IGP Sirro, yule askari aliyefanya udhalilishaji mkubwa wa kijinsia dhidi ya Ester Matiko achukuliwe hatua kali za kisheria na za kijeshi

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,617
37,815
IGP, Habari za Mtwara.

Nafikiri umeiona Clip inasambaa ya Askari wako akifanya udhalilishaji mkubwa wa kijinsia wakati wa kampeni - ameonekana akimdhalilisha waziwazi kabisa Ester Matiko Mgombea Ubunge jimbo la Tarime mjini wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu.

Kwa sababu wewe IGP umesema wazi kwamba Jeshi letu l a Police linafanya kazi kwa weledi na ni la mfano kwa uadilifu ila kuna Askari wachache huwa wanalichafua, sasa tunakutaka kumchukulia hatua za kisheria na za kijeshi huyu askari wako maana alichokifanya si kitendo cha kibinadamu kabisa, ni kitendo cha aibu na cha kukemewa kwa nguvu zote.

Kifupi amelidhalilisha sana jeshi letu la Police kwa kiwango kikubwa.

Tunaomba achukuliwe hatua yeye pamoja na aliyemtuma kutekeleza ufedhuli huo unaokiuka haki za binadamu hasa kwa hawa mama zetu.

Nawasilisha kwa masikitiko makubwa!
 
Kuna mwingine pia kule Kawe alisema "wametuletea binti", wakati yeye ndiyo "-ke" na yule aliyekuwa akim-refer kama binti ni "-me"
 
Back
Top Bottom