Ijue Historia ya mchawi mmoja toka huko Kilombero - Morogoro

Heisenberg

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
1,248
2,000
Dunia ina mambo Mengi sana na mengine usiyoyajua

Nikiwa Maeneo hayo ya kilombero Niliwahi kuona uchawi ambao sitasahau.

Kuna kijana mmoja aliombwa aangue nazi kutoka kwenye mnanzi wa mzee fulani, Jamaa akavaa kamba miguuni akapanda akashusha nazi za kutosha.

Wakati anaendelea na hararakati zake za ukwezi juu ya mnazi mara akaanguka.

Ikapigwa yowe mara majirani wakaja kuanza kusaidia jamaa akawa kafa, wakati watu wanazidi kuongezeka kwenye Tukio mara vipande vya Sabuni ya mche vikaanza kuanguka toka juu ya huo mnazi,

Watu walihisi kitu wakakausha. Next day wakazika. ni ile misiba inakuwaga na wahuni wengi wa vijiweni na stand, so wakenda wakamzika mwana.

Jamaa wakarudi kijiweni wakaanza njama za kwenda kumdifit yule mzee mwenye mnazi ambae ndie alisadikika amemchujua jamaa KIMASKHARA

Wahuni wakapanga mission mambo yakaenda.

Siku moja mzee kaamka asubuhi ana mtindo wa kuzunguka kwenye compaund yake Akatahamaki Hamaaaaad watu hawa hapa wamejaa nje.

Mzee shikamoo, sisi ni wageni zako

Samahani wanangu ngoja niingie kwanza ndani ndio tuongeee

Hapana mzee hakuna kuingia ndani
Mshikeni mshikeni huyo asiingine ndani anaenda kuurudisha uchawi wake, mshikeni tumpeleke kwa kalembwana.

Baada ya hapo wakaagiza Guta ( Baiskeli ya pedili ya miguu mitatu) Wakamfunga na manati safari ikaanza kwenda kwa Bibi Kalembwana

Kelele zikawa kubwa mji mzima jamaa anapelekwa kwa Bibi kalembwana kwenda Kunyolewa.

BIBI Kalembwana ni nani????

Huyu ni bibi mganga alishakufa tayari, siku hizi wapo wajuu zake ndio wanafanya uganga

Yeye alikuwa mtaalam wa kuneutralize uchawi

Let say mm nimekuhisi au nimekukamata ww kuwa mchawi, basi tunatoka wote tunaenda kwa kalembwana yeye anatunyoa nywele zote, kichwani kwapani kila sehemu ananyoa hadi Vuzi, hadi Vuzy Mku.ndu anafyeka bila huruma

Kisha anakupakaa Dawa kama unga mweupe unalala hapo kwake kama siku mbili.

Pia yule alie mkamata mwenzake uchawinhuwa anatakiwa aende na kuku. Huyu kuku anachinjwa anapikwa kwa ajili ya kuliwa na wale mahasimu wawili waliopelekana kwa Bibi

Mara zote yule mchawi hawezi kula chakula. Akilenga tonge mdomoni linakimbia linaenda shavuni, yani hawezi kula kabisa,

Baada ya Kumjua Kalembwana ni nani basi tuendelee
Safari ikawa inaendela ya kwenda kwa kalembwani huku Guta linaendeshwa kwa nguvu watu wanalikimbiza nyuma

Yule mzee hakufanikiwa kuuacha uchawi wake alikuwa nao wakati anapelekwa kunyokewa

Safari anaanza kuwa ngumu

Wakati wapo njiani wamefika sehemu moja sijui kunaitwa wapi ila ni njia panda ya kwenda sijui ni wapi(Mnisahihishe) Babu akazua nongwa

Mara Guta likapata pancha safari ikawangumu wakapata sehemu wakaziba, mara mbele kidogo pancha tena, kumbe yule mzee ndio alikuwa anasababisha zile pancha kichawi

Jamaa walivyojua jua kuwa ni yeye walichuma viboko wakampiga Mbarati za kufa mtu
Akalia kinyama hadi huruma
ikabidi yule mzee kujiokoa akaiziba ile pancha kichawi mara tairi ikawa na upepo safari ikaendelea.

Wakati Wamefika karibia kwa mganga guta ikapata tena pancha. Hii ilikuwa pancha ya ukweli kabisa ya kukanyaga msumari,

Wahuni wawakujali wakampiga tena fimbo hatari mzee jinsi alivyokuwa nguli akaziba na hiyo pancha

Wakifika kwa kalembwana akaanza kuleta makeke baada ya kujulikana ni mchawi akawa hataki kunyolewa, kalembwana akasema muacheni alale atanyolewa kesho

Kesho yake akaamka akiwa kashanyokewa tayari mwili mzima na kapakazwa dawa, akaruhusiwa aondoke

Aliona aibu kurudi na watu ikabidi aende kuomba msaada kwa watu ahidhiwe akapelekwa mzee moja kwenye Mila sijui za wapogoro au wandamba wa huko Kilombero na ulanga wanamuita "Mbuyi"

Huyo mbuyi ndio akamhifadhi kwake kwa siku kadhaa kisha akamsafirisha kimazingara hadi kwenye vichaka karibu na kwake

Mbuyi ni nani?

Ni wazee wa kimila huko Kilombero na Ulanga na Malinyi.

Hawa wazee ni zaidi ya wachawi/ Waganga

Kwanza hawakai kwenyewe nyumba za bati ni mwiko kabisa, hata akiwa na nyumba ya bati lazima atajenga ya nyasi pembeni na ataishi hapo

pia Mambuyi huwa hawavai kitu chochote mguuni. huwa wapo peku mda wote

Mbuyi akitaka kusafiri Let say Dar to Moro anatembea kidogo tuu anaingia Kichakani anapaa anaenda kutua Moro chaaap Dk. 0 Kwenye kichaka kingine anaendelea na mishe zake

Mtu yoyote alie kaa maeneo ya Kilombero, Mlimba, Malinyi, Ulanga/ Mahenge lazima atakua anajua ligi za mambuyi

Mwisho.
 
Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,857
2,000
Wanaitwa kalembwani.
Ok.
Story nzuri sana
Uchawi uuzwe rasmi kwa uwazi hii itasaidia kuinua uchumi wa wachawi na taifa
 
mroya

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
282
250
Dunia ina mambo Mengi sana na mengine usiyoyajua

Nikiwa Maeneo hayo ya kilombero Niliwahi kuona uchawi ambao sitasahau.

Kuna kijana mmoja aliombwa aangue nazi kutoka kwenye mnanzi wa mzee fulani, Jamaa akavaa kamba miguuni akapanda akashusha nazi za kutosha.

Wakati anaendelea na hararakati zake za ukwezi juu ya mnazi mara akaanguka.

Ikapigwa yowe mara majirani wakaja kuanza kusaidia jamaa akawa kafa, wakati watu wanazidi kuongezeka kwenye Tukio mara vipande vya Sabuni ya mche vikaanza kuanguka toka juu ya huo mnazi,

Watu walihisi kitu wakakausha. Next day wakazika. ni ile misiba inakuwaga na wahuni wengi wa vijiweni na stand, so wakenda wakamzika mwana.

Jamaa wakarudi kijiweni wakaanza njama za kwenda kumdifit yule mzee mwenye mnazi ambae ndie alisadikika amemchujua jamaa KIMASKHARA

Wahuni wakapanga mission mambo yakaenda.

Siku moja mzee kaamka asubuhi ana mtindo wa kuzunguka kwenye compaund yake Akatahamaki Hamaaaaad watu hawa hapa wamejaa nje.

Mshikeni mshikeni huyo asiingine ndani anaenda kuurudisha uchawi wake, mshikeni tumpeleke kwa kalembwana.

Baada ya hapo wakaagiza Guta ( Baiskeli ya pedili ya miguu mitatu) Wakamfunga na manati safari ikaanza kwenda kwa Bibi Kalembwana

Kelele zikawa kubwa mji mzima jamaa anapelekwa kwa Bibi kalembwana kwenda Kunyolewa.

Huyu ni bibi mganga alishakufa tayari, siku hizi wapo wajuu zake ndio wanafanya uganga

Yeye alikuwa mtaalam wa kuneutralize uchawi

Let say mm nimekuhisi au nimekukamata ww kuwa mchawi, basi tunatoka wote tunaenda kwa kalembwana yeye anatunyoa nywele zote, kichwani kwapani kila sehemu ananyoa hadi Vuzi, hadi Vuzy Mku.ndu anafyeka bila huruma

Kisha anakupakaa Dawa kama unga mweupe unalala hapo kwake kama siku mbili.

Pia yule alie mkamata mwenzake uchawinhuwa anatakiwa aende na kuku. Huyu kuku anachinjwa anapikwa kwa ajili ya kuliwa na wale mahasimu wawili waliopelekana kwa Bibi

Mara zote yule mchawi hawezi kula chakula. Akilenga tonge mdomoni linakimbia linaenda shavuni, yani hawezi kula kabisa,

Safari ikawa inaendela ya kwenda kwa kalembwani huku Guta linaendeshwa kwa nguvu watu wanalikimbiza nyuma

Yule mzee hakufanikiwa kuuacha uchawi wake alikuwa nao wakati anapelekwa kunyokewa
Wakati wapo njiani wamefika sehemu moja sijui kunaitwa wapi ila ni njia panda ya kwenda sijui ni wapi(Mnisahihishe) Babu akazua nongwa

Mara Guta likapata pancha safari ikawangumu wakapata sehemu wakaziba, mara mbele kidogo pancha tena, kumbe yule mzee ndio alikuwa anasababisha zile pancha kichawi

Jamaa walivyojua jua kuwa ni yeye walichuma viboko wakampiga Mbarati za kufa mtu
Akalia kinyama hadi huruma
ikabidi yule mzee kujiokoa akaiziba ile pancha kichawi mara tairi ikawa na upepo safari ikaendelea.

Wakati Wamefika karibia kwa mganga guta ikapata tena pancha. Hii ilikuwa pancha ya ukweli kabisa ya kukanyaga msumari,

Wahuni wawakujali wakampiga tena fimbo hatari mzee jinsi alivyokuwa nguli akaziba na hiyo pancha

Wakifika kwa kalembwana akaanza kuleta makeke baada ya kujulikana ni mchawi akawa hataki kunyolewa, kalembwana akasema muacheni alale atanyolewa kesho

Kesho yake akaamka akiwa kashanyokewa tayari mwili mzima na kapakazwa dawa, akaruhusiwa aondoke

Aliona aibu kurudi na watu ikabidi aende kuomba msaada kwa watu ahidhiwe akapelekwa mzee moja kwenye Mila sijui za wapogoro au wandamba wa huko kilombero na ulanga wanamuita "Mbuyi"

Huyo mbuyi ndio akamhifadhi kwake kwa siku kadhaa kisha akamsafirisha kimazingara hadi kwenye vichaka karibu na kwakeNi wazee wa kimila huko kilombero na ulanga na malinyi.
Hawa wazee ni zaidi ya wachiwi/ Waganga
Kwanza hawakai kwenyw nyumba za bati ni mwiko kabisa, hata akiwa na nyumba ya bati lazima atajenga ya nyasi pembeni na ataishi hapo

pia Mambuyi huwa hawavai kitu chochote mguuni. huwa wapo peku mda wote

Mbuyi akitaka kusafiri Let say Dar to Moro anatembea kidogo tuu anaingia Kichakani anapaa anaenda kutua Moro chaaap Dk. 0 Kwenye kichaka kingine anaendelea na mishe zake

Mtu yoyote alie kaa maeneo ya kilombero, Mlimba, Malinyi, Ulanga/ Mahenge lazima atakua anajua ligi za mambuyi

Mwisho.
Mbuyi Yondani nae ni wa huko?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom