IGP wewe ni mzoefu katika hiki chombo sasa ni wakati wa kutumia weledi japo kuna shinikizo kubwa

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Habari IGP Sirro.

Matumaini yangu nikuwa huwa naamini katika utendaji wako uko makini!

Na mbaya zaidi hiki chombo cha Polisi unakielewa vizuri sana kwa kuzingatia wewe umepitia ngazi mbali mbali katika jeshi hili!,Umekuwa ukifanya kazi kwa weledi sana. Mimi nitoe Rai kwako hasa katika kipindi hiki kigumu kwako kwakuwa ni uchaguzi mkuu wa kwanza ukiwa kama IGP kwamaana sasa lawama zote utatwishwa wewe!

Hapa unatakiwa kutumia sayansi kutenda kazi yako katika Jeshi la Polisi ili unapostaafu unaacha alama na tukikutana uswahilini tunajumuika pamoja kama zamani tulivyokuwa tukijumuika maeneo yetu kama Tegeta,Bunju na kwingineko!.

Wanasiasa huwa wanatabia ya kufitinisha watu hivyo nikuombe hepuka kufitinishwa japo unaweza kupokea amri ipokee lakini hapo tumia sayansi ya kijeshi ku neutrize makali ya amri kulinda amani kunaanzia kwako IGP kwa sasa tupo kwenye mtego mkubwa jilinde ustaafu vizuri nchi za magharibi zinakuangalia wewe!.

Hivi vitendo vya kushambulia wagombea wa urais sidhani kama vina tija wambie makamanda wamikoa hata kama wamepewa amri na RC,RSO,Waziri,waepuke kutumia nguvu kwa sababu wagombea wote wapo katika category moja !.

Mimi mzee wangu IGP nakuomba tumia ile sayansi yako yakupoza mihemuko katika jeshi.
 
Hana na narudia hana uwezo wa kuzuia lolote linalofanywa na ccm yaani hana mamlaka, yeye kama yeye ila kauli anayoitoa inatokana na maelekezo kutoka kwa bosi wake ambaye ni ccm.

kumbuka bila katiba mpya hakuna kiongozi yeyote ndani ya serikali iliyo chini ya ccm anaweza kwenda kinyume na matakwa ya mwajili wake ambaye ni ccm.

Angalia hili la mkurugenzi wa tume ya uchaguzi, unadhani anaweza kuacha kumtangaza bosi wake, ila bila nguvu ya umma hawezi, maana anajua hata ndg, familia yake ameiacha nyumbani.
 
Yawezekana akawa hana ubavu lakini bado akatumia sayansi ya kijeshi bila kuleta madhara yoyote!Japo kwangu naona iko shida ya kuogopa kuvuliwa u IGP ikamlazimu kutenda uovu kwa wananchi hasa chama pinzani!
 
Hapo (red) ndipo ninapo maanisha kuwa HANA UBAVU.
Yawezekana akawa hana ubavu lakini bado akatumia sayansi ya kijeshi bila kuleta madhara yoyote!Japo kwangu naona iko shida ya kuogopa kuvuliwa u IGP ikamlazimu kutenda uovu kwa wananchi hasa chama pinzani!
 
Huu ndio muda pekee ambao mtu unakumbuka kwamba taulo unalofutia matako,ndio linatakiwa litumike kukausha uso pia.

Sirro kama sirro na vijana wake wanajua hawapendwi kabisa na wapinzani, si wakati wa amani tu, bali hata wakati huu ila ni kwa sababu watu wanataka wawatumie kama daraja.

Hivyo ni mwendo wa kupiga spana ili chuki iwe na uti wa mgongo.
 
huu ndio muda pekee ambao mtu unakumbuka kwamba taulo unalofutia matako,ndio linatakiwa litumike kukausha uso pia.

sirro kama sirro na vijana wake wanajua hawapendwi kabisa na wapinzani, si wakati wa amani tu,bali hata wakati huu ila ni kwa sababu watu wanataka wawatumie kama daraja.

hivyo ni mwendo wa kupiga spana ili chuki iwe na uti wa mgongo.
Sio tu wapinzani bali wapenda haki
 
Hapo tafsiri ya kutenda haki ndio penye utata maana Chadema huwa wanaona haki inatendeka pale tu matakwa yao yanapotimia hata kama sio sahihi.
 
Msijali IGP anafanya kazi kadri ya kiapo chake. Sio kwa maoni ya mtu yoyote
 
Back
Top Bottom