana na maji? Udongo? Au particles za nje ya dunia? (Coz either way, kuna sehwmu lazima atakuwa ametokea ili theory yako ya povu iwe applicable)

Na kama jibu ni ndio from any of above, upi uhusiano wa sasa kati ya binadamu na jibu lako, ukilinganisha na ulivyosema kuwa povu lina mnato na kuvutika mfanano na lile la sabuni??

Ukiweza kuclear haya yote vizuri, nakuwa muumini nà mfuasi wako, kwani utakuwa umefanya ugunduzi mzuri na wa kipekee kuliko maelezo.

Wanasayansi sasa wakataa chini kuanza ku-prove au kuendeleza fikra yako.

Sayansi haijali sana kama umesoma sanaa au la. Ukijua tuu, unajua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kulingana na dhana ya wazo langu kuhusu ulimwengu ni kuwa cha kwanza ni anga hewa ambalo linamgandamizo fulani mithili ya puto lililotuna pasipo na hewa ndani yake yaani vaccum ila nje ya tabaka ilo kuna forces mbalimbali pengine ni gases,mivutano na matabaka mengine n.k

Ambayo kwa namna fulani usababisha mgandamizo fulani ambao upelekea pressure kubwa ndani ya hili puto kubwa(ulimwengu) hivyo kutokana na mgandamizo huu ni possible kuwa kuta za ulimwengu ambazo uundwa na gesi nzito,

Uruhusu gesi kadhaa kupenya nakuingia kwenye vaccum iliyochemka nakupelekea mlipuko wa moto kutokana na jotoridi kali ndani ya mzingo huu unaokabiliwa na pressure kubwa ya ndani tokea nje, hivyo mlipuko na uwepo wa zile gesi sababishi upelekea ile hali ya moto kuwa endless process mpaka gesi zile ziteketee zote na msuguano/au mgongano wake uishe ndipo utokea supernova.

Na hapo ndipo chanzo pia cha wanasayansi kushindwa kujua inakuaje ulimwengu unazidi tanuka kila uchao unapojibiwa na nadharia hii,

Kuwa expansion utokea ndani ya puto ambalo haliruhusu hewa kupenyeza nje kirahisi na badala yake presha iliyopo ndani ikisaidizwa na mioto na gesi iliyojiunda uongeza jotoridi ndani ya puto hili ambalo uzidi kupush pressure ya nje nakuzidi kuutanua ulimwengu (uwepo wa ozone layer kuprotect dunia nakutoruhusu miali yenye madhara kupenya nakubalance hewa za uhai huku ardhini kinaleta tafsiri ya namna anga hewa lifananavyo katika kingo zake za mwisho)

Hivyo kwa mtizamo wangu ni kuwa ulimwengu utaendelea kutanuka ili mradi ndani yake kuna presha inayozid push zaidi limits, hivyo hili kumaintain equilibrium ni must forces za msukumo wa ndani ziwe

strong sawa na zile za nje hivyo kama yalivyo mapovu ya sabuni katika dishi bubbles zinavyozidi kupata presha utanuka zaidi na mwishowe upasuka na zile ambazo hazijapasuka bila shaka kuna ulinganifu wa kani msukumo kati ya zile bubble mbili au zaidi zilizoshikamana katika mgandamizo/msukumano sawia.

Naomba nikomee hapa kwa sasa baadae ntaendelea na sehemu ya pili ya ufafanuzi zaidi wa theory hii.
 
Hivyo jua au mioto inayoexist sasa ndani ya space hii uendelea kuwaka vikiexpand space na hatimaye kutokana na moshi,jivu na ile hali ya jotoridi vinapoungana utokea maji ambayo kwa namna moja au nyingine uanza kama matone hatimaye barafu,

Barafu zinapokuwa nzito uendelea kuelea katika anga tupu kumbuka humu ndani ni vaccum au patupu hivyo ni rahisi kitu kuelea kuliko kwenda kwenye bottom ya universe,

taratibu maji haya ambayo uundwa na vumbi jingi kuliko mnatiano yanapoendelea kusettle vumbi ukusanyika chini(kujitenga) na maji hivyo kwa namna hii sehemu ya nchi kavu uendelea kujiunga ila kutokana na mgandamizo wa kiumbo yani semi-disk ulivyoulimwengu kwa nje, upelekea umbo la sayari hizi kuundwa katika umbile duara au karibia na mviringo(ila katika kipindi hiki ardhi ubaki kuwa chepechepe/embryo stage).

Baada ya uwepo wa landmass na sehemu ya maji au bahari ambayo kwa asilimia kubwa bado imeungana japo umbile la juu uanza kuwa oval kutokana na umbile la anga/tabaka hewa.

Joto la jua linapogonga juu ya ardhi na maji ukumbana na hali ya hewa nyevu au mvuke hivyo kupelekea kuzaliwa kwa hewa inayosupport uhai wa viumbe yaani oxygen ambayo ili isivukizwe na kupotea uendelea kukandamizwa na mataba mengine ya hewa yaliyopo juu ya tabaka lake.

Kwa namna ya kipekee maji yalipoendelea kuexist kutokana na kutuama kwake yakiwa bado na uzito mithili ya tope tope na sivyo yalivyo sasa yalitengeneza krimu nzito za mapovu ambayo u-formulate pembezoni mwa majabali ya udongo,

Taratibu ardhi kulingana na mabadiliko ya jotoridi na uwepo wa gesi kadhaa japo mgandamizo bado ulikuwa mkubwa ardhi iliendelea kupokea chemical reaction mbalimbali za gesi,joto, maji,madini katika miamba hii milaini ya awali n.k

hii ilipopatana na maji ya bahari likaunda mapovu fulani lenye hali ya kuvutika vutika na baadae kuanza kuungana na kuunda kitu, ambapo kutokana na mseto huu viumbe viwili yaani miti na wanyama vikaanza kujiunda each katika aina tofauti tofauti kulingana na uniqueness ya composition iliyotumika kumuunda na mazingira yake.

Mapovu haya yalipelekea vipi uhai kuundwa ndani yake?

Nimeeleza kuwa povu hili zito linalovutika vutika na-imagine mfano wa tope tope zito,liunde bubbles kubwa na ndani ya yale maduara ya povu la tope kwa ndani kuwe na kama vile vaccum hivyo kama ilivyotokea kujiunda kwa ulimwengu, vile vile zile kemikali au madini na gesi vipenye mdogo mdogo ndani ya yale mapovu pasipo kuruhusu presha ipelekeayo povu kupasuka,

na hatimaye muunganiko huu upelekee kiumbe kipya kujiumba huku mazingira ya nje yanayolizunguka povu hili mfano pressure sawia,kuwa pembezoni au kwenye uvungu wa majabali au ufukweni uundwa jotoridi rafiki ambalo uwezesha kiumbe huyu kukua kwa amani (kama ilivyo ndani ya uterus)mpaka hatua ya mwisho nakuwa kiumbe kamili,

Hili upelekea uwepo wa viumbe vinavyobakia nchi kavu na vile vya baharini kuwepo na maumbile yake kuja kutofautiana kulingana na mazingira yao, yalipoendelea kubadilika aidha kujikuta maji yakizidi kuwa mepesi hivyo kubakia huko na ardhi kuendelea kushikamana na kujitenga na maji hivyo kupelekea viumbe vingine kubakia nchi kavu,

Hivyo tuendelee na mada tulipokuwa tumefikia; endapo process ikipata disturbance kabla ya kiumbe hiki kukamilika hizi dosari upelekea kuundwa kwa viumbe transparent au roho ambazo huwa na hizi kani za msukumo wa hewa ndani yake pasipo maumbile maalum yaani majini au mapepo,

lakini process ikiendelea vyema mpaka kwenye final stage na povu lipasukie mwishoni kiumbe akiwa kamili ndipo tunampata kiumbe mdudu,mti,mdudu au utando n.k

process ya kujiumba huku ni matokeo ya ule mfumo wa pressure ya hewa iliyopenya ndani ya povu na kupush zile dutu za madini/kemikali anuai kuungana na kuunda umbo la kiumbe

( ile hewa inayopush taratibu ujikuta katikati ya kiumbe au ndani yake na endapo zile parts zikifanikiwa kujiunganisha/kufungamana pande zote hewa ya ndani ya kiumbe ujaa na kutoruhusu iliyopo nje kuendelea kuingia tena kupitia uwazi uliobakia(njia ya hewa)

Hivyo kitendo hiki upelekea hewa ya nje na ile ya ndani kuendelea kusongamana(push&pull) kutokana na pressure ya juu ya povu, hivyo hapa hewa zinazoexist ndani ya povu uanza kupeana chansi kulingana na hewa ipi inauzito upi(kumbuka jotoridi katika hewa zote mbili yaani iliyopo ndani ya embryo na iliyopo nje uanza ku-differ) ndiyo iingie na ipi itoke nje kumaintain pressure,

kitendo hiki upelekea kupumua na kiumbe kipya utokea hapa nakuendeleza kitendo hiki maisha yake yote hivyo kiumbe huyu kadri anavyozidi kutanuka pressure yake upelekea pressure kubwa na hatimaye

povu upasuka na kiumbe huyu uanza kuexist na hapo ndipo kiumbe huyu ukutana na pressure kubwa ya hewa ya nje ambayo inazidi ile ya ndani wakati akitegemea msaada wa povu hivyo hewa hii uingia direct pasipo kizuizi kikubwa cha hewa ile ya ndani nakuoccupy space kwa ghafla,

kitendo hiki u-push hewa iliyokuwemo ndani ambayo ina joto na ni nyepesi kutoka na kuingia hewa baridi ambazo ni nzito na hivyo kitendo hiki hujirudia rudia nakuwa endless hivyo hali hii inapodumu ndipo

kiumbe ujongea na kumudu mazingira yake(kipindi cha uhai) na kutokana na hali ya mazingira ya nje ya kiumbe huyu yale madini yaliyomuumba uendelea kukosa uimara wake wa asili na hatimaye kuharibika na kuirudia ardhi kuruhusu process kukoma.

Kwanini process hizi haziendelei tena kama mwanzo ni kwa sababu mazingira ya mwanzo yaliyopelekea kuundwa kwa kiumbe hiki na hali zake zinakuwa hivi sasa zimeshatoweka na mazingira hivi sasa yanajipambanua katika msawazo wa kiumbe yaani solid, liquid na gases hivyo balance inakuwa imeshafikiwa katika uwiano wa kimazingira,

hivyo hakuna possibility kwa kiumbe kutokana na mazingira ya nje bali ndani yake ndipo kunapokuwa na ile hali ya vaccum na hewa inayopush tissues ku-respond na kubalance vyema jotoridi ambalo upelekea kuundwa kwa kiumbe hai kipya,

kupitia mfumo ule ule wa awali wa povu formula yaani mayai,kiini n.k kuwa na kokwa gumu la nje na mvutiko au utelezi kuallow process ya uumbaji kufanikiwa, hivyo ndiyo sababu hasa hivi sasa kiumbe uendeleza kizazi kupitia kiumbe chenyewe.

Na kutokea kwa kiumbe jike na dume pia nikutokana na uwiano wa kani msukumo ndani ya povu upelekea viumbe vingine kuwa na mifuko ya ziada au mazingira rafiki ndani mwao ya kuweza kutengeneza chanzo cha uhai au kubeba mimba na viumbe vingine kuwa na ziada ya madini yenye kuweza kurutubisha hivyo uzazi kuendelezwa.

Yapo mengi ya kueleza katika formula hii lakini naomba nikomee hapa niruhusu critics, arguments na maswali kupima possibility ya theory hii kuweza kukata kiu ya swali juu ya existence.
 
Back
Top Bottom