Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,481
IJUE NYOTA YAKO

Nyota ni Elimu ya Sayansi ya kiroho ambayo inatumika Dunia nzima. Kila mtu katika Dunia akitaka asitake, aamini au asiamini atakuwa amezaliwa katika moja wapo ya nyota hizi 12 zimechomoza wakati anazaliwa.

Pia elewa ya kwamba ndugu yangu nyota yako moja imegawanyika katika makundi manne yaani:

1: Nyota Iliyochomoza wakati unazaliwa. nyota ya kuzaliwa
2: Nyota iliyochomoza tarehe na mwezi uliozaliwa yaani nyota ya jua
3: Nyota iliyochomoza wakati unazaliwa Mbalamwezi ilikuwa eneo gani.
4: Nyota iliyochomoza wakati unapewa jina lako. au nyota ya jina.

Hii ndio sababu watu wengi wanapoangalia maswali ya nyota za kiroho huona ni uzushi na uongo uliopindukia lakini wanashangaa na kuona wengine zinawang'aria na kupata mafanikio kinyota kwa kuifuata vyema, kufuatilia nyota si dhambi zambi huja pale unapoileta wewe.

Na ieleweke kuwa elimu ya nyota sio kwamba ni Imani ya dini fulani hapana isipokuwa ni maarifa kama ilivyo maarifa mengine kama physics au baiolojia isipokuwa hii imebase zaidi katika mambo ya kiroho, hivyo ni elimu ya kusoma kama zilivyoelimu zingine.

Fahamu ya kwamba madaraja au mgawanyiko wa hizo sehemu tatu za nyota yako ndio hutoa maelezo sahihi ya nyota yako wengi wanawalipulia watu maelezo ya nyota vibaya na kuwafanya kupoteza kabisa ladha ya nyota zao na kuona nyota ni usanii fulani wa kubahatisha kipuuzi lakini ukweli sio hivyo.

Humo humo ndani ya nyota ndio kuna maelekezo ya wewe ni vipi unaweza kupata kitu fulani au tukio fulani kwa kufuata muongozo upi, na kufanya kipi. Ili uweze kufanikisha jambo fulani rejea hapa kujua milango 12 ya nyota yako.


Na pia kwenye nyota hiyo utaweza kujua mambo unayotakiwa kuyafanya kila siku au kuyapangilia ili uweze kujua vipi unaweza kufuzu kinyota.

Kumbuka soma mara mbili mbili kuweza kujua wengine hukuta mkang'anyiko wa mambo katika nyota zao hasa pale jina lako linaposema nyota yako ni fulani, na tarehe inasema tofauti na matendo yanaenda tofauti hapo ndio wengi huona huu ni usanii wa hali ya juu.

Karibu uweze kujua na kujifunza au kuongeza maarifa ieleweke kuwa nyota hizi sio mazao ya dini fulani hapana utaonekana usiyeelewa ikiwa utaendelea kuoanisha elimu ya unajimu na dini yoyote ile.

zodiac-signs-300x200.png

Nyota hizo zina athari kubwa katika maisha yako hasa ukitenda kinyume na matakwa ya nyota hiyo. Mfano ukifanya biashara ambayo siyo ya nyota yako, biashara hiyo itaathirika, au ukimchukua mpenzi ambaye sio wa nyota yako bila kujua, mtapendana lakini mwisho utakuwa mbaya, au ukifanya mambo ambayo nyota yako haikubaliani nayo mambo yako yatakwama na utajiona una mikosi.

Nimeandika maelezo haya ili kuweza kuwasaidia, kufahamu undani kuhusu nyota yako, mambo yanayohusu nyota hiyo, ikiwemo siku yako ya bahati, rangi, namba ya bahati, nani wa kushirikiana nae kimapenzi, kikazi, kibiashara, jiwe gani uvae, manukato gani yanakufaa, mafusho ya nyota yako, mambo muhimu ya kufanya, Kipaji chako, mambo ya kujiepusha nayo, chakula chako, magonjwa yako, mpaka nchi za kukaa kama una uwezo.

Ukifuatilia vizuri na kwa makini utaweza kujiepusha na matatizo mengi sana ya kimaisha, Ndoa zitadumu, biashara zitashamiri, na Mikosi itakuondokea.

Nyota zinatambulika kutokana na tarehe yako ya kuzaliwa,muda na saa au kama hujui basi inafaa na ndio bora zaidi kupigia hesabu jina lako la kuzaliwa pamoja na mama mzazi kwa nini tunatumia mama mzazi kwa sababu yeye ndio ana uhakika zaidi ya kwamba wewe ni mtoto wake.

Tukianza na nyota ya kwanza


NYOTA YA PUNDA: ARIES

10-Reasons-Aries-is-the-Worst-Astrological-Sign.jpg

Hii ni Nyota ya kwanza katika mlolongo wa Nyota 12.
Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Machi na 20 Aprili au wenye majina yalioanza na herufi A au M au Y au L au E.

Namba yao ya bahati ni 1,8 na 17
Asili yao ni Moto, nayo ni nyota dume.
(dume ikiwa na maana ya chanya/sio jinsia za wenye nyota)

Usawa wake ni Imara
Ni nyota ya utendaji,yenye nguvu,inafaa na yenye msukumo na nyota yenye matumaini,iliyowazi katika mabadiriko na hali mpya.

Sayari yao ni Mars (Mariikh).
Marikh kwa historia za kale ni kuwa ni sayari ya Kiumbe wa vita,vurugu,uovu na ubaya.
katika elimu ya nyota hii husimama kama sayari ya hamu/shauku na upinzani huleta hisia za ajali na humiliki moto na Hatari

Siku nzuri katika wiki ni Jumanne
Malaika anayetawala nyota hii anaitwa Samael au Izrael,
ambaye ni malaika mtoa roho za watu,

Jini wa nyota na sayari hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar au Phaleg

Alama ya nyota hii ni Punda ambapo maana yake ni msisitizo, kingono na kupanda chat zaidi

Maarifa makuu kabisa ya punda ni ujasiri

Nyota inayoipa nguvu zaidi ni Mizani:
Punda ni nyota ya ubinafsi yaani umimi kwanza, ni nyota yenye uelekeo wa ubinafsi zaidi mizani ambayo ndio nyota yenye nguvu hasi kuweza kuing'arisha Punda kwa sababu yenyewe ni chanya na basi mizani huwa ni nyota pweke na yenye kuzoea upweke hivyo ikiungana na Punda basi huwa na nguvu maradufu, na hasa wakiungana kimapenzi basi hung'ara zaidi.

Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu kwa maana huwakilisha moto ambao ni asili ya Punda, Rangi zinazowafaa kwenye Nyumba au Vyumba vyao ni rangi nyekundu (Scarlet).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za kijani na kijani kibichi. Rangi inayowapa uwezo wa kifedha ni rangi ya Kijani

Manukato yao ni Marashi ya Asali (Honeysuckle)

MAMBO MUHIMU:-
punda ni watu ambao kama ilivyokuwa ni nyota ya kwanza basi wao huwa mstari wa mbele sana katika kufanikisha mambo kwa haraka lakini pia ni watu ambao hawaoni shida kuanza moja kwa jambo lolote lile wao huonekana kama watu wa maajabu sana katika maisha

Ubora unaohitajika kwa watu wa Nyota hii ili kusawazisha mambo yao ni “kuwa waangalifu”

Maadili yao ni “Utumiaji wa nguvu, Ujasiri, Uaminifu, kuwa huru na kujitegemea

Matakwa yao ni Vitendo

Tabia za kujiepusha nazo: Kutokuwa na subira, kufanya mambo haraka haraka bila kufikiri, kutumia nguvu bila akili na kuharakisha mambo.


USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao “Wanaelewana” nao ni nyota za Simba na Mshale

Nyota za watu ambao “Hawaelewani” nao ni nyota za Kaa, Mizani na Mbuzi.

Nyota inayomsaidia “Kikazi” ni nyota ya Mbuzi

Nyota inayomsaidia “Kipesa” ni nyota ya Ng’ombe

Nyota inayomsaidia katika “Ubunifu” ni nyota ya Simba.

Nyota bora ya “Kujifurahisha” ni nyota ya Simba

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya “Kidini na kiroho” ni Nyota za Mshale na Samaki.

Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumanne

KIPAJI CHA PUNDA
Wenye nyota hii wana kipaji cha Hisia, ni rahisi kwao kutafsiri jambo lolote, wanaweza kwa urahisi kutafsiri ndoto, vilevile wana kipaji cha kusikia sauti ndani ya kichwa kuhisi jambo litakalotokea na ikawa kweli.

Ikiwa watafanya Taamuli (Meditation) kwa dakika ishirini wakati wa usiku au kitu cha kwanza wanapoamka asubuhi, akili na miili yao itatulia na watapata ufunuo wa mambo mengi sana.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na hali ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia.

Ni watu wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”.

Kimapenzi Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.

KAZI NA BIASHARA ZA PUNDA :
Wote wake kwa waume waliozaliwa katika nyota hii wana kipaji cha asili cha uongozi na wasiwasi wa kushindwa katika utekelezaji. Kazi zinazowafaa ni Jeshi, Kazi za Uokoaji, Michezo, Uuzaji, Upasuaji, Kufundisha (Ualimu), Masuala ya Fedha. Biashara za kubadili fedha,Biasharaza kuuza vifaa vya michezo, biashara za vifaa vya shule au maduka ya madawa.

MAVAZI NA MITINDO:
Mavazi yao yanatakiwa yawe ya mitindo mikali na tofauti, yenye kuchangamsha na Kusisimua ya rangi nyekundu.Vitambaa vyao viwe vya sufu (wool), Fulana, na vitambaa vilivyo na kishiwa kwa nyuzi za rangi ya chuma. Wasikose kuvaa kofia, wanawake wapendelee sana kuvaa na Suruali

MAGONJWA YA PUNDA:
Nyota hii inatawala kichwa, Ubongo, Macho, Mifupa ya uso na fuvu la kichwa.
Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni kuumwa na Kichwa, Kuzimia, Homa ya ubongo, maradhi ya kupata ajali ndogo ndogo za uso na kichwa Maradhi ya chunusi na magonjwa ya mishipa ya kichwa.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA PUNDA:
Punda vyakula vyao vikuu ambavyo vitawaletea bahati ni Mananasi,Viungo vya pilipili, Vitunguu na nyama ya mbuzi.
Nchi ambazo wanaweza kupata mafanikio ni England, Germany, Poland na Switzerland na miji yao ni Florence, Marseilles,Verona Liverpool na New Orleans

MAUA:
Maua ya nyota hii ni Geranium,honeysuckle na sweet pie

MADINI:
Madini yao ni Chuma

VITO:
Vito au Mawe ya bahati na miujiza ni Almasi Hii kwa sababu huvuta mapenzi mafanikio ya kimaisha,bahati za kupitiliza hili jiwe huwapa bahati sana wenye nyota ya punda linapovaliwa upande wa kushoto, mawe mengineyo ni Ruby, Hematite, Aventurine, Bloodstone, Carnelian, Citrine, Diamond, Lapis Lazuli, Mexican Lace Agate na Quartz

MNYAMA:
mnyama wa nyota hii ni kondoo hasa dume

MAFUSHO:
Mafusho yao yanaitwa Qist ,isome zaidi kwenye post iliyopita yako kama vipande vya mizizi na yana rangi ya kahawia. Ili kupata bahati wanatakiwa wachome mafusho haya kila Jumanne asubuhi saa 12 mpaka saa 1 na saa 7 mpaka saa 8 mchana..

FUNGUO:
Funguo yao ya mafanikio ni "UMIMI"

HATARI:
Hatari ya punda ni kujiweka mbali na vitu vikali pamoja na moto pia hutakiwa kujiweka mbali na kukimbiza hovyo magari maana wao hupoteza muelekeo kwenye spidi vichwa vyao huvijua wao wenyewe na hupenda kujiweka karibu na vurugu na sehemu za hatari hivyo kama wewe ni Nyota yako hii epuka mambo hayo


NYOTA YA NG'OMBE: TAURUS

sign-of-taurus.jpg

Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 20 April hadi May 20 au wenye majina yalioanza na herufi B au V au U jinsia ya nyota hii ni Jike.

Sayari yao ni Venus (Zuhura).
Siku yao ya bahati ni Ijumaa.
Namba yao ya bahati ni 6.
Rangi yao ya bahati ni kijani.
Asili ya nyota yao ni Udongo.

Ng'ombe ni nyota yenye sifa za ukimya, upole, sikivu, usawa, ujeuri na kutokukubali kubadilika.

KIPAJI CHA NG'OMBE

(BODY-CENTERED)
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa kilicho ndani ya mwili wao ambacho ni pamoja na kuelewa mambo kimbele, hesabu, kuponya kwa kutumia mikono na kwa kumwagia mtu maji.

TABIA YA NG'OMBE:
Wenye nyota hii ni watu wanaopenda kujishughulisha katika shughuli nyingi. Ni watu wakarimu na wanaopenda kusaidia watu, na wana tabia ya uvumilivu na subira katika jambo lolote wanalolifanya.
Ni watu wenye malengo na wenye msimamo thabiti, wasiopenda kupindishwa na wana tabia ya ubishi na ukaidi hasa katika jambo lao wanalolitaka.

TABIA YA NG'OMBE KATIKA MAPENZI:
Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
Pamoja na kwamba asili yao ni udongo, wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi makubwa kwa wapenzi wao.
Uhakika wa mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.

Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao. Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.

Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi kubadilishwa.

MATATIZO YA KIAFYA:
Nyota hii inatawala shingo, koo, koromeo, kidevu na sehemu ya chini ya taya.
Kwa asili wenye nyota hii ni watu wabishi na wenye kufanya mambo kwa upole na wagumu kubadilika.

Wanapenda sana vyakula vitamu na vyenye mafuta na huwezi kuwabadilisha katika hilo na wengi wao wanakuwa wanene kupita kiasi na inakuwa ni vigumu sana kuwashawishi kuamka na kufanya mazoezi ya mwili.

Tatizo lingine ni kufanya kazi kupita kiasi ambalo linawafanya wapate matatizo ya mvutano na misuli hasa katika sehemu zilizotajwa. wenye nyota hii wanatakiwa wajihadhari na mpangilio wao wa chakula na wafanye mazoezi kwa wingi.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'OMBE:

Wenye nyota hii wana falsafa ifuatayo kulingana na kazi; "panda mbegu iote, mti uote halafu ule matunda". Ni watu ambao wanafuata mpangilio wa kikazi na wanaopenda kujituma na kujishughulisha. Wengi wenye nyota hii ni wafanyakazi wazuri na wanapenda wapewe muda kujenga vipaji na utaalamu wao wa kazi.

Kazi zao zinakuwa kazi za muziki, kazi zinazohusiana na chakula, hoteli, migahawa, kazi za ujenzi, kazi za mashamba, kazi za uhasibu, na kazi za sanaa hasa uchoraji au uchongaji vinyago.

FAMILIA ZA NG'OMBE:

Wazazi wa familia za Ng'ombe ni watu wenye msimamo, wakutegemewa na wanaothamini familia zao, na wako tayari kugombana na mtu yeyote kwa ajili ya watoto wao. Ni wazazi wanaopenda kufuata mambo ya kizamani au ya asili hasa katika masuala ya nidhamu. wanapenda sana kuheshimiwa na watoto wao na huwashawishi au kuwashauri wawe huru.

Ni wazazi wanaotegemea watoto wao wafuate nyayo zao hasa katika biashara au kazi wanazozifanya, hivyo watoto wa wazazi Ng'ombe wanakuwa na muda mdogo wa kufikiria mambo mapya. Ni wazazi ambao hufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wao hawakosi wanachokitaka na wanapenda watoto wao wawe na elimu nzuri. Hata hivyo ni wazazi ambao wanategemea watoto wao wafuate wanavyotaka wao vinginevyo inakuwa matatizo.

MADINI YA NG'OMBE:
Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa ALMASI au EMARALD.
Mawe haya yanawafanya wenye nyota ya ng'ombe wawe katika hali yao ya kike kike (Feminine) vili vile thamani ya mawe haya ni uthibitisho wa nyota hii katika fedha.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:
Tabia ya uaminifu na ukweli waliokuwa nao wenye nyota ya ng'ombe inakuwa ni faraja kubwa kwa nyota ya Nge ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi na kudhania maovu, kutuhumu na kushuku.

VYAKULA VYA NG'OMBE:
Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao; Tofaa (apple), (oysters), viazi mbatata (potatoes), na dover sole.

NCHI ZA NG'OMBE:
Ili kupata mafanikio ya kinyota, kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; baadhi ya nchi hizo ni USSR (Urusi), Ireland, St louis,na Lucerne (Switzerland).

RANGI ZA NGOMBE:
Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za kijani au rangi za pinki au rangi ya bluu ambayo haijakoza katika nyumba zao au sehemu zao ya biashara ili kuleta mvuto wa kinyota.

FUNGUO:
Funguo za mafanikio yao ni "NINACHO" kujihisi kuwa teyari kashakimiliki anachokitaka basi hukipata


NYOTA YA MAPACHA: GEMINI

2018-horoscope-Gemini-897046.jpg

Hii ni nyota ya tatu katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Mei na 20 Juni au wenye majina yalioanza na herufi C au O au K au G
Asili yao ni Upepo.Sayari yao ni Mercury (Attwarid). Siku yao ya bahati ni Jumatano na namba yao ya bahati ni 6

Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail na Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa, Barkaan au Ophiel, Herufi ya Jumatano ni T

Rangi zao ni Bluu, Njano, Njano ya Chungwa Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za njano au bluu isiyoiva ambayo inapendeza ndani ya nyumba.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi ya Samawati (Sky Blue)

Rangi inayowapa uwezo wa kifedha ni rangi ya Kijivu na rangi ya Fedha

Kito (Jiwe) ni Agate na Aquamarine Celestite Howlite Chrysocolla,Quartz, Emarald na DiamondMadini yao ni Fedha

Manukato yao ni Marashi ya Mrujuani (Lavender), Lilaki maua ya rangi ya zambarau isiyoiva (Lilac), Yungiyungi (Lily of the valley).

MAMBO MUHIMU:-

Sifa zao ni kubadilika badilika katika mambo au maamuzi yao.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Kuwa na Fikra za ndani kuliko za juu juu.

Maadili yao ni Ujasiri katika mawasiliano, Uwezo wa kufikiria haraka haraka na uwezo wa kujua na kufahamu vitu haraka.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kusengenya, Kuumiza wengine kwa maneno makali, Mambo ya juu juu na kutumia maneno ili kuwapotosha watu (Propaganda).

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaoelewana nao ni nyota za Mizani na Ndoo.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mashuke, Mshale na Samaki.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Samaki

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Kaa

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mizani

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mizani

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni Nyota za Ng’ombe na Ndoo.

KIPAJI CHA MAPACHA:
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa cha kuwasiliana na watu ambao wako mbali kwa kutumia akili zao au hisia walizokuwa nazo. Telepathic:

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mapacha ni watu wenye hisia kali sana ambao wanakasirika upesi, ni watu wasiotulia na wenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kuzungumza.
Wanaweza sana kushawishi watu. wanapenda sana mabadiliko na tofauti na kujua mambo, wanapenda watu na wanapenda kujumuika na watu lakini wakati mwingine hawaeleweki.

Wanapenda sana kusafiri na wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika. Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana, ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Katika Mapenzi wanahakikisha kwamba hawawachoshi wapenzi wao. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.

Katika mapenzi, wao wanapenda vitu au mambo tofauti tofauti, wakihisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.Uaminifu ni kitu kigumu kwa Mapacha. Mara zote wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje, hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.

KAZI NA BIASHARA ZA MAPACHA:
Kwa vile wenye nyota hii asili yao ni upepo na wao ni wenye kuzaliwa kwenye mawasiliano na uhusiano, wanapenda sana uhuru na uwazi katika kazi zao. Kazi zao hasa ni zile zinazohusiana na mambo ya utangazaji wa Radio na Televisheni. Kazi ambazo zinahusika na mambo ya vitabu au uchapishaji vitabu. Kazi za kufundisha na kazi za ushauri nasaha.Vilevile wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi za ukalimani au kazi za biashara lakini zinazohusiana na safari za nje.

MAVAZI NA MITINDO:
Mapacha wanatakiwa kuvaa Nguo zenye Mitindo ya kisanii, nguo ziwe Nyepesi na zilizonyooka Ziwe za Rangi ya Njano na Nyeupe. Kitambaa kiwe kama hariri, chepesi na chenye kumeremeta. Wake kwa waume wapendelee kuvaa Suti na ikiwezekana wasikose kuvaa Gloves.

MAGONJWA YA MAPACHA:
Nyota hii inatawala mabega, mikono, viganja na sehemu ya juu ya mbavu.Tatizo la kutopumzika kwa sababu ya kutafuta mambo mapya ndio yanayosababisha maradhi kwa wenye nyota hii.Wanasahau miili yao na mara nyingi wanapata matatizo ya neva kutokana na uchovu kwa mishughuliko mingi.Magonjwa yao makubwa ni kukosa pumzi (bronchitis), pumu (asthma), matatizo ya kifua, mafua, flu, ajali za mara kwa mara kwenye mikono na mabega.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MAPACHA:
Mapacha wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao, kuku, rasiberi, karoti na uduvi.
Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo inayotawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Ubelgiji na Wales, na baadhi ya miji ni London (Uingereza) na San Fransisco (Marekani).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mapacha ni Fedha. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Mapacha yanaitwa Kashuu Muhlib (kachiri). Mafusho haya yako kama mauwa yaliyo kauka, rangi yake ni kahawia. Kwa kuleta bahati choma siku ya Jumatano kati ya saa 12-1 asubuhi au kati ya saa7-8 mchana.

FUNGUO:

Funguo ya nyota ya mapacha ni "ninafikiria" basi wao wakifikiria kitu hukamilika

NYOTA YA KAA: CANCER

76710085-cancer-zodiac-sign-horoscope-symbol-vector-illustration.jpg

Hii ni nyota ya nne katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Juni hadi 22 Julai au wenye majina yalio anza na herufi D au H au P.Asili yao ni Maji,

Sayari yao ni Mwezi (Moon)
Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumatatu.
Namba yao ya bahati ni 2 na 7.
Malaika wake anaitwa Gabriel au Jibril,
Jini anayetawala Jumatatu anaitwa Murratul Abyadh au jina la utani anaitwa Abú nuuril abyadh au Phul
Madini yao ni Fedha (Silver)
Kito (Jiwe) ni Moonstone, Lulu (Pearl). Quartz, Diamond, Moonstone, Peacock Ore Manukato yao ni Yasimini (Jasmine) na Msandali (Sandalwood).
Rangi zao ni Nyeupe, Bluu, Hudhurungi (Puce) na rangi ya Fedha (Silver), Wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi zozote ambazo siyo nzito au zenye uwiano na rangi nyeupe.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi(Black) na Bluu iliyoiva (Indigo).

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni rangi ya Machungwa na rangi ya Dhahabu.


MAMBO MUHIMU:-

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo yao ni kujirekebisha na tabia yao ya kusikitika sikitika na kunung’unika.

Ubora wa Nyota hii ni Uongozi.

Maadili yao ni Kung’ang’ania, kuwa na uwezo mkubwa wa kihisia na kupenda malezi.

Matakwa yao ni Maisha ya Kifamilia pamoja na Nyumba yenye amani na maelewano.

USHIRIKIANE NA NANI?
Tabia za kujiepusha nazo ni kupunguza kuwa na hisia kali na kunung’unika nung’unika na kusikitika pasipokuwa na haja ya kunung’unika.

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Nge na Samaki

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Punda, Mizani na Mbuzi.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Punda.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mizani.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Simba

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Nge.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mbuzi

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Nge

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mapacha na Samaki.

KIPAJI CHA KAA:
Kaa wana kipaji cha hisia ya kugundua mambo yanayotendeka ikiwa ni pamoja na kubashiri mambo, kumwelewa mtu kwa undani na kujua jambo ambalo mtu anataka kulifanya au jambo litakalotendeka hasa kwenye watu wengi. (Sensitive):

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Kaa ni watu wenye tabia ya hisia nzito, wapole na wenye huruma. Ni wenye dhamira ya ulezi na kuwaangalia au kuwahurumia watu wengine, hiyo inaonekana waziwazi katika nyumba zao na familia zao.

Upande mwingine ni watu ambao wana “Gubu,” wakali, wenye kupenda kujishughulisha na wanajiamini sana. Ni watu ambao wanaweza kubadilika lakini wenye msimamo na itikadi, wanaweza kuwa ni wenye wivu mkali na wenye kupenda kudhibiti wapenzi wao.

Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa Kaa, pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanaopenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu, wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.

Kaa bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha, hivyo basi huwa hawana raha. Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi, wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.

KAZI NA BIASHARA ZA KAA:
Kaa,Wanatakiwa wafanye kazi za Utabibu kama vile Madaktari au Wauguzi, kazi za baharini kama vile mabaharia, kazi za huduma ya chakula kama hoteli, migahawa, kazi za kuhudumia watoto kama katika shule za chekechea, kazi za benki au kazi za maneja utumishi au kazi za kuandika.


MAVAZI NA MITINDO:
Mavazi yao yawe ya kupwaya pwaya kama ni Magauni yawe ya kuninginia, nguo ziwe zinazo badilika badilika. Mavazi yawe ya rangi ya Fedha na rangi ya Bahari. Vitambaa vyao viwe laini na vyenye kutiririka. Nguo za kike ziwe zenye marinda na Blauzi ziwe laini

MAGONJWA YA KAA:
Nyota hii inatawala njia kuu ya chakula kuelekea tumboni, mbavu, mfupa wa kidari, tumbo la uzazi, utumbo mdogo na utumbo au sehemu zote za kusagia chakula.Vile vile inatawala bandana na matiti.
Maradhi yao makubwa yanakuwa maradhi yanayosababishwa na gesi, vidonda vya tumbo au kiungulia au maradhi yanayotokana na mwili kuwa mnene au umbo kubwa.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA KAA:
Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula na matunda yafuatayo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao, Mapeas, Kaa au vyakula vya baharini, na mboga kama kabichi na saladi (lettuce).
Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota hii wanashauriwa watembelee au waishi katika miji au nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao.Miji hiyo ni New York (Marekani) na Venice (Ugiriki) au nchi za New Zealand na Scotland.

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Kaa ni Fedha. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Kaa ni Ubani wa aina yeyote wa kawaida au ubani maka unachoma siku ya Jumatatu kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:

Funguo ya kaa ni hisia "nahisi" basi wao wakihisi uwepo wa kitu hukipata


NYOTA YA SIMBA: LEO

2018-horoscope-Leo-897060.jpg

Hii ni nyota ya Tano katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Julai hadi 22 Agosti au wenye majina yanayo anza na herufi E au Q au S au T.

Usawa wake ni Dume.
Asili yake ni Moto.
tabia yake ni thabiti
Sayari yake ni Jua(Sun).
Siku yake nzuri ya bahati ni siku ya Jumapili,
Namba ya bahati ni 1,3,10,19 na 4 .
Malaika wake anaitwa Michael au Raukayaeel
Jini anayetawala Jumapili anaitwa Abdulahi Saeed al Madhhab au Och.
Rangi zao ni rangi ya Dhahabu (Gold), Nyekundu (Red) na rangi ya Machungwa (Orange)

NGUVU YA NYOTA HII:
Wenye nyota hii huwa na nguvu ya Ubunifu, shauku, ukarimu, moyo safi, furaha, wenye kupendelea kucheka,

UDHAIFU WA NYOTA HII:
kiburi, ukaidi,kujitegemea,uvivu, asiye na akili.

WANACHOPENDA:
wenye nyota hii hupenda sana maeneo yenye kujichanganya kwa watu kujionyesha,kuchukua likizo,kupenda mambo makubwa ya gharama,rangi zenye kuwaka,na kujifurahisha na marafiki.

WASICHOPENDA:
Kupuuzwa,kukubaliana na hali,kutokutukuzwa kama mfalme au malkia.

MAMBO MENGINE KUHUSU WAO:
Wenye nyota hii ni watu wenye bahati sana hasa kulingana na nyota yao, katika maswala ya kiuchumi, japo kuwa ni nyota ya watu wenye kutumia sana pesa hovyo na inayeyuka kama vile moto vile vile watu wenye nyota hii ni watu wenye kuogopwa sana na kukimbiwa na watu kutokana na ukali wao.
simba pia wanasifa za kuwa na shauku, nguvu, kujipanua na ubunifu, ukarimu na ubaguzi wa kisiri siri,pia uwezo kimantiki na wenye maoni
watu waliozaliwa kwenye nyota hii wao ni viongozi wa asili,ni watu wa ajabu ambao wabinafsi na wenye kupenda zaidi kujitegemea, ni watu wazito sana na wakubwa katika kuwapinga ikiwa unataka kumpinga,wao huweza kufikia malengo yoyote yale ya sehemu ikiwa wanajitolea, kuna nguvu maalumu huwa nayo simba hasa ukirejea kwenye Status yao kuwa ni "mfalme wa nyika".
mara nyingi huwa na marafiki wengi kutokana na kuwa na ukarimu na uaminifu, hii ni kama vile jua linavyounganisha sayari nyingi na kuwa source ya nishati,
na hisia zao za ucheshi ndio huwafanya kuwa karibu zaidi na watu wengi sana.

Watu wote wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi zilizochangamka na zenye kuonyesha utajiri kama Dhahabu na Njano nzito au iliyoiva.

Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Nyeusi,
ambayo hiyo mara nyingi hufaa zaidi siku ya jumamosi
Bluu iliyoiva (Indigo) na Bluu ya Samawi (Ultramarine).
ambazo pia hufaa zaidi siku ya Alhamisi.

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni, Njano (Yellow) na Njano-Machungwa.
ambayo inamfaa zaidi akivaa siku yake ya bahati.

Kito (Jiwe) ni Amber,Ruby,Chrysolite, Yellow Diamond, Petrified Wood Garnet, Diamond, Jasper, Quartz na Onyx.
kila kito kina kazi maalum kwake. lakini kito kikuu kwake ni Ruby.

Madini yao ni Gold (Dhahabu). Manukato yao ni Miski (Musk) na Uvumba.

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Uimara na Kutokubadilika.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni Unyenyekevu.

Maadili yao ni Uwezo wa Uongozi, Kujiamini, Ukarimu, Ubunifu na Kupenda raha.

Matakwa yao ni Starehe, Haja ya Kung’ara mbele za watu na Kujikweza.

Tabia za kujiepusha nazo ni Kujisifu, Kiburi na Kuamrisha.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Mshale.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Nge na Ndoo.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Nge.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mashuke.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mshale.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ndoo.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mshale.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Punda na Kaa.

KIPAJI CHA SIMBA:
Simba wana kipaji cha ufunuo wa kiungu , wana uwezo wa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwaletea fedha pamoja na kwamba hazikai.Wanauwezo vilevile wa kuponya kwa kutumia mikono yao kuponya watu na wanakipaji cha asili cha uongozi. (inspired):

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Simba ni watu wanaopenda ufahari mkubwa na kutukuzwa. Wanapenda kutumia na wanataka waonekane kwamba wana hali nzuri, wanapenda sana kuheshimiwa.
watu hawa huwa ni wakali sana katika mapenzi na mara nyingi huwa hawadumu kwenye mapenzi kutokana na ukali wao na huwa ni watu wenye ghadhabu za mara kwa mara hasa akikosewa au akipingwa kidogo tu, kimapenzi
Jambo kubwa walilonalo ni uwezo wa kuvumbua mambo ambayo watu wengine hawajui.

Ni watu wakarimu lakini wajeuri na wanapenda sana kuonea watu. Wana hisia kali, ni wakali na wanakiburi.Tabia yao ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanaowapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya Simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu. Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza.

Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika inakua vigumu sana kuyatengeneza.

Tatizo lao kubwa ni kujisahau Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.

KAZI NA BIASHARA ZA SIMBA:
Wenye nyota hii wanatakiwa wafanye kazi zifuatazo; kazi za usimamizi, kama katika kampuni yake binafsi au katika mashirika au biashara, kazi za michezo au uongozi wa michezo.Wanatakiwa wafanye kazi za usonara au kazi za kuuza au kutengeneza mavazi ya mitindo.Vilevile wanatakiwa wafanye kazi za uigizaji au uendeshaji sinema au kazi zozote zinazohusika na masuala ya vijana.Kazi yao nyingine ni ya ualimu katika taasisi, shule au vyuo vya ualimu.

MAVAZI NA MITINDO:
Simba mitindo yao iwe ya kifalme, Kitajiri na inayoashiria nguvu na mamlaka, Kitambaa kiwe cha hariri inayongaa au velvet au kilicho tariziwa, Rangi iwe ya Dhahabu. Mavazi yaambatane na Vito vya dhahabu, Wanawake wapendelee kuvaa magauni ya kutokea usiku yawe ya dhahabu au rangi ya machungwa

MAGONJWA YA SIMBA:
Nyota hii inatawala moyo, sehemu ya juu ya mgongo na bandama.Vilevile inatawala uti wa mgongo na mshipa mkubwa wa damu.Matatizo yao makubwa kiafya yanahusiana na maradhi ya kuumwa sehemu ya juu ya mgongo.Maradhi yanayotokana na damu kama shinikizo la damu la juu na chini na maradhi ya moyo.Vilevile wanaugua maradhi ya homa ya uti wa mgongo.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SIMBA:
Wenye nyota hii wanatakiwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, machungwa, maboga, vitu vichachu kama ndimu au malimao na wapende sana kula nyama za ng'ombe, mbuzi na kondoo. Simba wanatakiwa wakaishi au watembelee nchi zifuatazo ambazo zinatawaliwa na nyota yao. Nchi hizo ni Italia na Morocco na miji ni Bombay (India) na Roma (Italia)

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Simba ni Dhahabu. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Peridot au Ruby
Mafusho ya Simba ni Sandarusi unachoma siku ya Jumapili kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:

Funguo ya simba ni "nita" anaposema atapata au atafanya basi kitu hicho hukipata,

NYOTA YA MASHUKE: VIRGO

stock-vector-light-symbol-of-women-to-virgo-of-zodiac-and-horoscope-concept-vector-art-and-illustration-531614686.jpg

Hii ni nyota ya sita kwenye mlolongo wa nyota 12 na ni ya watu waliozaliwa kati ya Tarehe 22 Agosti hadi 22 Septemba au wenye majina yalio anza na herufi F au P au T au R.

Asili yao ni Udongo.
Siku yake nzuri katika wiki ni Jumatano.
Namba yao ya bahati ni 5.Sayari yao ni Mercury (Attwarid).

Malaika wake anaitwa Raphael au Mikyaail
Jini anayetawala siku ya Jumatano anaitwa, Barkaan au Ophiel,

Rangi zao ni Rangi ya udongo, Njano na Rangi ya machungwa. Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake nyumba zao au magari yao rangi Nyeupe au rangi ambazo siyo nzito au zenye kuonekana sana.
Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi Bluu.

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Kijani kibichi.
Kito (Jiwe) ni Cuprite, Diamond, Sugilite, Moss Agate, Quartz, Peridot,

Madini yao ni Quicksilver (Zebaki).
Manukato yao ni ya Mrujuani (Lavender) na Lilaki (Lilac).

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni wanakuwa na uwezo wa kubadilika badilika.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo kuangalia mambo kwa mtizamo mkubwa zaidi.

Maadili yao ni Uchambuzi, Wepesi wa Akili, Uwezo wa kuwa makini na Uwezo wa Kuponya.

Matakwa yao ni kuwa wenye uwezo wa Kutumika.

Tabia za kujiepusha nazo ni ukosoaji usiokuwa na malengo mazuri.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Ng’ombe na Mbuzi.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mshale na Samaki.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mapacha.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mshale.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mizani.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mbuzi.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Samaki.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mbuzi.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba.

KIPAJI CHA MASHUKE:
Mashuke wana kipaji cha kuhisi, kufikiri, kutambua tatizo au ugonjwa au kupata picha ya wazi akilini ya kutambua jambo lolote. Vilevile wana uwezo wa kuponya na wana uwezo wa kusoma michoro yeyote.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Mashuke ni watu ambao wanaopenda kusoma. Wana akili nzuri ambayo inatumika zaidi katika kupambanua njia ya asili ya mpangilio wa mambo. Kwa ujumla ni watu ambao wanapenda kufuata kanuni na kufanya mambo kwa usahihi kabisa. Ni waangalifu sana hasa katika mambo madogo madogo na wanapenda kushutumu hasa mambo yanapokwenda vibaya. Wanatabia ya kuchunguza mambo na kuhakikisha mpangilio unafuatwa kikamilifu. Wanajituma na kujishughulisha na wanapenda sana kufuata sheria au mpangilio maalum ulioainishwa.
Katika Mapenzi ni watu wenye aibu kwa undani lakini wanajiamini, wanapokuwa katika mapenzi hunawiri.

Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe. Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani.

Ni vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na Mashuke. Inawawia vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa. Kinachowasaidia ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua. Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.

Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi wake ili amshutumu. Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.

KAZI NA BIASHARA ZA MASHUKE:
Mashuke ni tegemezi, wenye bidii ya kazi na tabia ya kufanya kazi bila ya kuchoka. Wanapenda sana kazi zenye mpangilio na ambazo kila kitu kiko katika mpangilio maalum.Wanapenda kuwa huru katika kazi zao na kujitosheleza katika kila wanachokifanya, hufurahi kufanya kazi bila ya kusimamiwa.

Kazi zao ni zile zinazohusiana na uchapishaji, utangazaji, afya, udaktari, kazi za unesi, kazi za uongozi, elimu na kufundisha, biashara yoyote au kazi za ukatibu muhtasi.

MAVAZI NA MITINDO:
Mashuke wanatakiwa kuvaa Nguo zenye Mitindo ya kisanii, nguo ziwe Nyepesi na zilizonyooka Ziwe za Rangi ya Njano na Nyeupe. Kitambaa kiwe kama hariri, chepesi na chenye kumeremeta. Wake kwa waume wapendelee kuvaa Suti na ikiwezekana wasikose kuvaa Gloves

MAGONJWA YA MASHUKE:
Nyota hii inatawala utumbo, sehemu ya uvunguni mwa utumbo na neva zote zilizo chini ya kitovu.Kutokana na asili hiyo wale wenye nyota hii huwa wanapata sana matatizo ya maradhi ya ugonjwa wa tumbo au tumbo la uzazi au matatizo ya kizazi.Magonjwa ya mwili kushindwa kusaga chakula tumboni au magonjwa ya kujikunja utumbo na maambukizo ya utumbo.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MASHUKE:
Mashuke wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndio vinavyotawaliwa na nyota yao, kuku, rasiberi, karoti na uduvi. Ili kupata mafanikio ya kinyota wenye nyota ya Mashuke wanashauriwa watembelee au waishi katika nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; nchi hizo ni Austria na Norway na miji hiyo ni Jerusalem na Paris.

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mashuke ni Quicksilver (Mercury). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Green Sapphire.
Mafusho ya Mashuke ni Kashuu Muhlib (kachiri). unachoma siku ya Jumatano kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya mashuke ni "Nachambua" akisema anachambua au akilichambua sana akilini basi humfika


NYOTA YA MIZANI

2018-horoscope-Libra-897078.jpg


Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12,Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 23 september hadi 22 october au wenye majina yanayoanzia na R au T.
nyota hii Usawa wake ni Dume
Hali yake ni: Thabiti
Mizani ni nyota ya utendaji,ulaini wa mambo,yenye amani,kupenda uzuri na sifa njema,kidoplomasia na yenye kung'ara katika jamii.

Sayari yako ni VENUS (ZUHURA).
sayari hii wengine huitambua kama kiumbe wa mapenzi au mtawala mapenzi:
kinyota hujulikana kama sayari inayosimamia maelewano,amani,radhi ya uraia na kukimbilia mambo yakijamii,sanaa na kupamba, lakini pia ni yenye kujishughulisha na mapenzi ya starehe.

alama yake ni mizani: ambayo humaanisha usawa,msawazo,mpangilio na haki.

PICHA YAKE:
Picha yake au muhuri wake ni mizani ambayo huwakilisha kipimo sawa cha nyota hii, hii mizani ni alama ya kale ya ki Egypt ambayo ilikuwa ikiwakilisha kipimo cha Jua, ambayo ilikuwa inawakilisha pia kipimo cha dunia mbili yani katika maana za kialama inasema kuwa mwezi kama vile umelalia mistari miwili iliyopo sawa, mstari wa juu ukiwa na maana ya hisia na wa chini ukiwa na maana ki mwenza

Siku yako ya Bahati ni Ijumaa.

Namba ya Bahati ni 6 na 9.

Malaika wa sayari na nyota hii huitwa Anyail na Jini wa nyota hii huwa ni Jini wa sayari ya Venus pia anaitwa Zawbat na shetani wake anaitwa Succubi(jini mahaba)


Manukato ya Mizani:
Kama ilivyo kwa maua yao basi wenye nyota hii wapendelee zaidi kupaka marashi yaliyochanganyika na mauwaridi ndani yake na yenye harufu isiyokera

Rangi za Bahati:
Rangi za bahati kwa wenye nyota hii ni Kijani isiyoiva. Blue pamoja na lavender rangi hizi huwafaa zaidi kwa sababu huwasilisha mapenzi,furaha na urafiki ambapo pia watu hawa hupenda sana kujihusisha na mapenzi na yanayohusu hayo.

Asili ya nyota hii ni UPEPO.

KIPAJI CHA MIZANI
(Extra Sensory Perception)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa. na kuweza kumjua mtu vizuri kabla ya yeye kuanza kujielezea.

TABIA ZA MIZANI:
Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.
Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina
matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana
kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri

MAMBO MENGINE:

wenye nyota hii wanatakiwa kuwa waangalifu sana kwenye mapenzi hasa kipindi cha kuoa kinapofika kwa maana ndio maamuzi ya mwisho ya maisha yao kinyota, wenye nyota hii ni rahisi kupendeka na wenye ulaini wa mapenzi na ni watu wa kuvutia na wenye kuvutia kimaongezi kwa sababu wana kipaji cha kimvutia mtu kimaelezo na kumfanya ajihisi raha kuzungumza nao, wenye nyota hii ni watu wenye Tabasamu laini na wenye hisia za kimapenzi wakati mwingi na pia huonekana kama watu wa ajabu sana duniani,wao huzaliwa wakiwa na asili ya kujali wengine. Nyumba zao utakuta zimepambwa vizuri kwa maua kupendeza na mapambo ya thamani,nguo na manukato pia vinywaji huwa havikatiki ni nyota yenye kujipenda zaidi wao hufurahia kila kitu ambacho pesa inaweza kununua,
Nyota hii ni nyota ya mwenza hupenda sana kutembea na mtu na hawapendi kutembea peke yao hata barabarani unless imewalazimu.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota inayomfaa zaidi kindowa ni nyota ya punda

Nyota za watu ambao “Wanaelewana” nao ni nyota za Mapacha na Mshale.

Nyota za watu ambao “Hawaelewani” nao ni nyota za Ng'ombe, Mashuke na Mbuzi.

Nyota inayomsaidia “Kikazi” ni nyota ya Mapacha

Nyota inayomsaidia “Kipesa” ni nyota ya Mshale

Nyota inayomsaidia katika “Ubunifu” ni nyota ya Mapacha.

Nyota bora ya “Kujifurahisha” ni nyota ya Punda

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya “Kidini na kiroho” ni Nyota za Mshale na Samaki.

MITIZAMO YA WATU:
Wenye nyota hii watu wakiwaangalia mara nyingi, huwaona kuwa ni watu wa muhimu sana hata katika familia au vikao vya ukoo mtu huyu huwa hasahauliki kwa sababu tu ya kuyatanua mawazo ya watu walioyatoa na lakini pia mara nyingine huonekana ni watu wanaoleta vurugu na ujuaji kwenye mijadala au wanakuwa ni watu wenye mitizamo tofauti na wengine na kuna muda huonekana wapumbavu kwa tabia yao ya kung'ang'ania kitu wanavyoelewa wao ndio na watu wengine waelewe hivyo hivyo kwa wengine muonekano wake wote huwaonyesha kuwa ni mtu asiye na maana kwa muonekano anaokuwa anajiweka hili huwa linamuumiza pia

MAGONJWA YA MIZANI
Wenye nyota hii hussumbuliwa sana na magonjwa ya mgongo hasa karibu na makalio ni watu wenye kusumbuka na figo pia na mgongo wa chini hasa kwenye maungio ya makalio na maambukizi ya figo huwa ni magonjwa yanapendelea sana nyota hii.

MADINI YA MIZANI:
Madini ya wenye nyota hii ni Copper.

WANYAMA:
Wanyama wa nyota hii ni Nyoka na Mijuzi

VITO:
Wenye nyota hii wanatakiwa wavae kito cha Opal kwa maana kito hiki huwaletea mafanikio kipesa au kipato na humuondoshea mwenye nyota hiyo wivu na tamaa na huwaletea uelewa na ufahamu wa mambo yote wanayohitajia kuyajua.

MAFUSHO:
Mafusho ya mizani ni Ubani Mashtaka:
una rangi ya kijivu na ni mgumu pia unapukutika unga mweupe.

KAZI NA BIASHARA:
Wenye nyota hii kazi nzuri kwao huwa ni kazi za uhusiano wa jamii, Ushauri wa Ndoa, Biashara ya Sanaa, Ushauri wa Mambo ya Urembo, Uanasheria, Uhakimu pia biashara za kuziba pancha na kujaza upepo au kupamba maharusi zinawafaa zaidi
Kazini wenye nyota hii huwa ni washiriki wazuri na wenye upendo wa wafanyakazi wenzao na pia wenye nyota hii ni wajanja pia katika mbinu za kazi za ushirikiano nao huusishwa sana kwenye kazi za pamoja.

MAUA:
Maua yanayofaa katika nyota hii ni Uwaridi kwa maana nyota hii hutawala zaidi kwenye mapenzi

UHUSIANO WA KIMAPENZI
(Punda na Mizani)
Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

HATARI ZA MIZANI:
Nyota hii wao ni watu wa kupenda kuchochea hisia mbaya kutoka kwa wengine inapokuja kwenye suala la mapenzi na wao hujiweka rahisi sana katika kutamka maneno ya mapenzi kwa watu na kujieleza kimapenzi kirahisi yaani kujirahisi kimapenzi ni tabia walionayo Mizani na mapenzi yao huwa ya hasira na wenye kuvunja moyo wengine na ni rahisi sana wao kukusaliti na kutokukuamini. hivyo jiweke makini katika swala la mapenzi wewe na uwapendao.

FUNGUO:
Funguo ya mizani ni "ninalinganisha" akijilinganisha na kitu au mtu huyo basi humpata akifanya hivyo akilini kwake

NYOTA YA NG'E

scorpio-zodiac-signhoroscope-circlespace-dark-vector-11977985.jpg


Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Oktoba na 22 Novemba au wenye majina yaliyoanza na herufi H au N au Y au S

Siku yao ya Bahati ni Jumanne, Namba yao ya bahati ni 9.Asili yao ni Maji.
Sayari yao ni Pluto.

Malaika anayetawala nyota hii anaitwa Samael au Israeel na Jini wa siku hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar au Phaleg

Rangi zao ni Urujuani nyekundu. Nge wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi ya Kijani.

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Bluu.

Kito (Jiwe) ni Bloodstone, Malachite, Topaz. Ruby,Rhodochrosite, Kunzite, Moldavite, Opal, Diamond, Selenite, Quartz
Madini yao ni Chuma, Radiamu (Radium) na Chuma cha pua (Steel).

Manukato yao ni ya Msandali (Sandalwood), Tikiti maji (Watermelon), Nazi (Coconut), Mcheri (Cherry Blossom).

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Kuwa Imara.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni uwezo wa kuangalia na kujua mambo kwa upana zaidi.

Maadili yao ni Utiifu, Kuwa Imara, Kuazimia jambo, Ujasiri na Undani.

Matakwa yao ni Kuingilia undani wa kitu na kukibadilisha.

Tabia za kujiepusha nazo ni Wivu, Kulipiza kisasi, Kutokubali Kusamehe, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa mbishi, mng’ang’anizi.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Samaki.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Ndoo.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Simba.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ndoo.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mshale.

Nyota inayomsaidia katika Ubunifu ni nyota ya Samaki.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota bora ya Kujifurahisha ni nyota ya Samaki.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Kaa na Mizani.

KIPAJI CHA NGE:
Nge wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji. Mystical

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni wenye uelewa mkubwa, majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.
Wana tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.
Ni wasiri na wanaopenda kufanya mambo yao kwa siri sana. Kama ilivyo alama ya nyota yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.

Ni wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Nge vile vile wanaweza kujidhuru wao wenyewe. Mambo yanapowawia magumu.
Wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.

Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.

Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.

KAZI NA BIASHARA ZA NGE:
Nge ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni waerevu na wenye kung’amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.

Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono au biashara zinazoendana na mambo hayo.

MAVAZI NA MITINDO:
Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong’ara, zenye kuonekana na maridadi, zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja. Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta. Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali

MAGONJWA YA NGE:
Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi (cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).

Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono.
Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya kike na mabusha.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NGE:
Nge wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.

Miji hiyo ni Liverpool (Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Nge ni Chuma. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.

Mafusho ya Nge ni Qist. unachoma siku ya Jumanne kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.


FUNGUO:

Funguo za nyota hii ni "natamani" wao wakitamani kitu kikawa kaa rohoni basi hukipata


NYOTA YA MSHALE:
1145582

Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Novemba na 20 Disemba au wenye majina yalio anza na herufi I au D au P au U.

Asili yao ni Moto.Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Namba yao ya Bahati ni 5 au 7
Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).

Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeel na Jini anayetawala alkhamisi anaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor

Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea.
Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Njano na Njano-machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyeusi na Bluu iliyoiva.

Kito (Jiwe) ni Feruzi (Turquoise) na Kito chekundu (Carbuncle).Madini yao ni Bati.

Manukato yao ni Yasmini (Jasmine), Manemane (Myrrh).

MAMBO MUHIMU:-

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa Kuongoza, Kuratibu, Kuandaa, Kupanga na Kusikiliza kwa makini.

Maadili yao ni Ukweli, Kuona mbali, Ukarimu na Kuwa na uwezo wa kusikiliza mawazo ya wenzake japokuwa siyo lazima akubaliane nayo.

Matakwa yao ni Kupanuka kimawazo.

Tabia za kujiepusha nazo ni Kutegemea mambo kuwa yatakuwa mazuri siku zote, Kutia chumvi mambo na Kuzidisha Ukarimu kwa kutegemea hela za watu wengine.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Simba.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Samaki.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mashuke.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Samaki.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mbuzi.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Punda.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mapacha.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Punda.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba na Nge.

KIPAJI CHA MSHALE:
Mshale wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.(Prophetic)

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe kama wao.
Hawapendi mambo nusunusu.
Ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.
Mshale ni watulivu, waaminifu na wanapenda uadilifu,.hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake, mradi jambo hilo liwe la kweli.

Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe, huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.

Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.

Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali, inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.

KAZI NA BIASHARA ZA MSHALE:
Mshale ni waaminifu wanaopenda sana mafanikio, wako tayari wakati wowote katika kazi. Kutokana na hili wana bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.
Wenye nyota hii ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Wanawaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.

MAVAZI NA MITINDO:
Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha kama koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi kama maua au nakshi nakshi.
Rangi ya nguo zao iwe ya Zambarau au rangi ya Hudhurungi iliyochangamka au rangi ya blue.
Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda, na viatu viwe vya buti. Wanawake wapendelee kuvaa sketi.

MAGONJWA YA MSHALE:
Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao.

Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.

Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini (Liver Disorder) kupooza kwa miguu (paralysisi of limbs) na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MSHALE:
Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kunazi za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera.
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
Nchi hizo ni USA na SPAIN na miji ni Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mshale ni Bati. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Yakuti ya njano au Lapis Lazuli

MAFUSHO:
Mafusho ya Mshale ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya nyota ya mshale ni "nalenga" yeye akilenga kitu basi huwa hakosi hata akikipania


NYOTA YA MBUZI:


capricorn-zodiac-symbol-daniel-eskridge.jpg


Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Disemba na 19 Januari au wenye majina yalio anza na herufi J au V au K.

Asili yao ni Udongo.Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8
Sayari yao ni Saturn (Zohal).

Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron.

Rangi zao ni Nyeusi na Bluu iliyoiva. Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi (Black).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Hudhurungi (Puce) na Fedha (Silver).
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Samawi (Ultramarine).

Kito (Jiwe) ni Black Onyx. Madini yao ni Risasi (Lead).

Manukato yao ni yale yatokanayo na Msonobari (Pine), Maua yanayofanana na ya Jamii ya Choroko, Njegere au Dengu (Sweet pea) na Magnolia.

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Uongozi.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye Uchangamfu na Furaha.

Maadili yao ni Uvumilivu, Utiifu, Ustaamilivu, Kuratibu, Kuandaa na Uwezo wa kuona mbali.
Matakwa yao ni Kutawala, Kusimamia na Kuongoza.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutokutegemea kuwa mambo mabaya yatatokea, Kuwa na masikitiko, Kutokupenda mabadiliko na Kupenda vitu na mali kupita kiasi.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Ng’ombe na Mashuke.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Punda, Kaa na Mizani.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mizani.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Punda.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Ndoo.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Kaa.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mashuke na Mshale.

KIPAJI CHA MBUZI:
Mbuzi wana kipaji cha kuchambua mambo kidogo kidogo au kufuatilia kitu bila watu kujua na kupata ufumbuzi wa uhakika mwishoni.Gradual

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Mbuzi wanapenda kuwajibika, ni wenye bidii ya kazi, katika kazi yeyote watakayofanya hata kama ikiwa ni ya kipuuzi.
Ni viumbe waaminifu sana, watu wastahamilivu na wenye kuweza kuvumilia matatizo yeyote.

Kwa upande mwingine ni watu wenye tamaa kubwa ya kimaisha na kimaendeleo, na kwa sababu ya kutekeleza malengo yao basi huwa wanakuwa wabinafsi na wenye uroho na uchu.

Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao, lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.

Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.
Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.

Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.

KAZI NA BIASHARA ZA MBUZI:
Mbuzi kitu muhimu katika maisha yake ni kazi na maisha mazuri na yanayoeleweka ambayo yako katika mpangilio wanaoutaka wao.
Ni watu ambao wanazingatia sana muda wa maisha na wana mpangilio maalum kwamba katika umri fulani awe amepata nini au awe na fedha kiasi gani.

Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo.Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno.

MAVAZI NA MITINDO:
Mbuzi wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya kijivu au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi.
Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikononi.

MAGONJWA YA MBUZI:
Nyota hii inatawala Mifupa, Magoti na Ngozi.Matatizo yao makubwa ya kiafya huwa yanasababishwa na muda mrefu ambao wanafanya kazi au kujishughulisha. Hii ni kwa sababu hawamwamini mtu mwingine afanye shughuli zao ambazo zina mipangilio ya muda mrefu,nguvu nyingi, na akili hutumika.

Shughuli zao nyingi za mizunguko na kufikiria huwaletea maradhi kama Baridi Yabisi (rheumatism).
Maradhi yao mengine makubwa ni ugonjwa wa Ngozi, matatizo ya Magoti na maradhi ya mifupa.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MBUZI:
Mbuzi wanashauriwa wapende kula vyakula au matunda yafuatayo.ambayo ndio yanatawaliwa na nyota yao.Wapende sana vyakula vya Nazi na Nyama yeyote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba (Shellfish).

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa watu wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee miji au nchi zifuatazo ambayo inatawaliwa na nyota ya Mbuzi.
Miji hiyo ni Brussels (Ubelgiji) na Oxford (Uingereza) au nchi za Mexico na India

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mbuzi ni Risasi (Lead). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni kama vilivyoonyeshwa katika picha hapa chini.
Mafusho ya Mbuzi ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya mbuzi ni "natumia" basi yeye pale ambapo huwa anatumia vitu hovyo basi huzidi kupata vingine

NYOTA YA NDOO:

2018-horoscope-Aquarius-897096.jpg

Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 20 Januari na Februari 18 au wenye majina yalio anza na herufi K au W au G au S.

Asili yao ni Upepo.Sayari yao ni Uranus. Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8

Malaika wake anaitwa Cassiel au Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu au Aratron.

Rangi zao ni Bluu, Kijivu na Samawi ya Bluu (Ultramarine blue). Wenye nyota ya Ndoo wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi zilizotulia kama Bluu au Kijivu.

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Dhahabu na Machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Aqua.
Kito (Jiwe) ni Lulu Nyeusi, Obsidian, Opali (Opal) na Johari (Sapphire).
Madini yao ni Risasi (Lead).
Manukato yao ni yale yatokanayo na Mgadenia (Gardenia) na Azalea.
MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya nyota hii ni Uimara na Kutoyumba.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa Wachangamfu na Wenye hisia.

Maadili yao ni Uwezo mkubwa wa Kiakili, Uwezo wa Kuwasiliana, na Kuelewa mambo ya muhimu, Kupenda mambo Mapya.

Matakwa yao ni Kujua na Kuleta mambo mapya.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutojali, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa na mawazo yasiyobadilika.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Mapacha na Mizani.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Nge.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Nge.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Samaki.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Mapacha.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Simba.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Mapacha.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mizani na Mbuzi.

Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Jumamosi.

KIPAJI CHA NDOO:

Ndoo wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote, Sudden Revelation.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.

Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.

Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.
Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.

Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.

Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.

Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu ambao husema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.

Katika ngono, kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.

KAZI NA BIASHARA ZA NDOO:
Ndoo ni watu wenye akili nyingi na wenye malengo maalum katika shughuli fulani. Ni wawekezaji asili na wana uwezo wa kuwabadilisha watu tabia zao kutoka mbaya kuwa nzuri.

Kwa uhakika mawazo yao saa zote yanafanya kazi. Ni watu ambao muda wote wanafikiri njia mpya na za uhakika za kutekeleza wajibu wao na kikazi.

Kazi zao wanazifanya kwa upole na uhakika, pamoja na kwamba wanafanya kazi kwa bidii mara nyingi huwa wanaonekana hawajafanya kitu au sifa huenda kwa watu wengine.

Watu wa Ndoo ni wenye mawazo ya ubunifu na wenye kugundua njia mpya na zenye uhakika katika kazi.
Kazi zinazowafaa ni za uhandisi wa umeme, kompyuta, utafiti wa Sayansi, utabiri, huduma za jamii na utafiti wa mambo ya kale.

MAVAZI NA MITINDO:
Ndoo wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya Kijivu, au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito. Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi. Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikono.

MAGONJWA YA NDOO:
Nyota hii inatawala kifundo na ugoko. Wenye nyota hii wana mawazo mapana ya kufanya mabadiliko ya Dunia na hii inawasababisha wajisahau hasa katika afya zao na mara kwa mara hupata matatizo ya kuugua.

Kutokana na ubishi wao mara nyingi wanakuwa wabishi kupokea ushauri kuhusiana na hali zao za kiafya.
Matatizo yao makubwa yanasababishwa na kuchoka kwa misuli kutokana na kazi nyingi, kwa kawaida ni wagonjwa wabishi wasiopenda ushauri.

Wanapofanya mazoezi wanashaurwa wasiwe na hasira kwani hiyo inawafanya wajiumize au wapate ajali ndogo ndogo hasa sehemu za miguu, ugoko, vifundo na uvimbe katika sehemu hizo.
Vile vile matatizo yao mengine ya kiafya ni mzunguko wa damu na mishipa ya miguu.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NDOO:
Ndoo wanashauriwa wepende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota zao, vyakula vya nazi na nyama aina zote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki Gamba.

Ili kupata mafaniko ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao. Nchi hizo ni Sweden na Zimbabwe na Miji ni Humburg (Ujerumani) na Leningrad (Urusi).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Ndoo ni Uranium ikiwa ngumu kupata tumia Lead (risasi). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni amethyst au Onyx.
Mafusho ya Ndoo ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:


Funguo ya wenye nyota ya ndoo huwa ni "najua" basi yeye akijifanya mjuaji wa mambo huwa anafanikiwa kwa mengi

NYOTA YA SAMAKI:

pisces-zodiac-symbol-daniel-eskridge.jpg


Hii ni nyota ya 12 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 19 Februari na Machi 20 au wenye majina yalio anza na herufi L na X au D na C au J.

Asili yao ni Maji.Sayari yao ni Neptune.Siku yao ya Bahati ni Alhamisi, Namba yao ya Bahati ni 8,

Malaika wake anaitwa Sachiel au Israfeell na Jini anayetawala Jumapili aanaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor

Rangi zao ni Bluu iliyochanganyika na Kijani na Aqua. Rangi zinazowapa uwezo wa Mapenzi, Mahaba na Furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Udongo, Njano na Njano-machungwa.

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyekundu. Wenye nyota ya Samaki wanatakiwa wapake nyumba zao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi ambayo haijakoza ya Bluu au Kijani au Urujuani (violet).

Kito (Jiwe) ni Almasi Nyeupe. Madini yao ni Bati. Manukato yao ni Yungiyungi (Lotus).

MAMBO MUHIMU:-
Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa kushikilia muundo na hali.

Maadili yao ni Uwezo mkubwa wa Kuhisi, Kujitoa Mhanga, Kuishi na Kutenda kwa ajili ya Manufaa ya Wengine, Uungwana, Utu, Ubinadamu, na Ubingwa wa Maono.

Matakwa yao ni Mwanga wa Kiroho, Uhuru na Haki ya kujiamulia la kufanya.

Tabia za kujiepusha nazo ni Tabia ya Ukwepaji wa Matatizo na mambo, Kununa, Kususa, Kunung’unika pasipokuwa na sababu ya Msingi, na Kuwa na Marafiki Wabaya.

USHIRIKIANE NA NANI?
Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Nge.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Mshale.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mshale.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Mapacha.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Punda.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Kaa.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mashuke.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Kaa.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Nge na Ndoo.

Siku yake nzuri katika wiki ni siku ya Alhamisi.

KIPAJI CHA SAMAKI:
Samaki wana wana kipaji cha kufikiria jambo na kuliunda na likawa vile walivyotaka wao visionary.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Watu wenye nyota ya Samaki ni wenye huruma, wapole na wenye moyo mzuri, hawawezi kukubali kumuona binaadamu mwingine akipata taabu au uchungu. Kwa hakika ni watu ambao wana hisia kali kwa wengine, hawajipendelei na wako tayari wakati wowote kujitoa mhanga ili watu wanufaike, mapenzi yao au huruma kwa binaadamu wengine hayana masharti yeyote.

Nafsi zao zimegawanyika katika nafsi ndogo ndogo kama vile muathiriwa mwenye kujitoa mhanga, mwokozi, na mkombozi.
Hayo yote yaliyotajwa wanaweza kuyatekeleza inapohitajiwa na akishatumbukia katika moja ya mambo hayo huwezi kumtoa.

Kwa ujumla nafsi za Samaki siyo za kidunia, ni watu wabunifu na wenye ndoto za kufikiri mambo ya baadaye na katika maisha yao, wanaona raha sana kuwa na mawazo ambayo yatawaepusha na ugumu wa maisha.

Ikiwa wamekwama katika jambo lolote basi wataitafuta faraja au watajituliza kwa ulimwengu wao wa mawazo. Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.

Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Wana hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.

Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Samaki huyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.

Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii.

Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo.

KAZI NA BIASHARA ZA SAMAKI:
Kugundua muelekeo wa kimaisha kwa Samaki wakati mwingine huwa ni matatizo.
Tabia yao ya kushughulikia sana binaadamu wengine huwafanya wasiwe na muelekeo.

Wanatakiwa wafanye kazi ambazo zinazohusiana na kusaidia watu. Kipaji cha kutafsiri mambo, huwasaidia vile vile kufanya kazi za sanaa kama vile kupiga picha na kazi za muziki au maigizo.

Kazi zingine zinazowafaa ni za kuhudumia wagonjwa, kucheza shoo, uaskari wa majini (Navy) kazi za dini au kazi za kutoa ushauri nasaha (Counselling).

MAVAZI NA MITINDO:
Samaki wanatakiwa wavae nguo za michezo kama vile fulana au za kiasili na zilizoongezwa madoido na vimbwanga vingi.Nguo zao ziwe za rangi ya Zambarau au Kahawia iliyochangamka na rangi ya bluu.Kitambaa kiwe cha sufi (tweed) Wanawake wapendelee sana kuvaa sketi, ikiambatana na mikanda na viatu vyao viwe vya buti.

MAGONJWA YA SAMAKI:
Nyota hii inatawala nyayo na vidole vya miguu. Matatizo yao ya kiafya yanakuja pale wanaposhindwa kutekeleza ndoto zao au mipangilio yao kimaisha au wanapokorofishana na wapenzi wao.
Wanapoathirika na hayo yaliyotajwa hukimbilia kwenye ulevi na utumiaji vidonge uliokithiri.

Tatizo lingine ni maradhi ya nyayo za miguu, uvimbe unaotokana na baridi kali hasa katika vidole vya miguu.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA SAMAKI:
Samaki wanashauriwa wapende kula matunda au vyakula vifuatavyo.
Matunda ya Kunazi, Nyama mwitu kama Swala, Nyati na kadhalika.Vile vile wapendelee kula Maboga.

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao.

Nchi hizo ni Tonga na Tanzania na miji ni Alexandria (Misri) na Seville (Ufaransa).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Samaki ni Platnum ikiwa ngumu kupata tumia Bati (Tin). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Aquamarine
Mafusho ya Samaki ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya samaki ni "Naamini" wao pale wanapokua na imani juu ya jambo basi hufanikiwa nalo mwisho wa siku,

Hizo ndizo nyota 12 na maelekezo yake mengi panapo majaliwa taongeza maelekezo mengine
wakuu ifahamike nyota hizi hazihisiani na dini yoyote na kama mtu anadai dini na nyota hizi ni vitu haviendani.

FAIDA:

Habari WanaJamiiForums?
Moja kwa moja twende kwenye mada bila kupoteza muda.
Ipo hivi, kuna wataalam na wajuvi wa masuala ya nyota wanasema unaweza kujua nyota yako kwa kutumia njia takribani tatu ambazo ni;

1.TAREHE NA MWEZI WAKO WA KUZALIWA.

2.JINA LAKO NA MAMA YAKO HALAFU UNAGAWANYA KWA 12.

3.HERUFI YAKO YA KWANZA YA JINA LAKO.

Kwa maelezo yao Wataalam na Wajuvi wa masuala haya wanasema njia hizo zilizotajwa hapo juu ndio hitumika haswa kwa mtu kuijua nyota yake.

Lakini cha kushangaza kila njia moja kati ya hizo tatu ukitumia inakupa jibu la tofauti sijajua ukweli ni upi?

Mfano:
a)Mimi nikitumia njia ya kwanza ambayo ni tarehe na mwezi niliozaliwa napata jibu ni nyota ya SIMBA.

b)Nikitumia njia ya pili ambayo nikijumlisha jina langu na mama yangu jibu ni nyota ya NGE.

c)Nikitumia njia ya tatu ambayo ni herufi ya mwanzo ya jina langu jibu linakuja nyota ya PUNDA.

Naomba kujua ukweli kwa yeyote mwenye Utaalamu na Ujuzi wa mambo ya Nyota anifafanulie vizuri ni ipi haswa njia nzuri ya kufuata ili kujua nyota yangu?
Na pia kama kuna sehemu nimekosea naomba kurekebishwa tafadhali. Ahsanteni
Naomba kuwasilisha.

Habari mkuu nina elimu pana sana ya hizi nyota ndio umeona kuna mkuu hapo kaamua kunitag ipo hivi hapo kwenye hizo nyota ni moja tu ndio umekosea kuijumlisha na hii ukitembea nayo hivyo basi utakuwa umejifungamanisha na kufifiza nyota yako hapo kwenye herufi ya jina na tarehe ya kuzaliwa upo sawa ;lakini kwenye jina lako na la mama hesabu zako hazipo sawa hapo inatakiwa kubaki 9 na sio nane yaani hapo wewe ni Mshale na sio Ng'e na ukijifananisha na ng'e kidogo tu walau kwa siku 7 basi teyari utakuwa umeshakumbwa na nuksi au mikosi.
Rejea hesabu zako vema au toa majina nikusaidie hapo lazima ibaki 9 sio 8
na kila nyota hapo zina sehemu yake ya kutizamiwa wewe kifupi hapo ni kundu la kwanza huwa Mwili, la pili Roho, la tatu ni Akili
kwa maelezo zaidi ya nyota pitia thread yangu hii


Rakims

Habari mkuu nina elimu pana sana ya hizi nyota ndio umeona kuna mkuu hapo kaamua kunitag ipo hivi hapo kwenye hizo nyota ni moja tu ndio umekosea kuijumlisha na hii ukitembea nayo hivyo basi utakuwa umejifungamanisha na kufifiza nyota yako hapo kwenye herufi ya jina na tarehe ya kuzaliwa upo sawa ;lakini kwenye jina lako na la mama hesabu zako hazipo sawa hapo inatakiwa kubaki 9 na sio nane yaani hapo wewe ni Mshale na sio Ng'e na ukijifananisha na ng'e kidogo tu walau kwa siku 7 basi teyari utakuwa umeshakumbwa na nuksi au mikosi.
Rejea hesabu zako vema au toa majina nikusaidie hapo lazima ibaki 9 sio 8
na kila nyota hapo zina sehemu yake ya kutizamiwa wewe kifupi hapo ni kundu la kwanza huwa Mwili, la pili Roho, la tatu ni Akili
kwa maelezo zaidi ya nyota pitia thread yangu hii

www.jamiiforums.com

Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako - JamiiForums
IJUE NYOTA YAKO Nyota ni Elimu ya Sayansi ambayo inatumika Dunia nzima. Kila mtu katika Dunia akitaka asitake, aamini au asiamini atakuwa amezaliwa katika mojawapo ya nyota 12 zilizopo. Pia elewa ya kwamba ndugu yangu nyota yako moja imegawanyika katika makundi manne yaani: 1: Nyota...
www.jamiiforums.com
www.jamiiforums.com
Rakims
Click to expand...
Asante mkuuu,
Nilikuwa nakusubiri kwa hamu sana nina imani unayajua na una elimu haswa ya masuala haya.
Naomba leo unimalizie kiu yangu ya kutaka kufahamu zaidi.
Hapo kwenye maelezo yako umeniambia nimepatia kwenye herufi ya mwanzo yaani A= PUNDA na tarehe au siku yaani 08/08 =SIMBA
Then umesema kuwa nimejumlisha vibaya ndio maana nimepata namba 8 ambayo ni NGE, ukasema kuwa nijumlishe vizuri jibu litakuja 9 ambayo ni MSHALE.

SWALI;
Inakuwaje nipate nyota za aina tatu tofauti yaani SIMBA, NGE na PUNDA?
Je, nyota yangu halisi ya kuifuata ni ipi hapo? Au nifuate zote? Na inawezekanaje kufuata nyota zote tatu kwa wakati mmoja?

Naomba mwongozo wako nijue nyota yangu ni ipi hapo? SIMBA, NGE au PUNDA? Na niifuate ipi?

Nimefanya hesabu zangu nimepata namba 9 ambayo ni MSHALE

Nimekuelewa vizuri sana mkuu,
Hakika wewe ni kisima cha elimu hii mkuu Allah akuzidishie inshallah!

Ila bado nna swali la ziada kama ifuatavyo;

1.Sasa ikatokea mtu kaniuliza mimi ni nyota gani nimjibu vipi? Nimwambie mimi ni MOTO au?

2.Nijuavyo kila nyota ina siku yake ya bahati,mafusho,kito,madini, kazi, rangi, namba n.k
Sasa kwa mimi ambae nyota yangu ya asili ni MOTO inakuaje kwenye kufuata hivyo vitu?
Swali nzuri mkuu, hapo cha kufanya jijue kabisa kuwa unautawala wa nyota yenye tabia moja katika nyuso tatu hivyo ukisoma nyota zote hizo na kuzifuatilia vema basi utafanikiwa kirahisi sana ila uelewe jambo muhimu ni kuwa kila moja ina nafasi yake hapo,
Ipo iliyochomoza wakati unazaliwa ambayo ni punda
ipo iliyochomoza katika msimu wa kuzaliwa ambayo ni Simba
na ipo ambayo ilichomozewa na mwezi ambayo ni Mshale

Sasa ili uweze kufanikisha mambo yako katika matabaka hayo matatu elewa kuwa moja inatawala mwili wako nyingine roho yako na nyingine akili yako hivyo ukitaka kufanikisha lolote fuata zaidi kulingana na sehemu iliyopo

Mfumo wako upo hivi:

AKILI = PUNDA
MWILI= SIMBA
ROHO= MSHALE

Hivyo basi mfano unataka kuoa au kupata mafanikio ya ndoa jua kabisa kindowa utatakiwa ujione ni MSHALE au ukitaka kusafisha nyota yako kiroho basi utatakiwa kutumia MSHALE ambayo ni utasafishwa nyota yako kwa maombi yaliyobase kwenye utawala wa dini tu. huwezi kufanikisha jambo la kiroho ikiwa utaenda kinyume na hivyo tofauti na watu wenye nyota ya roho kama MBUZI hawa hawafanikishi jambo la kiroho kirahisi hadi watumie mambo ya kichawi kama waganga wa kienyeji na mizimu sasa wanaotawaliwa na MSHALE wao hufanikiwa kwa tiba ambazo zinategemea mwenyezi mungu zaidi kama vile kufanyiwa maombi ya Qur.an au Biblia au Majini. huyu akipewa dawa haitamsaidia lolote labda ya kunywa kwa ajili ya maradhi kwa sababu yeye hufanikisha kupitia maneno au kauli za kiroho.

Sasa ukitaka kufanikiwa kama kupata pesa n.k utatakiwa ufuate nyota ya SIMBA

Na kuendelea mkuu nadhani hadi hapo umepata picha.



kama una swali ambalo ni personal na upo nje ya forum:

Wasiliana nami kupitia email hii:

Rakimsspiritual@gmail.com

au kwa namba hii

+255783930601

Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims
 
Kwa upande wakwako waita "Nyota ya mtu" ila wa upande wa pili huku, wanaita "Nuru ya mtu" .
Inakuaje mtu anampandishia mtu mwingine "Nyota"? Mara nyingi "Nyota" inahusishwa na Ushirikina
 
Kwa upande wakwako waita "Nyota ya mtu" ila wa upande wa pili huku, wanaita "Nuru ya mtu" .
Inakuaje mtu anampandishia mtu mwingine "Nyota"? Mara nyingi "Nyota" inahusishwa na Ushirikina

Hapana mkuu nyota sio ushirikina isipokua watu wanaofanya ushirikina wengi hujifisha kwenye kivuli cha nyota na hujisema kuwa wanarudisha nyota zilizoibiwa zilizokufa na zilizofanywa hivi au vile ukweli ni kwamba nyota ya mtu huwa ipo tu haiendi popote shida ni kung'ara au kuchafuka tu, na kukosea mfumo mzima, mtu anaona kuwa akisema anawangia watu ili wafanikiwe anaona tabu hivyo anajificha kwenye kivuli cha nyota za watu kwa kusema anasafisha nyota.

Wapi na wapi mganga wa kienyeji na unajimu? wapi na wapi padri wa kanisani na unajimu, lakini pia wapi na wapi nyota ya mtu na shehe wa msikitini. hivyo kuna vitu watu wanavuruga tu na kuonekana ni uchawi.

Nyota mwenye kuzifahamu ni aliyesoma mambo ya kiroho na unajimu, ndio maana unaona thread zangu nyingi watu wanakuwa hawaelewi mimi mganga wa kienyeji shehe au padre au mchawi kwa maana nafundisha vipi vinakuwa around humo lakini nimesoma na kupractice masomo ya kiroho hivyo lazima mote humo ujue ili uweze kujua unamsaidiaje aliyekumbwa humo katika utendaji. sijui umenielewa mkuu kwa faida ya wengine pia?

Rakims
 
Mkuu naomba ufafanue ni mambo yapi ambay kwa upande wako waona yanachafua nyota ya mtu au Nuru ya mtu!! Huo mfumo mzima unaousema ni upi na usahihishwa vipi?
ukirejea katika maelezo yangu hapo awali ni kwamba ili mtu aweze kwenda sawa na nyota yake anatakiwa afahamu ya kwamba nyota yake ni mpangilio katika maisha yako mfano kwenye series za battery panga betri 7 halafu zote zipeleke charge sehemu moja halafu huku chombo kile kinachowashwa na betri kiwe kinaendelea kufanya kazi muda wote ikatokea ukatoa betri moja au ukaigeuza nafahamu unajua nini kitatokea, tunaporudi kwenye system ya nyota mathalani mtu wakati anazaliwa sayari iliyokuwa inatawa jumatatu mfano ni mwezi sasa jumatatu huwa ina deal na uzazi, mambo yaliyofichika, amani, weupe n.k sasa mtu siku hiyo unakuta anavaa nguo ya jumanne yaani anataka kuipandisha jumanne kwa jumatatu mfumo mzima huwa umevurugika na umeme ukiwa mkali basi hata shoti humlipua, ndio hapo unaskia huwa kuna watu hawalogeki au kuna watu huwa wana bahati sana na kadhalika. sababu ya nyota yako kuchafuka na kung'ara kulogwa na kuwa na bahati mbaya yote chanzo huwa ni wewe na kuna taratibu ya kurekebisha ikiwa moja ya hayo limetokea

Rakims
 
Mbona kuna herufi za majina hazipo halafu Mbona hizo nyota znatofautiana na herufi za majna mfano unakuta wewe kutokana na tarehe uliozaliwa unaingia kwenye nyota ya samaki but herufi ya jina ipo kwenye nyota nyingine hebu elezea kidogo,
 
Halafu unapo Sema kuwa herufi ya siku Fulani ni hii huwa una Maana gani mfano samaki ni Alhamisi na herufi ni DH
 
Mbona kuna herufi za majina hazipo alafu Mbona hzo nyota znatofautiana na herufi za majna mfano unakuta ww kutokana na tarehe uliozaliwa unaingia kwenye nyota ya samaki bt heruf ya jina ipo kwenye nyota nyingine hebu elezea kidogo

Mkuu nimelieleza hili mwanzoni mwa thread ya kwamba ili uweze kujua nyota yako lazima ufahamu mambo manne na kuweza kuyalinganisha ndio unapata nyota yako sahihi sio wewe tu wengine huona hata maelezo yake ni batili na walivyo kwa sababu mtu unakuta anaangalia nyota ya mwezi wakati inakinzana na nyota iliyochomoza saa na siku anayozaliwa.

narudia ili kuweza kujua nyota yako sahhi hivi details lazima uwe nazo kama hauna kuna njia za kutumia ukazipata

Rakims
 
Alafu unapo Sema kuwa herufi ya siku Fulani ni hii huwa una Maana gani mfano samaki ni Alhamisi na herufi ni DH
Hizo ni herufi za majina ya utawala wa sifa za mwenyezi mungu siku hiyo mfano DH ni kifupi cha Dhahiru yaani kiarabu ni
75. Adh-Dhaahiru
kwamba mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu au kila jambo hii humfanya mwenye nyota hiyo anaweza kumsifu mwenyezi Mungu kwa sifa hii na akafanikisha jambo lake lolote analohitaji

Rakims​
 
Nyota zinatambulika kutokana na tarehe yako ya kuzaliwa,muda na saa au kama hujui basi inafaa na ndio bora zaidi kupigia hesabu jina lako la kuzaliwa pamoja na mama mzazi

Hayo mahesabu yanapigwaje
 
Kwanini nyota yangu inahusishwa na samaki, lakini haihusishwe na kitimoto, au panya?
Mkuu bujibuji ni kwamba maana ya nyota hizi kuwa na majina hayo ni kutokana na mwanzo wa historia ya kila nyota mfano: samaki

Hawa ni samaki wanaoogelea pamoja inaaminika kwamba historia yao walikuwa wamefungwa mikia na wanaogelea sehemu mbili tofauti na samaki hawa walikuwa wakionekana wanapita sehemu ya maji ya miji fulani ya Egypt walikua wakiashiria vita za ndani zinazohusu hisia na mambo yaliyojificha kama kusingiziwa mtoto au kusingiziwa kifungo kwa mtu na hili suala lilikuwa likichukuliwa hivyo zamani sana kama miaka 2000 kabla ya kuzaliwa Christo watu wa Babilon pia waliona kitendo hicho na baadae wakaanza kutangaza kuwa ikiashiria hivyo basi ni vita za ndani na watoto watakaozaliwa chini ya tukio hilo basi watakuwa wamezaliwa chini ya maarifa hayo na watakuwa ni watu wasiri na wenye vita za ndani, lakini baadae ilikuja kufahamika kuwa hili tukio likitokea samaki hao kufanya hivyo basi sababu yake huwa ni nyota 12 angani zikikaa katika mfumo huo, hapo ni baada ya wapima magimba kuanza ugunduzi lakini story nyingine huwa inasema kuwa Wagiriki walikuwa wakiita kitendo hicho kuwa ni kitendo cha miujiza kinachohusishwa na Zahara/Zuhura na Cupid(mungu wa kigiriki wa mapenzi) ya kwamba

Kulikuwa na mnyama aina ya Dragon aliyeitwa Typhon mwenye vichwa 100 na macho yanayowaka moto,akiwa na sauti ya nyoka, chini kidogo akiwa na umbo la ng'ombe na sauti ya ngurumo kama simba, siku moja Zuhura na mwanawe Cupid walikuwawakitembea jirani na mto mwembamba wa Euphrates pichani
1103834









akatokea huyo Typhon na kuwaachamia ulimi wake mweusi wenye kuwaka moto basi Zuhura alivyoona hana nguvu tena kwa woga akamuita baba yake Mushtar na baba yake huyo kwa haraka sana akawageuza na kuwa samaki wakaingia kwenye maji na kuogelea zao na kukimbia

Lakini hadithi nyingine inasema kuwa pale walitokea samaki wawili ambao ndio hao waliokuwa wakiogelea wawili kuonyesha vita za ndani na usiri wakawakomboa na kukimbia kwenye maji sasa kama zawadi hao samaki ndio wakarushwa juu ya anga na kujipanga pamoja na hizo nyota 12 na kuanzia hapo ndio wakawa hawaonekani na zinaonekana nyota peke yake.kila ikifikia kipindi hicho ndio maana kwa utafiti wakaja kugundua kuwa kila anaezaliwa chini ya nyota hizo huwa na mambo hayo ya sifa za hiyo nyota. Nakwambia hii story sio nakuaminisha haya hapana nakwambia ili ujue sababu ya hizo nyota kuitwa majina hayo tofauti na Nguruwe na fisi ni kuwa wana historia ya kuitwa hivyo lakini ukitaka unaweza kugeuza jina la nyota yako ikawa chambo ila maelezo uyajue kuwa yanabase na nini ndio maana wachina kujionyesha kuwa wanajua sana story hii wakawaita miungu wao wawili Yin & Yang wakiashiria samaki wawili walipoanza kuwaabudu ikabidi wageuze jina la samaki kuwa nguruwe

Rakims
 
Mwanamke ana nyota ya MIZANI na Mwanaume ana nyota ya MBUZI je hawa wanaweza kuoana?
Kwanza kabisa fahamu ya kuwa nyota ya Mizani asili yake ni upepo na mbuzi asili yake ni udongo watapendana ikiwa mwanamke atakuwa mdogo sana kiumri lakini wakiwa wanakaribiana basi ndoa yao itakuwa yenye mali bila furaha na mwisho wa nyote mwanaume hukimbiwa na mwanamke au mwanamke kumfukuza mwanamume,

Rakims
 
Back
Top Bottom