Igunga: Mwenyekiti wa muda wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi aonya kuhusu vurugu

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka watu wote wanaoshiriki katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga kuacha kufanya vitendo viovu, ikiwemo kuzingatia sheria , taratibu na maadili ya uchaguzi.

Aidha tume hiyo imetoa masikitiko yake dhidi ya vitendo vya kiuhuni na visivyo vya kistaarabu vinavyofanywa na baadhi ya Vyama Vya Siasa katika uchaguzi huo. Huku ikisema kuwa viongozi wake watakwenda Igunga kuzungumza na vyama hivyo ili kuwakumbusha sheria na maadili ya uchaguzi huo.

Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Mwenyekiti wa Muda wa NEC, Profesa Amon Chaligha wakati akitoa tamko la tume hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kufutia kuwepo kwa matukio mengine ya ukwiukaji wa maadili ya uchaguzi huo.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawaasa wale wote wanaofanya na wanaoendeleza vitendo hivyo waache mara moja kwa usalama wa taifa letu na ustawi wa wananchi wa Jimbo la Igunga kwa ujumla,” alisema Profesa Chaligha.

Aliyataja matukio hayo kuwa ni kurushiana risasi za moto, kuwa na silaha katuika mikutano ya kampeni, kutumia lugha za matuzi na vitisho katika mikutano ya kampeni na kutumia lugha za kikabila badala ya Kiswahili.

Alisema baadhi ya matukio hayo ymashawasilishwa katika kamati za maadili ya uchaguzi ngazi ya jimbo kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ambapo yatajadiliwa na kutolewa maamuzi.

Aliongeza kuwa tume hiyo inategemea kuwa wale wote wanaoshiriki katika uchaguzi huo, na kata 22 katika halimashauri mbalimbali nchini ,wataendelea kuendesha kampeni zao kwa kuzingatia sheria za uchaguzi, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya tume iliyotoa.

Tume hiyo pia imesema kuwa matukio ya awali ya kumwagiwa tindikali, kudhalilishwa kwa Mkuu wa Wilaya na kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga yaliwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi huo na aliyawasilisha kwenye kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, ambapo maamuzi yalitolewa na kamati hiyo kuwa masuala hayo yalishafika mahakamani, hivyo mahakama iachiwe iendelee kuyashughulikia .

My take:
Kwanini tume inakuwa na mwenyekiti wa muda wakati ilifahamika wazi kuwa Jaji Lewis Makame anastaafu?

Kwa nini uteuzi wa mwenyekiti mpya wa kudumu usifanyike?
Je kuwepo na mwenyekiti wa muda ni kwa ajili ya:-

  1. Kusubiri mchakato wa katiba ukamilike na kuweka wazi jinsi ya kumpata mwenyekiti wa Tume iliyo huru?
  2. Mkakati wa CCM wa kutoa muda kwa Usalama wa Taifa kumfayia huyu mtu wa REDET (Prof Amon Chaligha) Veting ya kuona kama ni mtu wa CCM na yupo Tayari kupindisha matakwa ya wananchi kwa kumtangaza mshindi atakayewekwa na vyombo vya dola?
  3. Wanafanya utafiti wa kupata mtu wa CCM ambaye hataonekana kuwa ni CCM ila kufanya kazi kwa masilahi ya CCM?
kwa isifanyike kama ilivyokuwa kwa jaji mkuu Jaji mkuu, mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa JWTZ et al?

Mtu anateuliwa kabla ya muda wa aliyetangulia kumalizika ili akiondoka tu mteule anachukua nafasi? Haya mambo ya mwenyekiti wa muda yanamnyima huyu mtu kuonesha uwezo wake wa kusimamia haki akihofia kuwa muda wowote anaweza kuondolewa akionekana hayupo kwa masilahi ya CCM.

Ni hatari sana kuwa na watendaji kwenye mazingira kama haya.
 
Mkuu huyo Prof. mwenyewe amechoka then anaonekana kaa gamba vile.. yale yale! mwenye CV ya hicho kibabu atuwekee maana nae kama kesho anastaafu vile.... Nchi inaendeshwa kisikaji kishikaji sana.
 
kwanza ni zezeta sana hata akikemea wajukuu zake ndo kwanza watamvuta nisharubu yake ile..hakuna alichoongea
 
Ccm angalieni msijechakachua matokeo ya Igunga,msituletee vita Kama mnakufa basi kufeni kimya kimya.
 
Back
Top Bottom