Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,968
Kuna tatizo kubwa limejitokeza sasa hivi kama nchi ambapo kila tuhuma inayoihusu nchi wanaibuka watu kujibu kama wasemaji wa serikali na nchi wakati wasemaji wapo. Kila mmoja anatafuta kuwa mtetezi wa serikali. Na katika kufanya hivi ndipo makosa yatokea zaidi.
Angalia sasa mfano wa matukio mawili ya hivi sasa la Zitto na benki ya Dunia na hili la Marekani na Makonda. Wameibuka watu wanatangaza hadharani tena wakiwa kwenye mihimili ya nchi kuwa Zitto auwawe. Mwingine kaamka alikoamkia kaandika barua kuijibu Marekani na eti kapeleka nakala kwa rais. Unajiuliza je rais alimtuma? Hivi waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa atafanya kazi gani kama kila mtu ni msemaji wa serikali.
Kila mtu anaongea. Sasa tumsikilize nani na nani yupo sahihi? Hawa wasemaji wa kujitolea ni vizuri wapigwe pini wanaiaibisha serikali na kuifanya dhalili. Wanatafuta sifa na vyeo matokeo yake wanatupoteza. Miluzi mingi ilimpoteza mbwa!
Sent using Jamii Forums mobile app