IGP Sirro: Wananchi wa Pemba walimnyang'anya Silaha Askari na Kumchinja

Loxodona

JF-Expert Member
Apr 3, 2019
354
618
Katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV nimemskia Kamanda Sirro akisema kuwa Polisi walilazimika kutumia nguvu waliyotumia Ili kudhibiti wananchi huko Pemba baada ya Wananchi hao kumnyang'anya Askari Bunduki na Kumchinja.

Aidha, ameelezea kuwa takriban risasi nane zilizokuwa kwenye Bunduki ya Askari aliyechinjwa zilitumiwa na wananchi hao. Sirro kaelezea kuwa kuna baadhi ya Wananchi wamekutwa na mabomu Hali inayoashiria vurugu.

IGP Sirro amesema kuwa Wagombea wa Wapinzani walijipanga kufanya fujo Kwa vile walikuwa wamekata Tamaa na waliona hawawezi Kashinda. Baada ya Kubanwa vizuri, Sirro akapoteana.

Kimsingi kauli za Sirro zimejaa utata mwingi na Kwa sehem kubwa anawakandamiza wagombea wa upinzani. Ni dhahiri kuwa hayupo neutral.

Nimemskia pia Sirro akiwashkuru Sana Watanzania Kwa kulipa heshima Jeshi la Polisi.

Nini maoni yako kwa kauli hizi chache za Sirro kuhusu utendaji wa Polisi na Sababu zake.
 
Wananchi pemba waliandamana wakiwa na "VIFARU VYA KIVITA" sambamba na "MANOWARI" pamoja na "NDEGE ZA KIVITA AINA YA DRONES".

Ana halalisha wizi wa kura na mauwaji ya watu wasio na hatia, kwasababu yalifanyika kwa amri ya boss wake mtakatifu.

 
Sirro kwenye hii issue anachanganya taaluma na siasa ndipo anapokosea.

Anaonekana bado yuko under pressure anaogopa kuongea neno lisije kumkwaza bosi wake, bado ana kauli za kikampeni hajui uchaguzi ulishapita.
 
Muongo mkubwa huyu wangenyanganywa Silaha si pangechimbika pale wanatengeneza utetezi baada ya kuona maji ya shingo sasa
 
Siro ana mipasho kama mwimba taarabu. Leo wakati akizungumza na Waandishi wa habari alikuwa very biased na Wapinzani eti walipanga kuvuruga uchaguzi.
ICC inamwandalia jarada hata aje nini kutaka kuwabambikia watu tuhuma feki
 
Back
Top Bottom