Igunga: Chadema wataka mgombea wa CCM aenguliwe

joseeY

Senior Member
Nov 4, 2010
108
17
Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa Chadema, Tundu Lissu, alisema jana kuwa tayari Chadema kimemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kulalamikia kitendo cha Mbunge wa Tabora mjini, Ismail Aden Rage, kutembea na bastola waziwazi hadharani.Kutokana na kitendo hicho, Chadema kimemwomba mwenyekiti wa kamati hiyo ya maadili kukiomba mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu, aondolewe kwenye kampeni kutokana na ukiukwaji huo wa maadili.

Lissu alisema Ibara ya 2(2) ya Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho Septemba 20, mwaka huu inakataza kubeba silaha yoyote inayoweza kudhuru mtu yeyote katika mikutano ya kampeni.Alilitaka Jeshi la polisi kumkamata Rage na wabunge waliofyatua risasi na kuwaweka rumande akisema kama hilo litafanyika ataamini jeshi hilo linatenda haki kwa usawa na bila upendeleo.
 
Hizo ni habari za kweli hiyo tume,polisi,takukuru na usalama wa taifa vyote ni vya sisiyem wanaweza kumkwaza boss wao?
kwani hao si ni vibaraka tuu hawana ubavu wa kumuwengua huyo kafyumu.
mfano mzuri ni kushindwa hata kumhoji tuu huyo rage hadi waziri anawaambia wamhoji na hiyo pia bado ni danganya toto.
ila polisi waangalie kwa jicho la pili kwani wasipotenda haki kwa lolote litakalotokea hizo DAMU zitawalilia hao vibaraka wa sisiyem.
 
Ushindi wa mezani ni aibu wanaume pambaneni hakuna mkate wa bure kwenye karne hii ya sayansi na teknolojis
 
Waislamu tunao maslahi gani katika wagombea wote makafir Igunga kiasi cha kufanya BAKWATA kutudhalilisha kila siku na mitamko yasiyokua na mashiko huko?
 
Waislamu tunao maslahi gani katika wagombea wote makafir Igunga kiasi cha kufanya BAKWATA kutudhalilisha kila siku na mitamko yasiyokua na mashiko huko?

Very stupid argument! Kwani, kwa mfano, wagombea wote wangekuwa waislamu ndio mngekuwa na maslahi gani ambayo kwa sasa mnayakosa au hayapo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom