zubedayo_mchuzi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2011
- 4,873
- 1,216
Wana Jf imekaaje hyo.
Source-TBC HABARI
Source-TBC HABARI
Hapana,TBC iko kwa ajili ya watawala wa chama , nimeshangaa wanatangaza kwa dk 4 mgombea wa CCM wakampa na wasaa kusema atakayowafanyia wana igunga,sijamsikia wa chadema wala cuf,,bila kurudisha TBC mikononi mwa umma tutazidi kuumia,Nyerere alitulisha elimu ya woga wa kufanya maamuzi ndio tulipofika hadi leo, mwaona wenyewe JK hajamwajibisha waziri yoyote hata walio na tuhuma kawaacha.
HKwa mujibu wa katiba yetu (pamoja na makengeza yake) chombo pekee chenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni MAHAKMA. Jeshi la Polisi kujigeuza na kuwa mahakma si tu ni ukiukwaji wa mgawanyo wa madaraka lakini baya zaidi ni kwamba linatishia ustawi wa jamii yetu ya watanzania -bila kujali itakadi, dini jinsia na hata umri. Pengine hapa tunaanza kuelewa ni kwanini polisi wanapouwa raia wasio na hatia hakuna jambo lolote linalofanyika mfano, upelelezi na hata kuchukua hatua za kinidhamu. Mwaka huu pekee polisi imeshauwa zaidi ya watu 20 na hakuna lolote lilifanyika juu ya mauaji hayo. Sasa leo tuko kwenye uchaguzi anatoka polisi mwenye dhamana ya kusimamia sheria anaamua kutangaza kuwa watu wana ruhusa ya kuvunja sheria. Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu hata kidogo ya kupoteza kodi za watanzania ili kumlipa polisi maana tayari kiongozi wao ameshatangaza kuwa hakuna kitu kinachoitwa 'kuvunja sheria'! Polisi iondoke Igunga.
H
Hebu fikiria kama kada wa Chadema angekutwa na kadi 100 za wapiga kodi. Usingesikia mwisho wake.
kwani mwenye nayo kazi yake nni???Imekaa poa tu, ukinikuta na kitambulisho cha mtu mwingine ni kosa?
IGP Said Mwema amesikia hizo habari, maana namuona kama ana busara kidogo. Bila shaka atamchukulia hatua!!!!!!!!!! Mfumo wa uongozi wa kipolisi wa kina Zombe kazi zao ni kunyamazisha raia kudhurumu na kulinda mfumo wa utawala wa CCM. Hiyo ndio kazi yao kubwa, hawajui kuwa serikali inaweza kuondoka madarakani ikaja serikali nyingine na polisi akaendelea na kazi zake za kulinda usalama wa raia!!!!!!!!!!!!Kwa mujibu wa katiba yetu (pamoja na makengeza yake) chombo pekee chenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni MAHAKMA. Jeshi la Polisi kujigeuza na kuwa mahakma si tu ni ukiukwaji wa mgawanyo wa madaraka lakini baya zaidi ni kwamba linatishia ustawi wa jamii yetu ya watanzania -bila kujali itakadi, dini jinsia na hata umri. Pengine hapa tunaanza kuelewa ni kwanini polisi wanapouwa raia wasio na hatia hakuna jambo lolote linalofanyika mfano, upelelezi na hata kuchukua hatua za kinidhamu. Mwaka huu pekee polisi imeshauwa zaidi ya watu 20 na hakuna lolote lilifanyika juu ya mauaji hayo. Sasa leo tuko kwenye uchaguzi anatoka polisi mwenye dhamana ya kusimamia sheria anaamua kutangaza kuwa watu wana ruhusa ya kuvunja sheria. Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu hata kidogo ya kupoteza kodi za watanzania ili kumlipa polisi maana tayari kiongozi wao ameshatangaza kuwa hakuna kitu kinachoitwa 'kuvunja sheria'! Polisi iondoke Igunga.