IJUE FAMILIA YA GADHAFI- Watoto wa nyoka ni nyoka tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IJUE FAMILIA YA GADHAFI- Watoto wa nyoka ni nyoka tu

Discussion in 'International Forum' started by Mpasuajipu, Feb 24, 2011.

 1. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kanali Muommar Gadhafi miaka 68- alipata madaraka katika mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu mwaka 1969- alimpindua aliyekuwa mfalme wa Libya wakati huo Mfalme Idris.

  Watoto wa Gadhafi

  1. Muhammad
  Mtoto wa kwanza wa Gadhafi na mkewe wake wa kwanza, Fatiha waliyetengana naye miezi sita tu baada ya ndoa yao.
  Muhammad ni kiongozi wa kamati ya olimpiki na ni mwenyekiti wa shirika la Posta na mawasiliano-telecom co.  2. Saif al-Islam


  Heir apparent Saif al-Islam has a PHd. From the London School of Economics

  Mtoto wa pili wa Dhadafi - umri miaka 38, and Phd katika masuala ya Uchumi.

  Kwa kutumia Charity organization ya baba yake, alitoa misaada mingi sana kipindi kile haiti ilipoharibiwa na tetemeko la ardhi.
  Walibya wengi wanadhani ni mtu mwadilifu anayefaa hata kuiongoza Libya baada ya baba yake. Hata hivyo, ukweli ni kwamba ni fisadi mdogo anayemiliki hisa nyingi ktk makampuni ya mafuta yaliyowekeza Libya. Pia anapenda wanawake, na katika tukio moja, inasadikika kuwa aliwahi kumlipa Mariah Carey dola za kimarekani millioni moja ili kuonyesha tamasha la muziki.
  Hivi karibuni, wakati waandamanaji wakijitokeza kwa wingi kumpinga baba yake, alitokea kwenye televisheni ya taifa na kuwaita waandamanaji walevi, watumia dawa za kulevya na magaidi.


  3. Saadi Gadhafi

  Saadi Gadhafi- A senior Engineer and Former pro soccer player with “a troubled past”
  Saadi ni mtoto wa tatu wa kiume wa Gadhafi mwenye historia mbaya ya maisha kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na kupambana na polisi katika nchi kadhaa za ulaya hasa Italia kuhusiana na matumizi ya pombe na madawa ya kulevya. Aliwahi kuwa mcheza soka wa kulipwa huko Italia lakini akafukuzwa katika kikosi kwa kutumia dawa za kulevya.

  4. Muatassim
  Mtoto wa nne wa kiume wa Gadhafimwenye ushindani mkubwa na Saif katika kutaka kurithi biashara ya familia ya Gadhafi.
  Alikosana na baba yake na kulazimika kwenda kuishi maisha ya kikimbizi nchini Misri mwaka 1990 . Aliruhusiwa kurudi nyumbani mwaka 2006 na kuchaguliwa kuwa mashauri wa mambo ya kiusalama. Mwaka 2009, alitembelea washington na kubahatika kukutana na mkuu wa wa Idara ya mambo ya nje ya Marekani Bi. Hillary Rodham Clinton kitendo ambacho kilimkasirisha sana Saif. Muatassim inadaiwa pia aliwahi kumlipa mamilioni ya dola za kimarekani Beyonce na Usher katika “party” moja ya mwaka mpya huko St. Bart’s.


  5. Hannibal
  Ni mtoto wa tano wa kiume wa Gadhafi. Inashukiwa pia kuwa aliwahi kumpiga mkewe Aline mara kwa mara. Aliwahi kufukuzwa katika hoteli moja huko London baada ya kumpiga mkewe na kumjeruhi usoni. Hali hii ilimlazimu mtoto wa kike wa Gadhafi, Aisha (ambaye alikuwa mja mzito karibia na kuzaa) kwenda London kusuluhisha ugomvi huo na kudanganya kuwa Aline aliumia katika ajali.

  Hannibal alikuwa pia anatabia isiyo ya kawaida na alijihusisha na matukio mengi ya ajabu ajabu huko ulaya. Inasemekana kuwa, mwaka 2001 katika hoteli ya Rome aliwashambulia polisi watatu kwa kutumia gasi ya kuzimia moto “Fire extinguisher” na pia aliwahi kufanya shambulizi kwa wafanyakazi wake “wapambe” huko Geneva mwaka 2008. Alikamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka, hata hivyo aliachiwa baada ya siku mbili tu. Kwa tukio hilo, Libya ilizuia uingizaji wa bidhaa zote za Switzerland, ikazuia utoaji viza kwa raia wa Switzerland na kulazimisha makampuni yote ya nchi hiyo kufunga offisi zake huko Libya.


  6.Khamis

  Ni mtoto wa sita wa kiume wa Gadhafi ambaye hajulikani sana.
  Ni kamanda wa kivita anayeheshimika sana katika vikosi maalum na mtetezi mkubwa wa sera za baba yake.
  Amepata mafunzo ya kijeshi Russia na ana PhD katika “millitary sciences” aliyopipata mwaka 2007.
  Anaongoza kikosi cha 32 Brigedi ambayo inajulikana kama ni mojawapo ya vikosi madhubuti sana chenye mafunzo ya hali ya juu na na vifaa vya kisasa kabisa katika jeshi la Libya. Kikosi hiki kinaaminika kuwa ndicho kimeshiriki sana katika kuwashambulia waandamanaji wanaoipinga serikali ya Bwana Gadhafi.  7.Aisha Gadhafi


  Aisha Gadhafi is a trained lawyer who served on Saddam Hussein’s defence team.

  Mtoto pkee wa Kike wa Gadhafi ambaye anaaminika kama ndiye shauri wa familia yenye matatizo ya Gadhafi.
  Aisha, alichochea kwa kiasi kikubwa mzozo kati ya Libya na Uswisi kufuatia kukamatwa kwa kaka yake Hannibal na hivyo kuongeza hasira ya baba yake katika mzozo huo. Aisha alilikuza tatizo hilo kiasi ambacho ilishindikana kupatikana kwa suluhisho kati ya nchi hizo mbili


  8.Saif al-Arab
  Mtoto wa nane wa Gadhafi anayeishi Ujerumani katika mji wa Munich.

  Inasemekana anafanya biashara sizizohalali na anamatumizi makubwa katika kujimwaga yaani “party”.
  Serikali ya Uerumani imeanza kumnyooshea kidole dogo huyu na ni jambo la muda tu kila kitu serikali itachukua hatua kwa kufuatia mwenendo hali wa mzozo unaoendelea Libya kwa baba yake.

  Hiyo ndiyo orodha ya watoto WATUKUTU WA MFALME GADHAFI KAMA ANAVYOJIITA YEYE.
  KWELI MTOTO WA NYOKA NI NYOKA TU
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Dah!!!!!!!!
   
 3. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Poa huyu Khamis ndiye jana na leo kikosi chake anachoongoza kinashambulia vikali mji wa z Ziwahi. Kwa ukatili wanaoendesha naona karibu wata-suppress waandamanaji maana wanawauwa Walibya utafikiri akil zao zinawambia wanauwa wanyama, sijawahi ona haya, yaani saadam Husseinalikuwa na unafuu
   
 4. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nachofurahia ni kwamba watoto wamepiga shule sio kama watoto wa viongozi wetu hapa bongo,hudhani madaraka ya wazazi ni yao pia so husahau hata kukata shule
  nadhani walichonacho kinawafaa,na gaddafi kafanya mengi mazuri,tatizo kwa sasa waarabu wana kamdudu kamewaingia ila watakuja juta tu siku moja lets wait
   
 5. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ungesema kuwa ijue serikali ya kifamilia ya Ghadafi
   
 6. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mkuu ungeiweka na article ya kiingereza uliyoitafsiri.
   
 7. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  nice info jipu.
   
 8. zinginary

  zinginary JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2016
  Joined: Dec 18, 2015
  Messages: 1,795
  Likes Received: 1,085
  Trophy Points: 280
  Wapo hawa watoto,ukiachana na.aliefungwa ndan
   
 9. salazar

  salazar JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 13, 2016
  Messages: 688
  Likes Received: 372
  Trophy Points: 80
  Tupeni update basi
   
 10. M

  Mwanapropaganda JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2016
  Joined: Aug 19, 2014
  Messages: 4,277
  Likes Received: 2,142
  Trophy Points: 280
  Yule aliyeuawa na majeshi ya NATO kipindi anarudi Libya kutoka masomoni uingereza kipindi waasi wanapambana na baba yake Comrade Col. Muammar Gaddafi ni nani?
   
 11. Mibas

  Mibas JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2016
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,534
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Yule anaitwa Saif al Arab, alikua mwanafunzi huko Munich Ujerumani. 1476801146980.jpg Pichani ni waandamanaji wakilalamikia mauwaji yake.
   
 12. M

  Mwanapropaganda JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2016
  Joined: Aug 19, 2014
  Messages: 4,277
  Likes Received: 2,142
  Trophy Points: 280
  Ndo alikuwa akifanya matanuzi ya kifahari hadi serikali ya ujerumani ikamtilia shaka?
   
 13. Mibas

  Mibas JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2016
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,534
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Ndio huyo huyo, alikua mtata sana, ikiwamo kupigana na ma baunsa kwenye ma klabu, kumpiga na kumjeruhi mkewe, kuwapiga walinzi wake binafsi au tuhuma za kusafirisha begi lenye silaha kutoka Germany to france.
   
 14. New City

  New City JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2016
  Joined: Apr 17, 2014
  Messages: 1,003
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Zimebaki stori sasa,pumba na mchele vimeonekana.
  Kati ya Gaddaf na ISIS wakata vichwa ,nani bora sijui...!!?? Nadhani walibya wenyewe jibu wanalo,subiri sisi tuendelee kuhaliki vyuo hewa.
   
 15. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2016
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kuna mmoja alimlazimisha pilot achukue Ndege ya kivita akapige waandamanaji pilot akavurumisha Ndege kwenye kikosi cha mwanamfalme huyo na kikosi kikateketea
   
 16. M

  Mwanapropaganda JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2016
  Joined: Aug 19, 2014
  Messages: 4,277
  Likes Received: 2,142
  Trophy Points: 280
  Walibya walifanya kosa kubwa sana.
   
 17. shushushu VIP

  shushushu VIP JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2016
  Joined: Jul 24, 2016
  Messages: 4,503
  Likes Received: 3,730
  Trophy Points: 280
  hawa watoto ni noumaa
   
 18. kibanga 3

  kibanga 3 JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2016
  Joined: Jul 6, 2015
  Messages: 1,380
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi wanajuta
   
 19. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2016
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mtoto wa nyoka ni nyoka, hana tafauti na Bush Sr na Bush Jr.
   
 20. aloycious

  aloycious JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2016
  Joined: Dec 17, 2012
  Messages: 5,516
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 180
  Sifa za kijinga.
   
Loading...