Igunga: Mwananchi amuomba Rais Magufuli ‘kuachia pesa’ mtaani, Rais ajibu hakuna vya bure zaidi ya kuchapa kazi

Jibu la Rais Magufuli kwa mkazi wa Igunga aliyemtaka kuachia pesa mtaani linaonyesha kuwa Rais hujui ni kiasi gani wananchi wanataabika kwa kukosa pesa maana pesa ndio kila kitu. Chakula, mavazi, malazi, matibabu, elimu yote yanahitaji pesa.

Sasa kutoa majibu mepesi kuwa fanyeni kazi, mbona watu wanafanya kazi siku zote na hakuna mtu anayelisha familia ya mtu yeyote yule. Huu ni uungwana kweli?
 
Magufuli anze kulipa madeni ya ndani ya wakandarasi na suppliers ili pesa izinguke. Serikali imeshikilia pesa nyingi sana za wafanyabiashara wa ndani kupitia madeni.
Japo ametoa jibu lakini na uhakika hii issue itamganda kichwani hizi wiki chache.
 
Inasikitisha sana tunaona watu mtaani wanakosa chakula, wanafariki kwa kushindwa kulipia matibabu halafu mtu anajibu kirahisi namna hiyo.
 
Alipe watumishi fedha wanazo dai waone,nyingi zitaingia kwenye mzunguko,pamoja na madeni ya ndani
 
IMG_20191126_150223.jpg

Mbona yeye anaenda kukopa si afanye kazi?
 
Kuzurura kule yeye anaona anafanya kazi, fikria mtumishi ambae anajituma kazini hakuna nyongeza yoyote ndani ya miaka minne, atafanya nini tena ili apate pesa.
 
The Sheriff, Nilishasema hapa huyu jamaa siyo mwanasiasa kabisa na ukienda na kiki za kisiasa kwakwe mtapishana mapema tu na atakuumbua huyu Ni mtendaji, Mchapa kazi.. Anaeamni Katika kufanya kazi kuliko kitu kingine.
Guys let us work hard!! Ushauri Mzuri Sana wa Rais kwa watu wake.
 
Ngoja bei ya kupanda kwa chakula inoge serikari itaomba poo tu baadae.

Watch this space
 
Nilishasema hapa huyu jamaa siyo mwanasiasa kabisa na ukienda na kiki za kisiasa kwakwe mtapishana mapema tu na atakuumbua huyu Ni mtendaji, Mchapa kazi.. Anaeamni Katika kufanya kazi kuliko kitu kingine.
Guys let us work hard!! Ushauri Mzuri Sana wa Rais kwa watu wake.
Inaonekana Tanzania watu ni wavivu sana,kuna kazi ila hawataki kufanya.
 
Nilishasema hapa huyu jamaa siyo mwanasiasa kabisa na ukienda na kiki za kisiasa kwakwe mtapishana mapema tu na atakuumbua huyu Ni mtendaji, Mchapa kazi.. Anaeamni Katika kufanya kazi kuliko kitu kingine.
Guys let us work hard!! Ushauri Mzuri Sana wa Rais kwa watu wake.
Hivi mnalisha familia ya nani asiyefanya kazi.
 
Nani amemwambia wananchi wanataka pesa za bure? Awe anaelewa maswali, hata hivyo wamempanga muuliza swali lakini kashindwa kujibu swali, sasa akikung'utwa swali la kushtukiza sijui itakuwaje?
 
Ameshindwa kumjibu aliona aibu sasa watu wataanza kumwambia ukweli na inawezekana hapo mbele atakuwa asimami simami tena
 
Kulikuwa na hoja 2 , kuachia fedha na kutawala milele , umemsikia akizungumza kitu kuhusu kutawala milele ?
Mbona ameshazungumza mara nyingi tu kuhusu kutawala milele, hukuwahi kumsikia? Kashasema kwa kurudia rudia sana kuwa muda wake ukiisha atampisha mwingine. Yeye siyo Rais wa Maisha.

Ila pia sioni tatizo, kama wanaompenda watataka aendelee sawa tu. Viongozi kama Magufuli na Mbowe ni nadra sana kuwapata zama hizi, hivyo tuwaache tu waendelee kutuvusha. Au siyo?
 
Back
Top Bottom