Ni kweli kitendo kilichofanywa na kijana Hamza(r.i.p) sio cha kiungwana na hakifai kuigwa katika jamii

lakini vile vile, afande sirro amepotoka kwa kauli yake kwamba wazazi wasizae watoto kama 'hamza' kwa sababu kuzaa ni mipango ya Mungu ambayo binadamu hawezi kujipangia au kuamua azae mtoto wa aina gani

Pia mzazi anaweza kuzaa mtoto na kumlea kwenye makuzi na maadili mema ila akaja kubadilika ukubwani na kufanya vitendo viovu pasipo wazazi wake kufahamu.

Msikilize hapa Sirro akibeza uzazi wa mama zetu

View attachment 1912695
Ila tuwazae kina Ole Sabaya wengi!!! Mwenyezi Mungu atunusuru
 
Siro acha ushamba!watoto kama Hamza hawazaliwi wanatengenezwa kuwa walivyo na maaskari msiojali utu kama nyie!!!!Kwa miaka sita mmezalisha chuki kali katika jamii dhidi ya serikali inayotawala kwa kuwatesa na kuwaumiza wapendwa wao maksudi kabisa!!!vuneni mlichopanda!!!HAMZA ALISEMA WAZI KABISA ANA WATAKA NYIE WALA SI RAIA BALI NINYI!MJIULIZE WAPI MMEANGUKA MJIREKEBISHE!!!
Kwa hiyo HAMZA alikuwa gaidi wa polisi huku polisi nao wakiwa magaidi wa vyama vya upinzani
 
Kuwa IGP katika Tanzania haihitaji uwe na hekima kiasi gani bali ni namna gani unaweza kuipigania ccm na kupambana na Chadema.

That's the key job qualification that Mr. Sirro was believed to possess.
 
Wazaz wanahusika nini hapo,kuna clip inatembea jamaa anasema anamtaka inspecta wa polisi akimtaja jina kwa kuua waislamu.Kwa kauli hii toka police inaleta mshituko,operation za polisi zinaua watu wasio na hatia,wazaz hata wasihukumiwe.
Hivi huwa umejaribu kufiria dhi ulichokiandika. Labda nikuulize swali jepesi tu tangia umezaliwa mpaka Sasa una miaka mingapi? Je Kuna wakati Igp ametoa oda ya kuja kukuua wewe? Watu huwa tunaongea Sana bila kufikiria. Lakini simaanishi kwamba hakuna wanaoonewa. Ila watu huwa tunapenda Sana kuongea yaliyotukia lakini hatusemagi Yale ya nyuma ya pazi. Kama una mtoto wako akija kwako kukwambia amepigwa muulize Ni kwa nini amepigwa utakuja kushangaa majibu yake yatakavyokuwa.
 
Na wazazi wa hawa polisi ambao kila siku wanabambikia watu kesi za ugaidi, uhujumu uchumi na utakatishaji fedha wanajisikiaje?

Hivi watoto wa igp ambaye anaongoza jeshi la hovyo, kinalobambikia watu kesi, linaloua watuhumiwa mahabusuni, linalolaumiwa hata na Rais kwa kutotenda haki, wanajisikiaje?
Lakini hivi wewe umeshawahi kubambikiziwa kesi? Mbona tunapenda kuyasema maneno tusiyokuwa na uhakika nayo? Nimejifunza mengi Sana kwa wanadamu katika kuwa nafuatilia ukweli wa mambo ambayo yanaizungu jamii inayonizunguka Mimi mwenyewe. Fanya utafiti kwenye moyo wako wewe mwenyewe ambaye na mambo unayoyafanya na uongo unaowadanganya watu wa karibu yako halafu jiulize hao unaosema wanasingiziwa.
 
Dah.... IGP ni kiongozi mkubwa, achunge kauli zake, hazisaidii; zinaongeza tu mipasuko. Kuna wazazi wengi tu wana struggle kulea watoto kwenye njia njema, bila mafanikio. Sio makusudi.
Je yeye mwenyewe watoto wake wote ni watakatifu na watiifu? Je kitendo alichowahi kufanya Zombe ndio tuseme ni mfano wa kutolea kwa makamanda wetu? Anyway kila mmoja ana busara zake katika matamshi
 
Acheni ushabiki kwenye mauala ya msingi!

Tukemee uovu!

Amani ya nchi yetu ni muhimu sana kuliko kitu kingine!

Risasi siyo kitu cha kukizoea kusikia!
 
Ni kweli kitendo kilichofanywa na kijana Hamza(r.i.p) sio cha kiungwana na hakifai kuigwa katika jamii

lakini vile vile, afande sirro amepotoka kwa kauli yake kwamba wazazi wasizae watoto kama 'hamza' kwa sababu kuzaa ni mipango ya Mungu ambayo binadamu hawezi kujipangia au kuamua azae mtoto wa aina gani

Pia mzazi anaweza kuzaa mtoto na kumlea kwenye makuzi na maadili mema ila akaja kubadilika ukubwani na kufanya vitendo viovu pasipo wazazi wake kufahamu.

Msikilize hapa Sirro akibeza uzazi wa mama zetu

View attachment 1912695
Yeye anafaida gani au ana uzuri gani? Yeye anatofauti gani na huyo anayemsema. Anatumika kuvunja katiba na sheria za nchi kila siku

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo huyu mtu anataka tuzae viumbe viovu kama yeye?! Au anataka tufyatue kama mroto/mrutu?!
Walah natafuta demu msomali tufyatue kitu design ya Hamza....🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Back
Top Bottom