Ijue njia utakayotumia kupaa (Kwenda against Gravitational Force)

Habari za wakati huu wakuu wa Jamii Forums?

Wengi wetu tunafahamu ni kwa kiasi gani tunahitaji kupaa kwenda juu, lakini kutokana na nguvu zilizo nje ya uwezo wetu tunajikuta tupo pale pale ardhini!
Hii inatokana na nguvu ya uvutano ambayo inavuta vitu na watu at the center of the Earth.

Sio kosa ku aim high japokuwa ni vigumu kufika pale juu unapopahiaji.
Ila kuna mbinu ninakupa itakayoweza kukufanya upae na ufike pale unapopataka.

Kwanza lazima tutambue kuwa Gravitational force ipo na inafanya kazi ya kuvuta vitu kwenye centre ya Dunia.
Hivyo inahitaji nguvu ya ziada ili kuweza kuizidi hii Force ili uweze kupaa.

Kama tujuuavyo dunia ina mambo mengi ambayo yanakuvutia uendelee kubaki hapo ulipo tukianzia Anasa na starehe, shida mateso na karaha na mengineyo, kiukweli hivi vitu ndivyo vinaturudisha chini wengi wetu ambao tunataka kupaa yani kuwa juu.
Kwa mfano tukiangalia hata Shetani mamlaka yake yapo huku Duniani ambayo anazidi kuchochea mambo ambayo yanazidi kupull jitihada zetu.

Kuna wengi wamejitahidi kuruka lakini wakaishia kuvunjika na wengine kufa kabisa kwa kuwa hawakujua ili uende juu unahitaji nguvu kubwa sana itakayoishinda Gravitational force.

Sasa mbinu ni kwamba nguvu ya kuruka na kufika juu iko ndani yetu. Yani nikimaanisha kile tulichonacho ndani yetu tukikiweka positive kinaweza kuishinda gravitational force.

Bwana Yesu alivyopaa kwenda mbinguni alikuwa ana nguvu kuu iliyomwezesha kupaa. Na pia nguvu iyo tukiweza kuifufua au kuikarabati hakuna chochote kitachotushinda katika jitihada zetu za kupaa.

Niwe muwazi Mungu Baba tunasadiki kuwa yupo mbinguni na wengi wetu tunaamini mbinguni ni juu yani juu Mbinguni. Hivyo yatupasa tuyaishi yale yote aliyoyaamuru Baba Mungu ili tuweze kufika kwake.

Yani kwa lugha nyepesi Yesu ni njia, na njia aliyoitumia Yesu kupaa ndio hiyo hiyo inapasa tuitumie ili tuweze kupaa na kuishinda Dunia na vivutio vyake.

Asante kwa kusoma wakuu
Unachekesha sana aisee,
Hata ufanyeje katika hali ya kawaida huwezi kupaa kamwe,
Labda uwe mchawi
 
Mmmh inamaana kama huna hiyo nguvu yakupaa huwezi kuyashida ya dunia? Kama ni hivyo basi Kumbe yesu pekee ndo alishinda na Elia, sisi wengine tutashinda kwa neema tu.
 
Back
Top Bottom