Jifunze na uelimike kuhusu kinywaji maarufu cha Coca Cola

Zero 2 Hero

JF-Expert Member
Dec 16, 2012
335
519
Kanuni ya kutengeneza Kinywaji cha coca cola ambacho hutengenezwa kwa zao la cola (colanut) na majani ya mmea wa coca iligunduliwa na mfamasia wa kimarekani John S Pemberton mwaka 1886 huko atlanta.

Alilenga kugundua Kanuni ya kutengeneza dawa ya kifua, dawa aliyoigundua ilishindwa kutibu kifua lakini watu waliojaribu kutumia dawa hiyo wakajikuta wanaipenda kama Kinywaji cha kuchangamsha mwili(refreshing drink/beverage) .

Mwaka 1891 mmarekani Asa Candler aliinunua kanuni hiyo na kuanzisha kampuni ya Coca cola huko Atlanta-marekani na kujipatia umaarufu mkubwa na kuiza kwa Ernest Woodruff mwaka 1919.

Kinywaji hicho kimepitia mabadiliko na misukosuko mingi sana. Iligundulika na kulalamikiwa kuwa kinywaji hicho kinaleta uteja kwa watumiaji wake kujikuta hawawezi kukiacha kwa sababu kinawekwa cocaine. Mwaka1903 coca cola walikubali kuindoa cocaine kwenye Kanuni ya kinywaji hicho na badala yake wakaweka caffein.

Mwaka 1906 iligundulika kwa kinywaji hicho kinaweza kumsaidia mlevi kuachana na vinywaji vyenye kilevi. Ugunduzi huo ulikuza soko la Kinywaji hicho na kupunguza ulevi nchini marekani kwenye miaka ya mwanzoni mwa 1900 lakini
Mwaka 1911 serikali ya marekani iliishitaki kampuni ya coca cola kwa matumizi yake ya caffein kwenye Kinywaji hicho kuwa inaleta madhara ya kiafya kwa watumiaji na kusababisha wawe teja (addicts) wa Kinywaji hicho, lakini kampuni hiyo ilishinda kesi hiyo dhidi ya serikali.

Pia mwaka huohuo ilitengenezwa sehemu salama (vault) ya kuhifadhia kanuni ya utengenezaji wa Kinywaji hicho ili kuficha siri ya mchanganyo wa kinywaji hicho. Kumbuka watu wengi wamejaribu kuiga lakini wameshindwa kupata kanuni halisi ya kinywaji hicho, kama ilivyokuwa kwa Mmarekani Celeb Bradham aliyegundua Pepsi-cola mwaka 1898.

Mwaka 1916 mahakama kuu ya marekani iliiamrisha kampuni hiyo kupunguza matumizi ya caffein kwenye vinywaji vyake.

Baada ya Kinywaji hicho kujipatia umaarufu mkubwa watu wengi waliiga na kuiba siri za utengenezaji wa Kinywaji hicho mfano Viungo (ingredients) zinazotumika kuchanganywa kwenye kinywaji cha Coco Cola na kukifanya kuwa na ladha tofauti na vinywaji vingine vyote duniani ni moja ya vya siri nzito katika ulimwengu wa biashara (trade secret). Mchanganyo wa viungo hivyo unajulikana kama '7X' ili kuficha kanuni.

Kampuni mama ya coca cola huko Atlanta marekani hutengeza mchanganyo '(concentrate) ' yenye viungo hivi na kuwauzia 'bottlers' wenye vibali kutoka kwao kila pembe ya dunia ambao wao wanachanganya 'concentrate' hiyo na maji (carbonated water) na kuongeza kiwango cha sukari na kusindika kisha kuuza kwa walaji.

Kwa mfano, Bonite Bottlers ya Bw. Reginald Mengi wao wananunua concentrate kutoka makao makuu marekani na kuchanganya na maji na sukari na kuuza kwa walaji.

Wamiliki wa kampuni mama ya coca cola wameweka masharti kama kwa kampuni tanzu za kinywaji hicho, kwa mfano hairuhusiwi makampuni hayo kuingiliana kwenye masoko mfano coca cola ya zambia haiwezi kuuzwa nchini. Kwa sharti hilo kiwanda bonite bottlers cha moshi kinaruhusiwa kuuza coca cola kwenye mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na wilaya mbili za mkoa singida, wilaya hilo ni Singida na Manyoni.

Kwa mara ya kwanza coca cola ilizalishwa nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla mwaka 1952 chini ya mfanyabiashara wa kigiriki Aris Cassolis
 
Mzee hii taarifa yako inajichanganya sana yaani unaruka mwaka afu unarudi juu. em soma tena mwenyewe uone
 
Mimi jaman na Azam cola nimekuwa mlevi kabisaaa.yaan Niko radhi niache kunywa maji ili ninywe azam cola.
 
coca cola wanasema ni kinywaji pekee kinacho faa zaidi kwa kusafishia masinki ya chooni.
 
So zile ingredients katila kizobo chake ni danganya toto kula mboga mbichi!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom