Igunga: Kashindye wa CHADEMA afunika kijiji cha Matinje

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Kiwanga+na+Kasulumbai.JPG


MAANDAMANO YA KUMSIKIKIZA KASHINDYE KWENYE GARI LAKE WAKIWEMO KAMANDA SUSAN
KIWANGA NA KAMANDA KASAMBALYA. HAWA NI WANAKIJIJI WENYEWE NA SIYO WAKULETWA NA
MALORI KUTOKA MBALI.
 
Makamanda wana kamua kwa kwenda mbele, kweli inatia moyo. Ukiangalia maisha na mazingira ya hawa watu yanitia huruma sana wanahitaji kiongozi wa kweli sio msanii. Nawatakia kila la kheri CDM Igunga
 
Picha hii inatoa taswira tofauti na picha za mikutano ya hadhara ya CCM iliyojaa watoto wanaoshangaashangaa kinachotokea. Hawa ni watu wazima, wapiga kura na wanaofahamu wanachokifanya.
 
Cheki walivyochoka na ugumu wa maisha, angalia hata wanavyovaa, wanatia huruma. Wamekuwa chini ya unyonyaji wa RA kwa miaka 16 jamani, wanahitaji mkombozi na wanafurahi wamemwona mkombozi wao CDM amekuja. Hata kwenye maandiko matakatifu, kuna kisa cha mwanamke aliyetokwa na damu kwa muda mrefu na siku alipoambiwa Yesu anakuja akajikongoja kwenda kumgusa. Mimi nawafananisha hawa watu na kisa kile.

Ukiwaona wazee wameibukia CDM ujue wanamagamba kwishnei
 
Wanatia huruma, wamechoka na ugumu wa maisha. Wanahitaji mbunge anayeyajua matatizo yao.
 
yaani huyo Dr Kafumu nadhani anajuta kwanini alikubali kusimama kugombea huo ubunge....
 
Naomba muusamehe ujinga wangu!

Hivi hilo jimbo ni Igunga mjini au vijijini; au ni la mjini likichukua na baadhi ya vijiji? Siku zote mimi nafikiri RA alikuwa ni mbunge wa lgunga mjini!

Samahani tena!
 
Kiwanga+na+Kasulumbai.JPG


MAANDAMANO YA KUMSIKIKIZA KASHINDYE KWENYE GARI LAKE WAKIWEMO KAMANDA SUSAN
KIWANGA NA KAMANDA KASAMBALYA. HAWA NI WANAKIJIJI WENYEWE NA SIYO WAKULETWA NA
MALORI KUTOKA MBALI.
Kwa hapa mnatishia usalama ndiyo maana wanatumia mbinu mbadala za kijinga kwa kweli MWL. kaza butiiiii keleweke tu
Kwa
 
Picha hizi kwa nini zisikuzwe zikabandikwa kila kijiji zisaidie kampeni kwenye vijiji ambavyo bado havijailewa chadema na kashinde? Mimi naona watu ambao hawamkubali kashinde wakiona hizi picha vijijini kwao watabadili mwelekeo.
 
Naomba muusamehe ujinga wangu!

Hivi hilo jimbo ni Igunga mjini au vijijini; au ni la mjini likichukua na baadhi ya vijiji? Siku zote mimi nafikiri RA alikuwa ni mbunge wa lgunga mjini!

Samahani tena!

Igunga ni kubwa ina igunga mjini na vijiji vyake 98, kata 26 na tarafa 3.
 
Igunga ni kubwa ina igunga mjini na vijiji vyake 98, kata 26 na tarafa 3.

Good knowledge, hebu tupatie na hali ya upepo eg kule Sakamaliwa, Kininginila, Ibutamisuzi, Mwanyagula, Mwabakima, Bukama, Mwamashimba, Hindishi etc hali ikoje mkubwa wangu
 
Mungu awasaidie wafanye uchaguzi ulio bora, kwani mbele zake kila kitu ni uchaguzi, ametupa uwezo wa kujua mema na mabaya, so its my prayers that they will be enlighted and know what they have to choose.
 
yaani huyo Dr Kafumu nadhani anajuta kwanini alikubali kusimama kugombea huo ubunge....

Kiukweli Dr Kafumu ni mtu safi. Ni bahati mbaya kuwa amekuwa victim of circumstances that are not of his own making. Wakati mwingine, sehemu ingine, angeweza kushinda, lakini siyo hapa wala wakati huu. Bila kukejeli, anastahili pole.
 
Ebwanaee!!!! hii inatisha hapo kumbuka kuna watu hawana uwezo wa kufika hapo na kwasababu CHADEMA haibebi watu kwa maroli imekuwa ni nafuu maana ingeweza kuitwa inavuruga amani Igunga
 
duh, si dhani kama RA aliwahi tembelea kijiji hicho? saa ya ukombizi na sasa
 
Back
Top Bottom