Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

kuna mantiki hapa maana kama angekuwa mweupe si rahisi kwenda misri kwa weusi na kama angekuwa mweusi si rahisi kwenda misri yenye weupe
Haujafikiri sahihi,na pia haujaisoma vizuri na kuijua habari ya Yesu kufichwa Misri,km kujificha ni kwa wenye ranging sawa na ww, hebu tafakari na hii
Muhammad na maswahaba wake(waarabu) walipodurumiwa kwao walikimbilia kushi ama Ethiopia ya sasa(kwa weusi tiii)kujificha,sasa ilikuaje wakajificha maana kujificha ilikuwa lazima uwe wa rangi ya huko ujifichako,
 
Habari rafiki nilikuwa Busy kidogo naona nikitoka na uzi unasimama kabisa! Wapi wenzangu tuwe tunasaidiana!
 
Jicho la 'Horus'/RA na ukweli kuhusu ulimwengu wa Maarifa na
Utambuzi.

Meditation ni moja ya elimu Muhimu ambayo ilianzia 'Misri ya
kale'. Mababu waliamini kwamba chanzo cha maarifa na utambuzi
katika maisha ya mwanadamu yapo katika Jicho la tatu, na hapo
ndipo Wazo wa ''jicho la Ra'' lilipopatikana!.

Historia inadai kuwa Adam/Atum/Temu(Mwanadamu wa kwanza) Ndiye
aliyekuwa mwanzilishi wa kitu hiki na Ndicho kilichomsaidia
kumuonyesha watoto zake SHU na TEFNUT kipindi ambacho walikuwa
wamepotea.
Misingi kama hii iliendelea kuwapo kwa miaka mingi baadae huku
asili tofauti za wanadamu zikijifunza Elimu hii.
Ujuzi huu ndio uliopelekea Misri ya kale kuendelea sana katika
nyanja zote zinazohusu maarifa.
Mababu wa kale waliamini, Katika ulimwengu wa roho, mwanadamu
ni moja wa viumbe wenye nguvu nyingi, na uwezo wake wa
kufikiri akiwa kwenye ulimwengu huo ni mkubwa kuliko akiwa na
amevaa mwili., Hivyo moja ya mambo ya msingi kwa kila binadamu
ni kuweza kujitawala kikamilifu katika ulimwengu wa mwili na
wa roho. Suala la kujitawala katika ulimwengu wa mwili
kikamilifu huitaji msaada kutoka katika ulimwengu wa roho.

Baadhi ya vitabu vya dini miaka mingi baadae vilikuja kuelezea
ujuzi huu kama ''IMANI''
Mf; Biblia inasema Yesu aliwaambia watu wake kuwa Ukiwa na
Imani Kama punde moja ya Haradali, unaweza kuuambia Mlima
utoke na ukajitose maharini nao ukakutii! Imani aliyokuwa
anaizungumzia Yesu ni ujuzi huu wa kuweza kuitawala na
kuiongoza Roho yako, kupitia hapo utaweza kuonyeshwa yaliyojificha, na kufanya mambo mengine mengi kadha wa kadha kwa Kuiongoza roho!
Wanadamu wengi huota ndoto! ndoto huwa ni taarifa, au kwa maana nyingine naweza kusema ndoto kuwa ni Umbea ambao mtu huletewa na roho yake kuhusu mambo fulani! lakini kutokana na watu wengi kuwa na nguvu hafifu ndoto/taarifa hizo huwa hazitufikii kiusahihi na muda mwingine hadi tunaomba mtu asaidie kutafsiri!
Mfano Nilikuwa na rafiki yaangu fulani, ambaye alikuwa akinihadithia kuhusu jambo fulani la yeye na mke wake,
Ni kwamba kila alipokuwa anachepuka kwenda kwa mwanamke mwingine, Kesho yake asubuhi mkewe alisema aliota ndoto akiona jamaa anamsaliti kwa mwanamke mwingine! na si mara moja! karibia mara tano! kila siku atakayolala na kimada wake basi kesho yake asubuhi mwanamke wake atampa habari kuwa aliota hivyo! So hicho ni nini!? Ni wazi kuwa mwanamke yule ana nguvu kubwa ya roho, ila hajijui! na suala la kukatisha tamaa ni kuwa imani aliyonayo mwanamke yule inakataza kuamini katika Ndoto! hivyo yeye mwenyewe akawa anamwambia mumewe, ila mwisho anamwambia aah! najua ni shetani tu huyu anataka kutugombanisha! na ashindwe!! huku mwanaume akifurahi kimoyomoyo na kuona ni kama bahati.

Mababu wa Misri waliamini mwili wa binadamu ukifa, basi roho ambayo
huishi katika eneo la katikati kabisa katika Ubongo huondoka
zake kutokana na sababu fulani. Sababu ya kwanza ilikuwa ni
mwili kuchoka. punde mwili unapochoka basi roho ambayo
iliwekwa kiutaalam katikati ya ubongo hushindwa kuuongoza
mwili na kuuacha.
Mababu hao wa kale waliamini kuwa Mwili ni vazi ambalo
huvaliwa na roho, na punde vazi hilo linapochoka/au kuchakaa
basi Roho ilitoka na kwenda kutafuta vazi jingine jipya, yaani
kwenda mahali mimba inapotungwa.(Na hapa ndipo kasheshe la
kutokujitambua kwa wanadamu wengi linapoanzia maana huitaji
nguvu kubwa kuliko kawaida ya hisia kali kuitambua safari yako
yote hata kabla hujazaliwa! Yote hii inapatikana kwenye
Meditation.

Kwa kulazimisha/command sehemu ya katikati ya Ubongo kufanya
jambo unalotaka liwe basi jambo hilo huwa/ili mradi sheria na
kanuni za kulazimisha zifuatwe.

Sababu ya pili ilikuwa ni vita za kiroho, Wao waliamini kuwa muda fulani Binadamu aliweza kupata shambulizi la roho! ambalo pia lingewezaa kuwa ni sababu ya roho kuuvua mwili!
TUTAENDELEA......​
 

Attachments

  • 4585604096_525x370.jpg
    4585604096_525x370.jpg
    17.4 KB · Views: 62
Mnaemuita firauni ni babu yenu, wa asili! alikuwa ni Mweusi tii!! jina lake aliitwa Mkuu Ramesses wa II au Sese!

Nimekuwa nikiona habari kutoka kwa watu, kuwa mwili wa Ramesses ll huwa ukizikwa, unarudi juu kesho yake!!!

Hivi hili linawezekanaje!! tena watu wenye akili timamu kabisa wanaamini hili! wenye Degree na PHD!! Kwa kweli ni maajabu makubwa mno haya! hapa utaamini kuwa Binadamu ni dhaifu sana kwenye imani!, na ni rahisi sana kumteka mtu yoyote akili kwa kutumia kivuli cha Dini/Imani..

Leo hii kitabu chochote kitakatifu kingesema Kuiba si dhambi na mtu ili ufike mbinguni ni lazima uwe mwizi, basi tungeshuhudia watu wengi wasomi na wasio wasomi wakiwa ni wevi!! Yote ni kwa sababu binadamu wengi ni weak mno kwenye Imani!

Turudi kwenye maada.

Great ramesses ll alizikwaje?

Mwanzo alizikwa kwenye kaburi KV7 katika Bonde la Wafalme, lakini kwa sababu ya uporaji wa vitu vya thamani alivyokuwa amevishwa, makuhani walihamisha mwili kutoka eneo hilo na kuupeleka ndani ya kaburi la malkia Inhapy.

Miaka mingi baadae waliuhamishia tena mwili kwenye kaburi la kuhani mkuu Pinudjem II. Yote hii ni sababu ya kumbukumbu katika hieroglyphics.

Kutokana na matetemeko yaliyoikumba Giza miaka kati ya miaka 1000 AD hadi 1500 AD vitu vingi vilipotea huku baadhi ya masanamu mengi yakiharibiwa vibaya na matetemeko hayo, na baadhi ya makaburi, majumba, na makumbusho mengine kupotea kabisa!
Huku mwili Wa Great Ramesses ll Nao ukipotea katika matetemeko hayo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huu ulipatikana tena pembezoni kidogo mwa Red sea.

Ramesses ll, hakufa kwenye Gharika la Mussa kama watu wanavyodai, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee, zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida.

Pia si mwili wa ramesses ll tu uliopo kwenye makumbusho ya misri, ni miili mingi ya Mapharao tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Egypt ya kale.

"Historia yake kwa Ufupi"

Ramesses II, au kwa jina jingine Sese alikuwa ni mfalme wa pili wa Uzao wa 19 wa familia ya kifalme. Na alikuja kuwa miongoni mwa Mapharao wenye nguvu kuwahi kuwepo Misri.

Ramesses II alipewa kiti cha Ufalme mapema kwenye umri wa miaka 20 na akaongoza (kati ya mwaka 1279 BC) hadi alipofariki miaka 67 baadae (1213 BC) kwa maradhi ya mishipa, na ini.
Aliongoza Misri kwa miaka 67 akiwa ni wa pili kuongoza kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya mapharao.

Mbali na Vita Ramses II anakumbukwa mno katika juhudi za utunzaji wa Historia ya Misri katika mahekalu ya Ramesseum pamoja na Abu Simbel.
Kwa kumbukumbu nyingi muhimu zilizomo katika mahekalu haya kwa sanamu, zana za kale, michoro na maandishi zinamfanya Ramsess kuwa mmoja wa mapharao muhimu wa misri ya kale.


Jeshi la Rammeses lilisaidia kulinda mipaka ya Misri kutoka kwa wavamizi na majambazi katika Meditrenian na Libya pia kutoka Hittites na Nubians.

Pia Alifanya kampeni za kurudisha ardhi iliyokuwa imeporwa na wavamizi kwa kusign mikataba ya amani kabla ya kutumia nguvu kuwapiga.

Katika historia Ramesses alishindwa vita moja tu! vita inayokumbukwa sana ni ile iliyofanyikia Kadesh (Syria ya leo) ambayo ilifanyika mwaka 1274 BC dhidi Wahiti. Ilikuwa ni vita kubwa iliyotumia zana za kisasa zaidi wakati huo katika historia ya vita za kale. Rameses alifanya makosa kwa kugawa vibaya vikosi vyake kitu kilichofanya moja ya kikosi kufyekwa chote! Hatimaye mpinzani akajitangazia ushindi na Ramesses ikampasa arudi nyuma sababu ya kujiandaa kubaya na matatizo ya vifaa.

Dhana iliyozushwa Juu ya Kifo chake!

Vitabu kadhaa vya Dini kama vile Bible na Quran vimekuwa vikizungumzia kifo chake katika hali ya kushangaza!
Wao hudai kuwa Ramesses au Sese alifia kwenye maji wakati akiwafukuza waisrael!
Wamisri wa kale wakipinga kabisa madai hayo na kudai Sese alifariki akiwa na miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi! ya kibinadamu!
Moja ya ushahidi ni wa Mwili/mummy wa Sese ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki akiwa mzee kabisa!
Pia jambo jingine la kujiuliza ni kuwa Kina Musa wakati wakimkimbia Ramesses na kuwa wameshafanikiwa kuvuka bahari, huku nyuma waliwezaje kumuona Ramesses katikati ya kikosi cha askari wa misri akifa maji!? Hayo ni mambo yanayowatatiza wengi, huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa Ramesses mwili wake huwa hautaki kuzikwa!

Huyu Ndo Great Ramesses II au Sese mmoja wa Mapharao Muhimu zaidi Eghypt ya kale na leo katika historia,

View attachment 500056
MWILI WA PHARAO RAMESSES ll / Firauni Uliopo kwenye maonyesho ya Ancient Egypt.
View attachment 463572
SANAMU YA GREAT RAMESSES II ILIYOPO GIZA EGYPT

Nawasilisha
Secret Star

Wakuu kwan viroba vimerudi mtaani??
 
Hata Yesu Kristo mwana wa Yoseph alikuwa mweusi tii na nywere za kipilipili! Na ndio sababu utotoni alifichwa Misri kumkwepa Herode, kama angekuwa mzungu kama tunavyoonyeshwa kwenye sinema huko Misri wasingemficha...ila kwakuwa alikuwa mweusi basi alichangwanywa na weusi wenzanke.
Lugha ya mifano aliyokuwa akiitumia Yesu kwa mujibu wa biblia, asili take ni hapa usukumani...wazungu hawafundushi kupitia mifano ya "mpanzi na mbengu zilizoanguka kandokando ya njia..."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom