IGP wa Uganda na wewe nae ulikuwa na taarifa kabla ya ubalozi kutoa tahadhari?

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
IGP wa Uganda nae ajitokeze aseme kuwa taarifa walikuwa nazo hata kabla ubalozi haujatoa tahadhari.

Wamarekani ni watu wenye tecknolojia ya hali ya juu sanaa na wao ndio wanaomiliki mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook , wasapu, gmail, n.k kwa hiyo wana uwezo wa kutrack mawasiliano ya watu wote wanaotumia mitandao hiyo.

Tofauti na sisi tunaomilkki jamiiforum n.k .

IGP wa Uganda usikurupuke kuongea kwenye vyombo vya habari kwenye masuala ya kijasusi .


Updates

Kulingana na tahadhari hiyo iliochapishwa katika ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa balozi hiyo, kuna uvumi wa mipango ya mashambulizi katika maeneo yanayopendwa sana na raia wa kigeni katika Afrika Mashariki ikiwemo Uganda.

Ubalozi huo umesema kuwa ijapokuwa hauna ushahidi wa kutosha kuhusu tishio hilo ama habari kuhusu wakati ambapo mashambulizi hayo yatafanyika umewaonya wakaazi kuchukua tahadhari.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Umewataka raia kuwa macho wakati wowote katika maeneo wanayozuru, kutahadhari dhidi ya makundi ya watu wengi mbali kufuatilia habari zinazochipuka mara kwa mara .

Aidha umewataka raia kuwa macho katika maeneo yanayopendelewa sana na watalii hususan wale wa mataifa ya magharibi.

Tahadhari hiyo inajiri siku moja tu baada ya ubalozi huo kutoa tahadhari nchini Tanzania ambayo imewatakaa wakaazi kuchukua tahadhari hususan wale waliopo katika eneo la Masaki.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo

Tahadhari hiyo ilibainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyokuwa tunapokea taarifa juu ya tahadhari hiyo.
 
Acha kwanza tukio litokee ili tujue ni la aina
Gani na lengo la tukio ili kama nchi tujue makosa yetu
 
Tuliona Nyerere hana akili kwa kukataa kuwa na Balozi kule uyahudini

Ukimkaribisha Myahudi ni sawa na kukumbatia Mzoga hupaswi kushangaa Nzi wakikuzengea
 
Vyombo vyao vya dola vimejizatiti mkuu. Wananchi wale bata kwenye mahoteli makubwa kama kawaida.

Ila uzuri ni kwamba intention ya ubalozi imetimia. Wenye akili, the actual people with the money to spend kwenye said hotels wanaelewa uzito wa alert hiyo, na watachukua tahadhari husika.
 
Tuliona Nyerere hana akili kwa kukataa kuwa na Balozi kule uyahudini

Ukimkaribisha Myahudi ni sawa na kukumbatia Mzoga hupaswi kushangaa Nzi wakikuzengea
Acha chuki, mbona una viashiria vya Kiarabu, hao Waarabu wapo nchini kwetu na wamejenga na hawana wasiwasi!
 
Acha chuki, mbona una viashiria vya Kiarabu, hao Waarabu wapo nchini kwetu na wamejenga na hawana wasiwasi!

Mtu akikwambia ukiwa karibu na Wayahudi unakuwa target ya kushambuliwa na wanaochukia wayahudi ni chuki?

Lakin pia sipaswi kushangaa kwa kuwa sie watu weusi hatupendi kusikia ukweli mchungu , hata ikitokea ukatahadharishwa kuwa kuna viashiria vya shambulizi dhidi yako unaanza kutukana aliekupa tahadhari kuwa ana lengo la kukutia hofu

Any way una uhuru wa kuwaza vyovyote upendavyo
 
Back
Top Bottom