Ijue Nehushtani, nyoka wa shaba aliyeabudiwa na Israeli

Shemasi Jimmy

Member
Apr 23, 2021
93
104
79fc44047f40574d9d6aef6576630907.jpg
Nehushtan.jpg

IJUE NEHUSHTANI, NYOKA WA SHABA ALIYEABUDIWA NA ISRAELI.

Joka la Shaba alilitengeneza Musa jangwani na kugeuka kuwa mungu wa Israeli.

Na Shemasi Jimmy 0659 611 252

Bwana Yesu apewe sifa wapendwa. Ikiwa ni siku njema Bwana ametupa kibali cha kuiona siku hii ya leo, si kwa sababu sisi ni wema sana au wakamilifu bali ni kwa neema tu, ilikwamba tumrudishie sifa na utukufu kwa kufanya mapenzi yake.

Leo Bwana ameniongoza tujifunze habari ya nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa jangwani na baadae kuabudiwa na waisraeli baada ya kufika katika nchi ya ahadi..

KUMBUKA:Jina la nyoka aliyetengenezwa na Musa jangwani, aliitwa ‘’NYOKA WA SHABA’’.

Baada ya waisraeli kufika kanaani walianza kuitumia sanamu hiyo ya nyoka wa shaba kwa siri kama mungu wao, jina la mungu huyo aliitwa ‘’NEHUSHTANI’’(2Fal 18:4)

Ni katika nyakati zile Mungu alipowaondoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya ugeni kama alivyohaidi mababu zao(taz Mwa 15:13). Wana wa Israeli walianza vitimbi njiani. Baadhi yao walitamani kugeuka na kurudi Misri huku wakitoa lawama za kila aina kwa Mungu na Musa.

Maandiko matakatifu yanasema wakati wana wa Israeli wakiwa jangwani kuelekea katika nchi ya maziwa na asali, walipita mlima Hori kisha bahari ya shamu huku wakiizunguka nchi ya EDOMU, baadhi yao walikosa uvumilivu na wengi wao walikata tamaa ya kuendelea na safari. Walianza kulaumu Musa na Mungu huku wakiuliza kusudi la kuwatoa Misri.

IMEANDIKWA: wakamnung'unikia Mungu na Musa, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!(Hes 21:5). Kitendo hiki kiliamsha ghadhabu ya Mungu, Mungu akatuma nyoka za moto na baadhi yao walikufa.

IMEANDIKIWA: Ndipo BWANA akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa (Hes 21:6).

Ikiwa baada ya watu kufa kutokana na nyoka hao, Wana wa Israeli wanaamua kutubu na kujinyenyekeza kwa Mungu ili kwamba hilo tatizo liondoke katika jamii yao(taz Hes 21:7).Pamoja na makosa yao hayo, lakini Mungu anawapa nafasi nyingine ya kusahihisha makosa yao na kumrejea tena. Mungu anamwambia Musa atengeneze nyoka ya Shaba kasha aiweke juu ya mti ili kila aliyeumwa apokee uponyaji kwa kuitazama (Hes 21:8)

WAISRAELI WAABUDU NEHUSHTANI BAADA YA KUFIKA KANAANI NA KUMUACHA MUNGU:

Ikiwa baada ya Mungu kutimiza ahadi yake aliyompa Ibrahimu ya kuupa uzao wake nchi ya kanaani (taz Mwa 12:7, 15:13) . Pamoja na maonyo mengi waliyopewa wana wa Israeli na Mungu juu ya kutotengeneza sanamu na kuziabudu, watu hawa waliiacha njia ya Bwana kuenenda kinyume na maagizo yake.

IMEANDIKWA: Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu (walawi 26:1 BHN).

Waliambatana na sanamu ile (kwa siri, asijue mtu) aliyoitengeneza Musa jangwani na baadhi yao walianza kuiabudu hata ulipotimia wakati wa utawala wa mfalme HEZEKEIA.

Maandiko matakatifu yanasema Hezekia alikua moja ya wafalme wema, mtiifu na mwadilifu mbele ya Mungu, alifanya mambo mengi mema na yenye kumpa Mungu utufu. Ni HEZEKIA mwana wa Ahazi aliyevunja vunja sanamu ya nyoka wa shaba ama Nuhushtani iliyotengenezwa na Musa jangwani, amabayo baadhi ya waisraeli waliitumia katika ibada zao zilizokua chukizo kuu mbele ya Mungu.

MEANDIKWA: Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya Shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.(2 fal 18:4)

TENDO LA MUSA KUINUA NYOKA WA SHABA JANGWANI LA FANANA NA TENDO LA KRISTO KUINULIWA MSALABANI.

Nyoka wa shaba aliyeinuliwa ili kila atakae mtazama apokee uponyaji na yeyote asiyemtazama alikufa(Hes 21:8-9). Ni sawa kabisa na jinsi Bwana wetu Yesu kristo alivyoutoa mwili wake kwa kila kiumbe ili kwamba kila amtazamae na kuamini basi ataokolewa na asiyeamini atahukumiwa(marko 16:16). Niheri sasa ndugu yangu ambaye bado hujampokea kristo na kumfanya awe Bwana na mwokozi wako, fikiria sasa uamizi huu.

YEYE ANASEMA’’Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha’’(Mt 11:28). Wewe uliyepata neema ya kusoma ujumbe huu,geuka na ufikiri sasa kumfuata Yesu. Nitafte shemasi wako kwa namba hii 0659 611 252 popote ulipo tutakufikia na utapokea wokovu kwa njia ya ubatizo wa maji na roho(mdo 2:38)

Mungu akubariki wewe uliyetumia muda wako wa thamani kusoma chapisho hili. Bwana akubariki wewe na familia yako. Akubariki uingiapo na kila utokapo kwa jina la Yesu, amina
 
"Ni HEZEKIA mwana wa Ahazi aliyevunja vunja sanamu ya nyoka wa shaba ama Nuhushtani iliyotengenezwa na Musa jangwani, amabayo baadhi ya waisraeli waliitumia katika ibada zao zilizokua chukizo kuu mbele ya Mungu."
..........
..........
"IMEANDIKWA: Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya Shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.(2 fal 18:4)"
...........
............

Mtoa mada unanchanganya.
Huyo nyoka wa shaba alikuwa chukizo mbele ya Mungu.
Na sanamu hiyo ililetwa na Musa.
Sasa kama ni chukizo mbele ya Mungu kwa vile sanamu hityo inaabudiwa, itafananishwaje na Yesu Kristo ambaye tunamwabudu?
 
Nahisi kuna mahala hujaelewa ndugu, kuna nyoka wa shaba(jina la nyoka aliyetengenezwa na Musa jangwani)
na
kuna nehushtani(baadhi ya waizraeli walimchukua nyoka huyo wa shaba kwa siri na kuanza kumtumia kama mungu wao). nyoka wa shaba hakua na tatizo lolote kwa maana lilikua agizo la Mungu. soma Hes 21:8

muhimu kuelewa ni kwamba, TENDO LA MUSA KUINUA NYOKA WA SHABA JANGWANI LALILIFANANA NA TENDO LA KRISTO KUINULIWA MSALABANI. unaweza pia kusema kua tendo hilo lilikua kivuli cha Yesu kuinuliwa msalabani kutokana na mambo yafuatayo

1. israeli walioasi na kuumwa na nyoka walipokea uponyaji kupitia nyoka huyo sawa sawa na zama hizi watu wote wamekombolewa na tendo la Yesu kuinuliwa na kisha kufa msalabani.
 
Bado kuna ukakasi katika hiyo argument yako.
Sasa kama nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa na kuinuliwa na kuwa ukombozi, baadaye kitendo cha kumuabudu nyoka huyo wa shaba kuwa chukizo kwa Mungu, tendo hilo la nyoka wa shaba linakosa uzito wa ufananisho, maana nyoka yule alikatazwa kuabudiwa.
Sisi tunamwabudu Yesu Kristo wa pale msalabani ambaye hawezi linganishwa na nyoka wa shaba aliyepigwa marufuku kuabudiwa.
 
Uelewa wako mdogo sana!
 
unatambua kua agano la kale ni kivuli cha agano jipya?
kwamba mwana- kondoo wa pasaka ya israeli ilikua kivuli cha masihi?
unatambua kua mfalme melkizedeki alikua kivuli cha kristo
unatambua kua damu ya mwanakondoo iliopakwa katka miimo ya wana wa israeli wakati wapo misri ilikua ni kivuli cha masihi?

kwa nini unashindwa kuelewa kua nyoka wa shaba ilikua kivuli cha kuinuliwa kwa Yesu msalabani?
 
Wakristo hawamuabudu Yesu, Ila wanamuabudu Mungu kupitia Kwa Yesu Kristo.

Ni Kama vile Waisrqel hakuabudu Yule nyoka isipokuwa waliambiwa Wamtumie nyoka Yule wa Shaba kuomba uponyaji.

Kilichofanywa na Musa ni ishara ya kile atakachofanya Yesu msalabani
 
Yesu Kristo na Mungu ni Mwana na Baba, kwa hiyo ni kitu kimoja.
Lakini nyoka wa shaba hawezi kuabudiwa na kama Yesu Kristo na ndio maana HEZEKIA mwana wa Ahazi aliyevunja vunja sanamu ya nyoka wa shaba
 
Yesu ni Mungu ni wamoja katika utendaji lakini sio katika uhusika.
Yaani ni Sawa na Mke na Mume kuwa mwili mmoja lakini sio katika uhusika Bali katika masuala ya ndoa na kifamilia.

Mungu ni mmoja pekee.
Hata wewe na Mungu mnaweza kuwa wamoja labda Katika Jambo Fulani lakini kwenye uhusika hamuwezi kuwa wamoja.

Kila Binadamu anayemcha Mungu ni mwana wa Mungu lakini haimaanishi huyo binadamu naye anakuwa Mungu.

Baadhi ya Wakristo wamekuwa wakichanganywa na hiyo Falsafa/teolojia ya umoja baina ya Mungu na Yesu, mpaka imefikia hatua Wanamuita Yesu ni Mungu Jambo ambalo ni Kufuru kubwa.
 
Katika hili unaleta fasihi na sio uhalisia wa kile kilichoandikwa katika Biblia ! Nashauri ujikite katika fasihi ma mashairi Yako! Hili la theolojia ya utatu mtakatifu na Umungu wa Bwana wetu Yesu Kristo waachie wanazuoni wa Biblia walifafanue kwa wasio Jua! :
1. Yn 1:1-14 SUV
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. (Soma uelewe)
2. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo
Maria anaambiwa utabeba mimba na utamzaa mwana na Jina lake utamwita EMMANUEL maana yake, Mungu pamoja Nasi, (ni Mungu Mwenyewe amejidhihirisha katika ulimwengu wa mwili
Kasome:
  • Mt 1:23 (SUV)

    Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Kasome pia Thomaso anamshuhudia Mungu pale Yesu alipomtokea, ikiwa Yesu hakua na Umungu Ndani yake alipaswa kumkemea Thomaso isipokua alicoment: heri Wewe uliyeona ma kusadiki, baada ya Thomaso kusema "BWANA WANGU NA MUNGU WANGU"
Kasome:
Yohana 20:28 NEN
Tomaso akamwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu!”
Je ni Nani awezaye kuutoa uhai? Ni Mungu pekee na sio mwingine ambayw aweza kuutoa uhai na kuurudisha tena
Kasome:
Yohana 10:18 (NEN)
Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena
Je ni Nani awezaye kufufua wafu? Ni Mungu Mwenyewe aweza kufanya hayo; rejea Yesu anamfufua Lazaro;
Lakini kama haitoshi wawwza kuendelea kusoma Biblia na kupata uhakikisho usio kwa na shaka
Nani awezaye kusamehe dhambi? Ni Mungu Mwenyewe
Kasome:

Mathayo 9:5 NEN​

Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’?

Endelea kuisoma Biblia vizuri pia Yesu baada ya kubatizwa alifunga kwa Siku arobaini na shetani akamjaribu
Majibu ya Yesu yalikua haya

Luka 4:12 NEN​

Yesu akamjibu, “Imesemwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”
Shetani alipogundua anaingia katika mtego wa kumjaribu Mungu alimwacha akaenda zake!
Yapo maandiko mengi katika Biblia yanayothibitisha Umungu wa Kristo nikiandika hapa hapatatosha, ndio mana likabakia Kuwa FUMBO LA UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA!

Ukiona mtu anasema Yesu ni Mungu ujue dini kaijulia ukubwani.
Kwa mtu aliyefunzwa Maandiko matakatifu kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka kitabu Cha ufunuo Kwa Biblia ya vitabu 66 hawezi sema Yesu ni Mungu.

Nitaanzisha Uzi ili kuweka mjadala huru ili Kuwafunza watu waliochelewa kujifunza maandiko na bado hawajahitimu Mafunzo lakini wanajadili ishu complicated kama hiyo ya Yesu kuwa ni Mungu.
Yesu anauungu lakini sio MUNGU Mkuu.

Hata wewe unaweza kuwa na uungu ndani yako lakini kamwe huwezi kuwa Mungu
 
Nimekusisitiza wewe endela na fasihi ambayo Ni imagination /fiction isiyo na empirical proof!

Haya mambo ya theolojia waache wenyewe, katika hili hakuna mjadala huru isipokua kutaka matamanio y'ako na Imani yako ifuatwe na watu wengine!

Andiko langu kama umelisoma nimetoa baadhi ya biblical quotes. Ambazo umeshindwa kuzikataa au kuzikubali!
Uungu aliokua nao Yesu Sio Sawa na kamwe hautakua ulio nao wewe au Mimi .
Ndio Maana nimefunga kwa kusema
Hilo Ni FUMBO LA UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA!
Kwa taarifa yako hata Yesu mwenyewe aliwapa mafundisho watu wazima na Sio watoto!
Kuijua dini au Imani ukubwani Ni jambo jema kwani akili huwa imekomaa na yaweza kuyachuja na kuyachunguza Maarifa au knowledge kuliko mtoto mdogo ambaye hukaririshwa bila kuhoji uhalali wa Maarifa amayopewa au kuyasikia!
Sababu watoao Maarifa au elimu hivyo Ni mammlaka (authoritative knowledge) kama wazazi walimu wa dini nk!
Bakia na fasihi itakusaidia!
 
Mkuu Hilo fundisho la utatu mtakatifu ni fundisho la kipagani/ukafiri.

Hata Yesu hakuabudu Kwa misingi ya utatu mtakatifu alipokuwa akimuabudu Mungu wake.

Kwa kukusaidia, tafuta historia ya Kanisa na Dini ya Ukristo, kisha fuatilia fundisho la utatu/Trinity liliingizwa lini katika Ukristo.

Huweziijua dini Kama hujui historia ya Dunia na historia ya Dini husika.

Kisha fuatilia kabla ya Ukristo watu walikuwa wanaabudu kwa namna ipi hasa Wayahudi.

Mambo ya kuzingatia ni haya;
I. Wewe unamfuata Yesu, Yesu ni Myahudi, dini yake ni Uyahudi mpaka anaondoka, Mungu wake ni Yahweh (Kwa maana ndiye mungu wa Wayahudi)
Jiulize Wayahudi na Dini Yao wanakitu wanakiita Trinity (utatu mtakatifu)?

ii. Alafu fuatilia Waliosambaza huo Ukristo (Warumi) je kabla ya kuwa Wakristo walikuwa dini Yao ni ipi? Na Mungu wao alikuwa yupi?
Je wanafundisho la Trinity hao warumi?
Kisha ndio uje tujadili.

Zingatia, Warumi ndio waliingiza baadhi ya tamaduni na ibada za Dini zao kwenye Ukristo,
Moja ya Ibada hizo ni pamoja na ibada ya utatu mtakatifu, Trinity.

Hujiulizi kwenye Torati ambapo ndio msingi wa watu kuabudu Ulipo Kwa nini hakuna huo upuuzi wa Utatu mtakatifu?

Muwe mnajiongeza,
 
Nimekusisitiza wewe endela na fasihi ambayo Ni imagination /fiction isiyo na empirical proof!

Haya mambo ya theolojia waache wenyewe, katika hili hakuna mjadala huru isipokua kutaka matamanio y'ako na Imani yako ifuatwe na watu wengine!

Andiko langu kama umelisoma nimetoa baadhi ya biblical quotes. Ambazo umeshindwa kuzikataa au kuzikubali!
Uungu aliokua nao Yesu Sio Sawa na kamwe hautakua ulio nao wewe au Mimi .
Ndio Maana nimefunga kwa kusema
Hilo Ni FUMBO LA UTATU MTAKATIFU MUNGU MMOJA!
Kwa taarifa yako hata Yesu mwenyewe aliwapa mafundisho watu wazima na Sio watoto!
Kuijua dini au Imani ukubwani Ni jambo jema kwani akili huwa imekomaa na yaweza kuyachuja na kuyachunguza Maarifa au knowledge kuliko mtoto mdogo ambaye hukaririshwa bila kuhoji uhalali wa Maarifa amayopewa au kuyasikia!
Sababu watoao Maarifa au elimu hivyo Ni mammlaka (authoritative knowledge) kama wazazi walimu wa dini nk!
Bakia na fasihi itakusaidia!

Embu soma hapa kidogo,

Alafu tafuta kitabu cha "IS GOD TRINITY"
Uongeze maarifa

The origin of the conception is entirely pagan"​

Egyptologist Arthur Weigall, while himself a Trinitarian, summed up the influence of ancient beliefs on the adoption of the Trinity doctrine by the Catholic Church in the following excerpt from his previously cited book:

"It must not be forgotten that Jesus Christ never mentioned such a phenomenon [the Trinity], and nowhere in the New Testament does the word 'Trinity' appear. The idea was only adopted by the Church three hundred years after the death of our Lord; and the origin of the conception is entirely pagan . . .

"The ancient Egyptians, whose influence on early religious thought was profound, usually arranged their gods or goddesses in trinities:
there was the trinity of Osiris, Isis, and Horus, the trinity of Amen, Mut, and Khonsu, the trinity of Khnum, Satis, and Anukis, and so forth . . .

"The early Christians, however, did not at first think of applying the idea to their own faith. They paid their devotions to God the Father and to Jesus Christ, the Son of God, and they recognized the mysterious and undefined existence of the Holy Spirit; but there was no thought of these three being an actual Trinity, co-equal and united in One . . .

"The application of this old pagan conception of a Trinity to Christian theology was made possible by the recognition of the Holy Spirit as the required third 'Person,' co-equal with the other 'Persons' . . .

"The idea of the Spirit being co-equal with God was not generally recognised until the second half of the Fourth Century A.D. . . . In the year 381 the Council of Constantinople added to the earlier Nicene Creed a description of the Holy Spirit as 'the Lord, and giver of life, who proceedeth from the Father, who with the Father and Son together is worshipped and glorified.' . . .

"Thus, the Athanasian creed, which is a later composition but reflects the general conceptions of Athanasius [the 4th-century Trinitarian whose view eventually became official doctrine] and his school, formulated the conception of a co-equal Trinity wherein the Holy Spirit was the third 'Person'; and so it was made a dogma of the faith, and belief in the Three in One and One in Three became a paramount doctrine of Christianity,though not without terrible riots and bloodshed . . .

"Today a Christian thinker . . . has no wish to be precise about it, more especially since the definition is obviously pagan in origin and was not adopted by the Church until nearly three hundred years after Christ" (pp. 197-203).

James Bonwick summarized the story well on page 396 of his 1878 work Egyptian Belief and Modern Thought: "It is an undoubted fact that more or less all over the world the deities are in triads. This rule applies to eastern and western hemispheres, to north and south.

"Further, it is observed that, in some mystical way, the triad of three persons is one. The first is as the second or third, the second as first or third, the third as first or second; in fact, they are each other, one and the same individual being. The definition of Athanasius, who lived in Egypt, applies to the trinities of all heathen
 
Wafilipi 2 : 10 - 11 " Kwa ajili ya jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu "
 
unatambua kua agano la kale ni kivuli cha agano jipya?
kwamba mwana- kondoo wa pasaka ya israeli ilikua kivuli cha masihi?
unatambua kua mfalme melkizedeki alikua kivuli cha kristo
unatambua kua damu ya mwanakondoo iliopakwa katka miimo ya wana wa israeli wakati wapo misri ilikua ni kivuli cha masihi?

kwa nini unashindwa kuelewa kua nyoka wa shaba ilikua kivuli cha kuinuliwa kwa Yesu msalabani?
Shemasi naomba maelezo kidogo juu ya Mfalme Melkizedeki,kuna watu wanasema kwa sifa zake zilizotajwa ndiye Yesu mwenyewe na wengine wanasema sio,naomba ufahamu hapo
 
Wafilipi 2 : 10 - 11 " Kwa ajili ya jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu "
Huyu ndugu abakie katika Mashairi na fasihi ataeleweka lakini katika theolojia anajichanganya. Mimi nimeestablsh fact kupitia biblia Ila eye ameniletea kitabu alichoandika mtu mwingine nje ya Biblia. Ajenda imehama kutoka Umungu wa Kristo kwenda kwenye Holy trinity Doctrine!
Nimetamani sana aje na maandiko ya Biblia kuthibitisha madai yake!
 
View attachment 2404825View attachment 2404827

IJUE NEHUSHTANI, NYOKA WA SHABA ALIYEABUDIWA NA ISRAELI.

Joka la Shaba alilitengeneza Musa jangwani na kugeuka kuwa mungu wa Israeli.

Na Shemasi Jimmy 0659 611 252

Bwana Yesu apewe sifa wapendwa. Ikiwa ni siku njema Bwana ametupa kibali cha kuiona siku hii ya leo, si kwa sababu sisi ni wema sana au wakamilifu bali ni kwa neema tu, ilikwamba tumrudishie sifa na utukufu kwa kufanya mapenzi yake.

Leo Bwana ameniongoza tujifunze habari ya nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa jangwani na baadae kuabudiwa na waisraeli baada ya kufika katika nchi ya ahadi..

KUMBUKA:Jina la nyoka aliyetengenezwa na Musa jangwani, aliitwa ‘’NYOKA WA SHABA’’.

Baada ya waisraeli kufika kanaani walianza kuitumia sanamu hiyo ya nyoka wa shaba kwa siri kama mungu wao, jina la mungu huyo aliitwa ‘’NEHUSHTANI’’(2Fal 18:4)

Ni katika nyakati zile Mungu alipowaondoa wana wa Israeli kutoka katika nchi ya ugeni kama alivyohaidi mababu zao(taz Mwa 15:13). Wana wa Israeli walianza vitimbi njiani. Baadhi yao walitamani kugeuka na kurudi Misri huku wakitoa lawama za kila aina kwa Mungu na Musa.

Maandiko matakatifu yanasema wakati wana wa Israeli wakiwa jangwani kuelekea katika nchi ya maziwa na asali, walipita mlima Hori kisha bahari ya shamu huku wakiizunguka nchi ya EDOMU, baadhi yao walikosa uvumilivu na wengi wao walikata tamaa ya kuendelea na safari. Walianza kulaumu Musa na Mungu huku wakiuliza kusudi la kuwatoa Misri.

IMEANDIKWA: wakamnung'unikia Mungu na Musa, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!(Hes 21:5). Kitendo hiki kiliamsha ghadhabu ya Mungu, Mungu akatuma nyoka za moto na baadhi yao walikufa.

IMEANDIKIWA: Ndipo BWANA akapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa (Hes 21:6).

Ikiwa baada ya watu kufa kutokana na nyoka hao, Wana wa Israeli wanaamua kutubu na kujinyenyekeza kwa Mungu ili kwamba hilo tatizo liondoke katika jamii yao(taz Hes 21:7).Pamoja na makosa yao hayo, lakini Mungu anawapa nafasi nyingine ya kusahihisha makosa yao na kumrejea tena. Mungu anamwambia Musa atengeneze nyoka ya Shaba kasha aiweke juu ya mti ili kila aliyeumwa apokee uponyaji kwa kuitazama (Hes 21:8)

WAISRAELI WAABUDU NEHUSHTANI BAADA YA KUFIKA KANAANI NA KUMUACHA MUNGU:

Ikiwa baada ya Mungu kutimiza ahadi yake aliyompa Ibrahimu ya kuupa uzao wake nchi ya kanaani (taz Mwa 12:7, 15:13) . Pamoja na maonyo mengi waliyopewa wana wa Israeli na Mungu juu ya kutotengeneza sanamu na kuziabudu, watu hawa waliiacha njia ya Bwana kuenenda kinyume na maagizo yake.

IMEANDIKWA: Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu (walawi 26:1 BHN).

Waliambatana na sanamu ile (kwa siri, asijue mtu) aliyoitengeneza Musa jangwani na baadhi yao walianza kuiabudu hata ulipotimia wakati wa utawala wa mfalme HEZEKEIA.

Maandiko matakatifu yanasema Hezekia alikua moja ya wafalme wema, mtiifu na mwadilifu mbele ya Mungu, alifanya mambo mengi mema na yenye kumpa Mungu utufu. Ni HEZEKIA mwana wa Ahazi aliyevunja vunja sanamu ya nyoka wa shaba ama Nuhushtani iliyotengenezwa na Musa jangwani, amabayo baadhi ya waisraeli waliitumia katika ibada zao zilizokua chukizo kuu mbele ya Mungu.

MEANDIKWA: Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ile nyoka ya Shaba aliyoifanya Musa; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake Nehushtani.(2 fal 18:4)

TENDO LA MUSA KUINUA NYOKA WA SHABA JANGWANI LA FANANA NA TENDO LA KRISTO KUINULIWA MSALABANI.

Nyoka wa shaba aliyeinuliwa ili kila atakae mtazama apokee uponyaji na yeyote asiyemtazama alikufa(Hes 21:8-9). Ni sawa kabisa na jinsi Bwana wetu Yesu kristo alivyoutoa mwili wake kwa kila kiumbe ili kwamba kila amtazamae na kuamini basi ataokolewa na asiyeamini atahukumiwa(marko 16:16). Niheri sasa ndugu yangu ambaye bado hujampokea kristo na kumfanya awe Bwana na mwokozi wako, fikiria sasa uamizi huu.

YEYE ANASEMA’’Njoni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha’’(Mt 11:28). Wewe uliyepata neema ya kusoma ujumbe huu,geuka na ufikiri sasa kumfuata Yesu. Nitafte shemasi wako kwa namba hii 0659 611 252 popote ulipo tutakufikia na utapokea wokovu kwa njia ya ubatizo wa maji na roho(mdo 2:38)

Mungu akubariki wewe uliyetumia muda wako wa thamani kusoma chapisho hili. Bwana akubariki wewe na familia yako. Akubariki uingiapo na kila utokapo kwa jina la Yesu, amina
Shemasi acha kupotosha umma!! Musa hakutengeneza nyoka wa shamba.labda kama biblia yako ni tofauti na biblia zingine! hivi ukikutana na mutu ambae hajasoma biblia suataamini Musa ndie aliyetengeneza nyoka wa shamba..

Kama huna elimu ya kutosha kuhusu mambo haya, uliza kwa wanaojua.
 
Back
Top Bottom