Sasa ndugu zangu CCM huyu mbunge anaongeza kura za CCM au anapunguza?jiulize anawambia hivyo watu wa uelewa gani...!kwa akili zangu ndogo tena sie watu wa vijijini tunajiju, mtu akisema kitu fulani kikitokea atafanya hv, kwa desturi zetu sie wenye uelewa mdogo ndio tunafanya hivyo ili tuone atakunywa sumu kweli au..???CCM inahitaji watu makini kwa mwendo huu haaa sijuiiKAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.
"Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu," alisema
Source:Tanzania daima.