IGP: Tutamhoji Mwigulu, mwenye kujua wahusika wengine wanitumie ujumbe 0754785557!

Mkuu wa Jeshi la polisi IGP Saidi Mwema amesema kwamba Jeshi la polisi litamhoji Naibu katibu mkuu wa CCM MWIGULU MCHEMBA, juu ya kauli yake alioitoa Katika kata ya Kimandolu wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani jijini Arusha.

Katika mkutano huo Mwigulu aliwaambia Wananchi waliokua wakimsikiliza kuwa wasipoichagua CCM watakufa.na baada ya siku moja tangia atoe kauli hiyo kweli watu waliuwawa kwa bomu.

IGP Mwema pia alilaani tukio hilo na kusema kwamba wote wenye taarifa na watu waliohusika na tukio hilo wamtumie ujumbe kwa simu no 0754785557 na majina yao yatafichwa.
Kinachonishangaza ni kuwa hadi sasa walio nyuma ya tukio hili la Kurusha Bomu katika Mkutano wa CHADEMA wanajulikana kuwa waliratibiwa na MWIGULU. Sio hivyo tu hata majeruhi wengi wa tukio lile hawakujeruhiwa na Bomu bali na Risasi zilizokua zikirushwa na Jeshi la polisi.

Ushauri wangu kwa IGP MWEMA, aweke kwanza pembeni swala la Siasa na afanye kazi kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi. Mwigulu na wenzake wakamatwe kama wahalifu wengine wowote, na Askari polisi wote waliokua sehemu ile ilipotokea tukio lile pia wakamatwe. Baada ya hawa kukamatwa kwanza ndipo upelelezi ukishirikisha vyombo huru vya uchunguzi uanzie hapo.

Kama tungekuwa tunajuzwa kiini cha mahojiano tungeamini amini hivyo. Ila yawezekekana watu wakakaa kupiga gahawa ili kuwaridhisha watanzania. Dawa iundeni Tume huru ya Kijaji ambayo watu wote watahusika kama kweli hakuna janja janja. Mahojiano mema.
 
Atupe majibu ya chunguzi zilizopita kwanza.ya Mwigu na CCM atuachie wananchi tutawapa adhabu muafaka.subirini muone!
 
Serikali hii si Mwema wala Kikwete anaaminika. Kila siku wamekuwa na maneno matamu ya kuonesha wanakusudia jambo fulani kumbo hakuna kitu. Utasikia 'Tutawasaka ndani na nje ya nchi'. Ni Mungu tuu anajua nilivyochoka na hawa watu.
 
yaani mpka ameua ndiyo wanajifanya kumhoji...mpango wa kilichofanyika siyo cha mwigulu nchemba tu bali hata amri jeshi ana jua na kinana ndiyo mratibu...polisi walitekeleza waliyoagizwa.
 
yaani mpka ameua ndiyo wanajifanya kumhoji...mpango wa kilichofanyika siyo cha mwigulu nchemba tu bali hata amri jeshi ana jua na kinana ndiyo mratibu...polisi walitekeleza waliyoagizwa.
Mmmm? Hawa jamaa wasije kabisa katika mikutano basi.
 
Ndugu zangu lisemwalo lipo na kama halipo basi laja!! Kila tukio baya linalotokea mara zote mtu anae nyooshewa Vidole ni MWIGULU MCHEMBA!! ni kwanini yeye tu?
Inastahili mtu huyu ajichunguze au vyombo vya dola vimchunguze kwani lazima kuna tatizo juu ya tabia na mwenendo wake.

Huyu mtu anayejiita mchumi wa daraja la kwanza amekua akitumia mbinu na hila chafu dhidi ya CDM na viongozi wake ili tu kujitafutia Sifa za kijinga kama hizi za kuuwa watu wasio na Hatia.

Ktk mlipuko wa Soweto Arusha mlemgwa alikua Mbowe na Lema na mrusha bomu alipoona Mbowe ameshuka jukwaani kwenda kukusanya fedha kitu ambacho Mbowe huwa hafanyi.lakini siku ile kile ndicho kilimuokoa. Mrusha bomu alijaribu kurusha alipo Mbowe lakini ikawa imedondoka takriban mt 10 na alipokuepo Mbowe. Watu wengi walipigwa risasi na Polisi na sio bomu pekee lilowajeruhi.
Mwigulu ni HATARI SANA KWA AMANI YA NCHI YETU.
 
Naapa,huu ni mchezo wa kuigiza.Nina hasira,nitatumia tafsida na mfikiri kwa makini ndio mtanielewa.Kuna MJUSI,KENGE na MAMBA wote wanafanana.Hakuna kitakachoendelea hapo hata kama mtapeleka mtapeleka mtuhumiwa kwamba ni huyu.Kazi zinafanyika kwa mazoea.
 
Naomba watanzania wapenda amani tushirikiane kumtumia sms au kumpigia kabisa IGP Said Mwema kuwa Mwigulu Nchemba Mb ni chanzo na mchochezi wa vurugu Tanzania. Kwa kurejea kauli zake Mwigulu ni wazi ndiye anayepanga haya yote ya uvunjifu wa amani Tanzania.

Nimeisikiliza video yake moja kampeni ya Arusha, anasema CDM ni wauaji bila kuthibitisha. Haiwezekani mtu mzima aropoke hivi na kuwajaza hasira wananchi wa kawaidi ambao wanaweza kuamini kauli za huyu mchochezi. Ninasikikitishwa sana na Mbunge huyu asiyemstaarabu kabisa.

Amemtembeza sana yule kijana aliyemwagiwa tindikali kuwa ni CDM wamefanya hivyo lakini chakushangaza ni kutotoa ushahidi mahakamani juu ya jambo hilo.

Narudia tena tumwambie IGP amshughulikie huyu mtu anayechochea vurugu na kudhalilisha utu wa binadamu. Wenye number na e- mail za IGP naomba muweke hapa.
Mwigulu Nchemba ni Mchochezi wa Vurugu Tanzania
 
Mwigulu ni muuaji wala asiachiwe anyongwe!jaman nchi yetu co ya vita watu mpaka mabomu mi nawambia ccm wasisahau kwamba na wao watakufa
"Binadamu hatadumu katika fahari yake atakufa tu kama mnyama"
 
Mkuu na imani hii ni danganya toto,walio Arusha waungane na wana Arusha kwenda kuwazika marehemu,serikali ya ccm,policcm tusitegemee lolote
 
Ndugu zangu lisemwalo lipo na kama halipo basi laja!! Kila tukio baya linalotokea mara zote mtu anae nyooshewa Vidole ni MWIGULU MCHEMBA!! ni kwanini yeye tu?
Inastahili mtu huyu ajichunguze au vyombo vya dola vimchunguze kwani lazima kuna tatizo juu ya tabia na mwenendo wake.

Huyu mtu anayejiita mchumi wa daraja la kwanza amekua akitumia mbinu na hila chafu dhidi ya CDM na viongozi wake ili tu kujitafutia Sifa za kijinga kama hizi za kuuwa watu wasio na Hatia.

Ktk mlipuko wa Soweto Arusha mlemgwa alikua Mbowe na Lema na mrusha bomu alipoona Mbowe ameshuka jukwaani kwenda kukusanya fedha kitu ambacho Mbowe huwa hafanyi.lakini siku ile kile ndicho kilimuokoa. Mrusha bomu alijaribu kurusha alipo Mbowe lakini ikawa imedondoka takriban mt 10 na alipokuepo Mbowe. Watu wengi walipigwa risasi na Polisi na sio bomu pekee lilowajeruhi.
Mwigulu ni HATARI SANA KWA AMANI YA NCHI YETU.

Kakika nimeisoma hii coment yako mpaka mwili ukasisimka ghafla.Watanzania wenzangu tusimame pamoja na kusema "sasa imetosha"nguvu ya umma ifanye kazi tutaendelea kunyanyaswa hadi lini,na tuache nidhamu ya woga.
Kumbuka
The future belongs to those who prepare it for today-Malcom X
 
Nasikia ametoa namba zake za simu kama kuna mtu anazijua plz naombeni nimwambie kitu ama za kamanda yoyote wa Chadema anaeweza kufikisha taarifa yangu nitakayo mpaa itasaidia sana narudia itasaidia sana kuanzaia ama kuendelea walipofikia kwa uchunguzi wa tukio la Arusha SOWETO
 
Mkuu na imani hii ni danganya toto,walio Arusha waungane na wana Arusha kwenda kuwazika marehemu,serikali ya ccm,policcm tusitegemee lolote

Inawezekana lakini tuoneshe kuwa Mwigulu ni hatari hata asipofanyia kazi lakini sisi tutimize wajibu wetu wa kuwashughulikia Wahalifu.
 
Haya sasa namba ya simu ndio hiyo ubaoni wajuaji andikeni utumbo tuwasahau.
 
Mwigulu na kundi lake wakamatwe kwanza,upelelzi na mahojiano yaendelee huku akiwa ndani!!Tangu tukio hili limetokea hawa watu wameingia mitini wanaona aibu,woga hata kuingia JF
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom