Ijue historia yetu

king majah

Member
Jan 10, 2013
61
50
Je unamjua Rashid Ally Meri?
Huyu ni kijana wa zamani ambaye alifanya kazi katika ofisi za Dar es salam municipal council akiwa kama mweka hazina.
Huyu alikuwa nmoja ya wajumbe 20 waliohudhuria mkutano wa mwanzo wa TANU wa mwaka 1955 wakiwa pamoja na kina mzee Chaurembo,Said Chamwenyewe,Abdul wahid Sykes,Dosa Aziz,L.Seat on,Clement Mtamila na wengine wengi.
Wakati TANU wanapanga safari ya Mwl Nyerere kwenda UNO pesa hazikutosha hivyo changisha changisha ikaanza,Mzee rupia akachangia theluthi tatu ya gharam,kisha Iddi faizi mafongo akatoa pesa za jamiatul muslim kuongezea gharama za nauri na chakula cha safarini kwa Mwl Nyerere.Lakini hazikutosha hivyo Mwl kahere Kule Tanga akaagiza TANU waende Tanga kuchukua mchango wao.
Wakati ule nauli ya kwenda marekani ilikuwa 12000.
Iddi faizi Mafongo alipoenda Tanga kuifuata pesa Special branch wakapta taarifa(usalama wa taifa wa enzi hizo)
Hivyo wakakusudia kumkamata njiani akiwa anarudi kutokea Tanga.
Walifanikiwa kusimamisha basi alilopanda pale Turiani lakini walipomkagua hawakumkuta hata na senti.Iddi faizi Mafongo pesa ile alimpa binti yake mdogo ambaye special branch hawakumkagua.Hivyo pesa ikawafikia TANU kama ilivyokusudiwa.
Turudi kwa mlengwa wetu Rashid Ally Meri ambaye nae baada ya kuona pesa hazitoshi alikwenda kubeba pesa za Dar es salaam municipal council na kuwapa TANU kwa sharti warejeshe pale tu watakapopata Kabla haijagundulika.
Chaajabu kesho yake tu special branch wakapata taarifa na kupekeleka auditors ofisini kwake na kuomba kukagua mapato na matumizi...
Siku ile ile jioni Rashid Ally Meri akawaona viongozi wa TANU na kuwahadithia. Kilichotokea.....TANU wakajichanga ili kumuokoa Rashid Ally Meri asije akafungwa.
Pesa ikapatikana akafanikiwa kuirejesha kabla mambo hayajaharibika
Huyo ndio Rashid Ally Meri ambaye historia yake huwezi kuipata kwenye vitabu vya historia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom