Igunga-polisi yasema kukutwa na shahada si yako si kosa

Imekaa poa tu, ukinikuta na kitambulisho cha mtu mwingine ni kosa?
 
TBC iko kwa ajili ya watawala wa chama , nimeshangaa wanatangaza kwa dk 4 mgombea wa CCM wakampa na wasaa kusema atakayowafanyia wana igunga,sijamsikia wa chadema wala cuf,,bila kurudisha TBC mikononi mwa umma tutazidi kuumia,Nyerere alitulisha elimu ya woga wa kufanya maamuzi ndio tulipofika hadi leo, mwaona wenyewe JK hajamwajibisha waziri yoyote hata walio na tuhuma kawaacha.
 
Polisi wako mfukoni mwa magamba hivyo hakuna chochote chenye maslahi kwa wananchi wanachoweza kuongea ama kufanya kwa sasa hususan huko igunga.
 
Tume inasema ni kosa, polis ndo wanasema si kosa, tena jamaa kasema kbs mtu anayelalamikiwa kukutwa na kad ilikuwa ya hawara yake, so ni fresh, polis nao ni magamba, hata siku ya kura wataruhusu m2 kutumia kad ya hawara kupiga kura,
 
Kwa mujibu wa katiba yetu (pamoja na makengeza yake) chombo pekee chenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni MAHAKMA. Jeshi la Polisi kujigeuza na kuwa mahakma si tu ni ukiukwaji wa mgawanyo wa madaraka lakini baya zaidi ni kwamba linatishia ustawi wa jamii yetu ya watanzania -bila kujali itakadi, dini jinsia na hata umri. Pengine hapa tunaanza kuelewa ni kwanini polisi wanapouwa raia wasio na hatia hakuna jambo lolote linalofanyika mfano, upelelezi na hata kuchukua hatua za kinidhamu. Mwaka huu pekee polisi imeshauwa zaidi ya watu 20 na hakuna lolote lilifanyika juu ya mauaji hayo. Sasa leo tuko kwenye uchaguzi anatoka polisi mwenye dhamana ya kusimamia sheria anaamua kutangaza kuwa watu wana ruhusa ya kuvunja sheria. Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu hata kidogo ya kupoteza kodi za watanzania ili kumlipa polisi maana tayari kiongozi wao ameshatangaza kuwa hakuna kitu kinachoitwa 'kuvunja sheria'! Polisi iondoke Igunga.
 
TBC iko kwa ajili ya watawala wa chama , nimeshangaa wanatangaza kwa dk 4 mgombea wa CCM wakampa na wasaa kusema atakayowafanyia wana igunga,sijamsikia wa chadema wala cuf,,bila kurudisha TBC mikononi mwa umma tutazidi kuumia,Nyerere alitulisha elimu ya woga wa kufanya maamuzi ndio tulipofika hadi leo, mwaona wenyewe JK hajamwajibisha waziri yoyote hata walio na tuhuma kawaacha.
Hapana,
Woga wako usimsingizie Nyerere. Alifanya alichoweza na kuondoka. Beba msalaba wako mwenyewe.
 
Kwa mujibu wa katiba yetu (pamoja na makengeza yake) chombo pekee chenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni MAHAKMA. Jeshi la Polisi kujigeuza na kuwa mahakma si tu ni ukiukwaji wa mgawanyo wa madaraka lakini baya zaidi ni kwamba linatishia ustawi wa jamii yetu ya watanzania -bila kujali itakadi, dini jinsia na hata umri. Pengine hapa tunaanza kuelewa ni kwanini polisi wanapouwa raia wasio na hatia hakuna jambo lolote linalofanyika mfano, upelelezi na hata kuchukua hatua za kinidhamu. Mwaka huu pekee polisi imeshauwa zaidi ya watu 20 na hakuna lolote lilifanyika juu ya mauaji hayo. Sasa leo tuko kwenye uchaguzi anatoka polisi mwenye dhamana ya kusimamia sheria anaamua kutangaza kuwa watu wana ruhusa ya kuvunja sheria. Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu hata kidogo ya kupoteza kodi za watanzania ili kumlipa polisi maana tayari kiongozi wao ameshatangaza kuwa hakuna kitu kinachoitwa 'kuvunja sheria'! Polisi iondoke Igunga.
H
Hebu fikiria kama kada wa Chadema angekutwa na kadi 100 za wapiga kodi. Usingesikia mwisho wake.
 
Jasusi huyu polisi wa Igunga sidhani kama anakaa chini na kuchanganua mambo kichwani kwake kabla ya kuongea. Kenya waliingia kwenye machafuko kwa sababu ya ukiukwaji wa haki na sheria wakati wa uchaguzi. Kama huyu Polisi anataka kujua nafasi/wajibu wake kwa jamii ya watanzania wote basi namshauri kesho aangalie Citizen TV ya Kenya kuanzia saa 9.30 alasiri, atamwona polisi mwenziwe wa toka Kenya akijibu mashtaka kule the Hague (ICC).

Hizi mbinu za kizamani za kunyanganya watu haki yao zitawaletea matatizo makubwa hawa mabwana. Tatizo ni mawazo mgando.
 
Binafsi nadhani kukujwa na shahada ya mtu si kosa. Ila kosa ni ile nia na mazingira ya hiyo shahada kukutwa nayo ndivyo vinavyoweza kusababisha kosa. Hata hivyo kama walivyosema wanajf wenzangu ilipaswa mahakama ndio itoe tafsiri.
 
Kwa mujibu wa katiba yetu (pamoja na makengeza yake) chombo pekee chenye mamlaka ya kutafsiri sheria ni MAHAKMA. Jeshi la Polisi kujigeuza na kuwa mahakma si tu ni ukiukwaji wa mgawanyo wa madaraka lakini baya zaidi ni kwamba linatishia ustawi wa jamii yetu ya watanzania -bila kujali itakadi, dini jinsia na hata umri. Pengine hapa tunaanza kuelewa ni kwanini polisi wanapouwa raia wasio na hatia hakuna jambo lolote linalofanyika mfano, upelelezi na hata kuchukua hatua za kinidhamu. Mwaka huu pekee polisi imeshauwa zaidi ya watu 20 na hakuna lolote lilifanyika juu ya mauaji hayo. Sasa leo tuko kwenye uchaguzi anatoka polisi mwenye dhamana ya kusimamia sheria anaamua kutangaza kuwa watu wana ruhusa ya kuvunja sheria. Kwa mantiki hiyo basi, hakuna sababu hata kidogo ya kupoteza kodi za watanzania ili kumlipa polisi maana tayari kiongozi wao ameshatangaza kuwa hakuna kitu kinachoitwa 'kuvunja sheria'! Polisi iondoke Igunga.
IGP Said Mwema amesikia hizo habari, maana namuona kama ana busara kidogo. Bila shaka atamchukulia hatua!!!!!!!!!! Mfumo wa uongozi wa kipolisi wa kina Zombe kazi zao ni kunyamazisha raia kudhurumu na kulinda mfumo wa utawala wa CCM. Hiyo ndio kazi yao kubwa, hawajui kuwa serikali inaweza kuondoka madarakani ikaja serikali nyingine na polisi akaendelea na kazi zake za kulinda usalama wa raia!!!!!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom