Igunga: Viongozi wa CCM wakamatwa kwa kuchoma bendera za CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Igunga: Viongozi wa CCM wakamatwa kwa kuchoma bendera za CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Sep 22, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  • Makada wake wakamatwa kwa kuchoma bendera za Chadema
  JESHI la Polisi Wilayani Igunga mkoani Tabora, linawashikilia kiongozi mmoja na kada mwingine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kosa kuchoma mabango ya picha ya mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kushusha bendera za chama hicho.

  Waliotiwa mbaroni juzi jioni ni Katibu wa Msaidizi wa CCM ambaye pia ni Mhasibu wa CCM Wilaya ya Sikonge, Bw. Bakari Luasa na Bw. Rajabu Said ambao walikamatwa katika kijiji cha Chagana Kata ya Itumba.

  Viongozi hao, walikamatwa saa 5:00 asubuhi juzi muda mfupi kabla ya msafara wa mgombea wa CCM, Dkt. Dalaly Kafumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Wilson Mukama na viongozi wengine kuwasili eneo hilo.

  Bw. Mukama na msafara wake walikuta tafrani baada ya wafuasi wa Chadema kuwashikilia viongozi hao na kuwadhiti hadi walipowakabidhi kwa polisi.

  Makada hao wa CCM walipandishwa kwenye gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1946 hadi Kituo cha Polisi mjini Igunga ambako walikabidhiwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Tathmini, Ufuatiliaji na Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika uchaguzi huu, Bw. Isaya Mngulu.

  Wakazi wa kijiji hicho wakiwamo wafuasi wa Chadema walikuwa na marungu, mapanga na mikuki ili kuwashughulikia, lakini jitihada zilizofanywa na kiongozi mmoja wa Chadema, Bw. Kibende Mwang'ombe ziliwatuliza.

  Mwang'ombe aliiambia Majira kuwa waliokamatwa walifika katika eneo hilo kufanya uhalifu wakiwa na mtu mwingine ambaye jina lake halikufamika mara moja, lakini alikimbia baada ya ugomvi kuanza.

  "Siku zote CCM wemekuwa mabingwa wa kueneza siasa za propaganda kwamba Chadema tunafanya fujo, nadhani ninyi wenyewe mmejionea. Jambo lililonifurahisha ni kwamba viongozi waandamizi wa CCM wamejionea wenyewe," alisema Mwang'ombe.

  Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Igunga, Bw. Selemani Majilanga, aliwaomba wananchi na wafuasi wa Chadema wasiwafanyie fujo wahalifu hao.

  "Nawaomba ndugu zangu wananchi msifanye fujo kwa watu hao, wako mikononi mwa polisi, basi acheni sheria ichukue mkondo wake, watashughulikiwa kwa taratibu zote zinazostahili," alisema Majilanga.

  Baada ya watuhumiwa kuondolewa, mkutano huo, uliendelea huku, Bw. Mukama akijinadi kwa wananchi kuwa ametumwa na Rais Jakata Kikwete kuwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo mgombea wa CCM, Dkt. Kafumu ili awe mbunge wao.

  Kwa upende wake, Mratibu wa Kampeni wa CCM ambaye pia ni Katibu wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba aliwataka wananchi kutokuchagua wapinzani kwa sababu hawana serikali.

  Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alilipandisha dumu la maji machafu lita 20 na kumuuliza mgombea wa CCM, Dkt. Kafumu atachukua hatua gani kuondoa adha ya kukosa maji iliyodumu miaka mingi.

  "Nimekuletea maji haya unayoone mwenyewe, sisi tunakunywa maji machafua kiasi hiki, je, ukipata ubunge utafanyaje ili tuondokane na aibu hii ambayo sasa imeonekana kuwa ya kawaida kila kukicha," alihoji mwananchi huyo.

  SOURCE: MAJIRA
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Sep 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  CCM na polisi wao bado wanafanya danganya toto kwa kuwakamata watu ambao hawana influence kwenye chama. wapo wahalifu wengi akiwepo Mukama, Msekwa, John komba lakini hawakamatwi.

  Adhabu yao kwenye sanduku la kura.
   
 3. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Waandishi Wetu, Igunga, Dar

  JESHI la Polisi Wilayani Igunga mkoani Tabora, linawashikilia kiongozi mmoja na kada mwingine wa
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kosa kuchoma mabango ya picha ya mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kushusha bendera za chama hicho.

  Waliotiwa mbaroni juzi jioni ni Katibu wa Msaidizi wa CCM ambaye pia ni Mhasibu wa CCM Wilaya ya Sikonge, Bw. Bakari Luasa na Bw. Rajabu Said ambao walikamatwa katika kijiji cha Chagana Kata ya Itumba.
  Viongozi hao, walikamatwa saa 5:00 asubuhi juzi muda mfupi kabla ya msafara wa mgombea wa CCM, Dkt. Dalaly Kafumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Wilson Mukama na viongozi wengine kuwasili eneo hilo.

  Bw. Mukama na msafara wake walikuta tafrani baada ya wafuasi wa Chadema kuwashikilia viongozi hao na kuwadhiti hadi walipowakabidhi kwa polisi.

  Makada hao wa CCM walipandishwa kwenye gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1946 hadi Kituo cha Polisi mjini Igunga ambako walikabidhiwa kwa Mkuu wa
  Kitengo cha Tathmini, Ufuatiliaji na Upelelezi wa Makosa ya
  Jinai katika uchaguzi huu, Bw. Isaya Mngulu.

  Wakazi wa kijiji hicho wakiwamo wafuasi wa Chadema walikuwa na marungu, mapanga na mikuki ili kuwashughulikia, lakini jitihada zilizofanywa na kiongozi mmoja wa Chadema, Bw. Kibende Mwang’ombe ziliwatuliza.

  Mwang’ombe aliiambia Majira kuwa waliokamatwa walifika katika
  eneo hilo kufanya uhalifu wakiwa na mtu mwingine ambaye jina lake halikufamika mara moja, lakini alikimbia baada ya ugomvi kuanza.

  “Siku zote CCM wemekuwa mabingwa wa kueneza siasa za
  propaganda kwamba Chadema tunafanya fujo, nadhani ninyi
  wenyewe mmejionea. Jambo lililonifurahisha ni kwamba viongozi waandamizi wa CCM wamejionea wenyewe,” alisema Mwang’ombe.

  Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Igunga, Bw. Selemani Majilanga, aliwaomba wananchi na wafuasi wa Chadema wasiwafanyie fujo wahalifu hao.

  “Nawaomba ndugu zangu wananchi msifanye fujo kwa watu hao, wako
  mikononi mwa polisi, basi acheni sheria ichukue mkondo wake, watashughulikiwa kwa taratibu zote zinazostahili,” alisema Majilanga.

  Baada ya watuhumiwa kuondolewa, mkutano huo, uliendelea huku, Bw. Mukama akijinadi kwa wananchi kuwa ametumwa na Rais Jakata Kikwete kuwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo mgombea
  wa CCM, Dkt. Kafumu ili awe mbunge wao.

  Kwa upende wake, Mratibu wa Kampeni wa CCM ambaye pia ni
  Katibu wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba aliwataka
  wananchi kutokuchagua wapinzani kwa sababu hawana serikali.

  Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alilipandisha dumu la
  maji machafu lita 20 na kumuuliza mgombea wa CCM, Dkt. Kafumu atachukua hatua gani kuondoa adha ya kukosa maji iliyodumu miaka mingi.

  “Nimekuletea maji haya unayoone mwenyewe, sisi tunakunywa
  maji machafua kiasi hiki, je, ukipata ubunge utafanyaje ili
  tuondokane na aibu hii ambayo sasa imeonekana kuwa ya
  kawaida kila kukicha,” alihoji mwananchi huyo.

  Madai ya wanazuoni wa kiislamu

  Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.

  Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.

  Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.

  "Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.

  Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.

  Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM

  Helkopta kukata anga

  Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.

  Nyumba ya Katibu CUF yachomwa

  Nyumba ya Katibu Kata wa Kata ya Nyandekwa, Bw. Hamisi Makala imeteketea kwa moto na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.

  Mratibu wa CUF Kata ya Nyandekwa, Bw. Emmanuel Ezekiel alisema wakati akifungua mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho kuwa tukio linahusishwa na mambo ya kisiasa.

  Kutoka na matukio ya kihalifu yanayoendelea katika jimbo la Igunga ambako kampeni za uchaguzi mdogo zikiendelea kushika kasi, CUF imewataka wananchi kuacha kujiingiza kwenye siasa za chuki.

  Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa wa CUF, Bw. Mbarara Maharagande akimwombea kura mgombea Ubunge wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona alisema siasa za kumwaga damu zisipewe nafasi kwani zinajenga uhasama kwa wana Igunga wakati waliosababisha hayo wakitanua Dar es Salaam na familia zao.

  Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga alithibitisha kutokea tukio hilo la moto na kumwagiza Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya kufanya upelelezi haraka.

  CHANZO: GAZETI LA MAJIRA
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Yule aliyemtafuna mke wa kanda wenzake kafikishwa vyombo vya dola au yamemalizwa ki utu uzima?
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Atafikishwa vyombo vya dola vipi wakati dola lenyewe ni la magamba??
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wanao sababisha amani kuvurugika katika kampeni za uchaguzi hapa tanzania ni;

  (a)polisi wasio taka kutenda haki.
  (b)wasimamizi wa uchaguzi na wakuu wa wilaya.
  (c)viongozi wa ngazi za juu wano amuru polisi kufanya wanavyo taka na siyo polisi walivyo ona inafaaa.
  (d)waroho wa madaraka wanaopendelea ccm kwa makusudi kwa matarajio ya kupandishwa vyeo.
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  tia maji tia maji, CCM ZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
   
 8. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  "Kwa upende wake, Mratibu wa Kampeni wa CCM ambaye pia ni Katibu wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba aliwataka wananchi kutokuchagua wapinzani kwa sababu hawana serikali".
  Kumbe usipokuwa na serikali hupaswi kuchaguliwa?Sasa tunashirikisha vyama vya upinzani kwenye chaguzi kwa sababu zipi?
   
 9. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  kuzini na mke wa mtu hata kama wa rais hakuna jinai, kuna madai tu wakubwa.na mlalamikaji inabidi aende mahakamani kufungua kesi ya madai dhidi ya mwizi wake. Polisi hapo hawahusiki kabisaaaaa
   
 10. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli nguvu ya CDM si mchezo wana washikilia viongozi hao wa magamba na kuwakabidhi polisi? Basi magamba hawana watu wa kuwaunga mkono na madhambi yao safari yao kwenda mapumzikoni( akhera) imewadia
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  "....Bw. Mukama na msafara wake walikuta tafrani baada ya wafuasi wa Chadema kuwashikilia viongozi hao na kuwadhiti hadi walipowakabidhi kwa polisi.Makada hao wa CCM walipandishwa kwenye gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1946 hadi Kituo cha Polisi mjini Igunga ambako walikabidhiwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Tathmini, Ufuatiliaji na Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika uchaguzi huu, Bw. Isaya Mngulu." Kama hli lina ukweli basi Polisi mwezi huu wapunguziwe mishahara, yani walikuwa wapi hadi Makamanda wa CDM wanakamata wezi halafu waje na LandCruiser tu kuwachukua? hakika hawastahili kulipwa salary hawa, labda sisiemu chama cha The walking Corpse kiwalipe wao....
   
 12. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Very true.!
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
 14. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Hivi ukweli ukisimama unaweza kuchakachuliwa wakati umeshasimamaaaaa....
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Makada wake wakamatwa kwa kuchoma bendera za Chadema
  *Mukama awaangukia wananchi, adai ametumwa na Kikwete
  *Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC
  *Nyumba ya Katibu Kata wa CUF Nyandekwe yachomwa moto

  Na Waandishi Wetu, Igunga, Dar

  JESHI la Polisi Wilayani Igunga mkoani Tabora, linawashikilia kiongozi mmoja na kada mwingine wa
  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kosa kuchoma mabango ya picha ya mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kushusha bendera za chama hicho.

  Waliotiwa mbaroni juzi jioni ni Katibu wa Msaidizi wa CCM ambaye pia ni Mhasibu wa CCM Wilaya ya Sikonge, Bw. Bakari Luasa na Bw. Rajabu Said ambao walikamatwa katika kijiji cha Chagana Kata ya Itumba.
  Viongozi hao, walikamatwa saa 5:00 asubuhi juzi muda mfupi kabla ya msafara wa mgombea wa CCM, Dkt. Dalaly Kafumu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Wilson Mukama na viongozi wengine kuwasili eneo hilo.

  Bw. Mukama na msafara wake walikuta tafrani baada ya wafuasi wa Chadema kuwashikilia viongozi hao na kuwadhiti hadi walipowakabidhi kwa polisi.

  Makada hao wa CCM walipandishwa kwenye gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1946 hadi Kituo cha Polisi mjini Igunga ambako walikabidhiwa kwa Mkuu wa
  Kitengo cha Tathmini, Ufuatiliaji na Upelelezi wa Makosa ya
  Jinai katika uchaguzi huu, Bw. Isaya Mngulu.

  Wakazi wa kijiji hicho wakiwamo wafuasi wa Chadema walikuwa na marungu, mapanga na mikuki ili kuwashughulikia, lakini jitihada zilizofanywa na kiongozi mmoja wa Chadema, Bw. Kibende Mwang’ombe ziliwatuliza.

  Mwang’ombe aliiambia Majira kuwa waliokamatwa walifika katika
  eneo hilo kufanya uhalifu wakiwa na mtu mwingine ambaye jina lake halikufamika mara moja, lakini alikimbia baada ya ugomvi kuanza.

  “Siku zote CCM wemekuwa mabingwa wa kueneza siasa za
  propaganda kwamba Chadema tunafanya fujo, nadhani ninyi
  wenyewe mmejionea. Jambo lililonifurahisha ni kwamba viongozi waandamizi wa CCM wamejionea wenyewe,” alisema Mwang’ombe.

  Mwenyekiti wa Wazazi CCM Wilaya ya Igunga, Bw. Selemani Majilanga, aliwaomba wananchi na wafuasi wa Chadema wasiwafanyie fujo wahalifu hao.

  “Nawaomba ndugu zangu wananchi msifanye fujo kwa watu hao, wako
  mikononi mwa polisi, basi acheni sheria ichukue mkondo wake, watashughulikiwa kwa taratibu zote zinazostahili,” alisema Majilanga.

  Baada ya watuhumiwa kuondolewa, mkutano huo, uliendelea huku, Bw. Mukama akijinadi kwa wananchi kuwa ametumwa na Rais Jakata Kikwete kuwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo mgombea
  wa CCM, Dkt. Kafumu ili awe mbunge wao.

  Kwa upende wake, Mratibu wa Kampeni wa CCM ambaye pia ni
  Katibu wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba aliwataka
  wananchi kutokuchagua wapinzani kwa sababu hawana serikali.

  Katika mkutano huo, mwananchi mmoja alilipandisha dumu la
  maji machafu lita 20 na kumuuliza mgombea wa CCM, Dkt. Kafumu atachukua hatua gani kuondoa adha ya kukosa maji iliyodumu miaka mingi.

  “Nimekuletea maji haya unayoone mwenyewe, sisi tunakunywa
  maji machafua kiasi hiki, je, ukipata ubunge utafanyaje ili
  tuondokane na aibu hii ambayo sasa imeonekana kuwa ya
  kawaida kila kukicha,” alihoji mwananchi huyo.

  Madai ya wanazuoni wa kiislamu

  Chadema kimesema kuwa hakiko tayari kujibizana na wanazuoni wa kiislamu bali kinasubiri uamuzi wa mahakama utakaoamua iwapo Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario alivuliwa hijabu kwa makusudi alipokamatwa na wafuasi wa chama hicho.

  Hatua hiyo ya Chadema imekuja siku moja baada ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (HAY AT) kukitaka chama hicho kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitaha yake na hivyo kumdhalilisha.

  Akizungumza na wandishi wa habari Makao Makuu ya Chama hicho, Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA Prof. Abdallah Safari alisema kuwa chama hicho hakiko tayari kujibizana na wanazuoni hao.

  "Si vizuri kuzungumzia mambo ambayo yako mahakamani lakini mahakama itaamua kama DC Fatma alivuliwa hijabu na kama alivuliwa ni kwa makusudi gani, ni uamuzi wa mahakama pekee ndio utaokaomua," alisema Prof Safari.

  Alisema kuwa Chadema haina sera ya udini kwa hiyo hakiwezi kushabikia mtu kuvuliwa hijabu kwa makusudi huku akionya viongozi wa dini kuacha kutoa taarifa zinazopotosha ukweli na zinazolenga kuvuruga mshikamano wa Watanzania.

  Prof. Safari ambaye ni mwanasheria na mwanazuoni wa kiisalamu, alisema kauli hizo zina lengo la kufarakanisha umma wa waislamu na chama hicho ambacho kinalengo la kuwaondoa madarakani viongozi wanaodaiwa kunuka ufisadi wa CCM

  Helkopta kukata anga

  Wakati huo huo Chadema kinategemewa kuanza kutumia helkopta kurudia kampeni katika Kata zote 26, lengo likiwa ni kuwakumbusha wananchi na kuwahamasisha kukichagua chama hicho zikiwa zimebaki siku tisa kufika uchaguzi.

  Nyumba ya Katibu CUF yachomwa

  Nyumba ya Katibu Kata wa Kata ya Nyandekwa, Bw. Hamisi Makala imeteketea kwa moto na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.

  Mratibu wa CUF Kata ya Nyandekwa, Bw. Emmanuel Ezekiel alisema wakati akifungua mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho kuwa tukio linahusishwa na mambo ya kisiasa.

  Kutoka na matukio ya kihalifu yanayoendelea katika jimbo la Igunga ambako kampeni za uchaguzi mdogo zikiendelea kushika kasi, CUF imewataka wananchi kuacha kujiingiza kwenye siasa za chuki.

  Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa wa CUF, Bw. Mbarara Maharagande akimwombea kura mgombea Ubunge wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona alisema siasa za kumwaga damu zisipewe nafasi kwani zinajenga uhasama kwa wana Igunga wakati waliosababisha hayo wakitanua Dar es Salaam na familia zao.

  Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga alithibitisha kutokea tukio hilo la moto na kumwagiza Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya kufanya upelelezi haraka.
   
 16. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole sana ccm bendera zikachomwa nyie mmekwisha kwani hata mtaji wa watu hamna
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakazi wa kijiji hicho wakiwamo wafuasi wa Chadema walikuwa na marungu, mapanga na mikuki ili kuwashughulikia, lakini jitihada zilizofanywa na kiongozi mmoja wa Chadema, Bw. Kibende Mwang’ombe ziliwatuliza.

  Nimepapenda hapa, nadhani CCM wataanza kuwa na adabu, yaani ingependeza kama wangecharangwa mapanga wageuzwe visusio
   
 18. M

  Marytina JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  ukiwa ccm unaweza lawiti kitoto kichanga pale makao makuu ya polisi na usiguswe
   
 19. e

  ebrah JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa ukweli inaleta hasira, natamani kujua mukama alidanganya nn?
   
 20. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  Tukiwapiga wanadai eti tumewabaka,hao kupigwa ni muhimu sana.
   
Loading...