Ijue Pegasus, software inayotumika kuwadukua wanaharakati na wanahabari

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Pegasus ni jina linalomaanisha Farasi Mwenye mbawa. Ambalo ni namna ya kuonesha kuwa software hiyo inafanya kazi kama Farasi wa Matrojan(Trojan Horse) lakini yeye anaweza kupaa.

Software ya Pegasus imegundulika 2018 na kampuni ya Israel ya NSO inauwezo wa kudukua hadi iOS 14.6. Kampuni waliotengeneza software hiyo wamesema waliunda mahususi kwa ajili ya kupambana na uhalifu.

Pegasus ambayo imesemekana kutumiwa na mamlaka mbalimbali kufuaili wanaharakati na wanahabari, inauwezo wa kuchukua kila kitu kwenye simu ya mtu bila kuathiri utendaji kazi wa simu kwa mtumiaji halali.

1626935995048.png
 
Mbona ujaeleza ni namna gani inafanya kazi na inadukua taarifa gani pia inasambazwa kwa njia ipi
 
Mbwembwe tu hizo za watu wanaotaka kuwapiga washamba mamilioni ya hela. Ila apps nyingi tunazoweka wenyewe kutoka kwenye appstore au Play zina uwezo mkubwa tu wa kuvujisha data zako na kukupeleleza.
 
Mbwembwe tu hizo za watu wanaotaka kuwapiga washamba mamilioni ya hela. Ila apps nyingi tunazoweka wenyewe kutoka kwenye appstore au Play zina uwezo mkubwa tu wa kuvujisha data zako na kukupeleleza.
Naona unajifariji, Sasa umeambiwa hiyo software inawekwa kwenye simu? Jitahidi kutofautisha mkuu hiyo Tool inafanya kazi remotely na haiwekwi kwenye simu bana wala sidhani kama kuna app yoyote inawekwa kwa victims..
 
Niona kwenye TV walikuwa wanaielezea hii Pegasus kwamba lazima utumiwe link kwenye simu ya anaetaka kuhackiwa.
 
Naona unajifariji, Sasa umeambiwa hiyo software inawekwa kwenye simu? Jitahidi kutofautisha mkuu hiyo Tool inafanya kazi remotely na haiwekwi kwenye simu bana wala sidhani kama kuna app yoyote inawekwa kwa victims..
Hamna kitu kama hicho. Software inakaa kwenye simu. Na lazima uiweke wewe mwenyewe. Hawa Pegasus wanachofanya wanakutumia meseji ya kizushi ila inayoendana na mambo unayopenda.

Ukibofya link tu ndo unakuwa umeinstall software yao.

Kuhusu remote connection apps karibia zote zinafanya kazi namna hiyo. Kwamba lazima iite nyumbani na ndo mambo ya ku-update na kuhamisha data zako na kukupepeleza yanavyofanyika.

Tofauti ni kwamba wakati app zingine ukiweka unaziona icons zake, app ya upelelezi kama Pegasus hauioni. Lakini kwa kutumia app za kawaida tu hizi ambazo mtu anaweka kwa hiyari yake bila kujua inafanya nini nyuma ya pazia unaweza ukafanya mambo yote ambayo Pegasus inafanya.
 
Nimeisoma 3 yrs Tel aviv, ni noma sana, lkn iko limited kuitumia. Ndio maana juzi tu mataifa wameiomba israel isisambaze hizi kitu za kudukulia, maana israel na kikosi chake cha vijana wadogo ni noma
 
Nimeisoma 3 yrs Tel aviv, ni noma sana, lkn iko limited kuitumia. Ndio maana juzi tu mataifa wameiomba israel isisambaze hizi kitu za kudukulia, maana israel na kikosi chake cha vijana wadogo ni noma
Naomba jina la chuo na kozi uliyosoma nikajiridhishe google
 
Back
Top Bottom