Igunga: Mwananchi amuomba Rais Magufuli ‘kuachia pesa’ mtaani, Rais ajibu hakuna vya bure zaidi ya kuchapa kazi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
205
500
Tangu Rais Magufuli aingie madarakani kumekuwa na malalamiko ya chinichini miongoni mwa Watanzania kuhusu hali ya kiuchumi kuwa ngumu. Ugumu huo ulizaa msemo ‘’vyuma vimekaza’’, jambo lililokemewa vikali na Mheshimiwa wa ngazi za juu.

Sasa basi, kufuatia hali ya kiuchumi kuendelea kuwa ngumu, mwananchi mmoja huko wilayani Igunga Mkoani Tabora, kwa nafasi adimu na adhimu aliyoipata ya kumweleza jambo Rais, amewasilisha malalamiko ya wengi.

“Maisha ni magumu fedha hakuna watu wana hali mbaya; akina mama wananyang’anywa televisheni, friji kwa ajili ya mikopo. Tunaomba mheshimiwa tuachie fedha mengine yote hatuna tatizo na wewe,” amesema mjasiriamali huyo.

Baada ya kutoa majibu ya matatizo mengine yanayowakumba wanaIgunga, Rais akajibu:

“Usipofanya kazi hela zitaisha tu. Ukitaka hela fanya kazi. Wapo wanaolima mpunga sasa hivi na baada ya miezi kadhaa watapata hela. Sasa wewe unakaa hapa kijiweni kila siku unalalamika kuhusu hela.”

“…cha bure hakipo, hata mimi sina. Kinachotakiwa ni kuchapa kazi, na hata maandiko yanasema hivyo. Asiyefanya kazi na asile.”

“…umeme umefungwa hapa. Waliokuwa wanachimba mashimo si walikuwa wanalipwa hela? Lakini kuna waliokuwa wamekaa wanatazama tu. Wapo wanaochimba mitaro ya barabara, wapo wanaolima pamba...”

“…kalime hata viazi au matikiti maji, ukisimama hapa yataliwa tu hata mpaka Dar es salaam. Lakini kiukweli vya bure vimeisha na bado vitaisha zaidi...”

“…nenda hata kwenye machimbo. We unataka mkono wako uwe soft alafu unataka hela – haipo!”

“…kwahiyo ndugu zangu, mimi sijaja kuleta hela, nimekuja kuhimiza kufanya kazi...”

“…serikali inatafuta fedha kwa ajili ya huduma muhimu za jamii na si kwa ajili ya kukulisha wewe na mke wako...”Rais yupo njiani kuelekea Shinyanga
 

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,461
2,000
Huyu muuliza swali amepangwa vizuri kuuliza swali.... Angalia hilo eneo alilotoka walinzi walikuwa makini nae
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,557
2,000
Jamaa kalalamikia money circulation kua ndogo, sababu ya money circulation kua ndogo ni ukosefu matumizi makubwa ya serikali. Matumizi makubwa ya serikali yaliyopo hayana matokeo chanya kwa sasa kwenye uchumi wetu kwa sababu pesa karibu zote zinaenda nje, manunuzi ya ndege pesa imeenda Marekani na Ulaya, reli pesa inaenda Uturuki, Rufiji pesa inaenda Misri, barabara hvyo hvyo wanachukua Kenoike ya Japan, Wachina na Wahindi, Kinyerezi pesa iko Japan, Daraja la Ubungo pesa watachukua Wachina, Daraja la Salenda itaenda Korea nk.

Ndio maana huoni pesa kwenye mzunguko kwa sababu inaenda nje ya nchi, inayobaki hapa ni kidogo sana pamoja na kua matumizi ya serikali ni makubwa. Ukosefu wa mzunguko mkubwa wa pesa unasababisha kupunguza uwezo wa watu kujipatia mahitaji muhimu kutokana na kukosa kazi na mambo kama hayo.

Hali bado itaendelea kua mbaya.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,842
2,000
KAULI YA MTANZANIA ABEL MPINGA KUTOKA IGUNGA TABORA KWAKE RAIS JPM lilikuwa…

" Maisha ni magumu fedha hakuna watu wana hali mbaya akina mama wananyang’anywa televisheni, friji kwa ajili ya mikopo. Tunaomba mheshimiwa tuachie fedha mengine yote hatuna tatizo na wewe “

JIBU MUBASHARA LA RAIS JPM KWAKE MTANZANIA ABEL MPINGA lilikuwa….

“ Hata Ulaya wanafanya kazi, wanalala kwenye mashimo, mimi nimeenda Ulaya wapo wenye shida kuliko huku kwahiyo ukitaka hela fanya kazi na naamini Watu wa Tabora mnafanya kazi hata yule (aliyesema hela ziachiwe Mtaani) nae naamini anafanya kazi ”

” Serikali inatafuta hela kwa ajili ya kujenga Barabara, kununua dawa na mengine, Serikali haitafuti hela ili kukulipa wewe na Mke wako bila kufanya kazi ”Nami GENTAMYCINE namalizia kwa kusema Ewe Mwenyezi Mungu tusaidie.
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,258
2,000
Muuliza swali ameuliza kwa ufupi sana. Rais amejibu bila ya kuelewa swali. Muuliza swali haombi hela bali anaomba sera na mipango inayoweza kusababisha uwepo wa mzunguko mzuri wa hela.

Kama hakuna mzunguko mzuri wa fedha, utalima matikiti, hakuna wa kununua. Utafungua genge la kongoro, hakuna wa kunywa supu. Utajifunza ufundi ujenzi, hakuna anayejenga nyumba.

Shida kubwa ni kwamba tuna miradi mikubwa ya kutoa hela ya ndani kupeleka nje. Hatuna miradi mikubwa ya kutoa fedha nje kuleta ndani au ya kupunguza utoaji wa fedha kwenda nje.
 
Top Bottom