Igunga: Mfuasi wa CUF kavamiwa na wafuasi wa CCM kapewa kipigo yupo hoi Hospitali

Mfuasi mmoja wa chama cha siasa( CUF), kavamiwa na vijana waliotambulika ni wa CCM na kumpa kipigo mpaka akapoteza fahamu.

Mfuasi huyo wa CUF alikutwa akipandisha bendera ya chama cha CUF nyumbani kwake, vijana wa CCM walimvamia na kumpa kipigo majeruhi huyo kalazwa hospitali, inasemekana kavunjika mbavu.

SOURCE: TBC HABARI
 
TBC 1 wameelezea kuwa msafara wa Shigela kiongozi wa UVCCM wamemshambulia kiongozi Wa Kata CUF huko Igunga kwa kupandiSha bendera na yuko hospitali ila kanyimWa matibabu. Jee ndoa ya CCM na CUF imevunjika au huu ni ugomvi wa ndani ya familia?
 
Hatimaye ccm wametembeza kichapo kwa wenzao wa cuf. Aliyebahatika kupata kichapo hiko ni katibu wa kata cuf aliyekuwa akipandisha bendera ya chama chake ndipo vijana wa ccm waliokuwa kwenye msafara wa shigela walipomsalimia kwa kichapo cha nguvu kilichomfanya alazwe hospitali.Hata hivyo polisi inamshikilia mtu mmoja kwa tukio hilo
 
umesikia vibaya. Mimi nimesikia chadema wamempiga cuf?

Hii culture ya kutumia mabavu kila mahali huku kwetu itatuondoka lini? Ni lini tuliacha ile desturi ya kiTanzania ya kujadiliana na kuheshimiana na tukaingia kwenye mambo ya kutishiana na kupigana ngumi? Ni lini ustaarabu utaturudia tuelewe kuwa waliotutangulia waliweza kuishi kwa amani hata kama hawakukubaliana kwenye mambo mengi ya msingi? Siku hizi kwetu kumekuwa kama msituni ambapo kama hukubaliani na la mwenzako unataka umwondoe kwa mabavu. Halafu ubaya wake ni kwamba ubabe mwingi unaongozwa na vijana wetu (taifa letu la kesho) na sisi tunakaa kimya na kuangalia tu kwa sababu ubabe huo unatusaidia sisi. Let’s get back to civilization, we can disagree on a lot of things but still respect each other enough to live side by side.
 
umesikia vibaya. Mimi nimesikia chadema wamempiga cuf?

Mkuu naona umeanza tena ile tabia yako ya umagamba,siku chache zilizopita ulikuja na post zenye matumaini hapa JF tukadhani akili zako zimepigwa flash!! sasa leo umekuja na uharo hapa...ACHA KUDANGANYA UMMA,HABARI INASEMA SHIGELA NA WATU WAKE NDIO WAMEMFANYIA VURUGU KIONGOZI WA CUF,na huyu Shigela kupitia TBC1 NEWS BULLETIN ameojiwa na kutoa kauli kuwa si yeye wala timu yake wanaohusika na tukio hilo...sasa unapokuja na siasa majitaka na uharo hapa hatukuelewi kabisa mkuu,kajipange vizuri nadhani una matatizo ya ugonjwa wa uzushi...
 
ni mwenyekiti wa mtaa fulani alikutwa anapandisha bendera ya cuf nyumbani kwake..
 
Shigella alitembelea kambi ya uvccm ulemo Singida ndo matunda ya kambi yameanza, japokuwa amekana pia madaktari wameonyeshwa toka jana mtu hajatibiwa hadi leo Mtatiro ndo alikuwa anahoji kwa huyo mtu hakupatiwa tiba?
 
kwani wewe una masikio mangapi?

Mkuu msamehe bure ana masikio mawili isipokuwa ana malaria sugu ambayo imeathiri ubongo wake na kwa hiyo mambo yafuatayo yametokea kwake...
  1. Uwezo wa kusikia umepungua,na kwahiyo asikii la mtu zaidi ya Magamba tu...
  2. Uwezo wa kufikiri ndio usiseme maana ubongo umepata serious demage...hawezi kufikiri kabisa..
  3. Uwezo wa kuona umepungua,anaona rangi za kijani na haoni umaskini wa watanzania...
  4. Uwezo wake wa kuhisi ndio kabisa maana anahisi kama kalewa...
Tumsamehe bure....
 
CCM wameanza kuwachokoza CUF, Mtu anapigwa sababu tu kapandisha bendera ya CUF nyumbani kwake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom