Ijue maana ya neno "Demka". Ni Kiswahili kutoka Zanzibar chenye asili ya lugha ya Kikae

Lutifya

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,608
2,000
Wewe Mataga acha kujitoa ufahamu! Walio ambiwa waache kudemka ni akina nani? Siyo wale ndugu zako wa kule bungeni wanao tumia muda mwingi kutaka kumlinganisha hayati na Rais wa sasa?
Walioingia Bungeni kwa uchafuzi wa Uchaguzi...
 

chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
751
1,000
Hongera Mh Rais Samia Suluhu kwa kutuongezea msamihati kwenye lugha yetu.

Katika kongamano na viongozi wa dini Rais Samia ametumia neno la kiswahili ambalo ni adimu kulisikia mitaani ingawa ni neno la kiswahili kutoka asili ya kusini mwa zanzibar.


demka Taz. demnga.
demnga V cheza ngoma kwa maringo; kujionea fahari katika uchezaji ngoma; kuonyesha
mbinu mbalimbali zilizo bora katika mchezo wa ngoma (play by swaggering):

Nanuhuyu kanademnga (demka) ja gurudumu bovu. ......Fulani anacheza
kama gurudumu bovu.
Watu pya wevu wakamlola yeye avyoja akademnga
(demka). ...Watu wote wakimtazama alipokuwa akicheza kwa maringo.

WATU WAACHE KUDEMKA ....WACHAPE KAZI IENDELEE
Hilo ni neno lenye asili ya makabila ya kibantu, na linatafsiri nyingi mfano makabila ya mkoa watanga KUDEMKA wanalitumia kwa uchezaji wa ngoma vineyard au mtoto wakiume akitembea uchi, ndio anaambiwa ADEMKA MWAZI
 

Immanuel Simon Mathew

JF-Expert Member
Apr 2, 2020
509
1,000
Wa kulaumiwa kwenye hili sakata la "kudemka" wala sio wakina Kibajaji au Msukuma, bali ni yule mpiga ngoma mkuu mwenye file hospitali ya Milembe. Yeye ndiyo anatolerate hyo ngoma ya Sindimba kupigwa ndani jengo la serikali Huku yeye akiwa ndiye mkatikaji mkuu! Bora Mama amemtolea uvivu kwani anakera sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom