Ijue kesi hii iliyoacha maswali kwa watu wengi

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
17,883
45,248
STAAJABIKA NA NA KESI HII YA MAUAJI YENYE UTATA ZAIDI. March 23 mwaka 1994 tabibu mkaguzi(medical examiner) anauchunguza mwili wa marehemu Ronald Opus na kufikia maamuzi kua Ronald Opus alikufa kwa kupigwa risasi kichwani, Hii inatokana na jeraha kubwa la risasi kichwani alilokutwa nalo marehemu Ronald Opus...Hapa ndipo tabibu mkaguzi pamoja na vyombo vya usalama wanakubaliana kua wana muuaji mikononi mwao.. Mpaka kufikia hatua hio,uchunguzi uliofanyika awali na vyombo vya usalama unabainisha kua marehemu Ronald Opus alijirusha kutoka kwenye jengo la ghorofa kumi kwa lengo la kujiua, aliacha kikaratasi chenye ujumbe mfupi kwenda kwa wazazi wake chenye maneno yafuatayo "I'm sorry I can't forgive you, I will be with God " (nisamehe, siwezi kuwasamehe, ntakua na Mungu) Marehemu Ronald opus alijirusha kutoka ghorofa ya kumi kwa lengo la kujiua,lakini wakati akishuka chini alipigwa risasi ya kichwani(juu kwa juu kabla hajafika chini) hali iliyopelekea kusitisha maisha yake papo kwa hapo Si marehemu Ronald wala aliyefyatua risasi alikua akijua kua kwenye jengo lile kuliwekwa neti za usalama(safety nets) kwa ajili ya kuwalinda waosha vioo wa jengo lile. Hizi neti za usalama hua zinawekwa kabla hujafika chini kwenye majengo au madaraja marefu ili ikitokea mtu akianguka basi aangukie kwenye hizi neti za usalama na asipate madhara. Mwili wa marehemu ulikutwa juu ya hizi neti za usalama, kwa maana hio kilichomuua Ronald ni risasi aliyopigwa angani na wala si kingine, isingekua risasi ile,dhamira yake ya kujiua Isingetimia... RISASI ILITOKA WAPI NA HUYU MUUAJI NI NANI?? Vyombo vya usalama vinaingia kazini, wanafanya uchunguzi wa kina(vetting) kwenye jengo lile lote na kubaini kua risasi iliyomuua Ronald Opus ilitoka kwenye chumba kilichopo ghorofa la 9 la jengo lile, hii ni kutokana na kukutwa kwa tundu la risasi katika moja ya madirisha ya chumba kile. Chumba hiki anaishi mzee wa makamo pamoja na mke wake, baada ya mahojiano inabainika kua mzee yule alikua na ugomvi mkubwa na mke wake, hii ilipelekea mzee yule kumshikia bunduki mke wake, mzee huyu alikua akitetemeka sana kutokana na hasira hali iliyopelekea kutoweza kushika bunduki vizuri,hivyo alivyofyatua risasi ilimkosa mke wake na kupita dirishani ikampata Ronald aliyekua kwenye harakati zake za kujiua SHERIA INASEMAJE?? Mtu ukiwa na lengo la kumuua mtu 'A' lakini katika jaribio hilo kwa bahati mbaya ukamuua mtu 'B' basi unakua na hatia ya kumuua mtu 'B' Hapa wana usalama wakaona wamepata muuaji wao, Utata ukazidi kuibuka, mzee huyu nae anasema kua hakua na nia ya kumuua mke wake Bali alikua na lengo la kumtisha tu, anadai kua katika maisha yake yote hua haachi risasi zikae ndani ya bunduki, hivyo anashangaa nani aliyeweka risasi ndani ya bunduki yake, yeye alifyatua akiwa na uhakika kabisa kua bunduki yake haikua na risasi ndani hata moja.. Hili Linadhibitishwa na mke wake ambaye anadai mume wake amekua na 'katabia' ka kumtisha na bunduki miaka nenda rudi katika ndoa yao wakikorofishana,lakini si siku hata moja risasi ilitoka hata akifyatua NANI HASA ALIWEKA RISASI KWENYE HII BUNDUKI? Uchunguzi zaidi unaibua shahidi anayedai kumuona mtoto wa huyu mzee na mke wako akiweka risasi kwenye bunduki ya baba yake, Mtoto huyu wa kiume alikua na uhasama mkubwa na mama yake hali iliyopelekea mama yake kusitisha huduma zote za kifedha kwa mtoto huyu, mtoto huyu ikafika mahali akatamani kumuua mama yake,kea kuelewa tabia ya baba yake ya kumtisha mama yake na bunduki basi akaamua kuiwekea risasi ili baba akimtisha tena mama safari hii amuue kweli MTOTO HUYU YUKO WAPI? Katika hali ya kusikitisha inafahamika kua mtoto huyu ndiye hasa marehemu Ronald Opus, Ronald ndie huyu mtoto wa hawa wanandoa, Risasi alizoweka Ronald Leo hii ndio zimekatisha maisha yake. Ronald baada ya kuona maisha yanakua magumu na mtego alioweka ili mama yake afe hautimii aliamua kujiua kwa kujitupa kutoka kwenye jengo waliokua wakiishi, lakini risasi iliyofyatuliwa na baba yake ikamuua!! Hii kesi ilikuja kufungwa kama kesi ya kujiua(suicide) Kesi hii ilitikisa ulimwengu miaka ya 94,hali iliyopelekea vyombo vya habari vilivyokua vikiiripoti kupokea zaidi ya barua 2000 na simu zaidi ya 400 kutoka kwa watu mbalimbali duniani wakiomba kupewa kibali ya kuliweka tukio hili katika vitabu vyao au filamu.
 
Imekuja kwenye hili jukwaa, nikafikiri wadau wamechambua matukio haya kisheria
 
Duuu nmejikuta nacheka tu wakt naisoma hii jumbe

Pasua kichwa unaweza kumhukum MTU asie na hatia hapo........
 
Hii ngoja niigoogle maana mimi tomaso ni ngumu sana kuamini coincidence ya hivyo bila ushahidi kutoka source za kuaminika
 
Hivi kesi kama hii kwa Mazingira ya Tanzania, hukumu ingekua the same?
 
Hii kitu iliwahi kuletwa humu jukwaani muda mrefu. Na haikuwa kesi ya ukweli isipokuwa ni nadharia iliyoandikwa na kijana mmoja huko majuu ili kuwafikirisha wanasheria wasomi na maofisa wa polisi pamoja na jamii kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom