Ijue historia ya mgogoro kati ya Iran na Marekani

SEHEMU YA KUMI NA SITA

Ikiwa bado tupo mwezi may 2019 akatika historia hii, nianze na kuwasalimu na kuomba radhi kwa kuchelewesha muendelezo wa historia hii, nadhani tunaweza kujionea matukio yanavyokimbizana katika dunia ya utandawazi, ukiamua kuelimika Zaidi unajikuta upo busy kusoma taarifa na vitabu , ukijumlisha na Kazi zako za kila siku basi unamalizia kwa kusema “MAMBO NI MENGI MUDA MCHACHE”

Ila yote yanawezekana kwa kupangilia ratiba yako vizuri. Basi tuendelee na mgogoro huu kwa kuanza na tangazo la John Bolton ambaye ni mshauri wa ulinzi katika serikali ya marekani kuwa marekani inapeleka USS Abraham Lincoln Carrier Strike Group na B-52 bombers kwenda mashariki ya kati ili kutuma ujumbe kwa Iran baada ya kupokea taarifa za kiintelijensia kutoka Israel kuwa Iran inapanga kushambulia majeshi ya marekani yaliyopo eneo la mashariki ya kati. Bolton aliongeza na kusema kwamba “Marekani haitafuti vita na utawala wa Iran bali imejidhatiti kujibu mapigo kwa shambulio lolote”.

USS Abraham Lincoln ni moja wapo kati ya meli mbili zilizopewa jina kumuenzi rais Abraham Lincoln , maskani yake ya kudumu ni bandari ya NAS North Island , hii ni meli yenye kubeba ndege za kivita , kwa watazamaji wa movies nadhani mmewahi kuona meli ambayo juu ina Runway ya ndege, nimewaambatanishia picha hapo chini , unaweza kujionea.

Sasa ukiongezea hapo mbele hilo neno la Carrier strike group unakuwa unazungumzia moja ya mfumo wa operesheni ya kijeshi nchini marekani ambayo inajumuisha wanajeshi 7500 , Aircraft carrier (sea going airbase) , Cruiser (Meli ya kawaida ya kijeshi), Destroyer squadron yenye destroyer Zaidi ya mbili (meli iliyobeba makombora na inauwezo wa kushambulia katika uelekeo maalum), pia kuna Carrier airwing yenye ndege 65 hadi 70, Zaidi ya hayo Carrier srike inajumuisha nyambizi, meli za silaha na meli ya kusupply mahitaji mbali mbali kama Oil.

B-52 ni jet ya kivita inayotengenezwa na boeing, inauwezo wa kurusha makombora ya masafa ya mbali.
Hapo unaweza kuimagine ni kitisho kikubwa namna gani marekani ilituma kwa Iran, Balaa hiyo ya marekani imepaki katiaka Arabian Sea nje kidogo ya Ghuba ya Persia. Hii kama umekuwa mgumu kuielewa basi kumbuka wakati watanzania waliokuwa wakishabikia vuguvugu la maandamano nchi nzima lililoanzishwa na Mange Kimambi, Jeshi la polisi likaanza kufanya mazoezi kona mbalimbali nzhini.

Tarehe 7 mwezi wa tano 2019 US secretary of state Mike Pompeo alifanya ziara ya ghafla usiku wa manane jijini Baghdad baada ya kughairisha mkutano wake na Chancellor Angela Merkel , Pompeo alimwambia rais wa Iraq Barham Salih na waziri mkuu Adel Abdul Mahdi kwamba wana wajibu wa kuwalinda wamarekani waliopo Iraq.

Kesho yake mshauri wa Ayatollah Khamenei alisema Iran inauhakika kuwa marekani haina nia wala uwezo wa kuanzisha vita na Iran. Pia Iran ikatangaza kupunguza kuzigatia mkataba wa JCPOA ambao marekani alishajitoa tangu mwaka mmoja uliopita , na Rais wa Iran akatoa siku 60 kwa umoja wa ulaya nan chi zenye nguvu duniani kunusuru mkataba huo (JCPOA) kabla hawajaanza kujitajirisha Zaidi na nguvu za nyuklia.

Marekani waliendelea kuongeza vifaa vya kijeshi katika eneo la mashariki ya kati kwa kisingizio kwamba wanalinda interest zao katika hilo, tarehe 10 mwezi September John Bolton Mshauri wa mambo ya ulinzi alijiuzulu , nadhani tumeweza kujionea namna alivyocheza nafasi yake katika mgogoro huu , kufuatia kujiuzulu kwake Iran ilisema haitopelekea mazungumzo kati ya Iran na marekani , Na tarehe 16 september Iran ikatoa tamko kuwa rais wao Hassan Rouhani hatokutana na Rais trump katika mkutano wa umoja wa mataifa labda kama vikwazo dhidi ya Iran vitaondolewa.

Mwaka huo huo wa 2019 mwezi wa tano , meli nne za kibiashara ukijumuisha mbili za Saudi Amarco (Saudi Arabia oil company inayofanya bishara ya mafuta na marekani) zinazobeba mafuta ziliharibia katika bandari ya Fujairah iliyopo Ghuba ya Oman, meli hizi zilikutwa na matundu yaliyosababishwa na milipuko kwenye pipelines, Serikali ya marekani baada ya kufanya ukaguzi ikaitupia lawama Iran na washirika wake kwamba wanahusika moja kwa moja au kwa namna nyingine.

Wakati mgogoro baina yao unazidi kukomaa ubalozi wa Marekani nchini Iraq ukasema Raia yeyote wa marekani asiruhusiwe kusafiri kwenda Iraq na wale ambao wameshafika basi waishi katika hali ya tahadhari na kutojionyesha, hioyo ilikuwa tarehe 13 may 2019, na siku hiyo hiyo New York Times liliripoti kuwa anae kaimu US defense secretary amewasilisha mpango wa kupeleka wanajeshi 120,000 mashariki ya kati endapo Iran watashambulia wamarekani au wakichukua hatua ya kutengeneza silaha za nyuklia. Rais Trump akapigilia msumari wa mwisho kwa kusema atatuma wanajeshi Zaidi ya 120,000 kama kukiwa na umuhimu wa kufanya hivyo.

Tarehe 14 mwezi may 2019 maafisa wa nchi zote mbili (Marekani na Iran ) walisema kwamba hawatafuti vita ingawa majibizano ya vitisho baina yao yanaendelea. Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Khamenei katika runinga ya taifa alitamka kwamba ( Hakuna vita itakayotokea ) pia Mike pompeo akiwa Russia alisema “Hatutafuti vita na Iran” , katika siku hiyo hiyo Waasi huko nchini Yemen walishambulia bomba la mafuta la Saudi Arabia kwa kutumia Ndege zisizo na rubani (Drones), Marekani waliokuja kutoa taarifa kwamba Iran ndio ilifadhili shambulio hilo.

Ingawa bado shambulio hilo halikujulikana chanzo chake kikuu ni kipi katia ya mgogoro wa Iran na Marekani au Vita ya wenyewe kwa wenyewe huko Yemen ambayo Saudi Arabia aliingilia. Kufuatia vuguvugu hilo kuendelea , Marekani akaona hatari inayowakabili raia wake hivyo tarehe 15 May 2019 ikaamuru wafanyakazi wote wasiohusika na huduma za dharura ubalozini nchini Iraq waondoke katika ubalozi huo.
Then tarehe 19, may 2019 rais Trump akatoa tamko kwamba Mgogoro huo unaweza kusababisha mwisho wa taifa la Iran kuwepo, Waziri wa mambo ya nje wa Iran akajibu kwa kusema “Mauaji yatakayofanywa na Trump hayawezi kuiangamiza Iran” , Siku hiyo hiyo kombora lilidondoshwa karibu na ubalozi wa marekani , Baada ya tishio hilo la kombora marekani wakaongeza wanajeshi katika ghuba ya Persia kama kujikinga na Iran, Pia wakatoa tamko kwamba wanauhakika asilimia zote kwamba Iran ndio ilihusika na tukio la kushambulia meli za mafuta pia wao ndio walirusha kombora karibu na ubalozi wa marekani nchi I Iraq.


Itaendelea………………………………………………….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninakumbuka 1980 tulikwenda kwenye maonyesho ya biashara Kilwa Road na mabanda yote mawili la Iran na Irak yalipendeza sana. Mzee wangu alinihadithia juu ya mapinduzi ya Iran ingawa sikuelewa vizuri wakati ule.
Kumbe wewe muhenga mwenzangu, mimi nakumbuka baba yangu alikua napokea nakara ya gazeti kutoka Iran kila mwezi linaitwa SAUTI ya UMMA au SU, lilikua linaelezea mambo mabaya ya Iraq na Rafiki zake including USA na mambo mazuri aliokua akiyafanya marehemu Khomein, zilikua ni habari za upande mmoja tu, sikujua hasa kilichokua kibaya kwa Iran. Hongera kwa mleta UZI
 
Hii wakuu , mtandao ulisumbua wakati wa kuattach
Screenshot_20200128-153959_UC%20Browser~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom