Elections 2010 Igunga: Mbunge Esther Bulaya [CCM] awaomba radhi polisi

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wakuu,
Mbunge wa ccm Estha Bulaya amewaangukia polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa aliwatukana askari wa jeshi hilo, siku ya tukio la kurushiana risasi lililohusisha vyama vya ccm na Chadema. Hayo yalisemwa jana na mkuu wa kitengo cha Tathamini na ufuataliaji wa jeshi hilo Ndugu Isaya Mngulu.
Gazeti la Nipashe, linapasha zaidi kuwa, Mngulu hakutaja matusi hayo, lakini alisema, siku moja baada ya tukio hilo mbunge huyo alienda ktk kituo hicho cha polisi na kuwaomba radhi.

My take,
Huyu Mh Mbunge wa ccm, amejutia makosa yake au ameagizwa kufunika kikombe ili mwanaharamu apite oct 2, 2011?
 
Chadema thubutu kumtukana hata house boy wa private wa polisi kama hujasota lumende mpaka uchaguzi uishe. Si mnakumbuka jinsi yule mwizi wa UDA alivyomkata mtama OCD akaenda kuwekwa ndani Shibuda eti yeye ndie aliyemuudhi Kisena mpaka kwa hasira akaenda kumpiga mtama OCD! Kweli magamba ni Nouma!
 
Ngoja niende kituo cha polisi nikatukane halafu tarehe 4.10 nitawaomba msamaha...
 
Wakuu,
Mbunge wa ccm Estha Bulaya amewaangukia polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa aliwatukana askari wa jeshi hilo, siku ya tukio la kurushiana risasi lililohusisha vyama vya ccm na Chadema. Hayo yalisemwa jana na mkuu wa kitengo cha Tathamini na ufuataliaji wa jeshi hilo Ndugu Isaya Mngulu.
Gazeti la Nipashe, linapasha zaidi kuwa, Mngulu hakutaja matusi hayo, lakini alisema, siku moja baada ya tukio hilo mbunge huyo alienda ktk kituo hicho cha polisi na kuwaomba radhi.

My take,
Huyu Mh Mbunge wa ccm, amejutia makosa yake au ameagizwa kufunika kikombe ili mwanaharamu apite oct 2, 2011?

CCM wanaomba radhi wanaachiwa huru,CDM wao wanakaa ndani...haya bwana!!
 
Lazima tukiri kuwa kamanda Mwema uwezo wake umefika mwisho, anatakiwa apatikane mwingine mwenye mawazo mapya
Tunaangalia kwanza ushemeji wake na JK, hayo ya uwezo wake si muhimu hata kidogo kwa Tanzania.
 
Samahani mkuu kile kitendo kilikuwa ni cha wana CCM kurusha risasi au ni kurushiana risasi....? mkuu usuwapunguzie ukali wa mameno hao wana magamba
 
Lazima tukiri kuwa kamanda Mwema uwezo wake umefika mwisho, anatakiwa apatikane mwingine mwenye mawazo mapya
Ukitembelea nyumbani kwa mtu halafu ukakuta watoto wake wana tabia mbovu za kila aina basi ujue wazi kuwa hata mzazi au wazazi wao wako hivyohivyo. Upuuzi wa Said Mwema na wengine wote waliokabidhiwa vitengo mbalimbali hapa nchini ni direct reflection ya huyo Vasco aliyewachagua. Huwezi kuwa makini halafu ukateua watu wa hovyo kufanya kazi, ni lazima na wewe uwe hovyo zaidi.
 
Ngoja niende kituo cha polisi nikatukane halafu tarehe 4.10 nitawaomba msamaha...

Taratibu mkuu,
Uchunguzi wa kesi yako utachukua miezi 6 huku unakaa lupango, Ila kwa ccm unaenda kwa muda wako na hufanywi kitu. Terrible.
 
Hivi ukiwaangukia polisi kesi ya jinai inakwisha?Mi sijawahi kuona upuuzi kama huu,uwa nashindwa sana kuwaelewa polisi na UCCM wao,mishahara kiduchu,maisha ya mabatini lakini wao ndio wanajifanya CCM damu.Angekuwa ni mbunge wa CHADEMA hakuna cha kuwaangukia wala nini angepelekwa Mahakamani Tabora kwa escort ya kutisha
 
Double standard, hii nchi haitabilriki bwana kila kukicha mambo yanabadilika, katukane wewe polisi kama hujaozea segerea, chezea geshi wewe!!!!!!!!
 
Lazima tukiri kuwa kamanda Mwema uwezo wake umefika mwisho, anatakiwa apatikane mwingine mwenye mawazo mapya

Kwa kiasi fulani ni kweli ameanza kuchoka ila kwa TANZANIA polisi inatumika kama kiranja wa CCM kwa maslahi ya CCM
 
Bulaya anawakilisha tu kwa uchache kiburi cha viongozi wa CCM. Kwao polisi si kitu kwani wanajiona wako juu za sheria nchi. Tungependa kujua msimamo wa polisi kabla na baada ya kuombwa msamaha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom