Watetezi wa Polisiccm Tambueni kuwa wapo Polisi wengi ni wasitarabu wenye utu ubinadamu hawapendi uonevu lakini hushinikizwa kuwaonea watu kuwabambikia kesi na uovu mwingineo mwingi
 
Katiba mpya ijayo ipige marufuku Polisiccm kuwabambikia kesi wanafamilia pindi mwanafamilia akitenda kosa yeye binafsi
 
Kweli kuna tatizo mahali. Kama hata armored vehicle walikuwa nayo, walishindwaje kumsogelea na kipaza sauti juu wakimtaka/kumshawishi ajisalimishe. Au hiyo vehicle hawaiamini kama ni 'armored one' maana mifumo wa manunuzi nchini nayo ina matatizo lukuki!!!
Nchi imejaa magumashi hivyo hata wao hawajui nini cha kuamini.
 
Mbona nasikia babake hamza alisha tanguli mbele za haki, labda angemkanya. Ila wazo la siro ni sawa, basi tukikamata vibaka takamate na babazao, makonda aliwahi kusema tukimkamata panyaroad tuna mkamata na mzazi wake
 
Sirro alikuwa ni miongoni mwa askari mahiri kabisa, lakini kila siku zinavyozidi kwenda anapoteza mvuto na anafanya mambo ya hovyo hovyo.
Kauli zake za hovyo hovyo.
Matendo yake nyuma ya carpet nayo ni hovyo hovyo tu.

Amekuwa mropokaji zaidi ya wanasiasa.
Amekuwa mla rushwa mkubwa kupitia maaskari wake maalum.
Note; Ma RPC wengi wamewekwa kimkakati wanamkusanyia pesa kupita kawaida na naweza kuwataja.
Na wengine ma RTO na wakaguzi magari stand zote nchini wanakusanya mzigo na kumpelekea.
Siku haya yakiwa wazi ataumbuka sana na mikelele yote hii.
Embu weka wazi mkuu.
 
Ni kweli kitendo kilichofanywa na kijana Hamza( R.I.P) sio cha kiungwana na hakifai kuigwa katika jamii

Lakini vile vile, afande Sirro amepotoka kwa kauli yake kwamba wazazi wasizae watoto kama 'Hamza' kwa sababu kuzaa ni mipango ya Mungu ambayo binadamu hawezi kujipangia au kuamua azae mtoto wa aina gani.

Pia mzazi anaweza kuzaa mtoto na kumlea kwenye makuzi na maadili mema ila akaja kubadilika ukubwani na kufanya vitendo viovu pasipo wazazi wake kufahamu.

Msikilize hapa Sirro akibeza uzazi wa mama zetu.

View attachment 1912695
Sirro ni hasara ya karne kwa Taifa hili. period
 
Ifike wakati lawama za kitendo cha mtu zimuendee mtu na sio mzazi....

Sio kweli kwamba Kaka zake wote Hitler wangekuwa kama yeye au Ndugu zake wote na Gandhi au Mother Theresa wote wangekuwa ni wanaharakati

Wewe leo unaweza ukawa sawa ila tendo litakalokutokea katika maisha yako likakufanya jambo utakalofanya kesho kila mtu akashangaa. Kila kiumbe ni tofauti na kila mtu hupokea vitu tofauti..., mwingine unaweza umponda na kokwa la embe akakutukana na kukuchukia wakati mwingine anaweza akakushukuru umempa mbegu ya kupanda...
Kabisa, hakuna mzazi anapenda kuzaa mtoto anayefanya maovu, hayo ni matokeo tu,sirro ateme mate chini aisee
 
Kamanda Sirro yupo kwenye stress. Apumzike weekend kwanza. Jumatatu atupatie majibu yaliyokamilika.

Ilikuwaje kada mwenzake kwenye chama akawavamia askari na kufanikiwa kuwaua wanne?

Ilikuwaje civilian aweze kupora AK47 za askari yeye akiwa na bastola?

Ilikuwaje mtanzania anayeonekana mtu wa kawaida kabisa, tena kada anayeshiriki mpaka kampeni za CCM na kukijengea chama matawi abadilike ghafla?

Ilikuwaje tetesi za kuporwa madini yake na askari, mbona hazikanushwi wala hazitolewi tamko?

.............R.I.P Hamza
Kamanda anachanganyikiwa kwa spidi ya 6G
 
Back
Top Bottom