Ijue mifumo mbalimbali ya soka la kisasa (Morden football) ruksa maswali kuhusu mfumo wowote ambao unatamani kuufahamu kwa kina

Hank_31

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
855
2,109
Kwanza naanza kwa kuwasalim wakulungwa wote wa jf na kuwambia vimbeni na jipigeni kifua maana mko mahali salaaaama.
Back to the topic.

Kumekuwa na mifumo mingi sana ya soka na uchezaji wa soka tangu pale mchezo wa soka ulipoanzishwa huko karne kadhaa nyuma na kumekua na mabadiliko ya mifumo na sheria mbalimbali kadri siku zinavyozidi kisonga.

Mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya uhitaji katika soko la soka kwa kuutoa mchezo kutoka katika sanaa na kuupeleka kua sayansi.

Leo nitaanza na mfumo wa kawaida ambao kila mtu anaufahamu, mfumo wa 4-4-2 (four-four- two). Mfumo unajumuisha mabeki wawili wa kati, mabeki wa pembeni( kulia na kushoto), viungu wanne na washambuliaji wawili.

Mfumo huu, upo wa namna nyingi but wengi wanatumia viungo wawili wakabaji, na viungo wawili wa pembeni na washambuliaji wawili kama kawaida au wengine hutumia viungo wawili wa kati na mawinger na washambuliaji wawili.

ITAENDELEA...

images%20(1).jpg
images.jpg
 
Faida za kutumia mfumo huu ni zipi na hasara au mapungufu yake ni yapi? Ukilinganisha na mifumo mingine?
Asante sana kwa swali zuri mku

(faida);
1: mfumo ni rahisi, hasa kueleweka kwa wachezaji, na kuuufundisha , na hata kuperfom.

2: mfumo umegawanya majukumu ya wachezaji vizuri uwanjani.kwa mfano kwa kuwatumia washambuliaji wawil hii inasababisha timu kua hatar hasa ikiwa mastraika ni wanacheza playing style ambayo ni ( targetman),mfano chritian benteke.

3:Timu inakua na uwezo wa kucheza mpira wa aina yoyote ile either possession game au counter attacks.

Hasara:
1:Mfumo uko rigid sana, na unakua mwepesi kama timu inayoutumia ikikutana na timu ambayo iko flexible.

NAWASILISHA,.......
 
nahitaji kujua namna 4-3-3 diamond unavyofany kazi,i mean ni jinsi gani unawez kutumika...
Mkuu Kimwerymdodo5 , nitafka huku but kifup mfumo upo na mabeki wanne, kiungo mkabaji mmoja viungo washambuliaji wawili washambuliaji wa pembeni wawili na straika.vile vile hyo tatu ya kati wanaweza wote kua viungo wa kati bu mmja hua anadrop deep kusaidia mabeki, mfano ni bercelona ya busquet,iniesta na raktic.
images%20(4).jpg
 
Asante sana kwa swali zuri mku

(faida);
1: mfumo ni rahisi, hasa kueleweka kwa wachezaji, na kuuufundisha , na hata kuperfom...
Ahsantee... Swali lingine
Ikitokea timu mbili zimekutana na zote zinatumia mfumo wa aina moja (mfano zote zikatumia 4-4-2) ugumu wa mechi utakuaje? Yaan inaweza sababisha timu zote zikatoka sare??
 
Hapo uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ndo utaamua(Individual performance)
 
Mkuu ukipata wasaa utuchambulie mfumo waliotumia Australia kwenye World cup 2010 yaani ''6-4-4'' ambayo ni basically 6-4-0.

Then kwanini timu siku hizi hazitumii 4-4-2 yenye pure strikers wawili!! But nyingi zinachanganya CF na SS/CAM hapo front two. Ambapo mmoja ana drop kukaba na mmoja anabaki kma pure 9.
 
Kwanza naanza kwa kuwasalim wakulungwa wote wa jf na kuwambia vimbeni na jipigeni kifua maana mko mahali salaaaama.
Back to the topic.

Kumekuwa na mifumo mingi sana ya soka na uchezaji wa soka tangu pale mchezo wa soka ulipoanzishwa huko karne kadhaa nyuma na kumekua na mabadiliko ya mifumo na sheria mbalimbali kadri siku zinavyozidi kisonga.

Mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya uhitaji katika soko la soka kwa kuutoa mchezo kutoka katika sanaa na kuupeleka kua sayansi.

Leo nitaanza na mfumo wa kawaida ambao kila mtu anaufahamu, mfumo wa 4-4-2 (four-four- two). Mfumo unajumuisha mabeki wawili wa kati, mabeki wa pembeni( kulia na kushoto), viungu wanne na washambuliaji wawili.

Mfumo huu, upo wa namna nyingi but wengi wanatumia viungo wawili wakabaji, na viungo wawili wa pembeni na washambuliaji wawili kama kawaida au wengine hutumia viungo wawili wa kati na mawinger na washambuliaji wawili.

ITAENDELEA...

View attachment 1703997View attachment 1703998
Yeah yeah, habari za asubuhi wakulungwa,wacha tuendelee na majukumu ya kulijenga taifa.
Leo nakuja na formation ya 4-5-1.
Kwanza nianze kwa kusema formation hii ni manipulated 4-4-2. Na 4-5-1, zipo za aina nyingi mfano wa hzo na ambazo ni common ni kama ifuatavyo

4-5-1(4-1-4-1),hii nilishaieleze kidogo maana kuna mdau aliuliza, but inaundwa na mabeki wanne, kiungo mkabaji mmoja, viungo washambuliaji wanne na straika mmoja.au mda mwingine timu inaweza tumia kiungo mkabaji mmoja,viungo wa kati wawili, na viungo washambuliaji wawili(RMF&LMF)

Faida.(4-1-4-1)
Ni rahisi na nzuri katika kujilinda, na ina inaipa timu wigo mpana wa kushambulia kutokana na kua na viungo washambuliaji wengi.

Hasara:
Inaweza kushambuliwa kiurahisi kwa kutumia counters attack, (refer game ya simba na azam ya mwisho) na pia inahitaji watu wa pembeni wawe na uwezo mkubwa wa kushambulia na kukaba.

Aina ya pili ya 4-5-1ni 4-2-3-1, tofauti na hiyo hapo juu hii hua na viungo wawili wakabaji, mfano ni mechi ya simba vs Vita club.

images%20(2).jpg

View attachment 1704401View attachment 1704402
Kuna infomation zingine apo juu zinaitaji wachezaji mahiri wenye weredi wa kukaba kwa macho tu.
Na nyingine kukaba mtu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom