IGUNGA: Kielelezo cha ukomavu wa siasa ya Tanzania.

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
Ndugu zangu wanajamiiforum wenzangu haswa wa Jukwaa hili pendwa la siasa nawasalimu!
Mtakubaliana nami kwamba tangu ndugu Rostam Azizi alipojihudhuru Ubunge wa Jimbo la Igunga mengi yameandikwa na kujadiliwa sana, sio tu hapa jamvini bali hata katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kama vile BBC, VOA, RFI, Dutch wele etc, Na mengi yataendelea kuandikwa na kuzungumza ktk vyombo hivi haswa katika kipindi hiki cha kampeni ya uchaguzi.

TATHIMINI YANGU: Kulingana na maandalizi yafanyayo na vyama husika vishiriki vya siasa katika Uchaguzi yani CCM, CHADEMA, na CUF ikiwamo matumizi ya helikopta, Makada wake mashuhuri ambapo Mh. Rais mstaafu Benjamin Mkapa atakuwepo katika uzinduzi wa chama chake cha CCM, Prof. Lipumba na Maalim Seif Sharifu Hamad kwa upande wa CUF, na Dr. Slaa, Mbowe, Tundu Lissu na Zito kabwe kwa CHADEMA inatupa picha nikwakiasi gani uchaguzi huu utakavyokuwa na ushindani mkubwa. Na nadhani ni uchaguzi utakaotupa picha shughuri ya 2015 itakuwaje.. So uchaguzi huu ni muhimu kwa vyama vyote vya siasa pia kwa watanzania wote wapenda maendeleo ya nchi yetu!

KUHUSU NEC: Ni mategemeo yetu wengi kuwa Tume ya Uchaguzi itakuwa makini this time kuhakikisha kuwa haki inatendeka kwa kufanya Uchaguzi ulio huru na wenye kufuata kanunu za kidemokrasia, sitegemei kusikia zile lawama ambazo tumekuwa tukizisikia katika chaguzi zilizopita kwani nategemea maandalizi ni mazuri.

Mwisho napenda kufungua mjadala kwa wote ambao kwa pamoja mwakubaliana nami juu ya umuhimu wa uchaguzi huu kutoa maoni na tathimini zenu, expectation zenu na ushauri kwa vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi mdogo huu. Kwa wale wenye mawazo ama mtazamo tofauti pia wanaruhusiwa na wapo huru kuchangia!
 
Back
Top Bottom