Igunga Ni Kielelezo Cha Uwendawazimu Wetu! ( Makala, Mwananchi Jumapili)

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,

Ndugu zangu,
Wahehe wana msemo unasema: ‘Isenga imbofu na isenga indenyeefu'. Maana yake, ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu. Wote watakufa njaa. Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.

Ndugu zangu, Kuna uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge utafanyika jimbo la Igunga. Kuna mengi yanatokea kule Igunga. Tafsiri yangu ; Igunga ni kielelezo cha uendawazimu wetu. Maana, haijapata kutokea katika historia ya nchi hii kwa kiti kimoja cha ubunge kikalifanya taifa zima lizizime. Leo njia zote zinaelekea Igunga.

Msomaji wangu mwuza samaki katika soko la Igunga ananiambia kuwa, Igunga sasa imevamiwa na wageni wengi na biashara yake ya samaki haijapata kuwa nzuri kama ilivyo sasa. Lakini anajua, kuwa baada ya Oktoba 3 biashara yake ya samaki itarudi kuwa ya kusuasua kama zamani.
Na ajabu ya Igunga ni hii; kuwa chanzo chake ni falsafa ya kujivua gamba. Rostam Aziz anasemwa kuwa ni mmoja wa magamba ndani ya chama chake. Akajiuzulu. Kiti cha ubunge kikawa wazi. Na Rostam ' gamba' akarudi Igunga kumwombea kura mgombea wa chama chake. Kioja. Rostam Aziz ametusaidia kutupambanulia zaidi tukajua; kuwa kama taifa tuna gamba tunalopaswa kujivua. Ona kule Igunga, kiti kile cha ubunge kimekuwa chanzo cha kupandikiza chuki zaidi miongoni mwetu Watanzania.

Tunaona kule Igunga; viongozi wa dini wanashiriki siasa za vyama huku wakijua kuwa waumini wao wana tofauti za kiitikadi. Tunaona watendaji wa Serikali wakishiriki kampeni huku wakijua wanaamsha manung'uniko kwa wafuasi wa vyama.

Tunaona vitendo vya kujichukulia sheria mikononi na hata kuwapiga raia, viongozi wa vyama na watendaji wa Serikali vikifanywa na wafuasi wa vyama. Tumeona jinsi uchaguzi wa Igunga ulivyovigawa vyombo vya habari na wanahabari. Tumeona hata kiongozi wa kisiasa akisimama jukwaani akiomba kura akiwa na bastola kiunoni. Tulipofikia ni pabaya sana.

Tumeona, kuwa mabilioni ya shilingi yanatumika kwenye kampeni na huku rushwa ya kuhonga wapiga kura na hata kununua shahada za kupigia kura ikifanyika. Yote haya ni katika kuwania kiti kimoja cha ubunge wa jimbo moja kati ya majimbo zaidi ya mia mbili ya nchi hii. Huu ni
uendawazimu.

Na ajabu ni kuwa uchaguzi wa Igunga ulikuja na sura ya kupambana na ufisadi. Tunachokiona Igunga sasa ni zaidi ya ufisadi. Ni janga. Tuna lazima ya kutafuta namna nyingine ya kuendesha mambo yetu kistaarabu na kulinda hadhi na maslahi ya taifa.

Tuna lazima ya kukaa chini kama taifa na kutafakari mustakabali wetu. Nchi yetu haijaishiwa watu wenye hekima na busara. Maana Inahusu ufisadi uliotamalaki. Na juzi hapa nilimsikia Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta kwenye kipindi hicho cha ' Enzi Hizo' kwenye TBC. Jaji Mkuu Mstaafu Samatta aliongea jambo la hekima sana. Alisema; " Kamwe, umma usikubali kelele dhidi ya rushwa zififie, bali ziongezeke".

Vita inayopiganwa sasa Igunga huenda haina maana yeyote kwetu. Maana, kuna cha kujifunza kutoka kwenye ngano ya mazungumzo baina ya Mfalme Pyrrhic na mpambe wake Cineas. Miaka mingi iliyopita alitokea Mfalme wa Epilus aliyeitwa Pyrrhic.

Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi, ni jeshi la Warumi. Lakini kabla ya Mfalme kuingia baharini na vikosi vyake kuitafuta Italia ya Warumi, msaidizi wake wa karibu, Cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na Mfalme. Alitaka kumwuliza maswali na kumshauri.

Cineas alimtamkia Mfalme; " E bwana Mfalme, Warumi wanasadikika kuwa na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana wameteka nchi nyingi. Je, Mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda Warumi, tutafanya nini na ushindi wetu? Mfalme akajibu: " Mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara tutakapowashinda Warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa Italia litakaloweza kupambana nasi."

Cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza Mfalme: " Tukishaikamata Italia ya Warumi, kipi kitafuatia?"
Mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa, itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho."

Cineas aliendelea kuuliza: " Bwana Mfalme unaongea juu ya mambo ya kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha Sicily kutakuwa na maana ya kukoma kwa vita?" Mfalme akajibu: " Hapo tutakuwa tumeikaribia Afrika. Na tukishaikamata Afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita?"
" Hakuna" Alijibu Cineas, kisha akauliza; " Na baada ya hapo tutafanya nini?"

Mpaka hapo Mfalme hakujua Cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya kifikra. Mfalme akajibu: " Baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa . Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima."

Kama ni hivyo, alisema Cineas; " Ni kitu gani kinachotuzuia kufanya hayo yote sasa bila kwenda vitani?
Mfalme hakuielewa mantiki ya Cineas. Akakaidi ushauri.
Akavipeleka vikosi vyake kupambana na Warumi. Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme liliwashinda Warumi. Hata hivyo lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu kuitwaa Sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye akakakamatwa na kuuawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya Argos. "Isenga imbofu na isenga indenyeefu." Ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu, wote watakufa njaa. Nahitimisha.


0712 95 61 31 / 0788 111 765/ 0754 678 252
http://mjengwablog.com

 

BABA JUNJO

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
241
14
maggid, Nchi hii ina maajabu mengi sio hayo tu baba. Ni kwasababu nchi hii hatujawahi pata uhuru wa kufikiri siku zote tumekuwa tukifikiriwa na watu wengine tu na hata tukijaribu kufikiri tuliambiwa nyamaza kufikiri ama watiwa kizuizini kwa hiyo hayo ndiyo matokeo yake. Wakoloni wetu kifikra leo wana haha kisa eti watu wameanza kufikiri wenyewe watajua mengi yaliyofunikwa itakuwa tabu wanajaribu sasa kufunika funika ili yamkini watu waache kufikiri. But time is out there is no way.....
 

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,534
8,622
Majjid,
Uchaguzi wa Igunga ni kielelezo cha demokrasia iliyoshindikana. Tumeiga demokrasia pasipo kuwa na itikadi pinzani zaidi ya kubadilisha vichwa vya watawala wetu..Lakini kuna tofauti kubwa sana sasa hivi na miaka ya nyuma kwa sababu angalau leo wananchi wamechoka na udhalilishaji wa CCM. Wananchi wana mwamko zaidi ktk kudai maisha bora na hivyo msingi wa kutaka mabadiliko haya unatokana na siasa mbaya za CCM ambazo zinawanyima fursa na mambo ya msingi kabisa ktk maisha yao. Tofauti na huyo Cineas wananchi leo wanataka kumwondoa Mfalme mwenyewe hivyo matokeo ya vita (kama yatakuwepo) ni kutokana na mfalme kukataa kuachia kiti kikubwa.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
na maggid mjengwa,

ndugu zangu,
wahehe wana msemo unasema: ‘isenga imbofu na isenga indenyeefu'. Maana yake, ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu. Wote watakufa njaa. Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.

Ndugu zangu, kuna uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge utafanyika jimbo la igunga. Kuna mengi yanatokea kule igunga. Tafsiri yangu ; igunga ni kielelezo cha uendawazimu wetu. Maana, haijapata kutokea katika historia ya nchi hii kwa kiti kimoja cha ubunge kikalifanya taifa zima lizizime. Leo njia zote zinaelekea igunga.

Msomaji wangu mwuza samaki katika soko la igunga ananiambia kuwa, igunga sasa imevamiwa na wageni wengi na biashara yake ya samaki haijapata kuwa nzuri kama ilivyo sasa. Lakini anajua, kuwa baada ya oktoba 3 biashara yake ya samaki itarudi kuwa ya kusuasua kama zamani.
Na ajabu ya igunga ni hii; kuwa chanzo chake ni falsafa ya kujivua gamba. Rostam aziz anasemwa kuwa ni mmoja wa magamba ndani ya chama chake. Akajiuzulu. Kiti cha ubunge kikawa wazi. Na rostam ' gamba' akarudi igunga kumwombea kura mgombea wa chama chake. Kioja. Rostam aziz ametusaidia kutupambanulia zaidi tukajua; kuwa kama taifa tuna gamba tunalopaswa kujivua. Ona kule igunga, kiti kile cha ubunge kimekuwa chanzo cha kupandikiza chuki zaidi miongoni mwetu watanzania.

Tunaona kule igunga; viongozi wa dini wanashiriki siasa za vyama huku wakijua kuwa waumini wao wana tofauti za kiitikadi. Tunaona watendaji wa serikali wakishiriki kampeni huku wakijua wanaamsha manung'uniko kwa wafuasi wa vyama.

Tunaona vitendo vya kujichukulia sheria mikononi na hata kuwapiga raia, viongozi wa vyama na watendaji wa serikali vikifanywa na wafuasi wa vyama. Tumeona jinsi uchaguzi wa igunga ulivyovigawa vyombo vya habari na wanahabari. Tumeona hata kiongozi wa kisiasa akisimama jukwaani akiomba kura akiwa na bastola kiunoni. Tulipofikia ni pabaya sana.

Tumeona, kuwa mabilioni ya shilingi yanatumika kwenye kampeni na huku rushwa ya kuhonga wapiga kura na hata kununua shahada za kupigia kura ikifanyika. Yote haya ni katika kuwania kiti kimoja cha ubunge wa jimbo moja kati ya majimbo zaidi ya mia mbili ya nchi hii. Huu ni
uendawazimu.

Na ajabu ni kuwa uchaguzi wa igunga ulikuja na sura ya kupambana na ufisadi. Tunachokiona igunga sasa ni zaidi ya ufisadi. Ni janga. Tuna lazima ya kutafuta namna nyingine ya kuendesha mambo yetu kistaarabu na kulinda hadhi na maslahi ya taifa.

Tuna lazima ya kukaa chini kama taifa na kutafakari mustakabali wetu. Nchi yetu haijaishiwa watu wenye hekima na busara. Maana inahusu ufisadi uliotamalaki. Na juzi hapa nilimsikia jaji mkuu mstaafu barnabas samatta kwenye kipindi hicho cha ' enzi hizo' kwenye tbc. Jaji mkuu mstaafu samatta aliongea jambo la hekima sana. Alisema; " kamwe, umma usikubali kelele dhidi ya rushwa zififie, bali ziongezeke".

Vita inayopiganwa sasa igunga huenda haina maana yeyote kwetu. Maana, kuna cha kujifunza kutoka kwenye ngano ya mazungumzo baina ya mfalme pyrrhic na mpambe wake cineas. Miaka mingi iliyopita alitokea mfalme wa epilus aliyeitwa pyrrhic.

Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi, ni jeshi la warumi. Lakini kabla ya mfalme kuingia baharini na vikosi vyake kuitafuta italia ya warumi, msaidizi wake wa karibu, cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na mfalme. Alitaka kumwuliza maswali na kumshauri.

Cineas alimtamkia mfalme; " e bwana mfalme, warumi wanasadikika kuwa na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana wameteka nchi nyingi. Je, mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda warumi, tutafanya nini na ushindi wetu? Mfalme akajibu: " mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara tutakapowashinda warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa italia litakaloweza kupambana nasi."

cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza mfalme: " tukishaikamata italia ya warumi, kipi kitafuatia?"
mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa, itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho."

cineas aliendelea kuuliza: " bwana mfalme unaongea juu ya mambo ya kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha sicily kutakuwa na maana ya kukoma kwa vita?" mfalme akajibu: " hapo tutakuwa tumeikaribia afrika. Na tukishaikamata afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita?"
" hakuna" alijibu cineas, kisha akauliza; " na baada ya hapo tutafanya nini?"

mpaka hapo mfalme hakujua cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya kifikra. Mfalme akajibu: " baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa . Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima."

kama ni hivyo, alisema cineas; " ni kitu gani kinachotuzuia kufanya hayo yote sasa bila kwenda vitani?
Mfalme hakuielewa mantiki ya cineas. Akakaidi ushauri.
Akavipeleka vikosi vyake kupambana na warumi. Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme liliwashinda warumi. Hata hivyo lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu kuitwaa sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye akakakamatwa na kuuawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya argos. "isenga imbofu na isenga indenyeefu." ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu, wote watakufa njaa. Nahitimisha.


0712 95 61 31 / 0788 111 765/ 0754 678 252
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo


mkuu maggid, acha ubahili changia jf mkono mtupu haulambwi, being a member for 5 yrs is not a joke!
 

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,641
1,214
MM Mwanakijiji,

You have spoken. Uliyosema yote ni sawasawa kabisa.

Hakika kinachofanyika Igunga kwa sasa ni zaidi ya WENDAWAZIMU. Tanzania imefikia pabaya, Nasikia harufu ya damu. Tunachokishuhudia Igunga kwa sasa si KAMPENI tena baali ni UHUNI,USHENZI.UPUMBAFU NA UJUHA WA CHAMA CHA MAGAMBA-CCM!!!

Kama hawatapatikana WATU wenye BUSARA NA KUINGILIA KATI kwa kipindi hiki cha wiki 1 iliyobaki kabla ya tarehe 2/1o/2011 ni dhahiri kwamba tunaenda KUSHUHUDIA YALE YALIYOTOKEA MWAKA 2007 KWENYE UCHAGUZI WA KENYA! Kwamba kuna watu WATAUAWA(Wana-Igunga na wasio) KWA AIDHA KUCHINJWA,KUCHOMEWA NYUMBA ZAO KWA MOTO AU KUPIGWA RISASI ZA MOTO.

Hili ndugu zanguni Watanzania liko wazi kabisa na CCM ndiyo wana andaa MAZINGIRA YA HALI HIYO YA KUTISHA. Kwamba JESHI LA POLISI KWA KUTUMIWA NA CCM LINAWEKA MKAKATI WA MAKUSUDI WA KUANDAA MAZINGIRA HAYO. Mikakati iko wazi kabisa na kila mtu anaweza kushuhudia. Kwa uchache tu labda nitoe highlights zangu:
  1. Wabunge na Vioingozi wa CCM kwa MAKUSUDI KABISA WAMERUHUSIWA NA JESHI LA POLISI KWENDA NA SILAHA ZA MOTO KWENYE MIKUTANO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI kinyume kabisa na sheria za Uchaguzi. Polisi imewaona lakini imewafumbia macho maana inajua the mortive behind.
  2. Maneno ya Katibu Mkuu wa CCM- W.Mukama kuwa CDM wameingiza MAKOMANDOO 33 trained kutoka Afghanistan sijui na Libya na kwamba wako Igunga kwa kazi ya kufanya vurugu na kuzuia watu wasipige kura. If you read between the lines maneno ya MUKAMA yana maana kubwa sana. Kwamba Mukama alisema makusudi kuandaa mazingira ya UHALIFU HUO UTAKAOFANYWA NA CCM WENYEWE(Makomandoo) HALAFU LAWAMA ZIENDE CHADEMA. Live example wa Comando hao ni ADEN RAGE(MB-CCM Tabora mjini),ESTHER BULAYA(MB-CCM Kuteuliwa),AESHI HILALI(MB-CCM Sumbawanga mjini).
  3. Nyumba KUCHOMWA MOTO na KUTEKEKETEA KABISA lakini KARATASI yenye maneno ya CHADEMA HAIKUWEZA KUUNGUA!!!Maajabu ya 9 ya Dunia.
  4. DC IGUNGA, Bi FATUMA JOHN KIMARIO kutumiwa na CCM kuvuruga kampeni za CDM na baadaye kusingizia kuwa ALIDHALILISHWA KWA KUVULIWA HIJAB na wafuasi wa CDM ilhali yeye NI MKRISTO ANAYEVAA MTANDIO NA MLA NGURUWE. Baada ya hapo tumesikia WAISLAMU NA BAKWATA yao wakinasa mtego wa CCM kwa kukubali na kulaani kitendo bandia kilichotengenzwa na CCM kuwarubuni Waislamu hatimaye kuwa amuru wafuasi wa dini ya KIISLAMU wasipigie kura CDM maana inaendekeza UKRISTO!
Kwa highlights hizi,mtu makini ANAWEZA KUBAINI KABISA KUWA CCM wameshashindwa Uchaguzi wa Igunga na wanachofanya kwa sasa ni kutaka KUVURUGA UCHAGUZI HUO USIFANYIKE AU KUTUMIA KILA MBINU HARAMU NA HALALI ILI KUJIHAKIKISHIA USHINDI!

Laiti kama ningeliweza KUJIPENYEZA KWENYE MIOYO YA WANA IGUNGA WAKAWEZA KUONA KILE KINACHOFANYIKA NYUMA YA PAZIA. Kwamba ROSTAM AZIZ AMEODOLEWA KWA SHINIKIZO NA CCM YENYEWE KWAMBA NI GAMBA. WANA IGUNGA WAKAMLILIA MB WAO NA WENGINE WAKAZIRAI. GAMBA HILO HILO KWENYE UCHAGUZI LIKAITWA KUOMBA KURA KWA AJILI YA CCM!!!!!HUU KAMA SIYO USANII NA KUCHEZA NA AKILI ZA WATU NI KITU GANI???? DAWA NI MOJA TU,KUWANYIMA KURA CCM kwa uhuni wanaowafanyia watu wa Igunga.

WAKTI WA CCM KUWAFANYA WA-TZ NI MAZUZU WASIOWEZA KUFIKIRI UMEKWISHA. SHIME SHIME WANA IGUNGA HEBU FANYENI KAMA NDUGU ZETU WA ZAMBIA WALIO DHIHIRISHA JUZI KWENYE UCHAGUZI MKUU WA ZAMBIA KUWA HAKI YAWEZA PATIKANA KWENYE SANDUKU LA KURA. Wazambia juzi walikipigia chama cha UPINZANI CHA BWANA MICHAEL SATTA na hivyo kumbwaga chini RUPIA BANDA WA CHAMA KILICHOKUWA KINATAWALA ZAMBIA CHA MMD.

Nimalize kwa kusema kwamba WANA IGUNGA,PLAY YOUR PART IT CAN BE DONE AND THAT FREEDOM IS COMING TOMORROW.
God Bless Igunga,God Bless Tanzania, God Bless all Voters in Igunga.
 

Queen Kyusa

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
663
161
Kwakweli bwana magidd umeongea vitu vya msingi sana lakini ukweli upo wazi wanaotaka kuvuruga amani na uchaguzi wa igunga ni ccm na polic kwakushindwa kusimamia haki na ukweli wamebaki kuwa watumwa wa ccm.
Hali imekuwa mbaya kwa ccm na wao wanaliona hilo sera ya kuvuana magamba waliona ni rahisi sana lakini sio rahisi kama walivyokuwa wanafikiria mambo yameanza kuwaendea kombo wanachotaka kufanya ni kuvuruga uchaguzi hata kwa damu kumwagika.
Lakini inapaswa kuwaachia wana igunga waamue ni kiongozi yupi wana mtaka bila kutumia propaganda za kishenzi ambazo zinatumika kwasasa za udini na makomandoo.
Kuna kiongozi wa ccm ametangaza kuwa kama ubunge utachukuliwa na cdm atajiua siasa kama hizi zinabaka demokrasia ya kweli na ndomana wanahaha usiku na mchaka kuleta vurugu nili yote kupata chance ya kuiba kura na kuvuruga uchaguzi.

Historia itaandikwa igunga ccm watake au wasitake. Mungu ibariki Tanzania
 

Alwatan

JF-Expert Member
May 19, 2009
409
127
Majjid,
Uchaguzi wa Igunga ni kielelezo cha demokrasia iliyoshindikana. Tumeiga demokrasia pasipo kuwa na itikadi pinzani zaidi ya kubadilisha vichwa vya watawala wetu..Lakini kuna tofauti kubwa sana sasa hivi na miaka ya nyuma kwa sababu angalau leo wananchi wamechoka na udhalilishaji wa CCM. Wananchi wana mwamko zaidi ktk kudai maisha bora na hivyo msingi wa kutaka mabadiliko haya unatokana na siasa mbaya za CCM ambazo zinawanyima fursa na mambo ya msingi kabisa ktk maisha yao. Tofauti na huyo Cineas wananchi leo wanataka kumwondoa Mfalme mwenyewe hivyo matokeo ya vita (kama yatakuwepo) ni kutokana na mfalme kukataa kuachia kiti kikubwa.

Mkuu, mi naona tatizo letu kubwa kabisa kama taifa ni ushabiki kwenye mambo yanayotakiwa tafakari ya kina.

Sasa hivi utaona watu wanataka mabadiliko. Ni kweli kila mtanzania atakwambia anataka mabadiliko. Ila mabadiliko gani?

Je ni mabadiliko ya sura za viongozi? Je ni mabadiliko ya majina ya vyama vinavyotawala? au mabadiliko ya mfumo mzima wa utawala utakaotoa fursa kwa wote bila ubaguzi, na kwamba kutakua na proper checks and balances ya mihimili mikuu mitatu ya utawala.

Sasa utagundua kelele nyingi za KATIBA MPYA ni kama zimebakia kama ni distant echo. Hii ni kwa sababu upepo sasa hivi unaelekea kubaya kwa
chama tawala na unavuma kusukuma mageuzi kwenye uchaguzi mkuu ujao 2015.

Je, tukibadili sura na chama, lakini tukaacha KATIBA ya kibabe ileile, inayominya na kumpa mkuu wa nchi mamlaka ya mungu mtu, je tutakua
tumetatua matatizo yetu?

Huu ushabiki kwenye mambo serious unani unsettle kwa kweli, kama tunataka mageuzi ya ukweli basi suala la katiba mpya lazima liwe ni la paramount importance kabla ya uchaguzi mkuu wa 2015. Ila kwa mwendo ulivyo hope zangu zinazidi kufifia.

Tutapiga kura, tutachagua sura na chama, halafu baadae tutakuja kugundua tumetengeza wakoloni wapya weusi.

Nilikuwepo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Top Bottom