Ijue maana ya neno "Demka". Ni Kiswahili kutoka Zanzibar chenye asili ya lugha ya Kikae

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,026
2,000
Hongera Mh Rais Samia Suluhu kwa kutuongezea msamiati kwenye lugha yetu.

Katika kongamano na viongozi wa dini Rais Samia ametumia neno la kiswahili ambalo ni adimu kulisikia mitaani ingawa ni neno la kiswahili kutoka asili ya kusini mwa Zanzibar.

demka Taz. demnga.
demnga V cheza ngoma kwa maringo; kujionea fahari katika uchezaji ngoma; kuonyesha
mbinu mbalimbali zilizo bora katika mchezo wa ngoma (play by swaggering):

Nanuhuyu kanademnga (demka) ja gurudumu bovu. ......Fulani anacheza
kama gurudumu bovu.
Watu pya wevu wakamlola yeye avyoja akademnga
(demka). ...Watu wote wakimtazama alipokuwa akicheza kwa maringo.

WATU WAACHE KUDEMKA ....WACHAPE KAZI IENDELEE
 

Nyamizi

Platinum Member
Feb 19, 2009
2,957
2,000
Kutwaaaa mnalia na story za kumsifia mtu aliyekufa hadi Mama samia amewachoka amewatolea uvivu.

Nadhani hii nyundo wamepigwa wale waliotaka kumtofautisha Samia na JPM au hukusikia anasema Samia na Magufuli ni kitu kimoja. Najua hamuamini mlichokisikia leo
 

Murashani GALACTICO

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
900
1,000
Kinara wa kudemka ni yule spika mbovu mwenye faili mirembe. Sijui atafanya nn maana bunge limesemwa huko mijadara yake haina afya kwa Taifa. Navyolijua lile baba angekuwa mtu mwingine lingesema kesho aje akutane na kamati ya hadhi na madaraka ya bunge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom