Igunga: CHADEMA yaibwaga CCM Kesi za Uchaguzi

FROWIN

JF-Expert Member
Jul 25, 2012
213
84
chadema.png
MAHAKAMA ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora juzi ilitupilia mbali kesi tano zilizokuwa zimefunguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka jana.



Kesi hizo zilifunguliwa na CCM katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga Aprili, mwaka huu, ambapo chama hicho kilikuwa kikipinga ushindi walioupata wenyeviti watano wa Serikali za Mtaa, ukiwemo wa Stoo, Kamando, Mwayunge, Nkokoto na Kijiji cha Simbo wilayani humo.


Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Leonadi Nkola, alisema madai yalitengenezwa na mtayarishaji mmoja, hivyo kila neno na sentesi zilifanana na tofauti yake ni katika majina na katika makosa yaliyofanywa baada ya uchaguzi, mawakala wao waliweza kusaini na kukubaliana na matokeo kwa msimamizi mkuu wa Uchaguzi wa Wilaya na kwenda kinyume cha sheria.


Aidha Hakimu Nkolo alibainisha kuwa katika madai yao pia hawakuweza kuonyesha barua yoyote ambayo walimwandikia msimamizi wa uchaguzi wa wilaya inayopinga matokeo ya ushindi.


Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Nkola alisema katika hati hiyo ya madai iliyoandaliwa haikuweza kutoa nukuu ya kifungu cha sheria kinachothibitisha ukiukwaji wa uchaguzi huru na haki kwa kuvunja sheria na kanuni za uchaguzi na kufanya madai yao kutokuwa ya msingi na sheria.


Kutokana na kukosekana uthibitisho wa madai hayo, Mahakama ilitupilia mbali madai hayo na kusema kuwa hao ni viongozi haramu wa Serikali za Mitaa.

chadema.png
 
Kitaleweka tu mwaka huu, mahakimu na majaji wameshasoma upepo unakoelekea, CDM hongereni watumikieni wananchi..
 
CCM.wanajaribu kuliziba jua kwa viganja vya mikono........CDM ni kusudio maalumu toka kwa Mungu,hongereni CDM......CCM wasubiri kimbunga hapo October na waandae wanasheria wa kutosha kufungua kesi kila kona.
 
Pole sn CCM,ila ifike mahala mjitambue na mjue kwamba muda wenu wa kuwa madarakani ndo unaelekea ukingoni,ni aibu mnajiita wana demokrasia ilihali sivyo.siku yenu ipo
 
chadema mnaipatia sana ccm....ukawa tutawabonda tu mifisadi...wooteee wezi hata huyo jaji ni mwizi tu........ili mradi karudi katika kundi la wezi sisi tutamuita mwizi tu.......badala ya kukaa kwake ale pension anaonyesha tamaa huyu......fisadi.

Anahitaji kukalia kiti ndani ya ikulu.
 
Wataelewa tu mwaka huu, Mungu humpa mtu haki yake hata kama ni mnyonge kiasi gani, haya huko anapkopita pita Kinana na baby ake Nape nawaomba muulizeni nape zile takwimu zake za ushindi azi edit halafu atoe mrejesho kabla ya october na ndio aongelee mengine. Mrejesho ni lazima.
 
Si uwa tunaambiwa na Dr.Slaa mahakama ni ya mali CCM kuliko tena leo Chadema washinde kesi kwenye mahakama za CCM.
 
Kwanini huyo hakimu hakuwaamuru ma-CCM kulipa gharama zote za kesi na usumbufu ili liwe fundisho kwa hawa ma-CCM kufungua kesi ziszo na kichwa wala miguu!
 
mungu endelea ku tenda muujiza ili ccm itoke madarakani mwaka huu mungu tusaidie ccm wagombane ktk uchaguzi huu kama wale wajenzi wa mnara wa baberi walivyo pishana lugha ndivyo ccm itokee mwaka huu
 
Duu ccm kwa wizi,ku foji hatari.mpaka hakimu kashtuka kuwa kesi zote 5 ni za kutunga
 
Si uwa tunaambiwa na Dr.Slaa mahakama ni ya mali CCM kuliko tena leo Chadema washinde kesi kwenye mahakama za CCM.
Kwa vyovyote vile watakuwa wameanza kujitambua. Wanaona hambebeki tena mkuu Ritz, jiandaeni kisaikolojia
 
Back
Top Bottom