Ifahamu Bodi ya Kimataifa ya Uhasibu (ACCA) kiundani na gharama zake

chikuyu

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
277
179
KUHUSU ACCA (ASSOCIATION OF CHARTERED CERTIFIED ACCOUNTANTS)
MAELEZO MAZURI KUHUSU ACCA AMBAYO HUJAWAHI KUYASIKIA SOMA MAKALA YOTE MPAKA MWISHO.. TWENDE PAMOJA…

ACCA NI NINI?
ACCA ni
Kifupi cha Association of Chartered Certified Accountants ambayo ni Bodi Kubwa (kuliko zote) ya Kimataifa ya Uhasibu Duniani ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Makao makuu ya Bodi hii yako Uingereza, Katika Jiji la Adelphi, London, Anuani yao ni hii hapa: ACCA, The Adelphi, 1-11 John Adam Street, London, WC2N 6AU, Namba ya simu: +44 (0)20 7059 5000.

Hii ndiyo Bodi Kubwa na inayokuwa kwa haraka zaidi Duniani yenye wanachama zaidi ya 208,000 na wanafunzi zaidi ya 503,000 ndani ya nchi 179 duniani kote.
KWA NINI MTU ASOME ACCA? Kwa ufupi tu ni kwamba:-
  • Inakuwezesha kuwa “Chartered Certified Accountant”. Kuwa Chartered maana yake ni mtu ambaye amethibitishwa na Bodi ya Watalaam kuwa ana Ujuzi na Weledi katika Fani Fulani na amepata Cheti cha Uthibitisho kutoka katika Bodi hiyo. Kwa hiyo mtu akitumia maneno ACCA baada ya herufi za jina lake, inaonyesha kwamba mtu huyo ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika sekta ya Uhasibu na Fedha pamoja na Utawala katika Biashara ya aina yoyote ile.
  • Inakupa matarajio makubwa ya kupata ajira nzuri mahala popote duniani kwa kuwa una uwezo wa kufanya kazi katika biashara ya aina yoy0te ile.
  • Inawapa uhakika waajiri kuwa una uwezo mkubwa wa Kukabidhiwa Majukumu Makubwa ya Kiutendaji (Senior Management Positions).
  • Mitihani inafanyika Mara NNE kwa mwaka mzima, yaani March, June, September na December kila mwaka. Hivyo unaweza kumaliza mapema ukiamua.

JE, NI MTU MWENYE ELIMU GANI ANAWEZA KUSOMA ACCA?
ACCA ina ngazi kuu mbili:
Foundations in Accountancy (FIA)
ACCA Qualifications

Foundations in Accountancy (FIA)

Ngazi hii haina vigezo vyovyote vya Elimu ili mtu aanze kusoma. Hii ni kwa ajili ya mtu ambaye hana ujuzi wowote wa uhasibu au hana Elimu yoyote rasmi, ila anataka kuwa Muhasibu.. Hivyo, hapa ni sawa na mtu anayetaka kuanza Darasa la Kwanza la Uhasibu. Unaanza na utangulizi kabisa wa Uhasibu.. Kujiunga ni MTU yeyote Yule ili mradi tu aweza Kujua Kiingereza akaelewa maana ya maneno yalioandikwa na Kufanya baadhi ya maswali ya Hesabu.

ACCA wana Online Platform ya bure kabisa kwa mtu anayehisi Kiingereza chake na Hesabu havipandi.. Anaweza kujifunza hapo kwa bidii huku akiendelea na shule yake ya FIA.

Hii ina maana gani?

Hii ina maana kwamba hata kama mtu kaishia Darasa la saba, ila akataka kujiendeleza Kielimu katika fani ya Uhasibu, anapata mahali pa kuanzia na kuendelea mpaka kufikia PhD akiamua.

Kwa hiyo kama wewe umeishia Darasa la saba, umefeli Kidato cha pili, umefeli Kidato cha nne, umefeli Kidato cha sita, etc. usikate tamaa ukahisi ndo mwisho wa elimu yako. Bado kuna njia ya kukufanya uendelee na shule yako na hatimaye ukawa Mhasibu anayetambulika Kimataifa (Ulimwenguni Kote).

Ili Kusajiriwa na Bodi hii kwa ngazi hii ya Awali ya Uhasibu (FIA), Mtahiniwa angalau anahitajika awe na Identity Card yoyote kama vile Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Kitambulisho cha Taifa, Hati/Pasipoti ya Kusafiria, n.k

Kutegemeana na elimu yako hiyo, utapata mahali sahihi pa kuanzia kusoma Kozi hizi za Kimataifa na Kupata Vyeti tofauti tofauti na katika madaraja tofauti tofauti ambavyo vitakupelekea mpaka kupata ACCA Qualifications.

Pia kuna ushirikiano ambao Bodi ya ACCA wanao na Vyuo Vikuu vya Kimataifa vyenye sifa duniani kama vile Oxford Brookes University ambao wanatoa BSc (Hons) Degree in Applied Accounting kwa wanafunzi wanaosoma ACCA waliomaliza mitihani kadhaa na kufanya Research and Analysis Project kwa muda wa miezi sita.

Pia ACCA wana ushirikiano na Chuo Kikuu maarufu Duniani cha University of London ambacho ni kati ya Vyuo 10 bora nchini Uingereza. Chuo hiki kinatoa MSc in Professional Accountancy kwa wanafunzi wanaosoma au waliomaliza mitihani ya ACCA ambapo wanatakiwa kufanya idadi kadhaa ya Mitihani na Kufanya Research Project ya Chuo hicho na Kupata Masters Degree yako kutoka Chuo hiki cha Kimataifa.

JE, MITIHANI GANI UNAFANYA YA FOUNDATIONS IN ACCOUNTANCY?
Kwanza kabisa Level hii ya Mitihani wanafanya wale walioishia Darasa la Saba, Kidato cha Pili au Cha Nne au aliyetoroka shule bila kumaliza elimu yoyote lakini anahitaji kujiendeleza kwenye Uhasibu na ana uwezo wa Kuelewa Kiingereza na Kufanya hesabu. Makundi haya yanaanzia mitihani tofauti tofauti kutegemeana na Uwezo wao wa Kitaaluma.

NGAZI ZA FOUNDATION IN ACCOUNTANCY NA MASOMO HUSIKA
  1. Introductory Certificate
FA1 Recording Financial Transactions
MA1 Management Information

Certificate hii ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 2, yaani Regulated Qualifications Framework Level 2 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 5), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Technician Certificate.
  1. Intermediate Certificate
FA2 Maintaining Financial Records
MA2 Managing Costs and Finance
Certificate hii ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 3, yaani Regulated Qualifications Framework Level 3 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 6), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Ordinary Diploma. Kwa NBAA ni sawa na Accounting Technician Level I (ATEC I)

  1. ACCA Diploma in Accounting and Business (RQF Level 4)FAB Accountant in Business
FMA Management Accounting
FFA Financial Accounting

Diploma hii ina maana gani?
Hii ni Sawa na RQF Level 4, yaani Regulated Qualifications Framework Level 4 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 7), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Higher Diploma (Diploma ya Miaka miwili), Kwa NBAA ni sawa na Accounting Technician Level II (ATEC II)

NB:
Mitihani yote ya Foundation in Accountancy (FIA) ni Computer Based Exams na inafanyika muda wowote ule unaohisi wewe uko fit kufanya mtihani. Hakuna limitation zozote. Mara tu umalizapo kufanya mtihani wako, majibu yako unapewa hapo hapo.

  1. Certified Accounting Technician (CAT) Qualification
Mitihani miwili tu kati ya hii hapa:
FTX
- Foundations in Taxation
FFM - Foundations in Financial Management
FAU - Foundations in Audit

Certificate hii siyo ya Lazima. Mtahiniwa anaweza kuamua kuendelea moja kwa moja kwenye ACCA Qualifications mara tu baada ya kumaliza mitihani yake ya ACCA Diploma in Accounting and Business (RQF Level 4). Anayefanya hii mitihani ni Yule mtu ambaye anatamani Kubobea katika taaluma Fulani. Hapa mtahiniwa anafanya mitihani miwili tu ya chaguo lake kutegemeana na taaluma ambayo huyo mtahiniwa anatamani kubobea.

Unaweza ukaamua kuwa mtaalam wa maswala ya Kodi, Mtaalam wa maswala ya Ukaguzi au Mtaalam wa maswala ya Utunzaji Fedha. Ni uamuzi wako sasa unachagua mitihani miwili kati ya hiyo. Mitihani hii ni Paper Based Exams, na unafanya kati ya MWEZI June na December either kwa pamoja au Mmoja moja.

CAT Qualificationsi ina maana gani?

Hii ni Sawa na RQF Level 6, yaani Regulated Qualifications Framework Level 6 kwa Uingereza, ambapo kwa Tanzania ni sawa na National Technical Awards (NTA Level 8), kwa Lugha rahisi iliyozoeleka kitaaluma ni Bachelor Degree. Kwa NBAA ni sawa na Foundation Stage.

ACCA QUALIFICATIONS

Ngazi ya pili ya Uhasibu baada ya Kumaliza mitihani hii ya FIA, ni ACCA Qualifications.
Hii ina Ngazi Tatu
Applied Knowledge exams

Accountant in Business (AB)
Management Accounting (MA)
Financial Accounting (FA
Applied Skills exams
Corporate and Business Law (LW)
Performance Management (PM)
Taxation (TX)
Financial Reporting (FR)
Audit and Assurance (AA)
Financial Management (FM)
Strategic Professional (essentials)
Strategic Business Leader
Strategic Business Reporting
Strategic Professional (Any two options only)
Advanced Financial Management (AFM)
Advanced Performance Management (APM)
Advanced Taxation (ATX)
Advanced Audit and Assurance (AAA)

VIGEZO VYA KUSOMA ACCA QUALIFICATIONS

Kwa mtahiniwa aliyeanzia kwenye Level ya Foundations in Accountancy akafikia ACCA Diploma in Accounting and Business (RQF Level 4)/Certified Accounting Technician (CAT Qualifications), huyo ataanzia Applied Skills exams. Yaani atasamehewa masomo matatu ya hapo juu kwenye Applied Knowledge exams kwa kuwa tayari kashayasoma kwenye hizo ngazi nyingine za Diploma.

Kwa mtahiniwa mwenye angalau Pass mbili (2) za Advanced Certificate of Secondary Education (ACSE) kuanzia Grade A-E, na mwenye Passes 3 O-Level kuanzia Grade A-D ikiwemo Kiingereza na Hesabu, anaanzia Kwenye ACCA Qualifications kwenye ngazi ya Applied Knowledge exams na kufanya masomo yote yaliyoonyeshwa hapo juu.

Wanafunzi wengi waliomaliza Degree za Uhasibu za Vyuo Vikuu, wanaanzia sawa sawa na mtu mwenye Certified Accounting Technician (CAT) Qualification yaani kwenye Applied Skills exams. Yaani atasamehewa masomo matatu ya hapo juu kwenye Applied Knowledge exams kwa kuwa tayari kashayasoma kwenye masomo yake ya Degree.

Kuna baadhi ya Vyuo Vikuu ambavyo vimepewa Msamaha wa Masomo mengi ya ACCA ambavyo vimeweza kukubaliana na Masharti ya ACCA ya kuweka Syllabus zao ziendane na Syllabus ya ACCA. Kwa Vyuo hivyo; watahiniwa wake waliomaliza Degree ya Uhasibu wanafanya MITIHANI NANE HADI MITANO TU Kutegemea na Contents; yaani wanafanya Mtihani Mmoja hadi Minne kwenye ngazi ya Applied Skills exams na Mitihani MINNE kwenye ngazi ya Professional Level, i.e Strategic Professional (essentials) anafanya mitihani miwili tu kama inavyoonekana hapo juu, na anachagua mitihani miwili tu kutoka kwenye Strategic Professional (Options) kama ilivyooneshwa hapo juu.

Je, ni vyuo gani hivyo vyenye offer nono kiasi hicho?

Vyuo hivyo ni MZUMBE(Mitihani 5), UDSM (Mitihani 5), IAA (Mitihani 7), MOCU (Mitihani 7) na CBE (Mitihani 8). Hii ina maana kwamba Vyuo vikuu hivi viwili vimekaa meza moja na ACCA wakakubaliana Syllabus Content zao ziweje kwenye Course za Uhasibu. Yaani kwa kifupi ni kwamba vyuo hivi vimekubali kuweka syllabus zao ili ziendane na Contents za ACCA ndo maana ACCA wakawapatia msamaha.

Japokuwa sasa, hii nayo inategemana umemaliza Chuo Kikuu hicho mwaka gani. Kama ni mwaka ambao bado walikuwa hawajakubaliana basi na wewe utaangukia kwenye makundi ya wanaoanzia ngazi ya Applied Skills exams (Yaani unafanya Jumla masomo 10).

KUJUA ZAIDI
masomo utakayosamehewa kutokana na chuo ulichosoma na mwaka uliomaliza Tembelea hapa ACCA Exemptions Calculator au Ingia Google andika ACCA Exemptions Calculator utaletewa mahali pa kuandika jina la Chuo ulichosoma pamoja na kuchagua nchi.. Then utachangua course watakayoileta, utaandika mwaka uliomaliza, baada ya hapo watakwambia ni masomo mangapi utakayosamehewa kutokana na Course contents ulizozisoma kwenye chuo hicho.

JE, CPA (T) HOLDER AKITAKA KUFANYA ACCA ANAANZIA NGAZI GANI?
Kumekuwa na mazungumzo kadha wa kadha kati ya Bodi hizi mbili za Kiuhasibu ya ACCA na NBAA juu ya kutoa misamaha ya masomo kwa mtahiniwa ambaye tayari kashahitimu Mitihani yake ya CPA lakini anatamani afanye na mitihani ya ACCA. Mazungumzo hayo yalichukua kipindi kirefu bila kufikia mwafaka. Lakini sasa makubaliano yaliyofikiwa yako hivi.

Kwa watahiniwa waliomaliza CPA kuanzia mwaka 2017 na kuendelea mbele hao wanaanzia kufanya mitihani ya ACCA kwenye Professional Level. Yaani wanafanya Mitihani MINNE tu kwenye ngazi ya Professional Level, i.e Strategic Professional (essentials) anafanya mitihani miwili tu kama ilivyoonyesha hapo awali, na anachagua mitihani miwili tu kutoka kwenye Strategic Professional (Options) kama ilivyooneshwa awali.

Kwa wale waliomaliza CPA Miaka ya nyuma, yaani kuanzia mwaka 2016 na kurudi nyuma, hao wanakuwa assessed kwa kutumia mfumo huo hapo juu kwenye ACCA Exemption Calculator maana walikuwa hawajafikia mwafaka wa makubaliano kati ya ACCA na NBAA.
NB: Kwa MTU mwenye ACCA, akitaka kufanya CPA, anafanya mitihani MITATU TU yaani Business Law-A5, Public Finance Taxation I-B4 na Public Finance and Taxation II- C4
GHARAMA ZA KUSOMA ACCA
(FOUNDATIONS IN ACCOUNTANCY MPAKA ACCA QUALIFICATIONS)

Watu wengi sana wamekuwa wakiogopa kusoma ACCA kwa kuogopa Gharama.. Lakini leo hii nakwambia ukipiga mahesabu vizuri unaweza kukuta ni nafuu kufanya ACCA kuliko CPA katika mazingira Fulani Fulani hiv.

Lakini kwa Ujumla, Gharama za kusoma ACCA ziko juu kulizo za kusoma CPA. Na hii ni kwa sababu Ukisoma ACCA Cheti chako kinatambulika Dunia nzima na unaweza kufanya kazi ya uhasibu katika nchi yoyote Duniani. Wakati ukisoma CPA Cheti chako kinatambulika Tanzania tu. Hata ukienda Kenya au Uganda/Rwanda etc. hawaitambui CPA yako. Hivyo, kazi zako za uhasibu unaweza kuzifanya ukiwa ndani ya Tanzania tu.

Ukivuka tu mpaka wa nchi kwenda nchi ya jirani, Cheti chako kinapoteza maana. Hivyo unatakiwa tena kusoma mitihani ya Bodi ya nchi hiyo husika ili wakutambue.. Sasa utafanya mitihani mingapi? Kila nchi kweli utaweza kufanya mitihani yao? Basi ukimaliza kusoma hii makala yangu, nakuomba ufanye maamuzi sahihi bila kujali Gharama za Kusoma ACCA bali jali zaidi thamani ya Cheti chako cha ACCA.

Sasa fuatilia Gharama za kusoma ACCA katika jedwali hapa chini. Gharama hizi zinaweza zikabadilika muda hadi muda, hivyo kabla ya kulipia gharama yoyote, hakikisha kwanza unachungulia kwenye website yao hii hapa:

Fees and charges
Gharama ziko katika makundi makuu mawili
Gharama zinazolipwa moja kwa moja ACCA
Gharama za Kusoma Review Classes

Gharama zinazolipwa moja kwa moja ACCA
Ziko katika Makundi Makuu mawili

Gharama za mwanzo za Kujisajili na za zile za Kila mwaka
Gharama za Kujisajili kwa Kila Mtihani utakaofanya

MAKALA HII IMEANDALIWA NA:
YUSTINO NYENDEZA
Fellow Member of the Association of Chartered Certified Accountants (FCCA)
Associate Member of Certified Public Accountants (ACPA)

MANAGING DIRECTOR
STEP AHEAD FINANCIAL CONSULTANT
Uhindini Street, Opposite Heritage Financing,
National Housing Mpwapwa Flats,
P.O. Box 17045,
DODOMA, TANZANIA

TEL NO. 0713388317 or 0757749641

UKIWA NA MASWALI USISITE KUNIULIZA
KARIBUNI SANA
IJUE ACCA_page-0007.jpg
IJUE ACCA_page-0008.jpg
IJUE ACCA_page-0009.jpg
 
chikuyu,
Saw kak .mm nimesoma development finance and investment, nimesoma bussiness law,financial management,financial accounting,management accounting,auditing, na public finance je naanzia level gani.
 
Saw kak .mm nimesoma development finance and investment ,,nimesoma bussiness law,financial management,financial accounting,management accounting,auditing,na public finance je naanzia level gan
Bachelor au Diploma? If Bachelor utaanzia Skiils Level.
 
View attachment 1132415View attachment 1132416View attachment 1132417
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa nikamaliza CPA yangu nitakuja ofisini kuangalia namna ya kusoma ACCA pia
 
Inatambulika, lakini hautapewa kibalii Cha kufanya kazi bila kupitia kwenye Bodi inayosimamia ( kuregulate) issue zote za uhasibu na wahasibu wenyewe. Yaani NBAA.

Ukienda kwenye Bodi kutafuta kibali ili uwe CPA-T utapewa mitihani ambayo inahusisha vitu au mambo ambayo yako relevant /applicable Kwa Tanzania pekee. Mfano Business Law na Taxation

Ukifauli utakua 'CPA-T equivalent'. Hapa Sasa unaweza kufanya kazi kama mhasibu.

Kila nchi Ina regulatory board. Ukienda kenya pia utafanya mitihani ambayo iko relevant na Sheria zao Ili u-suit kufanya kazi Kenya.

Kuna swali lolote?
 
Nina bachelor ya development finance with Investment...nataka nipate professionalism certificate unashauri nichukue kipi kati ya ACCA au CPA
 
Kama una mpango wa kufanya kazi abroad unaweza kufanya ACCA, ila Kama unataka kufanya kazi Tanzania CPA-T inatosha kabisa.

COST-WISE: ACCA Ina gharama kubwa kuliko CPA

UGUMU WA MITIHANI: ACCA ni rahisi lakini. CPA ya bongo ..

All in all, CPA ya bongo is the best
 
Back
Top Bottom