IGP: Tutamhoji Mwigulu, mwenye kujua wahusika wengine wanitumie ujumbe 0754785557!

mhalisi

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
1,181
320
IGP Said Mwema amewaomba wananchi wenye taarifa za kuweza kumtambua aliyerusha bomu pamoja na watu walionyuma yake wajitokeze au wamtumie message kupitia simu yake ya mkononi namba 0754 78 55 57 na kwamba uhusika wao utafanywa kuwa siri.

source: Gazeti la Tanzania Daima jumatatu, 17 juni 2013
 
Chonde chonde Mh. Mbowe wambieni wadau wa CHADEMA walipie gharama afu mtuonyeshe LIVE kupitia Star TV au ITV ili tushuhudie msiba huu mkubwa kwa taifa maana hata watu wa nje nao watapata bahati ya kujionea unyama huu mkubwa.
 
Chonde chonde Mh. Mbowe wambieni wadau wa CHADEMA walipie gharama afu mtuonyeshe LIVE kupitia Star TV au ITV ili tushuhudie msiba huu mkubwa kwa taifa maana hata watu wa nje nao watapata bahati ya kujionea unyama huu mkubwa.
Kwann unapindisha mjadala??? Mjilipue wenyewe ili kupata huruma halafu muanze kutupigia kelele hapa.
 
Mods nawaomba sana post hii msiiondoe na msiiunganishe na post nyingine ili wananchi wengi waweze kufikiwa na ujumbe uliomo kwenye post hii.
 
Kwann unapindisha mjadala??? Mjilipue wenyewe ili kupata huruma halafu muanze kutupigia kelele hapa.
Kama tumejilipua watukamate tulio husika ilituone uwezo wa serikali dhaifu katika kutimiza wajibu wao/ Sasapolisi walikuwa wamesimama hapo intelligensia yao haikuwambia kwamba tungejilipua? Unatoka kwenye ulanzi nini au umepiga viroba na matapu tapu
 
Haya ni mazingaombwe mengine!!! Mbona wenye akili timamu wanafahamu kuwa haya mauaji yanaratibiwa na polisi haohao? Inakuwaje tena huyo Said Mwema ajifanye kujihusisha katika uchunguzi?
 
Mwema hanaga mbinu nyingine zaidi ya kutoa namba yake ya simu. sijui kama hii mbinu inaweza kumaliza uhalifu, where is ELLIOT NESS to help us out of this mess.
 
Hongera mwema. Huo ndio uongozi. Transparent is important
Kijana shule ni muhimu kwako usipuuzie.. Kwa hiyo unampa hongera kwa kutoa namba za simu?!!! Halafu mbona kiingereza chako kimekaa tenge? Ulitaka kusema "transparency"? Unajua matumizi ya adverb, verb na noun????!!!
 
Mwema hanaga mbinu nyingine zaidi ya kutoa namba yake ya simu. sijui kama hii mbinu inaweza kumaliza uhalifu, where is ELLIOT NESS to help us out of this mess.
 
Mwema anatakiwa kujiuzuru sio kutoa namba ya simu, tumempa jukumu la kulinda raia wanauwawa mbele yaka yeye analeta utani kwa kutoa namba yake ya simu badala ya kujiuzuru kwa kushindwa kazi.
 
Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Saidi Mwema amesema kwamba Jeshi la polisi litamhoji Naibu katibu mkuu wa CCM MWIGULU MCHEMBA, juu ya kauli yake alioitoa Katika kata ya Kimandolu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani jijini Arusha.

Katika mkutano huo Mwigulu aliwaambia Wananchi waliokua wakimsikiliza kuwa wasipoichagua CCM watakufa.na baada ya siku moja tangia atoe kauli hiyo kweli watu waliuwawa kwa bomu.

IGP Mwema pia alilaani tukio hilo na kusema kwamba wote wenye taarifa na watu waliohusika na tukio hilo wamtumie ujumbe kwa simu no 0754785557 na majina yao yatafichwa.
Kinachonishangaza ni kuwa hadi sasa walio nyuma ya tukio hili la Kurusha Bomu katika Mkutano wa CHADEMA wanajulikana kuwa waliratibiwa na MWIGULU. Sio hivyo tu hata majeruhi wengi wa tukio lile hawakujeruhiwa na Bomu bali na Risasi zilizokua zikirushwa na Jeshi la polisi.

Ushauri wangu kwa IGP MWEMA, aweke kwanza pembeni swala la Siasa na afanye kazi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Mwigulu na wenzake wakamatwe kama wahalifu wengine wowote, na Askari polisi wote waliokua sehemu ile ilipotokea tukio lile pia wakamatwe. Baada ya hawa kukamatwa kwanza ndipo upelelezi ukishirikisha vyombo huru vya uchunguzi uanzie hapo.
 
Tumechoka na hizi danganya toto, kuna maswala mengi hayana majibu na huwa wanayamaliza kimtindo huu. Na hiyo POLISI jamii hatuitaki tena. Bora lisiwepo jeshi la POLISI tujue moja kuwa hatuna usalama kabisa.
 
Josephine pia ahojiwe, ni kwanini alikua anafanya mawasiliano na vijana wake baada ya tukio, tena ni wale vijana wanaotumika kudhuru watu.
 
Wenye taarifa zaidi tumeni sms kwenye namba hiyo na ole wake asipoufanyia kazi huo ujumbe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom