Ijue historia ya Firauni na uongo uliozushwa

Mnaemuita firauni ni babu yenu, wa asili! alikuwa ni Mweusi tii!! jina lake aliitwa Mkuu Ramesses wa II au Sese.

Nimekuwa nikiona habari kutoka kwa watu, kuwa mwili wa Ramesses ll huwa ukizikwa, unarudi juu kesho yake.

Hivi hili linawezekanaje!! tena watu wenye akili timamu kabisa wanaamini hili! wenye Degree na PhD. Kwa kweli ni maajabu makubwa mno haya! hapa utaamini kuwa Binadamu ni dhaifu sana kwenye imani!, na ni rahisi sana kumteka mtu yoyote akili kwa kutumia kivuli cha Dini/Imani.

Leo hii kitabu chochote kitakatifu kingesema kuiba si dhambi na mtu ili ufike mbinguni ni lazima uwe mwizi, basi tungeshuhudia watu wengi wasomi na wasio wasomi wakiwa ni wevi! Yote ni kwa sababu binadamu wengi ni weak mno kwenye Imani!

Turudi kwenye maada.

Great ramesses ll alizikwaje?
Mwanzo alizikwa kwenye kaburi KV7 katika Bonde la Wafalme, lakini kwa sababu ya uporaji wa vitu vya thamani alivyokuwa amevishwa, makuhani walihamisha mwili kutoka eneo hilo na kuupeleka ndani ya kaburi la malkia Inhapy.

Miaka mingi baadae waliuhamishia tena mwili kwenye kaburi la kuhani mkuu Pinudjem II. Yote hii ni sababu ya kumbukumbu katika hieroglyphics.

Kutokana na matetemeko yaliyoikumba Giza miaka kati ya miaka 1000 AD hadi 1500 AD vitu vingi vilipotea huku baadhi ya masanamu mengi yakiharibiwa vibaya na matetemeko hayo, na baadhi ya makaburi, majumba, na makumbusho mengine kupotea kabisa.

Huku mwili wa Great Ramesses ll Nao ukipotea katika matetemeko hayo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa Red sea.

Ramesses ll, hakufa kwenye Gharika la Mussa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee, zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida.

Pia si mwili wa ramesses ll tu uliopo kwenye makumbusho ya misri, ni miili mingi ya Mapharao tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Egypt ya kale.

Historia yake kwa Ufupi
Ramesses II, au kwa jina jingine Sese alikuwa ni mfalme wa pili wa Uzao wa 19 wa familia ya kifalme. Na alikuja kuwa miongoni mwa Mapharao wenye nguvu kuwahi kuwepo Misri.

Ramesses II alipewa kiti cha Ufalme mapema kwenye umri wa miaka 20 na akaongoza (kati ya mwaka 1279 BC) hadi alipofariki miaka 67 baadae (1213 BC) kwa maradhi ya mishipa, na ini.

Aliongoza Misri kwa miaka 67 akiwa ni wa pili kuongoza kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya mapharao.

Mbali na Vita Ramses II anakumbukwa mno katika juhudi za utunzaji wa Historia ya Misri katika mahekalu ya Ramesseum pamoja na Abu Simbel.

Kwa kumbukumbu nyingi muhimu zilizomo katika mahekalu haya kwa sanamu, zana za kale, michoro na maandishi zinamfanya Ramsess kuwa mmoja wa mapharao muhimu wa misri ya kale.

Jeshi la Rammeses lilisaidia kulinda mipaka ya Misri kutoka kwa wavamizi na majambazi katika Meditrenian na Libya pia kutoka Hittites na Nubians.

Pia Alifanya kampeni za kurudisha ardhi iliyokuwa imeporwa na wavamizi kwa kusign mikataba ya amani kabla ya kutumia nguvu kuwapiga.

Katika historia Ramesses alishindwa vita moja tu! vita inayokumbukwa sana ni ile iliyofanyikia Kadesh (Syria ya leo) ambayo ilifanyika mwaka 1274 BC dhidi Wahiti. Ilikuwa ni vita kubwa iliyotumia zana za kisasa zaidi wakati huo katika historia ya vita za kale. Rameses alifanya makosa kwa kugawa vibaya vikosi vyake kitu kilichofanya moja ya kikosi kufyekwa chote! Hatimaye mpinzani akajitangazia ushindi na Ramesses ikampasa arudi nyuma sababu ya kujiandaa kubaya na matatizo ya vifaa.

Dhana iliyozushwa juu ya kifo chake
Vitabu kadhaa vya Dini kama vile Bible na Quran vimekuwa vikizungumzia kifo chake katika hali ya kushangaza!
Wao hudai kuwa Ramesses au Sese alifia kwenye maji wakati akiwafukuza waisrael.

Wamisri wa kale wakipinga kabisa madai hayo na kudai Sese alifariki akiwa na miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi! ya kibinadamu.

Moja ya ushahidi ni wa Mwili/mummy wa Sese ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki akiwa mzee kabisa!
Pia jambo jingine la kujiuliza ni kuwa Kina Musa wakati wakimkimbia Ramesses na kuwa wameshafanikiwa kuvuka bahari, huku nyuma waliwezaje kumuona Ramesses katikati ya kikosi cha askari wa Misri akifa maji!?

Hayo ni mambo yanayowatatiza wengi, huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa Ramesses mwili wake huwa hautaki kuzikwa.

Huyu Ndo Great Ramesses II au Sese mmoja wa Mapharao Muhimu zaidi Egypt ya kale na leo katika historia.

Aisee !!😌
 
Ni changamoto kidogo kuchanganya historia ya vitabu vya dini na historia ya vitabu vya binaadam

Ila kuna vitu kidogo vinanitatiza katika hu Uzi wako hebu nifahamishe

1) Nasikia misri walipita mafarao wengi kwa nini wewe umemchagua huyo Ramesses

2) Je! Huyo Ramesses ndio aliye kuwepo kipindi cha Mussa na kama ndio kwa ushahidi upi?

3)Huyo Ramesses alikuwepo miaka ya 1200BC

Sasa mbona historia zinasema Mussa alikuwepo miaka 2000BC?
Akikujibu nitag
 
kuandika maneno na majina kwa usahihi hujui then unakuja na kelele nyingi kuwa sijitambui?
Jina gani sijaliandika kwa usahihi? sentensi ipi nimeshindwa kuipangilia kwa usahihi? JF kuna waelewasana kuliko unavodhani, km ulitaka nikutajie nilicho kitaja ka mwl wa UPE, hapa hapakufai utakunywa sumu bure,
na kama utani- judge kuwa mimi ni layman wakati hujui my Level of Matriculation siyo sahihi! umekusudia kuropoka tu dogo ajili ya jazba! Kama unavo wapigia debe hao majuha wa Middle East.
 
Mamood
Mahmoud (Abbas)
Hitle
Hitler (Adolf)
 
Unashangaza sana na histori yako new model yani tukuamini we nani hasa yani tuache kumuamini aliye muumba huyo farao ndio anasema alikufa maji tukuamini ww unaeenda chooni kunya
Kwani kwenye hivyo vitabu vitakatifu Kuna "Aya" au "andiko" lolote kuna saini ya mungu kudhibitisha kwamba hiyo Aya au andiko hilo kaandika mungu na si wanadamu mkuu

Sent from my itel S32 using JamiiForums mobile app
 
Mbona ni mahesabu rahis sana hayo?bc means kabla ya kristo.
..so kadi ujio wa yesu unavyokaribia miaka ilizid kupungua.cjui km umenipata!!
 
Nimeona hapo juu kwamba alianza kuongoza mwaka 1273 BC mpaka 1213BC why sio 1213BC mpaka 1273BC?
... tatizo hakuna anayejua exactly dunia/miaka ilianza lini ili tuanze kuhesabia miaka kutokea huko. Ingejulikana kwa mfano siku ya kwanza ya dunia ilikuwa 1 Januari 0001 na hadi leo imepita miaka say 502,020 tangu siku hiyo ya kwanza leo ingekuwa tarehe 10 Julai 502,020; shida ndio hiyo the very first day isn't known!

Na kwa kuwa kuhesabu siku inahitaji reference point, wataalamu wakaamua siku inayojulikana zaidi na wengi ni siku Mwokozi wa Ulimwengu yaani Yesu Kristo wa Nazareth katika nchi ya Yuda alipwasili duniani ndio ikaamuliwa iwe reference point ikahesabiwa zero. So, matukio yote yaliyotokea kabla ya Yesu Kristo kuja duniani yakahesabiwa kuanzi hapo (zero) kurudi nyuma (BC) na yaliyotokea baada ya hapo yakahesabiwa kwenda mbele (AD or After Christ). Kama umesoma japo hesabu ya darasa la tano na siku mwalimu anafundisha topic ya NUMBER LINE hukuwa uwanjani unacheza, hii kitu ni rahisi sana Mkuu.

Anyway, dini na tamaduni nyingine kwa kuona na kuiga style hiyo wakaamua nao kuanzisha kalenda zao with their own reference points - mf. Kalenda ya Kiislamu, n.k. Wengine, wanatumia BC/AD ila ili kutojinasibisha sana na kinachoonekana kama "Kalenda ya Kikristo" wakaamua kuongeza BCE/ACE yaani Before Common Era na After Common Era japo reference points ni zile zile za BC (Before Christ) na AD (Anno Domino/Mwaka wa Bwana/After Christ).
 
Kinacho nichanganya mimi mbona haozi.
Wataalamu wanaita 'mummification' aina flani ya ku preserve mwili wa kiumbe usiharibike karne na karne. Ilitumiwa na ancient Egypt kuzika viongozi wao. Na hakuwa Pharaoh peke ake, miili mingi ya dizain Ile iligundulika kweny mapiramidi.
 
Mnaemuita firauni ni babu yenu, wa asili! alikuwa ni Mweusi tii!! jina lake aliitwa Mkuu Ramesses wa II au Sese.

Nimekuwa nikiona habari kutoka kwa watu, kuwa mwili wa Ramesses ll huwa ukizikwa, unarudi juu kesho yake.

Hivi hili linawezekanaje!! tena watu wenye akili timamu kabisa wanaamini hili! wenye Degree na PhD. Kwa kweli ni maajabu makubwa mno haya! hapa utaamini kuwa Binadamu ni dhaifu sana kwenye imani!, na ni rahisi sana kumteka mtu yoyote akili kwa kutumia kivuli cha Dini/Imani.

Leo hii kitabu chochote kitakatifu kingesema kuiba si dhambi na mtu ili ufike mbinguni ni lazima uwe mwizi, basi tungeshuhudia watu wengi wasomi na wasio wasomi wakiwa ni wevi! Yote ni kwa sababu binadamu wengi ni weak mno kwenye Imani!

Turudi kwenye maada.

Great ramesses ll alizikwaje?
Mwanzo alizikwa kwenye kaburi KV7 katika Bonde la Wafalme, lakini kwa sababu ya uporaji wa vitu vya thamani alivyokuwa amevishwa, makuhani walihamisha mwili kutoka eneo hilo na kuupeleka ndani ya kaburi la malkia Inhapy.

Miaka mingi baadae waliuhamishia tena mwili kwenye kaburi la kuhani mkuu Pinudjem II. Yote hii ni sababu ya kumbukumbu katika hieroglyphics.

Kutokana na matetemeko yaliyoikumba Giza miaka kati ya miaka 1000 AD hadi 1500 AD vitu vingi vilipotea huku baadhi ya masanamu mengi yakiharibiwa vibaya na matetemeko hayo, na baadhi ya makaburi, majumba, na makumbusho mengine kupotea kabisa.

Huku mwili wa Great Ramesses ll Nao ukipotea katika matetemeko hayo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa Red sea.

Ramesses ll, hakufa kwenye Gharika la Mussa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee, zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida.

Pia si mwili wa ramesses ll tu uliopo kwenye makumbusho ya misri, ni miili mingi ya Mapharao tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Egypt ya kale.

Historia yake kwa Ufupi
Ramesses II, au kwa jina jingine Sese alikuwa ni mfalme wa pili wa Uzao wa 19 wa familia ya kifalme. Na alikuja kuwa miongoni mwa Mapharao wenye nguvu kuwahi kuwepo Misri.

Ramesses II alipewa kiti cha Ufalme mapema kwenye umri wa miaka 20 na akaongoza (kati ya mwaka 1279 BC) hadi alipofariki miaka 67 baadae (1213 BC) kwa maradhi ya mishipa, na ini.

Aliongoza Misri kwa miaka 67 akiwa ni wa pili kuongoza kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya mapharao.

Mbali na Vita Ramses II anakumbukwa mno katika juhudi za utunzaji wa Historia ya Misri katika mahekalu ya Ramesseum pamoja na Abu Simbel.

Kwa kumbukumbu nyingi muhimu zilizomo katika mahekalu haya kwa sanamu, zana za kale, michoro na maandishi zinamfanya Ramsess kuwa mmoja wa mapharao muhimu wa misri ya kale.

Jeshi la Rammeses lilisaidia kulinda mipaka ya Misri kutoka kwa wavamizi na majambazi katika Meditrenian na Libya pia kutoka Hittites na Nubians.

Pia Alifanya kampeni za kurudisha ardhi iliyokuwa imeporwa na wavamizi kwa kusign mikataba ya amani kabla ya kutumia nguvu kuwapiga.

Katika historia Ramesses alishindwa vita moja tu! vita inayokumbukwa sana ni ile iliyofanyikia Kadesh (Syria ya leo) ambayo ilifanyika mwaka 1274 BC dhidi Wahiti. Ilikuwa ni vita kubwa iliyotumia zana za kisasa zaidi wakati huo katika historia ya vita za kale. Rameses alifanya makosa kwa kugawa vibaya vikosi vyake kitu kilichofanya moja ya kikosi kufyekwa chote! Hatimaye mpinzani akajitangazia ushindi na Ramesses ikampasa arudi nyuma sababu ya kujiandaa kubaya na matatizo ya vifaa.

Dhana iliyozushwa juu ya kifo chake
Vitabu kadhaa vya Dini kama vile Bible na Quran vimekuwa vikizungumzia kifo chake katika hali ya kushangaza!
Wao hudai kuwa Ramesses au Sese alifia kwenye maji wakati akiwafukuza waisrael.

Wamisri wa kale wakipinga kabisa madai hayo na kudai Sese alifariki akiwa na miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi! ya kibinadamu.

Moja ya ushahidi ni wa Mwili/mummy wa Sese ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki akiwa mzee kabisa!
Pia jambo jingine la kujiuliza ni kuwa Kina Musa wakati wakimkimbia Ramesses na kuwa wameshafanikiwa kuvuka bahari, huku nyuma waliwezaje kumuona Ramesses katikati ya kikosi cha askari wa Misri akifa maji!?

Hayo ni mambo yanayowatatiza wengi, huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa Ramesses mwili wake huwa hautaki kuzikwa.

Huyu Ndo Great Ramesses II au Sese mmoja wa Mapharao Muhimu zaidi Egypt ya kale na leo katika historia.
Leta ushahidi unaoonyesha kuwa Biblia nayo ilipotosha historia ya huyo Filauni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom