Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Mwandishi wa gazeti la Mtanzania, Arodia Peter, ambaye amesafirishwa na kulipiwa na CCM Igunga, ametimuliwa na kutishwa na vijana wa ulinzi wa CCM katika mkutano wa chama hicho ulokua unahutumiwa na John Magufuli mjini Igunga, tofauti na ule wa Mkapa vijijini.
Mbali ya kumtimua mwandishi huyo vijana hao wamemtishia na taarifa kutolewa polisi RB GU\RB/1731/2011, Kimsingi wamesema wakimuona watamvunja.
Hiyo si mara ya kwanza kwa mwandishi huyo kupata kibano toka CCM na mwanzo ikiwa ni kuzuiwa kuingia wala kusogea ktk hoteli walipo CCM ya Peak.
Inaelezwa sababu kubwa ya mwandishi huyo kupewa kibano na CCM ni habari zake za msimamo ikiwamo kukamatwa ka viongozi wa CCM kwa kuvamia na kushusha bendera ya Chadema kabla ya kutaka kupigwa na wananchi.
Habari nyingine iliyowakera ni ile ya kusema ahadi za Magufuli ktk uchaguzi ni za kisanii ikiwamo ile ya Busanda. Na habari ya tatu ni ile iliyoelezea CCM kuteka wana chadema watatu.
Matukio yote hayo yalikemewa na viongozi wa CCM na polisi akiwamo Kamanda Mungulu na watu wa kitengo cha habari wa CCM, Daniel Chongolo na Gabriel Athumani na CEO wa New Habari, Hussein Bashe.