Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 15,792
- 28,434
Tupo pamoja
Duh, pole kama boss kubwa kaitwa hivyo mi nani mpaka niumie?
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Habari wandugu , tuendelee na tulipoishia baada ya Rouhan kukataa kukutana na Obama, tarehe 26 mwezi wa tisa serikali ya Iran na marekani zilifanya kikao kikubwa cha maofisa wa ngazi za juu ambacho hakikuwahi kufanyika tangu mwaka 1979.
Kikao hicho kiliongozwa na mkuu wa sera za mambo ya nje wa umoja wa ulaya Bi Catherine Ashton.
Maongezi hayo yalionekana kuleta matumaini ya kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili, siku iliyofuatia rais Rouhani na Obama walizungumza kwa njia ya simu, hilo tukio lilikuwa la kipekee ambalo halikuwahi kutokea tangu mwaka 1979.
“Marg ba Amrika” ni maneno yaliyosikika katika jiji la Tehran wakati Rais Rouhani akiwasili jijini hapo, maneno hayo yalitoka kwenye vinywa vya waandamanaji wasiopenda mahusiano ya nchi yao na Marekani, hii ni baada ya kupata taarifa kwamba rais wao ameongea na Obama. Kwa lugha ya Persians “Marg bar Amrika” ina maanisha “Death to America” yaani “Kifo kwa marekani” au “Mauti kwa Marekani”.
Msemo huu kwa wamiliki wa lugha ya kiingereza wanaupooza makali na kuutafsiri kama “Down with America”.
Kwa upande wa Iran kuna kundi kubwa la raia wanaotamani serikali yao ijenge mahusiano mema na marekani, na hii ilionekana katika kumbukumbu ya miaka 34 ya utekaji katika ubalozi wa marekani jijini Tehran (2013-1979=34) ambapo waandamanaji hao walikusanyika katika eneo lilikuwa ubalozi wa marekani mwaka 1979 kulaana kitendo cha kuchelewesha mahisiano kati ya nchi hizo mbili ambapo wao wanaona serikali yao ndio inakwamisha.
Barack Obama mtu asiye na kinyongo au kama vitabu vya kidini vinavyotamka “mtu asiye na hila” alikuwa akiwapa watu mikono na ikatokea amepeana mkono na waiziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, hii ndio mara ya kwanza kwa rais wa marekani kushikana na mwanadiplomasia mkubwa wa Iran tangu mwaka 1979 (mwaka wa mapinduzi ya Iran), hii ilikuwa ni mwaka 2015 tarehe 28 mwezi wa 9.
Baada ya handshake katibu wa serikali wa marekani akamtambulisha Obama kwa maafisa wengine wakubwa wa Iran walioshiriki JCPOA (Iran deal utaiona aya inayofuata). Kitendo hicho cha kupeana mikono kiliwachukiza baadhi ya wabunge wa Iran na kumtaka waziri aombe radhi hadharani.
Kabla sijazungumzia Iran Nuclear Deal naomba nielezee “Kura turufu” , yaani nazungumzia nchi zenye kura turufu, ni mataifa matano duniani ambayo yana nguvu Zaidi katika maamuzi ya umoja wa mataifa , ni nchi ambao ni wajumbe wa kudumu wa baraza la Amani la umoja wa mataifa, hivyo wao ndio wanakuwa na maamuzi ya mwisho katika mada za baraza hili na wengi wakipitisha jambo linaamuliwa na kama mjumbe hakushiriki haitabatilisha uamuzi.
Hivyo Joint Comprehensive Plan of Action (JCPOA, or the Iran Deal) ni makubaliano ya pamoja juu ya matumizi ya nyuklia nchini Iran , waliokaa kuweka makubaliaona hayo ni Iran na zile nchi tano zenye kura turufu ukiongeza na Ujerumani, unaweza kujionea kuwa nguvu za nyuklia zinahusisha moja kwa moja baraza la Amani duniani ndio maana kikao hicho kiliitiswah , hiyo ilikuwa ni mwaka 2015 mwezi was aba tarehe 14.
Mataifa yenye kura turufu ni Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa na China, katika kikao hicho aliongezeka na ujerumani bila kusahau uwakilishi wa umoja wa ulaya. Katika kikao hiki Ujerumani alikaribishwa kwa sababu kuu moja tu , alikuwa ndiye msingi wa biashara ya nyuklia huko Iran, yeye ndiye aliyekuwa kimuuzia vifaa na huduma nyinginezo. Vinu vya nyuklia Iran vinatumia softwares za kampuni ya ujerumani Siemens (Simatic WinCC step7).
Viwanda mbali mbali vya ujerumani vina matawi yake Iran na zaidi ya makampuni 12000 ya ujerumani ya wawakilishi wa biashara Iran.
Katika mkutano huo utawala wa Obama ulikubali kuwaondolea Iran vikwazo vya kiuchumi vilivyodororesha uchumi wao kwa miaka na Iran iliahidi kuachana na mpango wake wa Nyuklia na kuruhusu wakaguzi wa umoja wa mtaifa kwenda kukagua muda wowote wanaotaka.
Hivyo Iran ilikubali “Katika mazingira yoyote haitojaribu kutafuta, kutengeneza au kumiliki silaha yoyote ya nyuklia”. Ndani ya marekani mkataba huu ulikubaliwa na asilimia 50 pekee ya raia katika tafiti iliyofanywa.
Tukirudi tena tutaangalia Utawala wa Donald Trump, kuanzia 2017, kwa 2016 mgogoro huu ulikuwa wa kisheria Zaidi kwa mataifa hayo kutishia kudaiana fidia kwa matukio yaliyofanyiana katika historia lakini hamna lililotekelezwa.
Bado inaendelea…………………………………………………………..
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimetingwa kidogo , ila najitahidi niisogeze hivyo hivyoSema leo umeweka fupi mno mkuu TRANSPONDER
Aah babu kubwa 👏👊💯SEHEMU YA KUMI NA NNE
Mbaguzi wa rangi, Mnyanyasaji wa kijinsia, Kibaraka wa Urusi , Mwizi wa Demokrasia, Aliyeoa kahaba, Mbaguzi wa kidini na mbabe, Hayo ni baadhi ya majina yaliyotumika na wapinzani wake kumtaja rais wa 45 wa marekani Donald Trump.
Akiwa na wiki moja tu tangu aapishwe kuwa Rais wa marekani alikuja na Executive order 13769 nyaraka yenye kichwa kinachosema “Protecting the Nation from Foreign Terrorist Entry into the United States” naweza kutafsiri kwa kusema “kulilinda taifa kwa kuzuia magaidi kutoka nchi za nje kuingia marekani” , hii wanasiasa walikuwa wakiitafsiri kama “katazo hilo ni kwa ajili ya waislamu” wengine wakisema katazo hilo ni kupunguza wasafiri wanaoingia marekani .
Waliokumbwa na “travel ban” hiyo ni Iran pamoja na nchi zingine zilizohusishwa na ugaidi, hapa kama ni mfuatiliaje wa taarifa hizi nadhani utakumbuka kipindi kile marekani anaorodhosha nchi zitakazoathiriwa na ban hii , nchi hizo ni Iran, Iraq, Libya , Somalia , Sudan, Syria na Yemen, wasafiri Zaidi ya 700 walizuiwa kuingia marekani na VISA Zaidi ya 60000 zilikataliwa.
Hiyo ilikuwa 27 January 2017. Serikali ya marekani hairuhusu mtu yeyote ambaye ni raia au anayeshukiwa kuwa ni raia wa Iran kuingia marekani labda awe anapita kama njia, yaani zile ndege zinaenda nchi fulani basi lazima zipitie nchi fulani kujaza mafuta au kuongeza abiria. Abiria wote na wafanyakazi wa ndege zinazoingia marekani kutoka nchi yoyote ile lazima wahakikishe hawana VISA za Iran katika Passport zao yaani muhuri wa kuingia Iran usiwepo kwenye passport zao. Vilevile hakuna ndege ya moja kwa moja kutoka Iran kwenda marekani hivyo safari zote lazima zipitie katika nchi nyingine, Zaidi ya hayo hakuna ndege yoyote ya Iran inayoruhusiwa kupita katika anga la marekanin.
Katika harakati za kuidhoofisha Iran utawala wa rais Trump umeonekana kuingia katika njia ya kuimarisha umoja usio rasmi kati ya Saudi Arabia, Israel, U.A.E na mataifa mengine ya katika ghuba ya kisunni.
Kipindi cha kampeni za uchaguzi Trump aliwahi kunukuliwa akilaani JCPOA (Iran deal) kwa kusema ni dili la hovyo kabisa kuwahi kujadiliwa na linaweza kupelekea madhara makubwa Zaidi ya nguvu za nyuklia duniani, lakini katika hali ya kustaajabisha mwezi wan ne 2017 iliweka hadharani kwamba Iran bado inatimiza makubaliano ya JCPOA , Nadhani bado mnakumbuka ahadi ya Iran katika dili hilo kwamba haitomiliki , kujaribu kumiliki ama kutengeneza silaha za nyuklia.
Mgogoro huu unatumika sana kisiasa nchini Iran na marekani kama moja wapo ya sera za kumuingiza mtu ikulu, kama ulivyo umaskini nchi za afrika. Wenzetu wameendelea kidogo kwani wengi wao wanatumia sana mitandao ya kijamii kama Twitter , kutoka January hadi July pekee mwaka 2017 Twitter walitambua na kuzifungia account bandia Zaidi ya 7000.
Mchezo huo wa accounts bandia unatumika sana kwa wenzetu na ni katika level za kimataifa, accounts nyingi zilionekana kuwepo urusi na Iran na zililenga kutoa taarifa za uongo juu ya mgogoro huu au habari nyingine za siasa nchini marekani kwa ajili ya kuathiri uchaguzi ujao wa nchi hiyo,
yaani ni kama watanzania tuwachezee wakenya mchezo huu tukitaka aingie madarakani rais tunaemtaka sisi. Mfano kuwe na account Zaidi ya 100 kama za kigogo_14 halafu kumbe sio za Tanzania , wamekaa nchini kwao mfano (Rwanda) wanacheka tu namna waziri akijibizana nae kama ni mtanzania kumbe yupo Kigali na analipwa na serikali ya huko (NIMETOA MFANO, MSINI-QUOTE vibaya).
Mwezi huo huo July wabunge wengi wa Congress kutoka republican na democratic walipigia kura za ndio muswada wa CAATSA (Countering America’s Adversaries Through Sanctions Act) yaani kukabiliana na maadui wa marekani kupitia vikwazo. Maadui hao wakubwa ni Iran, Urusi na Korea ya Kaskazini. Mwezi wa nane tarehe mbili rais trump alisign na kuifanya kuwa sheria.
Kuiwekea Iran vikwazo nadhani mnakumbuka ni kinyume na JCPOA , Wakati utawala wa Trump ukitangaza kwamba wameridhika baada ya kuthibitisha Iran inafuata makubaliano ya mkataba huo. Sasa marekani anaweka vikwazo kwa maadui wake na kuijumuisha Iran. Yaani inakiuka mktaba wa JCPOA.
Maamuzi hayo ya Bunge yalikuwa mabaya kwa Iran kwani inairudisha katika mdororo wa kiuchumi , naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araqchi alisema kwamba “kwa mtazamo wetu ni kuwa mkataba wa nyuklia umekiukwa” na katika mkutano wa UN Septemba 2017 maraisi wan chi hizo mbili walitoa mitazamo inayopingana juu ya mkataba wa JCPOA.
Kufikia mwezi wa tano waka 2018 , Rais Donald Trump aliamua kujitoa katika mkataba wa JCPOA na kutangaza ataweka vikwazo vya kiuchumi kwa Iran kuanzia tarehe 4 mwezi November 2018. Kwa upande wa Iran Rais Hassan Rouhani naye akasema anaweza kuanza kutengeneza Nyuklia bila kizuizi chochote. Tarehe 5 mwezi wa saba Iran ikatishia kufunga Strait of Hormuz kama marekani itawawekea vikwazo katika biashara ya OIL baada ya kujitoa katika JCPOA.
Strait (mkondo bahari) ni sehemu nyembamba ya maji inayounganisha bahari mbili au maziwa, naweza kuita mkondo wa maji kwa Kiswahili kama sijakosea, hivyo strait of Hormuz inaunganisha Ghuba ya Oman na Ghuba ya Persia. Ni miongoni mwa sehemu muhimu Zaidi kimkakati duniani , kijeshi sehemu za namna hiyo zinaitwa “Choke Points”, hizi sehemu zinafaa Zaidi kwa ambush, lakini pia kwa hii kufungwa ingezuia meli kutoka ghuba ya Oman. Mfano ni mkondo bahari wa Gibraltar unaounganisha bahari ya Mediterranean na Bahari ya Atlantiki.
Nimeweka picha hapo chini unaweza kujuionea eneo hilo.
Kwa leo hapa inatosha , maadam tumefika kwa trump basi twende nae mdogo mdogo……………………………………………………………………………..View attachment 1332332
Sent using Jamii Forums mobile app
Adhuhuri inaisha mpk mda huu ni kimyaaa...SEHEMU YA KUMI NA NNE