II==Kuwadi wa Fisadi ==>

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Mtoto nipe kalamu, nikae chini nitunge,
Niseme jambo muhimu, na hoja zangu nipange,
Siyo kwamba natuhumu, fikara zangu nilonge,
Ni nani alo kuwadi, kuwadi wake fisadi?

Wapo wamejaa tele, majina twayasikia,
Wapo na kimbelembele, kila kona Tanzania,
Tena na kihelehele, ughaibuni watulia,
Amfichaye fisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo na mapesa yao, kurubuni waandishi,
Watumia vyombo vyao, kuendeleza uzushi,
Umekwisha muda wao, wako kama matapishi,
Mwenye kutunga uongo, ni kuwadi wa fisadi

Wapo wajitangazao, bila wao hatuendi,
Wanadai nchi yao, wengine tuko sitendi,
Wadunda kivyaovyao, maswali hawayapendi,
Watambao kifisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wanaogawana, hazina za nchi yetu,
Kwa mafungu wapeana, wala hawajali kitu,
Tukihoji wananuna, mitima yajaa kutu,
Amlindaye fisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wanaotazama, mafisadi wakiyeya,
Wamekubali kutama, wahalifu wapepeya,
Mwenye kuchuma achuma, kwao yote ni muuya,
Aliyekata tamaa, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wanaobariki, pale wanaponyamaza,
Kwa kimya wanaafiki, mlango wamevugaza,
Kumbe ndio manafiki, kwa kimya wanatuuza,
Mwenye kukaa kimya, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wale wanaswao, kwa mbinu za mikuyati,
Washikwa kama mbachao, hawana tena sauti,
Wacheza ngoma si yao, wamebanwa katikati,
Rafiki yake fisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wale wakanao, hadharani wanapinga,
Kumbe ndio hao hao, sirini wamejifunga,
Gizani wapewa vyao, mafisadi wanaringa,
Fisadi wa sirisiri, ni kuwadi wa fisadi!

Hoja nimeshaitunga, beti hazienda tena,
Mwenye hoja za kupinga, kizuizi mimi sina,
Toka Iringa na Tanga, na magwiji kila kona,
Fisadi ndiye kuwadi, kuwadi wake fisadi!

Shairi hili nimeliweka kwa heshima na kumbukumbu ya Mwalimu wangu wa Kiswahili Marehemu Mzee Hamisi Akida (wengi mlikuwa mkisikia kwenye RTD kipindi cha "Lugha Yeto" akiwa na kina Prof. Zakaria Mokiwa) aliyefariki katikati ya wiki hii. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin.

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
Email: mwanakijiji@klhnews.com
+ 1 248 686 2010
 
Mtoto nipe kalamu, nikae chini nitunge,
Niseme jambo muhimu, na hoja zangu nipange,
Siyo kwamba natuhumu, fikara zangu nilonge,
Ni nani alo kuwadi, kuwadi wake fisadi?

Wapo wamejaa tele, majina twayasikia,
Wapo na kimbelembele, kila kona Tanzania,
Tena na kihelehele, ughaibuni watulia,
Amfichaye fisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo na mapesa yao, kurubuni waandishi,
Watumia vyombo vyao, kuendeleza uzushi,
Umekwisha muda wao, wako kama matapishi,
Mwenye kutunga uongo, ni kuwadi wa fisadi

Wapo wajitangazao, bila wao hatuendi,
Wanadai nchi yao, wengine tuko sitendi,
Wadunda kivyaovyao, maswali hawayapendi,
Watambao kifisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wanaogawana, hazina za nchi yetu,
Kwa mafungu wapeana, wala hawajali kitu,
Tukihoji wananuna, mitima yajaa kutu,
Amlindaye fisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wanaotazama, mafisadi wakiyeya,
Wamekubali kutama, wahalifu wapepeya,
Mwenye kuchuma achuma, kwao yote ni muuya,
Aliyekata tamaa, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wanaobariki, pale wanaponyamaza,
Kwa kimya wanaafiki, mlango wamevugaza,
Kumbe ndio manafiki, kwa kimya wanatuuza,
Mwenye kukaa kimya, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wale wanaswao, kwa mbinu za mikuyati,
Washikwa kama mbachao, hawana tena sauti,
Wacheza ngoma si yao, wamebanwa katikati,
Rafiki yake fisadi, ni kuwadi wa fisadi!

Wapo wale wakanao, hadharani wanapinga,
Kumbe ndio hao hao, sirini wamejifunga,
Gizani wapewa vyao, mafisadi wanaringa,
Fisadi wa sirisiri, ni kuwadi wa fisadi!

Hoja nimeshaitunga, beti hazienda tena,
Mwenye hoja za kupinga, kizuizi mimi sina,
Toka Iringa na Tanga, na magwiji kila kona,
Fisadi ndiye kuwadi, kuwadi wake fisadi!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
Email: mwanakijiji@klhnews.com
+ 1 248 686 2010

Here we go again!!...New Tanzania : Siasa za Mass deception & character assassination..ufisadi ni fashion kama Chiriman, kila mtu anataka kuvaa sasa, wake kwa waume..Sasa unakaa unaandika shairi? duh!!!
 
M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba) unastahili pongezi kwa kutumia uwezo wako wa sanaa kuonya dhidi ya ufisadi na mafisadi. Hivi mashairi yanayotumiwa kufundisha kiswahili mashuleni na vyuoni ni yale ya mwaka 47? dhana ya elimu na sanaa inapaswa kwenda na wakati kulingana na matukio muhimu ktk jamii husika. Jamii yetu imevamiwa na UFISADI hivyo sanaa zote zilipaswa kutuo ujumbe juu ya ufisadi.

Waratibu/Waandishi/Maafisa wa elimu mnaonaje, si vema mashairi kama haya yakatumika kufundisha mashuleni? TUJENGE TANZANIA YA WAZALENDO WANAOCHUKIA UFISADI WA AINA ZOTE.
 
Sasa unaleta ngonjera zako huku kwenye siasa kwa nini? Hata kama ngonjera yako inahusu siasa ungeibandika kwenye mada husika.
 
We achana na mambo ya ufisadi bwana, ufisadi ufisadi, watu washachoka, wameshakubali hali halisi sijui wewe unalalamika nini. Mafisadi walikuwepo na wataendelea kuwapo, jifunze kuishi nao. Kwani hao mafisadi siyo watanzania? Tena wenzako siku hizi wakiitwa "fisadi" wanaona kama promosheni ya aina fulani hivi!

Fisadi ni watu kama sisi na wengine ni jamaa zetu na wengine kwa kutumia ufisadi wao wameweza kufanya mambo mengi tu kwa jamii kama kutoa ajira, misaada, mikopo n.k Hivyo siyo mafisadi wote wabaya!

Asante.
 
We Bi. vipi? unatatizo wewe, yaani unashangilia mafisadi kwa kuhusudia ajira zao? misaada na mikopo? kweli unalipenda taifa lako wewe?. Kweli wewe unapenda vya kupewa!!.
 
Hivi mnafikiri bila ufisadi Tanzania ingekuwa hapa ilipo? Umeona majumba Tabata huko (ukiondoa vijumba vilivyobomolewa), au Mikocheni, au kule "ng'ambo" (Kigamboni). Licha ya ubaya wao lakini mafisadi wameijenga nchi na kama kuijenga nchi ni ufisadi basi na miye kuwadi!

asante.
 
Kwani hayo majumba ya Tabata yanatusaidia nini sisi? si yanawasaidia wao wenye nazo? pia si wote waliojenga nyumba nzuri wanajenga kwa ufisadi. Maendeleo ya mtu mmoja fisadi yanaathari mbaya kwa Watanzania wengi kwa kukosa hudumu muhimu kama vile afya, elimu nk. Hivi kweli wewe Bi senti huoni ubaya wa ufisadi! wonderful
 
Hivi nyie mnaom'putdown' MKJJ mnajua inamchukua muda gani kutunga shairi deep kama hilo? Yawezekana alianza wakati uleee Mwakyembe Day, ndo kamaliza.
MKJJ, u deep, man, u rock!
 
We achana na mambo ya ufisadi bwana, ufisadi ufisadi, watu washachoka, wameshakubali hali halisi sijui wewe unalalamika nini. Mafisadi walikuwepo na wataendelea kuwapo, jifunze kuishi nao. Kwani hao mafisadi siyo watanzania? Tena wenzako siku hizi wakiitwa "fisadi" wanaona kama promosheni ya aina fulani hivi!

Fisadi ni watu kama sisi na wengine ni jamaa zetu na wengine kwa kutumia ufisadi wao wameweza kufanya mambo mengi tu kwa jamii kama kutoa ajira, misaada, mikopo n.k Hivyo siyo mafisadi wote wabaya!

Asante.

Ama kweli akili za watu zina mambo .Senti naona umeguswa kubaya na sasa unahemea juu juu .Khaa siamini niyasomayo unaweza pia ukakaa kimya Upumbavu wako ukawa umefichwa ama ?
 
Nini maana ya kujenga nchi? Kusshusha mahekalu binafsi au kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuboresha na kuimarisha miundo mbinu ambayo ni chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi?

Hekalu liliko Mikocheni linamsaidiaje mwananchi aliye Nkansi ambaye kutokana na ubovu wa barabara anauziwa mahitaji yake kwa bei kubwa ama mazao yake yananunuliwa kwa bei ya chini na hivyo kuishia kuumia.

Mahekalu ya Dar yanawasaidiaje wanafunzi wa shule za msingi ambao shule zao hazina madawati na matokeo wanaishia kukaa chini, huku wakijifunza kuandika kwa kutumia magoti. Kesho wakija na miandiko ya kibatabata mnalalamika kwamba watoto wa siku hizi hawajui kuandika na kumbe mazingira ndiyo yaliyowafanya wawe na poor handwritings ambazo hazisomeki.

Mahekalu hayo yanawasaidiaje wamama wajawazito na watoto wadogo wanaopoteza maisha yao kwa kukosa huduma za afya huko vijijini?

Bi. Senti Hamsini hayo mahekalu yanajenga familia zao na siyo yanajenga nchi, sana sana yanabomoa nchi. Iko siku watu watakuja kuyavamia na kuyachoma moto. Rwanda ni classes za makabila ziliifikisha hapo ilipo, Kenya imenusurika sababu ya ufisadi huu huu ambapo kabila fulani wamekuwa matajiri sana kuliko kabila jingine. Tanzania tutapata jamii ya mafisadi na walalahoi, siku akitokea Mtikila Jangwani na akahamasisha jeshi la walalahoi, hao wenye mahekalu watakuja kuyakimbia wenyewe na kujuta kwanini walijijenga wao badala ya kujenga nchi!
 
napenda vitu kama hivi vya kizalendo,si mafisadi tu hata makuwadi wao....! na pale tunapokuwa kuwa against na mtu kama RA na tunashangilia vilevile tunapokuwa against na mafisadi wengine pamoja na makuwadi wao tushangilie.....kwa hili nipo pamoja na MMKKJ na sipo pamoja na 50 CENT!
 
We LiMwanakijiji mbona unampa kila mtu thanks?

.........takrima hiyo kwani wewe hujui!!? MKJJ, shairi zuri sana, hata kama wakikubabia kwenye siasa bado future unayo kwani miongoni mwa mengi unaweza kuwa anchor wa kipindi cha "malenga wetu."
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom