Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki-3: Ujue Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,452
113,458
Kwa Maslahi ya Taifa,
Jumapili 18/09/2022
Kazi inaendelea

Screen Shot 2022-09-19 at 9.22.36 AM.png
Screen Shot 2022-09-19 at 9.22.16 AM.png

Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea kuhusu Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo nikijikita kwenye Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, nikiwapeleka sura kwa sura. Sura ya kwanza ni tafsiri tuu maneno, hii nimeiruka na kuanza na sura ya pili.

SURA YA PILI: UANZISHAJI NA MISINGI YA JUMUIYA
Sura ya Pili inajumuisha Ibara ya mpaka ya 8. Pamoja na uanzishwaji wa Jumuiya yenyewe Ibara ya Pili inahusu uanzishwaji wa Muungano wa forodha wa Afrika Mashariki na Soko la pamoja. Ibara ya 3 inahusu muundo wa Jumuiya. Kibali na kutaja nchi tatu za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda kama wanachama waanzilishi, imeweka sifa na masharti kwa nchi nyingine kujiunga ni kuubali Mkataba, kukubali kanuni za demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu, mchango madhubuti wa nchi inayotaka kuwa mwanachama katika uimarishaji ushirikiano; ujirani mwema, uanzishaji na uendelezaii wa soko huria, na kukubali sera za kiuchumi na kijamii za Jumuiya.

Ibara ya 4 inahusu uwezo wa kisheria wa Jumuiya. Mbali na kuwa na hadhi ya kuwa chombo cha ùshirikiano, Jumuiya itakuwa na uwezo wa kupata, kumiliki, kutumia na kuuza ardhi na mali nyingine. Itaweza kukopa, kushitaki na kushitakiwa pia. Katibu Mkuu ndiye atakayekuwa. mwakilishi wa Jumuiya.
Ibara ya 5 inataja madhumuni ya Jumuiya, ambayo ni pamoja na kuunda sera na pragramu zinazolenga katika kuendeleza ushirikiano katika nyanja za siasa, uchumi, jamii, utamaduni, ulinzi, usalama, sheria na shughuli za mahakama. Katika kutimiza madhumuni haya, Nchi Wanachama zinakubaliana kuchukua hatua za kuanzisha muungana wa farodha, Soko la pamoja, na baadae, muungano wa sarafu na hatimaye Shirikisho la Kisiasa.

Ibara ya 6 inahusu misingi muhimu ya Jumuiya, ambayo ni pamoja na amani, upendo, mshikamano, ushirikiano, kuaminiana na ujirani mwema, utatuaji wa migogoro kwa niia ya amani, nchi kufuata misingi ya utawala bora, ugawanaji sawa na kwa haki manufaa ya Jumuiya.

Ibara ya 7 inahusu misingi ya utekelezaji ya Jumuiya, ambayo ni pamoja na ushirikiano unaoendeshwa na watu wenyewe kwa utaratibu wa Soko huria, uandalizi wa sera zinazovutia na miundombinu bora, uanzishaji wa sera za kiuchumi. zitakazosaidia uzalishaji wa bidhaa za kuuza nje, kufuata kanuni ya kusaidiana; na ugawanaji wa haki wa faida itokanayo na shughuli za Jumuiya.
Ibara ya 8 inahusu hatua za jumla za utekelezaji.

SURA YA TATU: UANZISHAJI WA VYOMBO VYA JUMUIYA
Ibara ya 9 inahusu auanzishwaji na uundaji wa vyombo na taasisi za jumuiya na idara na vitengo mbalimbali vya Jumuiya. Kila chombo kina majukumu yake maalum. Vyombo hivi vinapewa uwezo na majukumu kutoka jumuiya yenyewe. Mkutano wa Wakuu wa Nchi unaweza kuanzisha chombo kingine kipya.

Kwa sasa vyombo vya Jumuiya ni 7, Mkutano wa Wakuu wa Nchi, Baraza la Mawaziri, Kamati ya Uratibu, Kamati za Sekta, Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bunge la Afrika Mashariki na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

SURAYA NNE: MKUTANO WA WAKUU WA NCHI
Sura hii inajumuisha Ibara ya 10 mpaka Ibara ya 12.
Ibara ya 10 inahusu muundo wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi. Mkutano huu utawahusisha viongozi ambao ni wakuu wa nchi au wakuu wa serikali za Nchi Wanachama. Kwa sasa hivi, wakuu hawa ni Maraisi wa Nchi Wanachama, wan chi zote 7 zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaani Rais wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini na DRC.

Ibara ya 11 na ya 12 zinahusu kazi za Mkutano wa Wakuu wa Nchi. Mkutano wa Wakuu wa Nchi ndio utakuwa unatao maelekezo ya jumla kwa jumuiya. Hata hivyo, wakuu hawa wa nchi wanaweza kukasimu madaraka yao kwa maofisa au Vyombo vingine.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi ndio utakaokuwa ukitathmini hali ya amani na usalama katika eneo la Jumuiya. Utaangalia pia uwezekano wa kusonga mbele katika kuanzisha shirikisho la kisiasa.
Mkutano huu utakuwa ukiongozwa na mwenyekiti ambaye ni Rais wa mojawapo ya nchi za Afrika Mashariki. Uenyekiti huu utakuwa ukidumu kwa mwaka mmoja mmoja, na utakuwa na mzunguko kutoka nchi moja hadi nyingine miongoni mwa Nchi Wanachama.

Shughuli nyingine zitakazofanywa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi ni pamoja na kuteua Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki, kupokea wanachama wapya, au kukaribisha watazamaji.
SURA YA TANO:BARAZA LA MAWAZIRI Sura hii inajumuisha Ibara ya 13 mpaka Ibara ya 16.
Ibara ya 13 inazingatia muundo wa Baraza la Mawaziri. Baraza hili litaundwa na mawaziri ambao watakuwa wamekwishateuliwa tayari na nchi zao kwa malengo ya ushirikiano wa kimataifa au kwa malengo ya ushirikiano wa Jumuiya.

Ibara ya 14 inahusu kazi za Baraza la Mawaziri ambazo zitakuwa ni pamoja na kutengeneza sera za Jumuiya. Baraza litakuwa pia na kazi ya kuangalia shughuli za kila siku za Jumuiya ikiwa ni pamoja na kukagua na kusimamia shughuli hizo. Baraza hili ndilo litakalokuwa na jukumu la kuangalia kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inaendelea na shughuli zake kama kawaida. Baraza la Mawaziri litakutana mara mbili kwa mwaka.

Wiki Ijayo nitaendelea kwa kufundisha kuijua Mahakama ya Afrika Mashariki na Bunge la Afrika Mashariki- EALA.
Wasalaam
Paskali 0754 270403
 
Ukiyasema haya utwambie ni namna gani tutaenda kutafuta na kupata kazi huko kwenye jumuiya yetu pendwa, prospectus gani tutumie kuangalia kazi huko jumuiani!!

je kunatenda za kuwalisha wafanya kazi wa jumuiya je hao viongozi wanapokutana wanakula nini bila sisi kupewa tenda za kulala na chakula bora kwao??...shule kwetu sisi na watoto wetu zinapatikana jumuiani??

Wafanya biashara sisi tunataka Masharti nafuu ya jumuiya yetu pendwa kotekote tunapataje?..wafanya kazi wa kawaida hawa wasio wa jumiya kwa mfano madaktari waalimu,makarani nk!

Hao wafanya kazi wanapataje vibali au u free wa kwenda kutafuta kazi kwingine ndani ya jumuiya? mfano CO /SNO ataajiliwaje Kinshasa?? mchakato ukoje!.....

Mimi/sisi ...wanafunzi/watoto wetu/ watu/ wa kawaida wenye uchungu wa hali na Mali na jumuiya hii ya EA wakereketwa, mnatupa nafasi gani ya kuunga mkono jumuiya hii....

je twawezaje kuhudhuria vikao hivo japo hata kwa muda na gharama zetu binafsi hiyo nafasi ipoooo! Naweza kuwa Mwandishi wa habari mwenye mapenzi wa jumuiya hii ki vipi?......

walio tyari kujitolea ajili ya kusongesha jumuiya wanapokelewa wapi! na wana ruhusiwa kujitolea Bure kwa miaka mingapi! ....any way ninayo mengi ila tuanzie hapo kwanza!

kama una prospectus mwaga hmu!
 
Back
Top Bottom